DP World kuanza mchakato wa kuajiri, Wafanyakazi wa TPA wadaiwa kutakiwa kuchagua kwenda DPW au kubaki TPA

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891
Wale waliokuwa wakitetea kuwa DP World wakija hawatapunguza watu kazi njooni hapa mtueleze. Jamaa ndio wameishauziwa taratibu wanaanza kuondoa watu. Kiko wapi?

433720205_1426656151280759_5530512626943812729_n.jpg
---
Tarehe 22 Oktoba, 2023 Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) iliingia Mkataba na Kampuni ya DP World ya Falme ya Dubai unaohusu uendeshaji wa Gati Na. 0 hadi 3 na Gati Na. 4 hadi 7 za Baridari ya Dar es Salaam kwa kipindi cha miaka thelathini (30). Kutokana na makubaliano hayo yanayohusisha usimamizi na uendeshaji wa maened tajwa, Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam wanapaswa kuchagua kati ya kubaki TPA au kusitisha mkataba wa ajira wa TPA na papo hapo kuajiriwa upya na Kampuni ya DP World.

Menejimenti imekamilisha zoezi la utoaji elimu kwa Watumishi wote wa TPA walio kwenye maeneo husika lililoanza Tarehe 4 hadi 19 Machi, 2024 kwa lengo la kuwapa Watumishi wote uelewa sahihi wa mabadiliko ya uendeshaji yanayoendelea Bandari ya Dar es Salaam. Pamoja na masuala mengine, elimu hii inahusisha mabadiliko ya uendeshaji wa bandari, utaratibu wa makabidhiano, utaratibu wa mtumishi kusitisha mkataba na TРА па раро hapo kuajiriwa upya na Kampuni ya DP World (KWA MTUMISHI ATAKAYEKUWA AMEAMUA KUFANYA HIVYO KWA HIYARI YAKE MWENYEWE BILA KUSHURUTISHWA), pamoja na stahiki ambazo zitatolewa na TPA kwa mtumishi atakayeamua kusitisha mkataba wa ajira wa TPA na kuajiriwa upya na Kampuni ya DP World.

Kwa msingi huo, nawajulisha Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam kuwa, makabidhiano kati ya TPA na Kampuni ya DP World yameanza kutekelezwa. Kwa kuwa zoezi la utoaji elimu kwa Watumishi limekamilika, Watumishi watakaoamua kuajiriwa upya na Kampuni ya DP World wanatakiwa kufika na kuorodhesha taarifa zao Jengo la TPA Makao Makuu, Ukumbi wa Mikutano Ghorofa ya 32 kabla au ifikapo Tarehe 29 MACHI, 2024.

Update:
- Mamlaka ya Bandari (TPA) yatoa ufafanuzi kuhusu hali ya ajira za Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam
 
Mkuu mbona tangazo lipo wazi au mimi ndio sielewi? Huwezi kuwa mtumishi wa serikali halafu hapo hapo ukawa mtumishi wa DPW. Mumishi anachagua abaki TOA au aende DPW na huo ndio utaratibu na hao watumishi wamepewa elimu na muda wa kuchakata suala hili tangu mapema sana.

Kwa ninachofahu na nilichoelewa ni kuwa Ukiamua kwenda DPW utapewa terminal benefits zote kisha unaajiririwa DPW ambapo huko ni private sector na tunajua huko hakuna mbambamba ni kazi kwa kwenda mbele tofauti na serikalini ambako hata uharibu vipi basi unaangaliwa au watakuhamisha kitengo. Lakini private sector huwa wapo strictly.

Sasa hapo ni uamuzi na uchaguzi wa mwajiriwa mwenyewe abaki au aende lakini hakuna aliyetimuliwa wala kulazimishwa kuchagua atakacho
 
Vipi ikiwa utasitisha Mkataba TPA na kisha Usiajiriwe DP World?
Kwa mujibu wa mafunzo yaliyotolewa wakati wa elimu ni kuwa hicho kitu hakuna. Ni either ubaki serikalini au uende DPW. Yaani ukiacha serikalini basi unapelekwa moja kwa moja DPW bila hata interview lakini huko DPW utapimwa kulingana na kazi yako na taratibu zao kwani ni private sector
 
Back
Top Bottom