Kila nikijaribu kumsamehe/kuwasamehe nashindwa

NothinGold

Member
Nov 2, 2019
56
206
Mnamo mwanzoni mwa 2009 nilianza urafiki na mwanamke mmoja ambaye nilikutanishwa na Ndugu yangu mmoja hivi undugu wa Mbali kidogo. Tulidumu Kwenye mahusiano kwa miaka miwili yeye akiwa anakaa kwao, mwaka 2011 alipata ujauzito baada ya kupata ujauzito tuliamua kuanza kuishi pamoja.

Kabla sijaendelea zaidi nieleze vitu fulani fulani. Baada ya mimi kumaliza Chuo na kuanza maisha nilijitahidi kununua kila kitu kinachotakiwa ndani ya Nyumba. Na kwa vile sikuwa na wategemezi sana zaidi ya mama yangu kwa hyo mshahara wangu haukuwa na mambo mengi. Vitu nilivyokuwa nanunua vilikuwa classy kweli kweli. Zaidi ya yote nilikuwa nalipwa mshahra mzuri kwa hyo hela ya kununu labda sofa seat ya zaidi ya 2M ilikuwa sio tatizo.

Nilikuwa nimepanga Nyumba ya vyumba 3 yenye sitting room Kubwa dining room na jiko. Chumba changu kilkuwa chumba kweli kweli. Kitanda 6*6, kabati Kubwa la Nguo, carpet Kali sana la manyoya, na vikorokoro kibao. kusema ukweli chumba changu kilikuwa chumba kweli kweli. Kuna demu Mmoja nilimuingizaga chumbani kwangu siku moja alitaka kung'ang'ania asitoke, alikaa kwangu kama week moja hivi nikaona anataka kuamia ikabidi nimtoe kwa akili. Vyumba viwili vilivyosalia kila kimoja kilikuwa na kitanda 5*6 godoro lake na kikabati cha kishikaji cha Nguo. Wakati huo nilikuwa nakaa na Mtoto wa bro ambaye alikuwa Chuo kwa hyo ndo alikuwa ananisaidia Kwenye mambo ya Usafi.

Sitting room kulikuwa kumesheeni kweli kweli, sofa seat Kali sana leather, TV flat Sumsung 32", carpert kali sana la manyoya chini, music system ya ukweli kabisa aina ya sony, na makorokoro mengi tu kama mapambo na nini na nini. Dinng room kulikuwa na dining table six seats, kabati Kubwa la vyombo likiwa limesheeni dinner sets classy kabisa na vitu vingine kibao vinavyohusika mezani.

Fridge kubwa milango miwili aina ya Sumsung likiwa limetulia kabisa kwenye corner. Jikoni kulikuwa na jiko plate nne la gas na Umeme, microwave ya Kenwood na vikorokoro vingine kibao kama masufuria classy kabisa non stick, jug la kuchemshia maji etc kwa kifupi Nyumba ilikuwa imekamilika. Nilikuwa pia na kausafiri kangu Toyota Mark II Grande( Gx 110). Kwa kiasi maisha yalikuwa yamekamilika ingawa bado nilikuwa napanga.

Wanawake hapa wanaweza uliza mimi mwanaume nilijulia Wapi kununua vitu Vya ndani na kupangilia Nyumba. Nikiwa bado A level nilikuwa naishi na bro Wangu. Bro alikuwa anajua sana vitu vizuri na ni mtu anapenda kuwa na vitu classy sana, zaidi ya yote alipata mwanamke ambaye na yeye alikuwa mjanja sana Kwenye vitu Vya ndani ya Nyumba na shopping nyingi za vitu Vya ndani nilikuwa naenda naye kwa hyo ujanja mwingi wa vitu classy niliupata kwa bro na mke wake. Washikaji Wangu walikuwa wakinitembelea lazima watatoka na gumzo. Nakumbuka kuna mshikaji Wangu Mmoja aliniomba nikamsaidie Kununua vitu kwake ingawa alikuwa na mke baada ya kunitembelea siku moja.

Basi bwana tukaanza kuishi na yule mwanamke aliyekuwa na ujauzito Wangu. Kama nilivyoeleze hapo juu Kuhusu Nyumba yangu, hvyo basi mwanamke alipofika ndani hakuna tuliochoongeza zaidi tu ya kuanza kutumia maana kuna vitu vingine vilikuwa havijawai kutumika. Mwanamke alikuta kila kitu ndani.

Tuliendelea kuishia kwa Amani kabisa huku tukilea mimba kwa furaha kabisa. Baadae nilienda kwao kijitambulisha na mambo mengine mengine. Huyu mwanamke alikuwa na mama tu kwani baba yake alikuwa ameshatangulia mbele ya haki. Alikuwa na Dada zake wawili ambao walikuwa wameshaolewa na kaka yake mmoja ambaye Naye alishaoa na alikuwa anaishi Nyumba moja na mama yake ( Nyumba alijenga baba yao)

Mwishino mwa mwaka 2011 tulifanikiwa kupata Mtoto mzuri sana wa kike. Nyumba ikawa imeongeza furaha Kubwa sana. Mtoto wetu alikuwa ni wa kipekee sana maana hata ile hadha ya Watoto Sijui kulia usiku hatakuwai kuexperience, mpaka majirani walikuwa wanatuuliza huwa mnampa nini Mtoto mbona hatusikiagi akilia.

Mtoto akakua vzuri sana bila adha ya magonjwa wala nini na kila hatua ya ukuaji wake akawa anazidi kuwa Mrembo kabisa. (Natamani hata kuweka baadhi ya Picha zake hapa ili kuleta uhalisia ) Na mpaka Sasa ni Mtoto wa kipekee sana, mstaarabu sana hata shule walimu huwa wanampendea ustaarabu wake tu. Hata ukikutana naye kwa mara ya kwanza tu huwezi acha kumpenda, she is such a special girl kwa kweli.

