Bandari ya Dar yazidiwa na wingi wa meli zinazosubiria. Baadhi ya Meli zimeanza kupelekwa Bandari ya Mombasa

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,042
49,727
Kwa mujibu wa jarida la The Standard likinukuu taarifa Kutoka The Ports of Africa ni kwamba Bandari ya Dar imezidiwa na meli kiasi kwamba hadi jumanne ya wiki hii ya Disemba kulikuwa na meli 38 zinazosubiria kushusha mzigo.

Aidha imefikia mahala muda wa kusubiria unafikia siku 30 jambo ambalo limeleta hofu ya gharama za kukomboa bidhaa.

Kutokana na Hali hiyo, meli nyingi ambazo zilikuwa zitie nanga kwenye Bandari ya Dar zikiwa na mzigo wa Tanzania na Nchi majirani zimelazimika kuanza kwenda kushushia mizigo Bandari ya Mombasa Kenya ambayo inaonekana Ina nafasi.

Ikumbukwe hii ni disemba ambayo Huwa na mizigo Mingi sana Kwa Ajili ya matumizi ya msimu wa mwisho wa mwaka lakini TPA hawafanyi jitihada za kukabiliana na seasoned cargo volumes.Huku ni Kuchezea Uchumi wa Nchi kama sio hujuma.

Swali Kwa Mamlaka na TPA.

Hivi mumeshindwa kabisa kuondoa tatizo la msongamano ambao unaongea gharama za bidhaa na kutatuza Ufanisi wa Bandari yetu?

Kama tatizo ni nafasi ndogo ya Hiyo Bandari, Serikali inajivita vuta Kwa nini kuanza Ujenzi wa Bandari kubwa ya Bagamoyo?

Uchumi unazidi kukua wa ndani ya Nchi na Nchi jirani aelfu ya mizigo yatalazimika kupita hapo Sasa mbona sioni jitihada za kuwa mbele ya mda badala yake tunafanya kazi ya zima moto?

Kama shida ni uchache wa gati na space ndogo ya Bandari sitarajii Ufanisi wowote kutoka DP World Kwa sababu tatizo la msingi ni ufinyu wa nafasi.

Ni jambo la kusikitisha kwamba tunafukuzana na wauza mikaa,mama ntilie nk wakati tunachezea Uchumi wa Jiografia Kupitia Bandari zetu.

Inasikitisha sana.

View: https://twitter.com/StandardKenya/status/1732724180854993029?t=QEC5GMSCcoQNO8FW0fWYnw&s=19
 
Haraka za nn mpaka unaandika visivyoeleweka..
bandari ya Dar imezidiwa halafu meli Tena zinapelekwa bandari ya Dar, ndio upupu gani huo?
Ujuaji mwingi mbele kiza
Hata mm sijamwelewa yaani bandari ya Dar imezidiwa halafu mzigo umehamishiwa bandari hiyo hyo ya Dar,kazi kwelikweli.Tuwe tunatulia tunapoandika vitu.
 
Kama shida ni uchache wa gati na space ndogo ya Bandari sitarajii Ufanisi wowote kutoka DP World Kwa sababu tatizo la msingi ni ufinyu wa nafasi.
Mbona mko hivi nyie walamba miguu ya Waarabu? mnataka kutuhadaa na kutulaghai

Kwamba kuna ufinyu wa nafasi za kuegesha Makontena tena?

Yaani unasema DPW wamefanya uamuzi wa kuwekeza bila ya kufanya tathmini? Halafu tukisema mliwagawia Bandari kwa ulafi na uchu wa madaraka mnavimbisha mashingo na mashavu

Kwamba mabilioni ya fedha za mikopo inayokwenda kuwamaliza Watanzani na iliyotumika kuboresha Bandari yetu were in vain? Ni hasara tupu?

Kwamba DPW waje kuwekeza, kuboresha, na hatimaye kuongeza ufanisi (hoja zenu za kugawa bandari) and so forth na madudu mengine kama hayo halafu pakitokea masuala hasi muwalalamikie Watanzania na mamlaka ya Bandari wakati wao DPW ndio waendeshaji wa Bandari?? TENA?

Sasa mnajitokeza kuanza kujenga hoja kwamba DPW wameshindwa kazi kwa sababu kuna uchache wa "gati" na "Space" au kama wanavyosema wataalam 'you're creating a plausible deniability' yani mnajenga mazingira ya kwenda kusema huko mbele kwamba DPW imeshindwa kwa sababu ya gati na nafasi.

isitoshe, mnawalalamikia TRA na TPA.
Niwaulize enyi walamba makobazi, hivi vile vifaa mlivyosema Rais atawekewa na DPW vya kumonitor yanayojiri bandarini ndio vipi tena....anaona michanga? au nako mseme kwa sababu ya kukatika umeme mfumo haufanyi kazi iliyokusudiwa! sasa mkatae alikuwa hajui haya.
 
Meli haiwezi ikabadili (Port of Discharge) bandari ya kushushia mzigo kisa foleni ya gati. Changamoto za meli kukaa nje muda mwingine usababishwa na sababu za hali ya hewa kwa meli zenye mizigo ya kichele(bulk cargoes).
 
Back
Top Bottom