Mengi usiyoyajua kuhusu Bandari ya Dar es Salaam

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
430
623
Hizi hapa dondoo 15 muhimu za kuzingatia dhidi ya propaganda hasi kwa bandari ya DSM

1.Magati yote 12 pamoja na maeneo ya kuhudumia shehena za mafuta yanahudumia meli hadi kufikia muda huu wa leo tarehe 28 Januari 2024, tofauti na wapotoshaji wanaoposha kwa makusudi kuwa ni magati mawili (2) tu ndio yanayofanya kazi kati ya magati 12 yaliyopo.

2.Taarifa zinaonesha ukweli halisi watu wakichapa kazi katika magati yote 12 na kuongeza ufanisi. Kwa mfano, Gati namba Sifuri (0) ambalo ni mahsusi kwa kushusha shehena ya magari nalo linahudumia meli MV Yangze 32 ya mizigo mchanganyiko.

3. Idadi na wingi wa meli bandarini unabadilika ukiona leo foleni meli 20 na keshokutwa ukaona meli 20 haina maana ni zilezile maana yake kuna meli zimehudumiwa na nyingine zimekuja kutaka kuhudumiwa.

4. Ni sawa na shuleni mtu anaweza kuhoji mbona kila mwaka shule zinakuwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne. Maana yake ni kuwa kadri wengine wanavyomaliza shule ndivyo wengine wanaanza shule, wa kidato cha nne akimaliza wa kidato cha tatu anapanda cha nne, wa cha pili anapanda cha tatu, wa cha kwanza anapanda cha pili na aliyemaliza shule ya msingi anapanda cha kwanza ni mzunguko. Ndivyo mzunguko wa meli unavyokuwa

5. Mara kadhaa TPA wametufafanulia kuwa meli kuongezeka ni neema sio laana. Tumshukuru Mungu kila meli zinapoongezeka maana yake ajira zinaongezeka, mapato yanaongezeka, makusanyo yanaongezeka na mzunguko unaongezeka.

6. Ni rahisi kusema kuwa meli zinakimbia bandari ya Dar zinakimbilia Mombasa lakini kiuhalisia huu ni uongo na hautekelezeki.

7. Tabia za kibiashara za bandari ya Dar zinaifanya iwe ya kipekee kwa wenye meli kwa kuwa wana uhakika wa kupata mzigo wa kurudi unaotokana na exportation ya nchi jirani hasa madini tofauti na Mombasa ambayo haina mzigo wa kurudi.

8. Haiingii akilini pia kusema mteja wa mzigo kutoka Lusaka Zambia akashushe mzigo wake Mombasa kisha autembeze kutoka Kenya-Tanzania-Zambia wakati anao uwezo wa kutumia Bandari ya Dar moja kwa moja
 
Waajiriwa wote wametoka mkoa mmoja wameajiriana kindgu ndyo maana uwizi na ufisadi haukomi bandari
 
Back
Top Bottom