Baadaye mama yake na huyu mwanamke walianza kukwaruzana na mkamwana wake na mikaruzo ilifika Mbali zaidi mpaka yule Kijana wake wa kiume akamfukuza mama yake mzazi Kwenye ile nyumba waliyokuwa wanaishi pamoja. Baada ya mama kufukuzwa alienda kupanga na baadae akafanya mipango wa kujenga kajumba kadogo Kwenye shamba Dogo la kwao ambalo lilikuwa nje ya mji waliokuwa wanaishi.

Katika ule Ujenzi ilifika muda mama alikwama kwani alikuwa tu anafanya biashara ndogo ndogo. Siku moja Mtoto wake akaniambia mama amekwama Kwenye ujenzi ndo hapo nilijua kuwa alikuwa amefukuzwa nyumbani maana walikuwa hawajanieleza. Nikamuuliza Mtoto wake mama yake kakwama nini akaniambia amekosa hela ya Kununua bati za kupauwa Nyumba yake. Nikamuuliza bati ngapi akaniambia 20, basi kidume bila hiana kabisa na kwa roho moja nikatoa hela ya bati 20 mama akatumiwa pamoja na hela ya FUNDI na misumari.

Siku moja tukaenda kumsalimia mama Kwenye Nyumba yake mpya nikakuta Mazingira sio poa kama choo kilikuwa tu kimezungushiwa Magunia ikabidi nimpe mama hela nikamwambia ajenge choo kizuri. Na kuweka mazingira fresh pale kwake. Huku na kule mama akanililia shida kuwa Anataka awe analima ila hana shamba mpaka akodi, ila akaniambia kuna shamba kama hekari nne linauzwa 1,400,000 kama itawezekana nimnunulie. Kidume kwa Mara nyingine nikajitoa kwa roho safi kabisa nikamwambia mama aende akaelewane na Mwenye shamba ampunguzie mpaka 1,000,000tsh na amwambie atamlipa kwanza nusu ya hyo hela na nyingie atamalizia badae.

Mama akaenda kuongea na mwenye shamba na akakubali kupunguziwa, mama akawasiliana na sisi kwa hyo nakimtumia ile nusu na nusu iliyobakiwa nikawa nimemtumia miezi miwili badae. Kuna kipindi mama aliugua mkanda wa jeshi na kwa kiasi kikubwa hela ya matibabu yake nilitoa mimi.

Kama nilivyoeleza mwanzoni kuwa mimi sikuwa na wategemezi wengi zaidi ya mama yangu na yeye sio kuwa ni tegemezi sana ila nilikuwa tu najisikia furaha kumtumia mama yangu hela au kumnunulia zawadi yoyote kila mwisho wa mwezi. Kwa hyo baada ya kuanza kuishi na huyu mwanamke kila mwisho wa mwezi chochote nitakachomtumia mama yangu Lazima na kwa kiasi nimtumie mama yake huyo mwanamke.

Kwa mfano nikamua labda mwezi huku nimtumie mama yangu 50,000tsh Lazima nitamtumia mama yake na yule mwanamke 25,000tsh. Nikiamua labda nimtumie mama sukari 10kg, nitamtumia vile vile mama yake 5kg. Kwa hyo ndo mambo yalikuwa yanaenda hvyo na kusema ukweli maisha yalikuwa ya furaha sana ambayo ilikuwa inachagizwa na binti yetu mrembo kabisa.

Kuna wakati Watoto wa Dada zake walikuwa wanakuja kukaa kwetu wakati wa likizo, wakishamaliza likizo Lazima nitawanunulia wote uniform za shule Mpya, madaftari ya kutosha, pens na kila kitu wanachohitaji kwa ajili ya kwenda kuanza muhula mwingine. Kusema ukweli nilikuwa nawajali sana familia ya yule mwanamke na Dada zake walikuwa wanashukuru sana kwa mambo niliyokuwa nawafanyia.

Baadae tukakubaliana na mwenzangu kuwa aanze tuitions kwa ajili ya kurudia baadhi ya masomo ambayo hakufanya vzuri form four ili apate alama zitakazomsaidia Kutafuta Chuo asome. Nilianza kwanza kwa kumtafutia Chuo cha kujionoa kiingereza maana english yake haikuwa nzuri, akasoma kwa miezi 3 akawa amekuwa vzuri kidogo Kwenye lugha. Baadae nikatafutia sehemu ya tutions akaanza kupiga shule ili mwaka utakaofuata akajiandikishe kwa ajili ya kurudia Yale masomo ambayo hakufanya poa.

Ikumbukwe kuwa wakati huo mimi nikuwa naenda job asubuhi narudi home mida ya saa kumi jioni. Tuition yake ilikuwa kuanzia saa nane mpaka saa kumi kwa hyo mimi nikitoka job nampitia tunarudi wote home ingawaje alipokuwa anasoma sio Mbali sana na tulipokuwa tunaishi.

Siku moja nikawa nimepiata kumpick mwenzangu tuition ila sikumkuta, nilipomuuliza mwalimu wake akaniambia hata yeye hajui kwa nn mwenzangu hakwenda tuition siku hyo. Nilipofika home nikamuuliza mwenzangu mbona hujaenda tuition leo? akanijibu mimi sitaki tena kusoma Nataka niwe anafanya Biashara kwa hyo nisaidie hela ya mtaji. Ile kitu haikuingia akilini kabisa nikamwambia haiwezekani lazima usome, yeye akashikilia kuwa anataka afanye Biashara, tulikwaruzana kidogo asubuhi nilipoondoka kwenda job nikamwambia aende tuition lakini cha kushngaza hakwenda niliporudi nikamkuta yupo home tu.

