Bandari ya Mtwara yaipita Bandari ya Tanga, yashika Nafasi ya Pili Nyuma ya Dar kwa kuhudumia Shehena Kubwa za Mizigo

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,115
49,838
Ufanisi huu umetokana na kukamilika Kwa Maboresho yaliyogharimu mabilioni ya Shilingi.

Aidha Bandari ya Mtwara imeanza kupokea Shehena ya mafuta yanayotumika Mikoa ya Kusini mwa Nchi.
---
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema Bandari ya Mtwara imeshika nafasi ya pili baada ya Dar es Salaam na kuipita Tanga kwa wingi wa mizigo inayopita bandarini na huduma zinazotolewa kwa wateja.

Naibu Mkurugenzi wa TPA, Juma Kijavara amesema shilingi bilioni 147.8 ziliwekezwa wakati wa ukarabati wa bandari hiyo uliohusisha ujenzi wa magati mapya pamoja na vifaa vya kisasa vya kutunzia mizigo.


My Take
Naendelea kujiuliza ilikuwaje awamu ya 5 ikaamua kumwaga matilioni ya kujenga Sgr Kupeleka Mikoa ambayo Haina hata mzigo wa kuhudumia?
 
Back
Top Bottom