Wanabodi,
Hii ni mada ya Thinking Aloud Kwa Maslahi ya Taifa, kukuomba ushirikiano wako kwa ushirikishwaji, kutoa maoni yako na mawazo yako kumshauri mwana jf mwenzenu, ikitokea ni wewe umeitwa kufika mbele ya Tume ya Jaji Chande, Je Utatoa Ushirikiano?, Na Ukifika Mbele ya Tume, Utoe Hoja Gani zenye Maslahi kwa taifa?.
Sisi JF tuna members wa aina tatu kuu wa jf.
1. Active members, ambao wanachangia na kushiriki mijadala, miongoni mwao, wako baadhi yao kwao jf is a serious thing, wanashiri mijadala very objectively kwa kutoa hoja zenye maslahi kwa taifa. Wako members kwao jf ni just a favourite pasttime, wakipata muda dio wanaingia, wengi huishia kusoma tuu bila kuchangia, na kuna wengine, kwao jf, ni kama kijiweni kwao, kutwa kucha ni kutukana, kulalamika na badała ya mujibu hoja kwa hoja, nao wanajibu hoja kwa viroja.
2. Kuna Inactive members humu, majina yao yapo lakini hawako active, wako dormant ila kwenye platforms nyingine nyingine wapo na tunawasoma.
3. Kuna wasomaji wa jf, ambapo hawa ndio wengi, wanaingia kama guest, kazi yao ni kusoma tuu, hawachangii chochote, miongoni mwa hawa guests, wapo pia viongozi wengi tuu wakiwemo viongozi wakuu!, mimi ninaushahidii, wa kiongozi mmoja mkubwa tuu, anaingia jf usiku. Kuna usiku mmoja, nilipandisha bandiko fulani humu jf, kuhusu issue fulani, kesho yake huyo Kiongozi Mkuu, akiwa mubashara, alijibu hoja za JF na kutekeleza ushauri wa jf, tangu hapo jamaa humu wakaanza kuniogopa kwa kudhania mimi ni wale majamaa zetu, haiwezekani ushauri jambo leo, kesho litekelezwe!,
Thinking Aloud: Hongera JF kulisaidia Taifa, "Atakuwa anaingia JF in person na kutusoma!". 2021 let's be more responsible, more strategic
Hata huyu aliyepo sasa, alikiri kuwa huwa anaingia jf na kutusoma ila yeye huwa anaishia kucheka tuu!, huo ndio uwezo wake, kuona vile vya kumchekesha tuu, yale maushauri ya kumwaga humu, huwa, hayaoni!, angeyaona, akachukua hatua, kile kilichotokea October 29 wala kisingetokea.
Kuna watu wamekuwa wakiitwa mbele ya Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya October, 29, inayoongozwa na Jaji Chande, baadhi hukubali na kutoa ushirikiano, baadhi hukataa na kutoa sababu za kukataa huo wito au kutotoa ushirikiano.
Mada hii ya "thinking aloud Kwa Maslahi ya Taifa" ambayo ni moja ya mada zangu za abstracts za hypothetical situations, kumaanisha ni mada ya kufikirika tu lakini inafikirisha, na sio lazima hiki kitu kiwe ni kweli, au ni sisi JF tumekisababisha, lakini likitokea jambo likasemwa humu, likajadiliwa, kisha vyombo vya maamuzi vikatoa maagizo au kufikia maamuzi kuhusu jambo hilo kwa jinsi ile ile lilivyojadiliwa humu JF, kama zilivyo baadhi ya zile mada zangu za "the voices from within", ambazo japo nyingine huwa hazitokei, lakini nyingine ni za kweli hutokea kweli!, sasa zinapotokea kweli, hata kama the cause sio sisi, lakini kama tumepigia kelele jambo fulani, tukashauri na kisha hatua zikachukuliwa, tuna haki kabisa ya kujipongeza kuwa tulichangia!.
Kwenye mada hii, the hiypothetical situation, ni suppose wewe ni mwana jf, na umepokea mwito wa kufika mbele ya Tume ya Jaji Chande. Wewe kama mwana jf, utamshauri nini mwana jf huyu?.
1, Je Aitike Wito na kutoa ushirikiano na Tume kwa kufika mbele ya Tume?.
Akifika mbele ya Tume, tumchangie mawazo akatoe hoja gani zenye mashiko?
2. Agomee huo mwaliko, asuse na kukataa kutoa ushirikiano.
Akiamua kususa, je atoe sababu gani za kususa kutoa ushirikiano kwa Tume, kama wengi waliosusa na kutoa sababu zao za kususa?.
Naomba maoni yako!.
Natanguliza Shukrani kwa Ushirikiano wako.
Ubarikiwe sana!
Paskali.