Nilikaa Naye nikajaribu kumwelewesha sana umuhimu wa yeye kuendelea na tuition lakini Wapi hakuelewa. Ilifika mpaka nikashirikisha Mwalimu wake na yule Dogo tuliyekuwa tunaishi naye nao wakajaribu kumshawishi sana aendelee na shule Wapi akakataa. Nilimshirikisha mpaka mama yake na yeye akaongea naye ila mwenzangu akashikilia lake kuwa Anataka Biashara. Mwishowe mama yake akaniambia kama amakataa kusoma basi niachane naye maana huwezi kumlazimisha mtu afanye kitu ambacho hataki.

Mwishowe nikamua kumpa mtaji akaanza Biashara ya vitenge akafungua na sehemu ya kushona vitenge karibu na tulipokuwa tunaishi. Ile Biashara kwa kiasi fulani ilikuwa na faida ila sikuwa najishughulisha nayo sana maana haikuwa Kwenye mipango yangu juu yake. Akaanza kuwa ananunua vitenge anamtumia Dada yake mkoani alipokuwa anaishi kwa makuabaliano kuwa akiuza atampa commission. Huyu Dada badae ndo alikuja sababisha ile Biashara kufa, sutaingia ndani sana ila ni kwamba alimdhulumu Mdogo wake kwa kumdanganya kuwa aliibiwa pesa yote baada ya kuuza vitenge alivyomtumia. Huyu Dada nitamwelezea huko mbeleni kwa undani kidogo.

Mwaka 2013 tulifanikiwa kupata Mtoto mwingine wa kiume. Mimba ya huyu Mtoto haikupangwa ndo maana unaweza ona kuna tofauti ya miaka miwili tu kati ya mtoto wa kwanza na wa pili. Baada ya kujifungua na kurudi nyumbani mtoto alipata complications fulani za kiafya ambazo ilibidi alazwe hospital (neonatal department) kwa ajili ya uangalizi kwa muda. Wakati alipolazwa mwenzangu akawasiliana na dada yake ili aje akamsaidie pale nyumbani, kama kumpaleka chakula hospital na mambo mengine (wakati huo walikuwa hawajadhulumiana).

Yule dada alipofika pale nyumbani alifanya mambo ya ajabu sana sana, kwa mfano nikiondoka na kumwachi mtoto wa kazi pesa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani alikuwa anamwambia mtoto wa kazi ampe hela ili yeye akafanye manunuzi. Basi akienda huko atanunua vitu kidogo tena vya ajabu ajabu ili abaki na hela. Kuna jambo moja alifanya siku moja la ajabu sana, mimi nimeondoka asubuhi nikaacha hela ya kumwandalia mdogo wake chakula alichokifanya yule dada hela yote alitia ndani mchana akachukua wali uliobaki usiku akampelekea mdogo wake hospital.

Baadae jioni nampitia mwenzangu hospital nakuta malalamiko kuwa mzazi kapelekewa kiporo, cha kusikitisha yule dada akamwambia mdogo wake sikuacha hela ya matumizi ndo maana akampelekea kiporo wakati hela niliacha, kuna watu wa ajabu aisee. Mimi nilichofanya ni kuwa nilikuwa nikitoka job nanunua kama ni nyama au samaki halafu naamka saa kumi alfajiri napika kama ni Mtori au nini wakati nikienda job nampeleka mwenzangu, mchana namwambia anunue chakula canteen ya hospital maana walikuwa wanatengeneza Chakula hata kama ni special order. Jambo la kushangaza sana yule Dada siku zote nilizokuwa naamka alfajiri kupika hakuwai hata siku moja kuamka labda aniambie shemeji ngoja nikusaidie kupika, hakuwai.

Basi niliendelea Kufanya vile na baada ya week Mbili Mtoto akawa amerudi Kwenye hali yake na wakaruhusiwa kurudi nyumbani. Mwenzangu aliporud nyumbani yule Dada akakaa kama siku mbili hivi akaondoka bila hata kuniaga. Huyu dada ndo watoto wake walikuwa wanakuja kwangu kipindi cha likizo. Mtoto akawa anaendelea vzuri japokuwa alikuwa na changamoto za kulia sana. Mpaka Leo hii he is too emotional, kitu kidogo tu kikimkwaza Lazima ataanza kulia.

Mwaka huo huo 2013 mkataba Wangu wa kazi ukawa umeisha Kwenye kampuni niliyokuwa nafanya kazi na jamaa hawakurenew mkataba kwa hyo nikawa nipo home huku nafanya mishe za kupata kazi nyingine. Mungu saidia haikuisha muda nikapata Kazi ila mkoani. Kwa vile nature ya Kazi yangu ilikuwa na roster ya week sita kwa Mbili (yaani unafanya kazi week sita unapewa week Mbili za kupumzika) hatukuona sababu ya kuhama kwa haraka kuelekea mkoani Kwa hyo mimi nikasepa zangu mkoa nikamwacha mwenzangu na watoto.

Pale nyumbani alikuwepo yule Mtoto wa bro kwa hyo sikuwa na wasiwasi wowote Kuhusu usalama wao. Basi nikawa naenda napiga Kazi week sita week Mbili nakuja napumzika. Ila nikirudi nyumbani nilikuwa nakuta kuna mabadilko sana sana Kwenye afya ya Watoto pamoja na usafi wao kwa ujumla Ila nikikaa nao hzo week mbili za likizo wanakaa vzuri. Nikamuuliza mwenzangu mbona nikiondoka Watoto wanabadilika sana, anajibu labda wanakuwa wanakumiss sana ndoa maana wanakonda, nikimuuliza hata Usafi, anakaa kimya tu.

