The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Jamaa kumbe ni padre na ndiyo maana ni mpole na si mfisadi

International Eye H. Centre Certificate in Eye Health 1993 1993 CERTIFICATE
TransWorld Tutorial College, London Certificate in Management 1985 1985 CERTIFICATE
St. Thomas Aquinas University Advanced Diploma in Rural Development 1980 1981 ADV DIPLOMA
St. Urban University, Rome PhD (JCD) Law 1977 1981 PHD
Kipalapala Seminary Certificate in Theology 1974 1977 CERTIFICATE
Kibosho Seminary School Certificate in Philosophy 1972 1973 CERTIFICATE
Itaga Seminary School A-Level Education 1970 1971 HIGH SCHOOL
Dung'unyi Seminary School O-Level Education 1966 1969 SECONDARY
Karatu Primary School Primary Education 1962 1965 PRIMARY
Daudi Primary School Primary Education 1961 1961 PRIMARY
Kwermusl Primary School(Mbulu) Primary Education 1958 1960 PRIMARY

--------------------------------------------------------------------------------
CERTIFICATIONS
Certification Name or Type Certification No. Issued Expires
No items on list

--------------------------------------------------------------------------------
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
Tanzania Society for Blind Managing Director 1992 1998
Tanzania Episcopal Conference Secretary General 1985 1991
Diocese of Mbulu Development Director 1982 1985
Diocese of Mbulu Vicar General 1982 1985
Diocese of Mbulu Development Director 1977 1979
Diocese of Mbulu - Roman Catholic Church Padre 1977 1991

--------------------------------------------------------------------------------
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
CHADEMA Secretary General 2002
CHADEMA Vice Chairman 1998 2002
CHADEMA Member of Parliament (Karatu Constituency) 1995 Todate
CHADEMA Member of National Executive Committee 1995 -
Chama Cha Mapinduzi - CCM Secretary Foreign Branch(Rome) 1980 1982
Youth Union -TANU Secretary 1974 1977
TANU Chairman (Kipalapala Branch) 1974 1977
 
nadhani makosa tuliyoyafanya kwa Kikwete kwa kuchanganya umaarufu na uwezo wa uongozi yanatugharimu sana, watanzania.

Tanzania tunatakiwa tuombe Mungu atusaidie kutoka kwenye hili shimo kwanza. Hii habari ya kukurupuka itatupeleka Zimbabwe na Kenya na Congo na sehemu zingine ambazo tumeshuhudia mambo ya ajabu.

Tofauti pekee ni kwamba wenzetu wanaweza kuingia kwenye matatizo na kisha kutoka, watanzania kamwe hatutaweza kutoka kwenye matatizo kama tukiingia. Salama yetu ni kukwepa matatizo.
 
Tatizo letu sie wanachama na viongozi wa nyama vya siasa hatukubali kukosolewa bali tunapenda na kujua sana kukosoa. Kukubali kukosolewa kunasaidia kujua udhaifu na kujua njia mbadala ya katika kujiimarisha.

Post tatu tu, ya kwanza ndio hii. Eti Kubwa Jinga Jinga umeamua kuingia kwa jina lingine la mwanachama wa upinzani kuhalalisha hoja zako na kujipongeza?

Asha
 
Murra,

Uwezo wa kifendha wa Chadema ni mdogo sana na kama hizo kidogo zilizopo zikitumiwa vibaya kwenye uraisi, uwezo wa Chadema kushindana na CCM unapungua, na sio ajabu wakapoteza viti kama ilivyokuwa kwa Dr. Kaborou.

Dr Kaburu hakushindwa kwa kuwa CHADEMA ilitumia fedha vibaya kwenye urais. Kama sababu ingekuwa hiyo CHADEMA ingeshindwa na kampeni za udiwani kule Kigoma ambazo ni za chini zaidi. Mbona CHADEMA imeishinda CCM pale Kigoma ujiji na mpaka sasa ndio chama tawala pale katika ngazi ya halmashauri? Kwa hiyo hoja yako ni ya upofu wa mawazo

