For the sake of learning, naomba kushare story ya rafiki yangu kipenzi aliefariki kwa ukimwi mwaka 2002.
She was smart and intelligent, extremely beautiful but very decent. Mamake alimzaa akiwa form two, so you can imagine walikuwa kama mtu na dadake. Wakati akiwa form three (mie nikiwa form two) step dad wake akaanza kumtaka. Unajua tena shapely legs, kijungu na bado anavaa kaptula na tites. Baba alichofanya ni kusubbotage uhusiano na mama kwakudai mwanao ananidharau nitamfukuza hapa kwangu. In the end, mdada alifukuzwa alipomaliza form four!
Baba alikuwa anamtuma mahali, then anamfuata na kumbembeleza. In a panic anakataa na kukimbia. Akirudi home mama anaambiwa mwanao mjeuri kaenda mitkasi yake wala nilipomtuma hajafika. Kumbuka binti anatumwa kwa mguu, na baba anamfuata na gari! So obviously baba anarudi home kabla yake! Anamtuma ampelekee mtu hela, anafuata anamuambia hela zichukue tu, na dada anakataa!
Matokeo ya form four, dada ana div 1.10. Aliamua kuondoka nyumbani kwawarranty ya treni aliyofanyiwa mpango na mama wa rafiki yetu aliekuwa trc enzi hizo (mamake pia alikuwa trc). Unajua aliishia mikononi.mwa mtoto wa mwenye bus from dar to iringa. From there she never looked back. No home, no parents, na akajitambua ni mrembo.
Alifariki na hiv kama miezi 2 baada ya kumaliza st augustine. Chuo kilimsafirisha baada ya mitihani na ikalazimu apelekwe kwao. Still, akiwa marehemu alipigiwa brass band kwa kuwa best student. Alijilipia ada na kila kitu kwa michango ya wanaume!
Naandika hii na machozi. She was still a virgin i promise you. She was a good gal, and was forced into prostitution. Mamake hakuwahi kujua kilichotokea hadi alipoona mwanae anakuja kufia nyumbani. Bahati mbaya sana mamake nae alifariki kwa ukimwi.
Kitu cha ajabu, tulijadili hichi kitu na kumuambia usimuambie mamako kitamuumiza sana. Najishangaa sikumuambia mama, labda angemsaidia! Nilikutana nae mwanza in less than 6months kabla hajafariki. Sikumtambua, kwa jinsi alivyobadilika na kuchakaa.
Challenge kwenu wote: mwanao anaweza kukuambia baba ananitaka? Uncle ananitaka? Je kijana wako anaweza kukuamvia uncle ananishikaga makalio? Fanya leo: fungua mlango wa mawasiliano. Tell ur kids you can share ANYTHING with me. Ni wangapi humu mabinti zao wanavunja ungo hata hawajui na mama anajidai hawezi kuongea hayo mambo?
Copy:
AshaDii,
Asprin,
Dark City,
Kongosho