Basi ilibidi siku moja nimuite yule Dogo wa bro nikamuuliza Kuhusu maisha wanayoishi pale nyumbani nikiwa sipo. Yule Dogo akaniambia sababu Kubwa inayofanya Watoto wanakuwa vile ni kwamba mama yao kila kitu Kuhusu Watoto anamwachia Mtoto wa Kazi na yeye anakuwa yupo busy na Biashara ake ya vitenge. Ila kitu cha ajabu sana ni kuwa ile Biashara ilikuwa haimfanyi kuwa busy kiasi hicho maana pale alipokuwa anauzia kuna Mdada alikuwa fundi wa kushona kwa hyo hata yeye asipokuwepo pale Biashara bado ingefanyika tu.

Likizo moja nilirudi tena nikakuta Watoto Wako ovyo kama kawaida, nikamwita nikamwambia kama hyo Biashara ya vitenge ndo inakufanya ushindwe kuangalia Watoto basi nitaifunga. Nilipoondoka na niliporudi ten likizo nilikuta hali ya Watoto sio mbaya sana. Nikasema somo lilieweka.

Baadae katika harakati za kwenda kugonga Vyombo huko nilipokuwa nafanya job mkoani nikakutana na demu Mmoja tukaanza kulana kiaina ila nilimweleza kuwa mimi Nina familia na yeye akaniambia hyo haina shida sisi ni w kupoozana tu. Huku na kule siku moja nimerudi likizo nikasahau kufuta sms aliyoniandikia yule demu, basi bwana mwenzangu akawa ameiona ile sms, ilikuwa imeandika "pole na Kazi mpenzi". Mwenzangu alivyoisoma akawaka sana, nikajaribu kumwelewesha ila hakunielewa.

Kesho yake nikawa nimetoka kwenda town niliporudi nikakuta hayupo ameondoka na Watoto wote wawili. Nilipomuuliza mtoto wa kazi mama yake yuko wapi akaniambia ameondoka ila hajamuaga. Nikajaribu kumpigia simu hapokei, nikawa nimehisi atakuwa ameenda kwa mama yake. Nikampigia mama yake kweli akaniambia yupo kwake, basi kesho yake nikawasha gari nikaenda kwao. Tukakaa tukaongea tukayamaliza na mama yake akawa anamwambia mwanangu haya mambo yapo tu Kwenye ndoa kwa hyo mara nyingi yakitokea ni kuongea tu na kusameheana mnaendelea kuishi. Ikawa kama mambo yameisha tukarudi nyumbani.

Kumbe mwenzangu alichukua Namba ya yule demu kwa hyo akawa anamtumi sms mbaya mbaya sana, yule demu hakumjibu vibaya alimuomba tu samahani kwa kunitumia sms ile ila akakana kabisa kuwa hana uhusiano wowote wa kimapenzi na mimi. Basi nikawa naenda napiga mzigo narudi likizo. Hvo hvo ila wakati fulani nikawa nimemwambia mwenzangu inabidi tuhame ili wao waje ule mkoa nilikuwa nafanyia Kazi, mwenzangu hakukataa ila akasema Sasa Biashara yangu itakuweje, nikamwambia unaweza kuhama nayo au ukaacha iendelee na kule tunakoenda ukarungua tawi jingine.

Akawa amekubali ila kishingo upande maana alikuwa anasema ameshapozoea sana pale alipokuwa anafanya ile Biashara. Basi nikaondoka tena kwenda job, niliporudi nikakuta ile biashara imedorora sana sana, nilipomuuliza mwenzangu kisa cha Biashara kudorora akaniambia alichukua kiasi kikubwa cha hela akanunua vitenge akamtumia yule Dada yake, Dada yake ndo akaja na ile story kuwa aliibiwa hela baada ya kuuza mzigo aliotumiwa na Mdogo wake.

Mimi nikamuuliza, hv wewe kama Dada yako alishindwa kukujali ukiwa mzazi tena umelazwa hospital na Mtoto mchanga akiwa anapigania uhai wake, Leo unakuja muamini huyo mtu unachukua mtaji Wako karibia wote unamtumia nao mzigo? Nikaongeza, huyo Dada yako nilikuwa simwachii Mtoto wa Kazi hela ya Chakula anazichukua zile hela anakuletea kiporo hospital? Yeye alichojibu ni kuwa tusimuhukumu sana inawezekana kweli kaibiwa. Mimi nikamwambia jiandaeni nilienda nikirudi tunakuja kuhama maana sikuona sababu ya yeye kuendelea kukaa pale maana kama ni Biashara imeshakufa tayari. Muda wa kurudi job ukafika tukaagana kwa makubaliano kuwa likizo itakayofuata tutahamia kule nilipo.

Siku moja nipo job nikawa nimepata simu, hyo aliyenipigia akajitambulisha kuwa ni mama jirani yetu, akaniambia mbona mnahama bila kutuambia jamani. Nikamuuliza nani anahama? akaniambia mwenzako huku anahamisha vitu kidogo kidogo ila kwa taarifa tulizonazo hvo vitu ni kwamba anaviuza. Nikakata simu nikampigia mwenzangu nikamuuliza mbona nasikia unahamisha vitu unavipeleka Wapi? Akanijibu, aliyekuambia nahamisha vitu mwambie akuambie navipeleka Wapi akakata simu.