Asha
 
International Eye H. Centre Certificate in Eye Health 1993 1993 CERTIFICATE
TransWorld Tutorial College, London Certificate in Management 1985 1985 CERTIFICATE
St. Thomas Aquinas University Advanced Diploma in Rural Development 1980 1981 ADV DIPLOMA
St. Urban University, Rome PhD (JCD) Law 1977 1981 PHD
Kipalapala Seminary Certificate in Theology 1974 1977 CERTIFICATE
Kibosho Seminary School Certificate in Philosophy 1972 1973 CERTIFICATE
Itaga Seminary School A-Level Education 1970 1971 HIGH SCHOOL
Dung'unyi Seminary School O-Level Education 1966 1969 SECONDARY
Karatu Primary School Primary Education 1962 1965 PRIMARY
Daudi Primary School Primary Education 1961 1961 PRIMARY
Kwermusl Primary School(Mbulu) Primary Education 1958 1960 PRIMARY

--------------------------------------------------------------------------------
CERTIFICATIONS
Certification Name or Type Certification No. Issued Expires
No items on list

--------------------------------------------------------------------------------
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
Tanzania Society for Blind Managing Director 1992 1998
Tanzania Episcopal Conference Secretary General 1985 1991
Diocese of Mbulu Development Director 1982 1985
Diocese of Mbulu Vicar General 1982 1985
Diocese of Mbulu Development Director 1977 1979
Diocese of Mbulu - Roman Catholic Church Padre 1977 1991

--------------------------------------------------------------------------------
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
CHADEMA Secretary General 2002
CHADEMA Vice Chairman 1998 2002
CHADEMA Member of Parliament (Karatu Constituency) 1995 Todate
CHADEMA Member of National Executive Committee 1995 -
Chama Cha Mapinduzi - CCM Secretary Foreign Branch(Rome) 1980 1982
Youth Union -TANU Secretary 1974 1977
TANU Chairman (Kipalapala Branch) 1974 1977

Ahsante mkuu, CV inaonekana kuwa ni nzito maana sijui kama CV ya Kawawa aliyewahi kuwa waziri wetu mkuu inaweza fikia hii,

wakuu ninaomba kusema hivi msiongelee Tanzania kama Ulaya, Tanzania ni Tanzania, mambo yetu bado ni yale yale ya pole pole huwezi kujua uwezo wako on anything bila ya kujaribu, na kuhsindwa na kawaida katika mchezo wowote ule, wakali wa siasa hawahitaji kuingia bungeni kuonyesha ukali wao, kwa sababu ni wakali ukali wao huo upo hata wakiwa nje ya bunge, sasa hakuna tatizo lolote kwa Dr. Slaa kugombea urais, agombee ili aweze kuchomeka agenda nzito kwa taifa kwenye malumbano ya uchaguzi na ninaamini kuwa anyo nafasi kubwa ya kushinda, na hata akishindwa yeye ni mkali tu ataendeleza ukali hata akiwa pembeni, lakini kutojaribu kabisa eti kwa kuogopa CCM kuwa ni imara zaidi ni mawazo ya Mwalimu hayo yamepitwa na wakati!
 
Amesahau kuweka Master degree yake hapo, au ndio imejumlishwa na PhD humohumo?
 
Mimi nausongo na suala la flamingo wa L.Natron ambalo nasikia liko jimboni mwake! Kama ni hivyo, mbona amekuwa bubu?
 
Mimi nausongo na suala la flamingo wa L.Natron ambalo nasikia liko jimboni mwake! Kama ni hivyo, mbona amekuwa bubu?

nadhani yeye na mafisadi tu! si lazima afanye kila kitu jamani mwee. Hivi hii kitu inaitwa NEMC kazi yake ni nini?imeshindwa kusimamia haya mazingira?
 
Kalamu,
  1. Hapajawahi kuwepo kiongozi mwenye hizo sifa ulizozitaja kwenye upinzani kama Mrema. Mpaka wasomi wa UDSM walimkubali awe kiongozi wao, matokeo - akapigwa chini.
  2. Kama unafikiria wapinzani wana muda, basi ngoja waendelee kusubiri mpaka 2010 ndio waanze kujipanga, hala tutasikia matokeo.
  3. Mimi sipingi yeyote yule kujitokeza, ninachopinga ni kuwatoa kafara mtu kama Dr.Slaa, wakati vyama vyenyewe havijajiweka sawa.
Tunaweza tukaongelea mifano ya nchi hata 30, labda kwa vile tunaipenda, lakini hakuna hata mmoja ambao utatusaidia either kujenga upinzani wa dhati au kuiondoa CCM madarakani. Vyama kujisafisha na kuwa na maandalizi yanayofaa ndio solution peke yake.

