Maxence Melo
JF Founder
- Feb 10, 2006
- 4,230
- 13,415
Mkuu kampeni yako inaonekana kuwa nzuri na una dhamira kabisa. Jaribu kuwasiliana na Slaa uone kama analo lengo hilo. Unaweza kumsaidia sana.
By the way, mimi naamini humu humu JF kwa wale ambao tumejisajili na hata wale wasomaji tu wamo wanaotarajia kugombea nafasi flani kisiasa. Tafadhali choteni mawazo ya watanzania hapa na mkayafanyie kazi. Taifa linawahitaji na uzalendo wenu unahitajika sana.
Mkipata kuitumia busara katika kusoma mawazo ya wengi humu mtagundua kuwa system ya sasa imewachosha sana. Hawa wenye bahati ya kuingia mtandaoni ni wachache wa wale wengi wenye vilio vya namna hii. Mkiamua (hata mimi) basi kila kitu kinawezekana.
Ahsante kwa mwanzisha mada na wote mnaoendelea kuchangia. Maoni yangu kwa kifupi yalikuwa hayo. Niko tayari kumuunga mkono yule atakayejitokeza hapa na kuthibitisha dhamira yake ya kugombea aidha Ubunge ama Urais ili mradi kwa kauli yake ama maandishi yake adhihirishe kuwa amedhamiria kufanya yaliyo mema kwa jamii ya watanzania husika ili baadaye tumbane kwa kauli hizo.
Mac