Kupiga hapokei mwishowe akazima simu. Jioni baada ya Kutoka job nikampigia tena ila hakupokea, nikamtumia sms kuwa unapeleka Wapi vitu, akanijibu kuwa nimeishi na wewe kwa muda na hakuna nilichopata Kutoka kwako kwa hyo hivi vitu najilipa na sina tena mipango na wewe baki na huyo mwanamke Wako huko.

Daaah..mzee baba kijasho chembamba kikanitoka, nikampigia mama yake nikamwelezea situation ilivyo, mama akaniambia nimpe muda aongee naye, badae mama yake akanipigia akaniambia ameongea naye ila amesema hajauza kitu chochote ni kwamba kahamisha tu vtu Kutoka pale tulipopanga. Nilipomuuliza sababu ya kuhamisha akasema hata yeye kamuuliza ila hakumpa sababu. Nikampigia tena mwenzangu ila hakupokea, akanijibu tu kwa sms kuwa sitaki usumbufu.

Bahati mbaya sana hii ishu ilitokea yule Dogo hakuwepo home alikuwa field. Kesho yake asubuhi yule mama jirani akanipigia akaniambia gari imeletwa alfajiri vitu vyote vilivobaki vimepakiwa. Nikampigia tena mwenzangu hakupokea baadae simu yake ikawa haipatikani kabisa. Nikampigia tena mama yake nikamwelezea kuwa mwanae kapakia vitu vyote kaondoka navyo na simpati Kwenye simu. Yule mama alichonijibu aliniambia, wewe ni shetani tena pepo mbaya tena ushindwe kwa Jina la yesu, unataka kumchukua mwanangu ukamfanye mke mweza? Shindwa pepo Mkubwa kisha akakata simu.

Daaah, nilipigwa na ganzi nikajiuliza maswali mengi sana, ni huyu huyu mama niliyemnunulia bati, ni huyu huyu mama aliyeugua nikatoa pesa yangu kumtibu, ni huyu huyu mama niliyemnunulia shamba kwa pesa yangu, ni huyu huyu mama ambaye alikuwa anajisaidia Kwenye choo cha gunia nikampa hela ya kujenga choo bora, ni huyu huyu mama niliyekuwa namtumia zawadi kila mwisho wa mwezi ndo ananitamkia maneno kama haya??

Nilienda baa nikapiga pombe sana nikarudi home niko chakari nikalala ila pamoja na pombe Zote usingizi haukuja. Kesho yake asubuhi nikampigia tena mwenzangu akawa hapatikani. Nikajaribu kumpigia yule mama jirani kumuulizia kama anaweza jua ameelekea wapi ila akasema hata yeye hajui. Nikaenda job lakn Kazi zikawa hazifanyiki. Jioni nikajaribu kumtafuta ila akawa hapatikani, basi nikawa nimemshirikisha sister yangu nikamwambia ajaribu Kumtafuta yule mwenzangu akimpata ajaribu kuongea naye. Sister akawa amempata Kwenye simu akajaribu kumuuliza kulikoni, yule mwanamke alimjibu vibaya sana sister yangu.

Mwishowe sister akamwambia kama umeamua kuuza vitu nielekeze ulipo basi nije hata nichukue Nguo za mdogo wangu. Yule mwanamke akamwambia sister hata Nguo nazo nimeuza akakata simu. Baadae nikampigia nikawa nimempata nikamwambia hata kama umeuza hvo vitu nenda kwa hao uliowauzia uwaambie hvo vitu umeuza kwa makosa hata kama ni hela ya kuvikomboa mimi nitakutumia uvirudishe nyumbani, akaniambia sina huo muda mchafu, akakata simu. Nikamtumia sms nikamwambia tafadhali Naomba urudishe vitu vyangu, akanijibu, hivi zile takataka ndo unaniangaisha Nazo uniachi nikapumua?

Kuanzia hapo wakaungana na mama yake na Dada zake wakawa wananitumia sms za matusi na kashfa za hali ya juu. Wakuu hakuna tusi baya ambalo sikutukanwa na hao viumbe. Hakuna kashfa mbaya chini ya jua ambayo sikukashifiwa na hao viumbe. Walitukana na kukashfu sana kwa muda wa siku kadhaa ila sikuwajibu,(wakuu nilipigwa mtungo yaani), siku moja huyo mwanamke akanitumia sms akaniambia fulani we ni msenge. niliifoward ile sms kwa mama yake kisha nikamtumia yule mama sms kadhaa nikamwambia. Mama nashukuru sana kwa matusi na kashfa zenu, ila kabla hujanitukana na kunikashfu ungekumbuka hata vichache basi ambavyo nilishakusaidia.

Nikamkumbusha Kuhusu bati nilizomnunulia, shamba, matibabu yake niliyogharamia, vizawadi nilivyokuwa namtumia kila mwezi nk nk. Baada tu ya kumtumia hzo sms huyo mama hakuwai tena kunitumia sms wala kunipigia simu. Na tangia mwaka 2014 mpaka muda huu naandika hii thread sijawai wasiliana na huyo mama. Watoto wake waliendelea na matusi na kashfa zao ila speed ikawa imepungua. Baadae nikawasiliana na Mwenye Nyumba kutaka kujua kama alikabidhiwa nyumba yake, akaniambia Nyumba yake alikabidhiwa na kuambiwa kuwa tunahamia mkoani.