Kubwajinga:

Unataka tuamini hapa kuwa "umegundua tairi?"

This is no brainer!

Ni nani unataka aviweke vyama sawa kama sio hao viongozi imara unaowapinga wewe - eti wanatolewa kafara!

Yote haya yanafahamika na yalishazungumziwa hapa JF mara dufu; na hao wapinzani wanayajua vyema. Tatizo ni lile lile unaloling'ang'ania wewe - pasiwepo na viongozi kama akina Dr. Slaa, wenye uwezo wa kuhimiza na kusimamia hayo maandalizi kwa wakati muafaka kabla ya uchaguzi unaofuata.
 
Invisible,
Slaa ni kichwa kuwa president 2010 lakini tatizo timu atakayounda kumsaidia inaweza kuwa na vicheche watupu kiasi kwamba na yeye tukamuona kama JK. Muhimu hapa abaki humu humo bungeni na aendelee kufumua uozo anaouna na wenzake vinginevyo mzee tutampoteza katika ramani...Si unaju Freman Mbowe alipokuwa Mbunge alikuwa moto kuja kutia timu kwenye u-president maji ya shingo anaweza na yeye kupotea kama mzee wa kiraracha (Lyatonga Mrema) ni choka mbaya bwa shee!!
 
I dont mind kuwa na rais kutoka upinzani ila tatizo ni kumtoa CCM! kwanza tuimegue megue then ndio tumtafute mtu kama Slaa aingie....so far, not bad ! I am sure kwa haya yanayoendelea ndani ya CCM, matajiri wakina Rostam soon watakuwa upande wa upinzani; ila this time ndani ya CCM! i mean, watapigana wenyewe kwa wenywewe mpaka wasambaratike! Ishallah!kwa kweli, tunataka mabadiliko na kwa uzoefu huu wa mkapa na kikwete, umetufundisha kwamba kubadilisha rais hakutoshi, inatubidi kukibadilisha chama. hata kama hakuna chenye nguvu kwa sasa ila wakiungana watakuwa na nguvu na kwa mwendo huu wa CCM i am sure hata wakina Slaa wakishirikiana na vyama visivyo na usajiri kama JF, tunamatumaini INAWEZEKANA!!
 
Invisible,
Slaa ni kichwa kuwa president 2010 lakini tatizo timu atakayounda kumsaidia inaweza kuwa na vicheche watupu kiasi kwamba na yeye tukamuona kama JK. Muhimu hapa abaki humu humo bungeni na aendelee kufumua uozo anaouna na wenzake vinginevyo mzee tutampoteza katika ramani.

Si unaju Freman Mbowe alipokuwa Mbunge alikuwa moto kuja kutia timu kwenye u-president maji ya shingo anaweza na yeye kupotea kama mzee wa kiraracha (Lyatonga Mrema) ni choka mbaya bwa shee!!

Kwa hiyo hapa unachojaribu kusema ni kwamba nchi iendelee kuongozwa na watu kama kina Kikwete, kwa hili sikubaliani nawe kabisa kwa sababu I can't stand even a month of Kikwete Presidency.

Nchini mwetu na nchi nyingi za kiafrika Rais ana madaraka makubwa sana kiasi kwamba ni muhimu kufanywa kila aina ya mikakati kuhakikisha urais unakwenda kwa wapinzani, mikakati hiyo iendane pia na mpango thabiti kuhakikisha idadi ya wabunge wa upinzania wanaongezeka.

Ni Mgombea wa Urais imara na anayekubalika na wengi ndio atawezesha hata wapinzani kupata viti vingi vya ubunge, kwa hilo naamini kabisa Dr. Wilbroad Slaa ndio mtu anayefaa kuongoza mapambano dhidi ya CCM.
 
