Thinking Aloud Kwa Maslahi ya Taifa: Ikitokea Umeitwa Mbele ya Tume ya Jaji Chande, Je Utatoa Ushirikiano?, Na Ukifika Mbele ya Tume, Utoe Hoja Gani?

Thinking Aloud Kwa Maslahi ya Taifa: Ikitokea Umeitwa Mbele ya Tume ya Jaji Chande, Je Utatoa Ushirikiano?, Na Ukifika Mbele ya Tume, Utoe Hoja Gani?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,101
Reaction score
128,716
Wanabodi,

Hii ni mada ya Thinking Aloud Kwa Maslahi ya Taifa, kukuomba ushirikiano wako kwa ushirikishwaji, kutoa maoni yako na mawazo yako kumshauri mwana jf mwenzenu, ikitokea ni wewe umeitwa kufika mbele ya Tume ya Jaji Chande, Je Utatoa Ushirikiano?, Na Ukifika Mbele ya Tume, Utoe Hoja Gani zenye Maslahi kwa taifa?.

Sisi JF tuna members wa aina tatu kuu wa jf.
1. Active members, ambao wanachangia na kushiriki mijadala, miongoni mwao, wako baadhi yao kwao jf is a serious thing, wanashiri mijadala very objectively kwa kutoa hoja zenye maslahi kwa taifa. Wako members kwao jf ni just a favourite pasttime, wakipata muda dio wanaingia, wengi huishia kusoma tuu bila kuchangia, na kuna wengine, kwao jf, ni kama kijiweni kwao, kutwa kucha ni kutukana, kulalamika na badała ya mujibu hoja kwa hoja, nao wanajibu hoja kwa viroja.

2. Kuna Inactive members humu, majina yao yapo lakini hawako active, wako dormant ila kwenye platforms nyingine nyingine wapo na tunawasoma.

3. Kuna wasomaji wa jf, ambapo hawa ndio wengi, wanaingia kama guest, kazi yao ni kusoma tuu, hawachangii chochote, miongoni mwa hawa guests, wapo pia viongozi wengi tuu wakiwemo viongozi wakuu!, mimi ninaushahidii, wa kiongozi mmoja mkubwa tuu, anaingia jf usiku. Kuna usiku mmoja, nilipandisha bandiko fulani humu jf, kuhusu issue fulani, kesho yake huyo Kiongozi Mkuu, akiwa mubashara, alijibu hoja za JF na kutekeleza ushauri wa jf, tangu hapo jamaa humu wakaanza kuniogopa kwa kudhania mimi ni wale majamaa zetu, haiwezekani ushauri jambo leo, kesho litekelezwe!, Thinking Aloud: Hongera JF kulisaidia Taifa, "Atakuwa anaingia JF in person na kutusoma!". 2021 let's be more responsible, more strategic

Hata huyu aliyepo sasa, alikiri kuwa huwa anaingia jf na kutusoma ila yeye huwa anaishia kucheka tuu!, huo ndio uwezo wake, kuona vile vya kumchekesha tuu, yale maushauri ya kumwaga humu, huwa, hayaoni!, angeyaona, akachukua hatua, kile kilichotokea October 29 wala kisingetokea.

Kuna watu wamekuwa wakiitwa mbele ya Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya October, 29, inayoongozwa na Jaji Chande, baadhi hukubali na kutoa ushirikiano, baadhi hukataa na kutoa sababu za kukataa huo wito au kutotoa ushirikiano.

Mada hii ya "thinking aloud Kwa Maslahi ya Taifa" ambayo ni moja ya mada zangu za abstracts za hypothetical situations, kumaanisha ni mada ya kufikirika tu lakini inafikirisha, na sio lazima hiki kitu kiwe ni kweli, au ni sisi JF tumekisababisha, lakini likitokea jambo likasemwa humu, likajadiliwa, kisha vyombo vya maamuzi vikatoa maagizo au kufikia maamuzi kuhusu jambo hilo kwa jinsi ile ile lilivyojadiliwa humu JF, kama zilivyo baadhi ya zile mada zangu za "the voices from within", ambazo japo nyingine huwa hazitokei, lakini nyingine ni za kweli hutokea kweli!, sasa zinapotokea kweli, hata kama the cause sio sisi, lakini kama tumepigia kelele jambo fulani, tukashauri na kisha hatua zikachukuliwa, tuna haki kabisa ya kujipongeza kuwa tulichangia!.

Kwenye mada hii, the hiypothetical situation, ni suppose wewe ni mwana jf, na umepokea mwito wa kufika mbele ya Tume ya Jaji Chande. Wewe kama mwana jf, utamshauri nini mwana jf huyu?.

1, Je Aitike Wito na kutoa ushirikiano na Tume kwa kufika mbele ya Tume?.
Akifika mbele ya Tume, tumchangie mawazo akatoe hoja gani zenye mashiko?
2. Agomee huo mwaliko, asuse na kukataa kutoa ushirikiano.
Akiamua kususa, je atoe sababu gani za kususa kutoa ushirikiano kwa Tume, kama wengi waliosusa na kutoa sababu zao za kususa?.

Naomba maoni yako!.

Natanguliza Shukrani kwa Ushirikiano wako.

Ubarikiwe sana!

Paskali.
 