Baadae nikawasiliana na mama yangu nikamwelezea story yote kuanzia ile ya sms ya yule demu mpaka kuuza vitu na kutokomea kusikojulikana. Sikutaka kumuhusisha mama kwenye hii ishu ila ilibidi tu nimuhusishe. Mama akaniambia ngoja ntaongea naye kwa kirefu na yeye nimsikilize. Baadae mama akanipigia akaniambia, mwanangu, si ni Mungu alikusaidia ukapata vile vitu vyote, nikamjibu ndio mama, akaniambia basi Mungu huyo huyo atakusaidia utanunua vingine tena vzuri kuliko vile, mwache aende navyo wala usimuulize tena.

Nikamwambia mama na Watoto je, akaniambia usiwe na wasiwasi atawaleta mwenyewe, au asipowaleta atakuita ukawachukue. Mwisho mama akaniambia wala usimpeleke polisi wala sehemu yoyote wewe endelea na Kazi yako achana naye. Nikamuuliza kwani mmeongea nini mama mbona unasema hvo, mother akakata simu. Hapo nikajua tu Lazima yule mwanamke akatakuwa amemjibu vibaya mama yangu.

Basi MZEE baba nikakubaliana na Ushauri wa mother nikaendelea kupiga mzigo ila Sasa likizo yangu ikawa ni huko huko maana sina pa kwenda tena. Nilianza kuwa napiga sana mashanga, mpaka nikawa kama Nataka kuwa alcoholic. Kila nikitoka job Lazima niende bar nikapige vyombo. Siku moja nipo job jamaa Mmoja wakati wa lunch akaniita pembeni akaniambia aisee nakuona hauko Sawa nini kinakusumbua.

Kwa vile sikuwa sana na mazoea na yule bwana nikamwambia niko poa kabisa, jamaa akaniambia pls talk to me, may be I can help, kuna kitu kikaniambia mpe nafasi. Basi nikamwambia tukitoka job jioni tuongozane ntakuambia kinachonisumbua. Basi jioni nikamchukua jamaa tukaenda bar fulani, ile naagiza akaniambia usiagize kilevi chochote tuongee kwanza. Basi nikamwelezea jamaa ishu tangia mwanzo mpaka mwisho. Kwa kifupi yule jamaa ndo aliyeniokoa nilikuwa naenda kupotea mazima na inawezekana hata Leo hii nisingekuwepo hapa kuandika thread hii.

Baada kama miezi miwili yule mwanamke akanitumia sms, Naomba hela ya kununulia Watoto Chakula. Nikawa nimemwambia yule jamaa aliyeniokoa Kuhusu hyo sms, jamaa akaniambia mtumie wala hata usimuulize kitu we mtumie tu hela utakayojisikia. Basi nikawa nimemtumia laki tatu, hata nimepata sikuambiwa. Siku moja sister akanipigia akaniambia kuna sehemu mjini nimemuona mwenzako ila kwa hali niliyomuona nayo inaelekea mambo yake sio mazuri akaniambia fanya ufanyalo ujue Watoto wana hali gani uko walipo. Kumbuka mpaka muda huo sijui yule mwanamke na watoto wanaishi wapi maana nilishamuuliza sana wanaishi wapi ila akawa hataki kuniambia.

Kwa hyo wakati naongea na sister nikamwambia kwa nn hata usingemfuatilia ujue anapoishi, sisister akanijibu hilo wazo hata halikumjia. Badae nikawa nimempigia yule mwanamke ili nimuulize hali ya watoto ila hakupokea. Nikamtumia sms nikamuuliza Watoto wanaendelea akanijibu wako poa, nikamwambia wapige Picha unitumie, baada kama ya siku mbili akanitumia Picha. Duuuuu...hapa nisiongee sana ila kwa kifupi wale Watoto walikuwa wanasikitisha sana, nilimuonyesha yule jamaa aliyeniokoa ile picha, jamaa akaniambia mzee unatakiwa kufanya kitu hapa la sivyo unaenda kuwapoteza hawa Watoto.

Haikupita hata week yule mwanamke akanitumia sms kuwa Mtoto mdogo anaumwa anaomba hela ya kumpeleka hospital, nikaona hapa ndo chance ya kuwaona Watoto Sasa, nikamwambia sikutumii hela nakuja nikampeleka Mtoto hospital mwenyewe, akajibu haina haja we nitumie tu hela nitampeleka, nikamwambia Hanma kitu kama hicho. Baada ya majibizano marefu akakubali niende kutampeleke mtoto hospital pamoja.

Basi nikaomba ruhusa job ya week moja. Nilipofika town nikampigia nikamwambia anielekeze anakaa wapi ili niende kuwaona, akaniambia sipo nyumbani nitakupigia badae nikuelekeze. Mida ya saa jioni ya siku hyo akanipigia akanielekeza tukutane Wapi, nilipoenda nikamkuta yuko peke yake, amekongoroka balaa, hata sikumsalimia nikamuuliza Watoto Wako Wapi? akajibu wapo nyumbani, nikamwambia twende basi nikawaone, akasema we nipe tu hela mimi nimpeleka Mtoto hospital kesho, nikamwambia hilo halitawezekana na isitoshe nataka kuwaona Watoto Wangu pia.

Yakaanza majibizano mwishowe akaondoka kwa hasira, mimi nilichofanya nikaanza kumfuatilia bila yeye kujua, Mara akachukua boda, na mimi fasta nikachukua boda nikamwambia aifuate ile boda aliyopanda yule mwanamke. Tukaifuata mpaka nikajua alipokuwa anaishi mabondeni huko uswahilini sana yaani. Basi nikaenda zangu kulala kesho yake asubuhi nikawasiliana na Yule boda maana nilichukua Namba yake akanipeleka.

