Kuhusu Katiba Mpya na Kisa cha fisi kuufuata mkono wa binadamu akitumaini utaanguka. Upinzani mna malengo gani?

busar

JF-Expert Member
Dec 22, 2011
1,068
1,061
Asalam,

Kwanza naomba nikiri kuwa pamoja na kupenda sana siasa za kimabadiliko na kimapinduzi lakini pia ni realist. Realist kwa kawaida ni aina ya watu wanaouona klukweli kama ulivyo na unaamini tabia za mwanadamu zilizowahi kujionesha siku za nyuma na hamu ya kila mmoja kupata zaidi.

Suala la katiba sio suala dogo kwa CCM na Pia sio suala dogo kwa Upinzani. Katiba MPYA inamaanisha kifo kwa CCM na Kuingia Ikulu kwa Upinzani. Sasa hapa kwenye kuwa Realistic ni hivi, CCM HAWATAKUBALI KUACHIA MADARAKA WALAU KWA KIPINDI KIREFU KIJACHO.

CCM Wamejifunza kwa KANU, UNIP, na Almanusura ZANU PF wakati ule. Wametengeneza mifumo ya kuwafanya washinde, wameijaribu na kwa kiasi kikubwa umefanya kazi. Jaribio kubwa la aina yake kama kurusha kombora lilikuwa uchaguzi wa 2020. Pale kura zilipozidi hata idadi ya walioniandikisha, kama Kawe na Kahama. Kama kawaida, kwa sauti zile zile akina CHADEMA wakarudi zizini.

Ccm wameanza kujiandaa, Mzee kinana kaingia kazini, amekuwa msimamizi wa Chaguzi hizi za vyma vingi toka 1995 kutokea CCM. HUWA AKIWAPIGA WAPINZANI ANAKUJA KUIBUKIA TCD na Kukiri kuwa Uchaguzi ulivurundwa, na ghafla akina Lema, Zito, na Wengine wanajitokeza kumsifu. Huwa ni kama picha flan la kihindi.

Sasa, Mwinyi kule Zenji, Mama huku Bara kwa sehemu kubwa wameshapanga safu za Tume. Na mikakati imeanza, hii ni 2023, mwakani Uchaguzi wa Mitaa. Realists tunajua CCM ataibuka kinara kwa namna yoyote, atatangazwa mshindi. Realists tunajua hivyo.

Upinzani tunajua kwa sasa mnahamu na maisha ya mjengoni. Imeshakubaliwa mtapewa Viti kadhaa.

Ushauri wa realists kwa WAPINZANI
1. Achaneni na agenda ya katiba mpya. Wananchi wengi huko vijijini hawelewi uhusiano wake na maisha yao. Jielekezeni kwenye kuifanya waichukie ccm based on changamoto za eneo husika ( local politics)

2. Kwa kuwa CCM haitakubali suala la katiba mpya, nakubaliana na busara ya Mwenyekiti Mbowe kuwa CHADEMA sasa Chama Cha Ushauri Cha CCM (BASED ON MAKUBALIANO YA SIRI ALIYOFANYA NA CCM). Hili linafaida sana kwa kuwa litasaidia CCM Kufanya yale ambayo CHADEMA inatamani lkn bila wao kushika madaraka. Huu utakuwa ni Uzalendo wa Hali ya juu sana.

3. Vijana wa CHADEMA sasa wajisogeze jirani na vyombo muhimu kwa kusaidia amani ya Taifa hili. Hii itapunguza wao kukamatwa kamatwa na kuhangaishwa bila sababu.

4. CHADEMA kuomba walau nafasi mbili za Uwaziri. Mfano ipewe uwaziri wa Jinsia na Uwaziri wa masuala ya Mazingira. Hapo inawezekana na tutakuwa na taifa bora sana.

Mwisho, narudia iwe iwavyo katiba mpya Tz ni ndoto, hata Mama hana misuli ya kulifanya hilo, hana na hawezi kulijaribu.

Asanteni
 
Back
Top Bottom