Kwa hiyo hapa unachojaribu kusema ni kwamba nchi iendelee kuongozwa na watu kama kina Kikwete, kwa hili sikubaliani nawe kabisa kwa sababu I can't stand even a month of Kikwete Presidency. Nchini mwetu na nchi nyingi za kiafrika Rais ana madaraka makubwa sana kiasi kwamba ni muhimu kufanywa kila aina ya mikakati kuhakikisha urais unakwenda kwa wapinzani, mikakati hiyo iendane pia na mpango thabiti kuhakikisha idadi ya wabunge wa upinzania wanaongezeka. Ni Mgombea wa Urais imara na anayekubalika na wengi ndio atawezesha hata wapinzani kupata viti vingi vya ubunge, kwa hilo naamini kabisa Dr. Wilbroad Slaa ndio mtu anayefaa kuongoza mapambano dhidi ya CCM.

Mazee GQ,

Kuna watu wana mawazo kuwa hakuna yeyote anayeweza kuongoza nchi isipokuwa ccm peke yao. Wanaweza kushauri kuwa hata wabunge wote na madiwani watoke upinzani lakini presidente atoke ccm.

So far sijaona argument why wanafikiria hivyo!
 
Ni kweli kabisa mwafrika wa kike yaani inashangaza sana, unajua kuna watu bado wanaamini CCM ndio mtatuzi pekee wa matatizo ya Tanzania, hawa watu hata waone majambazi wa CCM wanafanya ufisadi kupita kiasi bado wataendelea kuamini CCM ndio Chama pekee kinachofaa kuongoza.

Nashindwa kuelewa kama wamepumbazwa na siasa za ujamaa na kujitegemea ambazo siku zote zinamlazimisha mfuasi wa chama kutii, kuzifuata na kuzidumisha fikra za mwenyekiti hata kama fikra hizo ni za kijinga, potofu, chafu, goigoi na zilikosa busara.
 
Ni kweli kabisa mwafrika wa kike yaani inashangaza sana, unajua kuna watu bado wanaamini CCM ndio mtatuzi pekee wa matatizo ya Tanzania, hawa watu hata waone majambazi wa CCM wanafanya ufisadi kupita kiasi bado wataendelea kuamini CCM ndio Chama pekee kinachofaa kuongoza. Nashindwa kuelewa kama wamepumbazwa na siasa za ujamaa na kujitegemea ambazo siku zote zinamlazimisha mfuasi wa chama kutii, kuzifuata na kuzidumisha fikra za mwenyekiti hata kama fikra hizo ni za kijinga, potofu, chafu, goigoi na zilikosa busara.

Taratibu tu media inafunguka na watu wameanza kuona kile ambacho walifichwa wakati wa serikali ya Mkapa. Mkapa alikandamiza media na upinzani to the point ambayo watu hawakuweza kupumua hata kidogo.

Serikali yake ilifanya kila inachoweza kumaliza wapinzania kisheria na kijasusi kwa kufuatilia hadi mabalozi wa vyama vya upinzani kule kijijini njaainaumasana. Mwanzoni Kikwete kwa kupitia Makamba walijaribu hili pia ila wakagundua kuwa watu wamechoka na wameamua kuacha mambo yafunguke taratibu.

Muda si mrefu kila mtu atajua kinachoendelea na itakuwa suala la kufa na kupona wakati wa uchaguzi. Kile kipigo walichopigwa wana Chadema kule kiteto sidhani kama ccm watakirudia tena mwaka 2010 unless kama wanataka nchi nzima iwake moto.
 
Kauli kwamba eti Dr. Slaa asigombee urais ila agombee ubunge ndiko anaweza kuwa more effective, ni kauli weak sana kama sio empty kabisaaa, kwa sababu kuwa effective Slaa sio lazima awe bungeni, Mhatma Ghandi, hakuwa kwenye bunge lolote na wote tunajua kuwa Mandela alikuwa more effective akiwa jela, kuliko hata alipotoka nje,

Slaa agombee urais kama inawezekana, kwangu itatusaidia sana CCM kuja na strong candidate knowing kwamba tukiweka goi goi ataondolewa, na pia itatusaidia CCM kujisafisha na ufisadi!
 