Nilipofika pale yule mwanamke hakuamini macho yake, akaniuliza nani kakuonyesha hapa, sikumjibu kitu, nikamuuliza Watoto wako wapi? Akajibu bado wamelala, nikamwambia awamshe maana alikuwa na chumba na sebule, akaniambia ingia chumbani ukawaamshe mwenyewe, nafungua tu Mlango wa chumbani Mtoto wa kike Mkubwa akaamka, akaniangalia kwa mshangao akaniita, Dadiii, akaanza kulia, nikaenda nikamchukua nikambembeleza akanyamaza, nikamwamsha yule Mdogo yeye kwa vile alikuwa bado mdogo akawa ananishangaa tu ila baada ya muda akawa kama amenikumbuka tukaanza kuchezacheza pale kitandani. Nikamuuliza yule mwanamke Mtoto anaumwa nini akajibu Mtoto hajatembea kwa hyo kuna rafiki yangu ameniambia nimpeleke ccbrt akafanyiwe mazoezi (yule Mtoto alikuwa na mwaka na miezi mitatu) Duu, sikutaka hata kuongea naye sana maana mawazo yote yalikuwa kwa wale Watoto kwa jinsi walivyokuwa na hali mbaya sana sana.

Basi nikamwambia hatutaenda ccbrt inabidi tuende kwa Dr/prof Massawe Moroco, akasema Sawa, basi nikashinda pale na Watoto ila sikulala hapo. Kesho yake nikafanya utaratibu wa kupata appointment ya kuonana na Dr/prof Massawe (Kwa watu ambao Watoto wao walishatibiwa na Massawe watakuwa wanajua complications za kuonana naye). Kwa hyo nikafanya mchakato nikapata appointment ya kuonana na Massawe, tulitakiwa tuonane naye mida ya saa kumi alasiri. Siku hyo asubuhi nikaenda tena kwa yule mwanamke nikakaa na Watoto mpka Kwenye mida ya saa saba nikamwambia amwandae Mtoto tuende hospital.

Yule mwanamke alichonijibu ni kuwa siendi Kwenye hyo hospital yako nitampeleka Mtoto Wangu ccbrt, akaingia chumbani na Watoto akajifungia huko. Kwenda kugonga akakataa kufungua. Haraharaka akili ikanijia kuwa hii ishu inatakiwa nihusishe Vyombo Vya dola maana Mtoto hali yake ilikuwa mbaya sana, Sana sana kiafya. Basi nikaenda kituo cha Polisi nikawaelezea ile ishu, nikapewa askari akaja akamlazimisha kuwa Mtoto apelekwe hospital, akakubali Mtoto akapelekwa hospital chini ya uangalizi wa polisi. Kuna wanawake wa ajabu sana huku dunjani.

Tukiwa tunasubiria kuingia kwa daktari yule askari akaniuliza Kuhusu ishu yangu na yule mwanamke. Baada ya kumwelezea kila kitu yule askari alikasirika sana akaniambia tukitoka hapa huyu mwanamke haendi nyumbani anaenda kulala kituoni na walionunua hvyo vitu nitawasaka Mmoja baada ya mwingine. Mimi nikamwambia haina haja maana hvo vitu nilishasamahe ila ninachojalia kwa muda huo ni Kuhusu mustakabali wa Watoto Wangu.

Yule askari akaniambia Ndugu yangu hawa Watoto bado ni Wadogo na kisheria hawaruhusiwi kuishi na mtu mwingine ila mama yao tu labda kama amekufa, ila tupa Sheria pembeni hawa Watoto Fanya uwezalo uwatoe mikononi mwa huyu mwanamke maana usipofanya hvyo kuna siku utaitiwa maiti. Akaniambia kama unataka nikusaidie kuwachukua hawa Watoto nitakusaidia litakalonitokea na linitokee. Yule mjeda aliongea kwa hisia Kali sana. Nikamwambia Kuhusu kuwachukua usiwe na shaka nitafanya mwenyewe. Mwishowe tukaingia kwa doctor Mtoto akatibiwa tukarudi nyumbani.

Siku hyo nikalala pale kwa yule mwanamke ila nililala Kwenye sofa maana katika zile sofa alizouza alibakiza moja la watu wawili ndo lilikua hapo sitting room kwake. Kesho yake nikawa nimewasiliana na yule Dogo tuliyekuwa tunakaa naye nikamwelekeza nilipo akawa amekuja. Tukawa tumeshinda pale nikawa nimempa mkakati jinsi tutakavyowachukua wale Watoto, jioni Dogo akaondoka mimi nikabaki kwa makubaliano kuwa kesho yake aje tena kwa ajili ya kukamilisha mkakati wa kuwachukua Watoto.

Kesho yake asubuhi Dogo akaja nikamwambia yule mwanamke inabidi tuende tukawanunulie Watoto Nguo, akasema Sawa ila Watoto watabaki kwa JIRANI, nikamwambia hapana huyu Mdogo tutaenda naye ila huyu Mkubwa atabaki na dogo. Hakukuwa na shida yule Mkubwa kubaki na Dogo maana alikuwa anampenda sana Dogo na alikuwa ameshamkumbuka. Basi tukaondoka kwenda kuwanunulia Watoto Nguo tukiwa na yule Mtoto Mdogo, nikamtumia dogo sms nikamwelekeza cha kufanya.

Tulienda Karume Kwenye Mitumba, kufika nikampokea Mtoto yule mwanamke yeye akaanza kuchagua Nguo za Watoto, baada ya kuona yule mwanamke amezama Kwenye kuchagua Nguo nikaondoka fasta na yule Mtoto nikarukia tax nikampigia Dogo simu nikamwambia aondoke na Yule Mtoto kule nyumbani achukue tax nikampa location ya kukutana. Dogo naye hakufanya kosa nikawa nimeshawaweka watoto wote mikononi mwangu. Wakati haya yanaendelea yule mwanamke akawa anapiga sana simu na kutuma sms ila sikupokea wala kujibu sms, baada ya kuwa nimeshakutana na Dogo nikamtumia yule mwanamke sms nikamwambia nenda nyumbani watoto wote ninao. Akapiga sikupokea, akatuma sms nyingi sana sikujibu hata moja.

