The state: Hakikisheni kwenye Katiba Mpya, mishahara na posho za kwenye siasa zinapunguzwa Sana na kuelekezwa kwenye miradi ya umma

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,525
17,434
Wakuu

Binafsi sielewi ni nani HASA alieamua kuwa kazi ya siasa ndio iwe na malipo na posho kubwa sana kuliko taaluma nyingine yeyote hapa nchini.

Wataalamu wa taaluma mbali mbali wameacha kada zao na kukimbilia siasa kuliko kujikita kwenye taaluma zao na kutuhudumia wananchi!

maprofesa wa vyuo, madaktari, mainjinia na n.k wamekimbilia kwenye siasa HASA ubunge ILI kufata malipo makubwa kuliko kutuhudumia jamii.

Siasa imezalisha rushwa, uchawa, mauaji, ulozi, migogoro hata umafia kutokana na malipo makubwa yaliyopo siasani.

Ipo haja ya kupunguza malipo na posho hizo kuwa za kawaida kama taaluma nyingine nchini na hiyo iwe kikatiba kabisa kuliko sasa mambo yalivyo.

Kuna familia zimeacha kujikita kwenye taaluma zenye tija KWA jamii na kukimbilia siasa tu na vyeo vya serikali na kusababisha u Mungu mtu KATIKA NCHI yetu!piga chini malipo makubwa ya siasa ILI watu wajikite kwenye taaluma na shughuli za kiuchumi kuliko Sasa mambo yalivyo.

Jaribuni kuifikiria Tanzania ninayo zungumzia hapa muone Namna ambavyo mtakuwa mmetatua Matatizo makubwa Sana yaliyopo!

Angalau mishahara na posho za wanasiasa Bungeni ziwe sawa na madaktari, Walimu, wanasheria, maafisa kilimo na mifugo na wengineo tena kawaida Sana posho isizidi 50000/= na mishahara isizidi MILIONI tatu tu kwa wote.

Tuepuke ubadhirifu unaoendelea na Vifo kibao vinavyotokea wakati wa chaguzi kwasababu ya migogoro ya kusaka vyeo vya siasa na kuifanya siasa iwe kazi ya kawaida Sana.

Someni, tafakarini na mfanyie kazi Haya kwa mstakabali wa Tanzania ijayo.

Asanteni kwa kusoma
 
wanasiasa wote ni sawa na vidole vya mkono linapokuja suala la ulaji, vidole vyote hushirikiana ili kufanikisha ulaji. Nakuhakikishia hakuna mwanasiasa atakayekubaliana na hilo. wote wataungana kutokukubaliana na hilo, bila kujali tofauti zao.
Bahati mbaya wao mdio waamuzi.
 
wanasiasa wote ni sawa na vidole vya mkono linapokuja suala la ulaji, vidole vyote hushirikiana ili kufanikisha ulaji. Nakuhakikishia hakuna mwanasiasa atakayekubaliana na hilo. wote wataungana kutokukubaliana na hilo, bila kujali tofauti zao.
Bahati mbaya wao mdio waamuzi.
Ndio maana nimewaomba wale jamaa !!si wajui japo naamini wao wapo loyal KWA Taifa letu!!wafanye jambo!!!siasa imeumiza WENGI SANA!!!
Wafanye jambo lao!!!
 
Back
Top Bottom