..wakubwa!
Mimi ni mgeni kabisaa! na sibingwa wa uandishi maana nina mwezi tangu nitoke kijijini kwetu, lakini kitu kilichonishangaza, ni ule usemi wa Jogoo wa shamba hawiki mjini...ninavyokumbuka yule jogoo niliyekuja naye kama zawadi aliwika tena saa mbili usiku baada ya kuona ule mwanga wa umeme..sijui alijua kumekucha ama vipi...lakini nataka kusema Ukweli jogoo wa shamba huwika mjini pia...
Napenda nikueleze Dada'angu kuwa haya mambo ya % (fulani alipata asilimia ngapi..na fulani ngapi ni mazuri kwenu ninyi mnaojua kutofautisha kati ya Phillips TV na Phillips Computer..huku kwetu sisi TV na Computer zote ni TV..remote ya Radio aina ya Sumsung na Mobile ya Sumsung kwetu zote ni simu za mkononi. Kama mimi nasema uongo naomba Mzee mwanakijiji akuelezee! maana anaifahamu hali yetu hapa kijijini..mfano zaidi ni hiyo T-shirt yake aliyoivaa ndiyo maisha yetu yalivyo.
Sasa kama tutaletewa hizo kofia na t-shirt na kanga tutaacha kuwapigia kura mafisadi?..maana hamtaki kuja kutuelimisha huku kijiini kwetu, mnang'ang'ana na %!!!! shauri yetu..tutachelewa kufikia lengo
Huku kwetu pia mtu akipanda ndege Swiss Air, Emirates, Gulf Air na nyinginezo, tunajua ameenda Ulaya..iwea kaenda Asia ama America, Africa Kusini .. tunasema kaenda Ulaya tu, hatujatofautisha kati ya Ulaya, Asia na Marekani..zote ni Ulaya!
Sasa kitu ambacho nataka kuwaeleza Maswahiba zangu wa TLP, CUF, CHADEMA, NCCR na Wengineo wenye Mapenzi Mema na Nchi hii..tuacheni kubishania asilimia zinatupotezea muda!!! Asha!! tutumie POINT yako ..ya KUANDAA MAZINGIRA MAZURI MAPEMA KABLA YA 2010 IKIWEMO KUJENGA MTANDAO WA VYAMA VYA SIASA WASHIRIKA NCHI NZIMA...nadhani hapo ndiyo uwezo wangu wakufikiri umeishia hapa, ilikuweza kuushinda Ufisadi.
.... Sasa Mbowe, Dr Slaa na wengine kama wanataka kugombea uchaguzi 2010 wataanza kuaandaa mazingira mapema kabla ya 2010 ikiwemo kujenga mtandao wa chama nchi nzima.
Asha
..Mwisho; sijisikii vyema kuviita vyama vyetu vitukufu vya siasa kuwa Vyama vya Upinzani..naona kama tunawajengea kapepo kadogo hawa akina SiSi-eM; kwanini wao wasiitwe kwa domain hiyo hiyo ya Chama Cha Upinzani Cha CCM? si wanapinzana na wenzao wa vyama vingine?...Kazi kwako Mch. Kishoka!ila nakupa onyo ukienda A-town/City usitumie jina hilo la Kishoka, maana kama utapita karibu na Ofisi za Tanesco unaweza kupata matatizo..
Mkitaka Kuja Kijijini nitumieni barua C/O.Mwl. Mkuu, Shule ya Msingi...., ambaye atampa Katibu Kata, kwani yeye anafahamiana na Mjomba'angu ambaye ni Mjumbe wa Shina, ili nije niwapokee...kisha niwapeleke nikawatafsirie kwa wanavijiji kama mtaenda wenyewe wanavijiji watabakia kushangaa hizo nywele zenu mlizo tia dawa ama kusuka rasta na suruari za kubana kwa wanawake..hivyo hawatawasikiliza zaidi ya kuwashangaa!
Massege Send!