Nikampigia yule mjeda nikamwambia nimeshachukua Watoto mjeda akafurahi sana, akaniambia inabidi uondoke mjini fasta na hao watoto akaniambia kuwa Makini sana maana watu wanaweza kuhisi kitu wakiwa wanakuona na hao watoto peke yako. Nikamwambia mjeda hasiwe na wasiwasi kila kitu kitaenda sawa.

Basi tukatafuta hotel nikachukua chumba double nikatoa order ya Chakula cha watoto Wakala wakawa wamelala. Nikamwacha Dogo pale room nikakimbia kariakoo fasta nikawanunulia watoto Nguo kiasi na Viatu. Nikawasiliana na sister akaja akawaona Watoto ila alipawaona alilia sana maana wale Watoto walikuwa wanatisha yaani. Basi sister akaniambia anaondoka na watoto ila mimi nikamwambia haiwezekani maana Lazima yule mwanamke ataenda kwake maana atadhani kuwa nimewapeleka Watoto kwake. Kweli kesho yake asubuhi na mapema yule mwanamke alienda kwa sister.

Ile grande nilikuwaga naiacha kwa mshikaji maana Nyumba tuliyokuwa tunakaa ilikuwa haina parking ya ndani kwa hyo nilikuwa nahisi nikiiacha pale na mwanamke peke yake wahuni wanaweza kuja kuivua kila kitu. Nikawasiliana na mshikaji nikampa location nikamwambia aniletee gari ila jamaa akawa ameshangaa sana kuwa kwanza nilikuwa nimekaa muda sijaja likizo halafu nikaja ghafla tu bila kumtaarifu. Nikamwambia nimekuja kwa dharura tu, basi akaniletea gari kesho yake tukondoka na Dogo nikawapeleka watoto kwa mother mkoa. Kufika nikamkabidhi mama watoto nikarudi zangu job.

Sio Yule mwanamke wala Dada zake wala mama yake aliwasiliana na mimi baada ya kuchukua wale watoto. Hakuwasiliana hata na mama yangu ingawa muda baadae alijua watoto Wapo kwa mama, angeanzia Wapi kuwasiliana naye wakati alimjibu shit. Baada kama ya mwaka Mmoja akaanza kuwa ananitumia sms anaomba msamaha. Dada zake nao wakaanza kunitumia sms wananiomba msamaha na wanamwombea mama yao pia msamaha. Kwa kifupi ni kwamba yule mwanamke alipigika sana sana mpaka akawa kama kituko vile.

Sikio la kufa halisikii Dawa yule mwanamke nasikia akaja kukutana na Konda wa mabasi ya mkoa akamrubuni akazaa naye kwa makubaliano kuwa atamuoa. Baadae Konda akatokomea kusikojulikana akamwacha na Mtoto. Huyu mwanamke ameshanitumia sms zaidi ya 100 akiomba msamaha ila nilishajibu sms moja tu. Nikamwambia wewe una maisha yako na mimi Nina maisha yangu kwa hyo tusisumbuane. Kwa Sasa anaomba tu awe anawaona watoto ila hilo nilishaapa kuwa sitakaa nimruhusu kuwaona Watoto. Kama nikifa sawa anaweza kuwaona ila nikiwa hai siwezi kumruhusu kuwaona. Au watoto wakifika umri wa kujiamualia mambo yao wakaamua kumtafuta mama yao sitawakataza ila wakiwa bado chini ya Amri zangu hilo halitakaa litokee.

Wakuu naweza kuonekana mimi ni mkatili sana ila kwa mambo aliyonifanyia yule mwanamke na familia yake huwa inaniwia ngumu sana kuwasamehe na kuruhusu angalu awaone watoto

Ameshafanya juhudi sana mpaka kwenda ustawi wa jamii ila waliponipigia nikawaelezea kisa chote huyo Afisa wa ustawi aliniambia, kaka endelea kulea watoto Wako achana na huyo, tena alikuwa mwanamke mwenzake.

Watoto wapo poa kabisa, Afya tele na wanaendelea na shule poa kabisa, yule wa kike anazidi tu kuwa mrembo na wa kiume anazidi tu kuwa handsome ingawa mimi baba yao ni wa kawaida tu. Ila ni baba mzuri sana na mume bora sana sema yule mwanamke dunia ilimzidi nguvu.

Hapa nimejitahidi sana kufupisha hiki kisa ila ni kisa kirefu sana sana.


BAADHI YA WANAWAKE SIJUI HUWA MNATAKA NINI KWA KWELI
 
Msamehe tu uwe huru moyoni mwako hata hivo s ushaamua kuendelea na maisha yako sasa kinachoufanya ushindwe kuwasamehe ni nn??

Acha dunia iwafunze barabara ww lea wanao tu wakikua watamtafta mama yao wakipenda lakini wasamehe
 
Nimesoma yote mzee...ila na wewe ulikuwa leiziafea sana...mwanaume hutakiwi kuzidiwa sauti na mwanamke...yaani mwanamke anakataaje tu from nowhere...na wewe unakubali tu amekataa...

Hapo hakuna cha kusamehe wala nini...ulishamsamehe siku mingi...ila kama zamani hakuna...
 
159 Reactions
Reply
Back
Top Bottom