Mazee GQ,

Kuna watu wana mawazo kuwa hakuna yeyote anayeweza kuongoza nchi isipokuwa ccm peke yao. Wanaweza kushauri kuwa hata wabunge wote na madiwani watoke upinzani lakini presidente atoke ccm.

So far sijaona argument why wanafikiria hivyo!

Ize....wenyewe watakwambia CCM ilianzishwa na baba wa taifa aliyekuwa na fikra sahihi. Watakwambia CCM ina dira na mwelekeo madhubuti na blah blah nyingine kibao.

I just don't buy that kind of B.S. Mimi nawalaumu wananchi wanaoendelea kudanganywa na wenyewe kudanganyika kuwa CCM ni madhubuti. Hakuna lolote zaidi ya maneno meeeeeengi na matendo sifuri. Kwa mtu yeyote mwerevu mwenye kuweka maslahi ya taifa mbele hawezi hata kidogo kuwapigia kura CCM.

Moja ya maadui waliotangazwa baada ya uhuru alikuwa ni ujinga. Adui huyu bado yupo na tusipoangalia atatumaliza hivi hivi mchana kweupe. Hakika mtu mwenye akili timamu hawezi kuwapigia kura CCM. No way!!
 
Kauli kwamba eti Dr. Slaa asigombee urais ila agombee ubunge ndiko anaweza kuwa more effective, ni kauli weak sana kama sio empty kabisaaa, kwa sababu kuwa effective Slaa sio lazima awe bungeni, Mhatma Ghandi, hakuwa kwenye bunge lolote na wote tunajua kuwa Mandela alikuwa more effective akiwa jela, kuliko hata alipotoka nje,

Slaa agombee urais kama inawezekana, kwangu itatusaidia sana CCM kuja na strong candidate knowing kwamba tukiweka goi goi ataondolewa, na pia itatusaidia CCM kujisafisha na ufisadi!

That's what I am talking about.
Kama CCM wakijua kuwa wapinzani watagombea uraisi basi nao watakuja na mtu strong. Suala la kuacha kugombea uraisi eti kwa sababu zisizoeleweka ni jambo nisiloweza kufikiri kabisa.
 
Ize....wenyewe watakwambia CCM ilianzishwa na baba wa taifa aliyekuwa na fikra sahihi. Watakwambia CCM ina dira na mwelekeo madhubuti na blah blah nyingine kibao. I just don't buy that kind of B.S. Mimi nawalaumu wananchi wanaoendelea kudanganywa na wenyewe kudanganyika kuwa CCM ni madhubuti. Hakuna lolote zaidi ya maneno meeeeeengi na matendo sifuri. Kwa mtu yeyote mwerevu mwenye kuweka maslahi ya taifa mbele hawezi hata kidogo kuwapigia kura CCM. Moja ya maadui waliotangazwa baada ya uhuru alikuwa ni ujinga. Adui huyu bado yupo na tusipoangalia atatumaliza hivi hivi mchana kweupe. Hakika mtu mwenye akili timamu hawezi kuwapigia kura CCM. No way!!

Ngabu, hiki ndicho JF na media makini tanzania zimeanza kufanya hii iwe halisi. Kuwaelemisha wananchi kuwa ni makosa na uzembe kuchagua chama ambacho kinachangia kwa kiwango kikubwa sana kwenye umasikini wa nchi kwa sababu tu ni chama kilichoanzishwa na Nyerere.
 
MwK na Nyani:

Wananchi wamekwishaanza kuacha kuwashabikia Chama cha Mafisadi.
Kwa mfano: Jumla ya wananchi wa Kiteto wenye sifa za kupiga kura, walioshiriki kupiga kura hata nusu haikufikia. Hii ni dalili wazi kuwa wapinzani walikuwa na nafasi nzuri sana ya kuwavutia hao waliogomea CCM ili wawapigie kura. Kazi iliyopo ni hao viongozi imara, wenye kuaminiwa na uwezo wa kuwashawishi wananchi wakubali upinzani.

Tusisahau mawaziri kuzomewa; vyama vya upinzani wachukue fursa hiyo kupigilia msumari wa mwisho katika jeneza la CCM. Ni kazi ngumu, lakini ni kazi inayowezekana sana pakiwepo na viongozi wanaokubalika na wananchi.
 
Back
Top Bottom