Kwanza inategemea na mualikwa ukweli kuna watu wakipewa nafasi izo hawawez kataa pengine kutokana na yaliowakuta,ofis au vyeo vyao mf(mualiko kwa kada ccm au mtumishi wa gvm)pia kama mt alipata majanga ile siku kama yakujeruhiwa,kualibiwa mali na akapata baati ya mualiko hawez kataa maana ni fulsa kwakweli
 
Lakin pia nadhan mtoa maada ndani ya moyo wako unajua kwani watu flan wakiitwa watakaaa na unajua kwanini watu wengine wataenda na bilashaka ata majibu watakayo yatoa yapo waz mf mt anaetumikia gvm lazima awe na majibu yakulinda ugali au cheo na mt ambae hayupo kwenye mfumo lazima tu atasema uko kwenye gvm ndio kulikua 7bu
 
Shida sio kwenda tatizo linaanzia pale ambapo watu wa taifa hili wamezoea kufanya vitu kisiasa zaidi

Tume kibao zimeundwa zimeshauri mengi na hatujaona lililofanyika

Nyingne ziliishia kuundwa zikatokomea huko na uchunguzi wake

Kwahiyo kwa ufupi uhuni wa wanasiasa unapoteza uharali wa hii Tume , kwasababu zipo Tume kama Ile ya kuchunguza uunguaji wa jengo la soko la kariakoo, Time ya kuchunguza kifo Cha mzee kibao, Tume ya haki jinai nk hatujawahi kuona matokeo yake chanya
 
Wito unapokeleka okt 29 imeshatokea hatuwezi rudi nyuma bali tunaweza angalia tunaenda vipi mbele.

Je serikali inachapa kazi? Inautamaduni wa kutafuta suluhisho la matatizo kadha wa kadha?

Je huko maofisini wananchi wanasikilizwa na kupewa majibu/utatuzi?

chama cha ccm ni heri kiendelee kung'ang'ania madaraka ila wachape kazi hata kama ni kwa kutumia mawazo ya wengine. Ila sio kazi hakuna na kuachia hakuna

Waepuke funikafunika ambayo ndo tunaona kila jambo hata litangazwe leo ni lszima kesho lihitaji ufafanuzi , sasa jana mlitoa taarifa isiyoeleweka kwa maana gani?
 
Wazee wenye tabia za kishoga kama wewe wanao endekeza njaa ndiyo wamefanya taifa lifikie hapa.

Pumbavu zako wewe, tume ya mchongo na aliyeiteua.
 
Binafsi ninashauri wanaopata fursa ya kuitwa mbele ya tume wasiitupe hiyo fursa,
Waende na ikiwezekana waueke ushahidi walioutoa hadharani nini waliwasilisha mbele ya tume
🙏
 
Aliyeunda tume ndiye muhusika mkuu wa kike kilichotokea.

Yaliyotokea October wanayachukulia kama "Matukio" lakini ukweli ni kuwa yake yalikuwa ni "matokeo" .

Ukiitikisa soda kisha ukafungua kwa nguvu lazima ilipuke. Kabla ya uchaguzi kulikuwa na mtikisiko mkubwa sana. October majibu yakapatikana.

Tume haina uhalali wa kuhoji maana Lila kilichotokea kinamrudia aliyeiunda.
 
Binafsi ninashauri wanaopata fursa ya kuitwa mbele ya tume wasiitupe hiyo fursa,
Waende na ikiwezekana waueke ushahidi walioutoa hadharani nini waliwasilisha mbele ya tume
🙏
Kwanza tatizo linaanza matukio yote ya October wao hawaya-adress kama maandamano ila wanaita "Fujo"

Sasa imagine mtu unaenda kutoa ushahidi wa matukio ya "fujo" yaliyopeleka "Uhabibifu wa Mali" na si vifo vya watanzania .

Sasa kwa muktadha huo, Baada ya kuweka ushahidi una-guarantee vipi usalama wa maisha yao kwenye nchi iliyooza kama hii?

Tetesi zinasema Kila aliyehusika kufanikisha swala la maandamano,iwe kweli au si kweli,ukishapointiwa kidole tu kwamba yule alihusika hakuna cha "msalie Mtume" wanakuzima kama taa.

Tetesi zikaenda mbali zaidi na kusema yule jamaa wa Arusha banjoo aliyetekwa mbele ya camera mbele ya majengo ya serikali aliuawa kwa sababu ilionekana alikuwa mmoja wa waliohamasisha vijana wadai haki na hatimaye kuandamana.

Na kwa Tanzania hii ya sasa ilipofikia,tetesi kama hizi siyo za kuzipuuzia.

Na siyo yeye tu,Kila anayeonekana amesababisha hayo kutokea anapotezwa kimya kimya. Sasa mpaka hapo Kuna muhimu Gani wa hiyo tume ya uchunguzi?

Ukiingia kichwa kichwa juu ya haya mambo utavagaa transfoma uungue. Hii nchi ishakuwa siyo!!
 
shikamoo mwalimu Pascal Mayalla

My friends, ladies and gentleman,
pamoja na kwamba wananchi wengi tayari sana wamekwishajitokeza na kujieleza mbele ya tume maalumu ya kuchunguza kinachoelezwa kutokea october2025, bado imedhihirika wazi kwamba wapo waTanzania wengi zaidi wameomba na wanapendelea kupata nafasi ya kueleza wanachokijua kuhusu october2025 mbele ya tume hiyo huru na maalumu ya uchunguzi.
Ni wazi kwamba,
matamanio na kiu ya wananchi kuitwa mbele ya tume ya uchunguzi ni mengi na makubwa mno ukilinganisha na muda ulioko mbele ya tume.

Hata hivyo,
ni hiyari ya mwananchi mwenyewe kukubali au kukataa wito wa tume huru na maalumu ya uchunguzi, lakini pia vilevile hakuna mwananchi yeyote atakaelazimishwa kutoa ushirikiano kwa tume hiyo maalumu, hata kama anatajwa na waliotoa ushirikiano kua sehemu ya kinachoelezwa kutokea october2025, ispokua kwa mujibu wa sheria na kwa wakati muafaka tu.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom