The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Waheshimiwa!
Mtu anaponunua gazeti siyo kwamba anataka kusoma habari zote, wengine Siasa, Uchumi, Nafasi za Kazi, Michezo na wengine Vikatuni ambavo mara nyingi huonekana mwishoni mwa gazeti fahamuni kuwa navyo vinawashabiki wake!

Itabidi niwe nakuja na mada katuni iliwale wataalamu wanaojua kuvisoma ujumbe wake, naamini hao watakuwa wanafaidika navyo.

Baada ya kuifuatilia mada hii kuanzia mwanzo wake mpaka hapa ilipofikia, nimegundua kunawatu wachache sana ambao ni wataalamu wakusoma vijikatuni;

Kumradhi kuwataja majina siyo vyema lakini ni vizuri nikiwataja iliwajitambue wao wana uwezo wa kusoma vikatuni.

1:Mama - huyu anauwezo wa kusoma vikatuni lakini ni mchoyo ama hapendi kuongea sana! Uwezo wake nimeuona kwenye Post 125, Pg 13

2: Kubwa Jinga- Huyu pia anauwezo wa kusoma katuni: Hata mimi kwa mara ya kwanza nilikuwa hata sitaki kusoma post zake nikiamaini ni kubwa jinga; nadhani jina ndilo linamponza mpaka watu wanafikiri hana lolote. Kwa jinsi nilivyomsoma kubwa jinga ni mtu anayevitakia Mema vya Siasa na wala siyo mshirika wa chama chochote cha Siasa, lakini hataki kuwafumbulia watu: Soma Post yake No.154, Uk.16. Mambo yote ameyaweka wazi ilikuviokoa vya vya Siasa, na ameniokolea muda sana maana nilitaka kuzungumzia kitu hicho hicho.

3: Jamco Za - huyu ni mtu mwenye malengo mema na vyama vya Siasa pinzani na SiSi-eM: Post 188;Uk 19, utatambua nia yake njema.

Tuendelee na staili yetu ya Kikatuni-katuni.

KAMA CHADEMA WANATAKA WASHUHUDIE ANGUKO KUBWA LA CHAMA CHAO...wampeleke Mh. Dr. Wilbroad Slaa akachukue FOMU ya KUGOMBEA URAISI.

Nieleweke vyema sina maana kwamba Chadema na vyama vinginevyo wasisimamishe wagombea Urais 2010..Wasimamishe lakini siyo Slaa, Zitto, Kimario..ah kumbe huyu ni wa CCM..lakini siyumo? maana hapa sizungumzii Ushabiki wa Kivyama.

Nataka niwathibitishie Wanavyama Shirika, katika vita vita waliyonayo SiSi-eM ni kumwondoa Slaa na jamii yake Bungeni, halafu ninyi wenyewe mnataka kuwasaidia kumwondoa Bungeni!!!??? Kweli ninyi ni njiti kweli..ah! samahani nimejikuta limenitoka tu haikuwa nia yangu kuwaita hivyo.

KIKATUNI:
Hawa watu mpaka wakaamua kutunga wimbo kupitia Bendi yao zamani TOT sijui leo nasikia inajina jipya ilikuhamasihana jinsi yakuwang'oa Bungeni hao jamaa wenye Siasa Chimbuzi (nadhani niwatumishi wa Umma)

Baadhi ya Mashairi yake yanasema:-

Eh,eh eh, eh!!! kitim-tim,
kitimtim umekiona leo,
Kwenye nyumba ya Starehe kijiko kimeingiaje?
Kwenye nyumba ya Starehe mwendawazimu kaingiaje?
....nakuendelea.....

Wenzenu walishafanya Bungeni ni Sehemu ya Starehe,sasa wakashangaa kuona kunakijiko kimeingia kuwatibulia starehe zao (UFISADI na matendo mengine yafananayo na hayo)- ambayo ndiyo akina Dr. Slaa na wenziwake!Cha ajabu ninyi wenyewe mnataka kuwasaidia kutoa kijiko kwenye nyumba ya starehe:

Naapa: HAKI YA MUNGU TENA VILE! CHADEMA WASIFANYE KOSA LA KUMUONDOA DR. SLAA BUNGENI!! ninaukakika asilimia 90,Siku tu Dr. Slaa atakapochukua FOMU YA KUGOMBEA URAISI kwenye radio vijijini, lazima huu wimbo utapigwa:

Oh! oh! MCHIMBA KISIMA, KATUMBUKIA MWENYEWE!!!!KAINGIAA!!
Nakisha Mkuu wa Kaya atakuwa na safari ya Kiserikali Ulaya..lengo lake itakuwa nikwenda kupumzika baada ya kazi ngumu inayosababishwa na Kijiko!! Asomaye na afahamu.

Tatitito watu wa humu wanapenda Ushahidi,sasa mimi nisiyekuwa nao nitafanya je sasa?

Ngoja nijaribu kupanga kama KJ:
1: Kwa wale walifuatilia kampeni kwa ajili ya Uchaguzi wa '05,Karatu nadhani kwenye bajeti ya SiSi-eM walitumia garama kubwa sana ilikuhakikisha Slaa harudi Bungeni.

2: FAIDA ZA SLAA KUWA BUNGENI - ndipo mahali pekee ambapo Chama Kinajitangaza kwa garama Nafuu kutokana na hoja zitolewazo na mbunge husika.

3: HASARA ZA SLAA KUGOMBEA URAISI- hili liko wazi, na nikubwa saana!,,Sina maana kwamba hafai, ila ukweli hatopata kura stahiliki (50%)ilikuweza kumuingiza Ikulu, halafu atakuwa amepoteza Ubunge, dhen atakapokuwa akitoa maoni watu watasema..ah! huyo si alishindwa Uraisi ndiyo maana anasema hivyo!

4: Mwl. ama Mzee haambiliki, japo alikataa asitwe kwa jina hilo na kuahidi kuwa litakwenda mtu. Alimshauri Mh. Lyatonga, aache kugombea Uraisi akagombee Ubunge watu wakajua, SiSi-eM imeshaona itashindwa! kwa vile wazo hilo lilitolewa na Mzee wa CCM, lakini angelifuata Ushauri wake NCCR ya Mrema ingekuwa wapi sasa hivi?..lakini baada ya kukataa ushauri bila kufikiria unakimbilia itikadi za kichama, nadhani ndiko kulikuja sababisha anguko la NCCR..sasa hivi, ALM akizungumza nani anamsikiliza tena?..hata kama hoja yake inaukweli ndani yake!

Namalizia kwa Kusema,
Sipendi kuwapa Ki-bri, ila tumeambiwa kwenye ukweli tuseme.

Huku Kijijini kwetu,ambako ndiyo wapiga kura wengi tupo Ukisema CUF tunajua ni Maalimu Self, hawa akina Lipumba na wengine mnawajua nyie, Ukisema CHADEMA tunajua ni Dr. Slaa mbuge wa Karatu, Mbowe, sijui nani hao mnawajua nyie, Pia ukitaja NCCR-MAGEUZI, haki yanani vile siyo utani bado tunajua ni Augustine Mrema, sasa kwa vile mimi ndiyo nimetoka Mjini naanza kuwaelimisha!

Ee! Mwenyezi Mungu sijui hawa wanadamu wamenielewa??? ..umenipa kazi ngumu sana kuwaelimisha.

Umeme umekaribia kukatika naomba nitoe ONYO: kwa Wanachadema na Wote wenye Mapenzi mema na nchi hii, naomba sana tusijekosea kukiondoa kijiko kwenye Nyumba ya Starehe; Kama ikiwezekane Dr. Slaa afie Bungeni, hata akifikisha umri wa Mugabe (84) asikubali kung'atuka, labda aje mwenye kasi yake.

MAWAZO MEMA YA HAWA JAMAA:
Mama
Yah, sipingi mada, napinga Dr Slaa kugombea urais 2010. Nimekupata kabisa

Jamco Za
Your right man, tunamhitaji zaidi Dr. Siraa bungeni na sio kwenye uraisi, ambako atazungukwa na mafisadi wa kila aina.

Kubwa Jinga
Mimi napingana na hilo wazo la kumpendekeza Dr. Slaa kuwa mgombea uraisi. Ku-focus kwenye uraisi pekee ni moja ya sababu kubwa ya wapinzani kushindwa kwenye kila uchaguzi. Ufumbuzi wa matatizo ya mtanzania hautatokana na upinzani kuingia ikulu, bali kwa kubadilisha mfumo mzima wa kiutawala. Ni vema tukaelewa yafuatayo;

1. Nchi haijengwi na mtu mmoja na ndio maana Nyerere yalimshinda. Kwa hiyo kama mfumo wa kiutawala hautabadilishwa na kuondoa madaraka makubwa aliyonayo raisi na serikali yake hivi sasa, na kuyahamishia bungeni, mahakamani na kwa wananchi, yeyote yule atakayeingia anaweza akaifuja nchi bila kipingamizi.

2. Hadi hivi sasa hakuna dalili zozote zinazoonyesha uwezekano wa CCM kushindwa kwenye kinyang'anyiro cha uraisi 2010, hata baada ya kulipuliwa kwa mafisadi wote wakiwa wanaCCM. Uchaguzi wa hivi karibuni Kiteto inatoa picha ya ugumu uliopo.

3. Mgawanyiko na tamaa katika kambi ya upinzani ni kikwazo kikubwa sana kwao kupata ushindi. Hata kama Nyerere angefufuka na kuwa mgombea wa chama kimojawapo cha upinzani, bado ingekuwa vigumu kwao kuunganisha nguvu zao kuing'oa CCM.

4. Uongozi mbovu ndani ya vyama vya upinzani nao ni kikwazo kikubwa katika kuwavutia wasomi na wafanyabiashara wengi ambao wanakerwa na CCM. Ni muhimu kutatua masuala kama ya udini, ukabila na umungu-mtu ndani ya vyama ili kuondoa hali ya hivi vyama kuwa na ushabiki wa kimajimbo na wenye upeo mwembamba.

5. Nyerere alisema upinzani wa kiukweli TZ utatoka ndani ya CCM, na mimi nakubaliana naye kabisaa hata baada ya kufariki. Hili litawezekana kwa CCM wenyewe kupingana au kwa wapinzani kuwa na vyama ambavyo vitawavutia walioCCM kuhamia kwao. Hivi sasa la awali la CCM kupingana linakaribia linalohitajika ni kwa wapinzani kuunda mazingira yatakayoweza kuwavutia wanaCCM kuhamia kwao.

6. Msisitizo kwa upinzani uwe katika kuandaa wabunge wengi iwezekanavyo. Na hii ndio sababu kubwa ya kupinga kumuingiza Dr. Slaa kwenye kinyang'anyiro cha uraisi. Uwezekano wa yeye kushinda ubunge ni mkubwa kuliko uraisi na isingekuwa vema akakosekana kwenye ulingo wa kisiasa kwa miaka 5, kama ilivyokuwa kwa Mrema, na kushindwa kufanya yale tuliyoona anaweza kuyafanya akiwa bungeni. Kila mpinzani aliye na uwezo wa kushinda ubunge, aanze kujengwa hivi sasa kwenye majimbo yao ili agombee ubunge na kuimarisha upinzani bungeni.

7. Upinzani wapunguze hili la ku-focus zaidi kwenye uraisi, na kutumia rasilimali zao kwenye ubunge. Kwa mfano CHADEMA walitumia zaidi ya TShs 220millioni (30% ya pesa waliyokuwa nayo) kwenye kukodisha helicopter tu. Lakini jumla ya pesa yote walizowapa wagombea wa ubunge wao ilikuwa ni TShs. 59 millioni tu (8% tu). Kama wangewekeza zaidi kwenye wabunge labda watu kama Bob Makani wangekuwa wabunge hivi sasa.

Changamoto langu kwa vyama vya upinzani ni kuungana na kuwekeza zaidi kwenye ubunge maana kwa hali ilivyo hivi sasa, sio rahisi kuing'oa CCM in 2010.
 
Safimbi, Mimi nilifikiria kuwa DoSantos alikumaliza kumbe alikumaliza kimwili tu, lakini naona kiubongo sio ajabu umechukua na digirii nyingine. Niliposoma huu mukhtasari wako nikakumbuka ule ubongo wa pale Daily News unaochemka na kuwachukiza wahariri, Adam Lusekelo.

Yeye anajua kuipamba nzitonzito katika mfumo wa kikatuni, na kuweza kufikisha ujumbe wake bila shida. Nafikiri hapa unamkaribia kama sio kuwa unaweza kumpita ukiongeza masaa kidogo kwenye kii bodi.

Umefanya kazi nzuri maana sikujua kama tuna vichwa viona mbali zaidi ya mashabiki. Kazi nzuri, keep it up.
 
Tunasema Dr. slaa awe President, ok, lakini hata akiwa rais nani atakuwa prime min? nani atakuwa vise pre? bado tunahitaji kupeleka changamoto ndani ya chama cha CHADEMA, ULE UKABILA UTOWEKE KWANZA KISHA itawezekana.

Sote tunajua CHADEMA ndiyo chama mbadara kama Asha anavyosema.
 
Kweli JF hapo ndipo ninapoiona umuhimu wake ni kama Osama na Marekani kwani Osama hajulikani aliko, lakini huzungumza. Ama Joseph Kony na Serikali ya Mseveni, mashambulizi bila kumuona adui: Twendeni kazi.

Kwa Mujibu wa taratibu za kutumia kazi ya mtu lazima upate kibali toka kwa mhusika Mkuu.(All rights reserved; No part of this post may be sold or hired, without the written permission of the publisher/ Writter). Hivyo ninaomba nipate Kibali kwa Mh. KJ ilikutumia Vigezo 7 alivyoviorodhesha hapo chini vitakavyo pelekea Ushindi kwa vyama vya upinzania kuelekea Ikulu 2015-2020, ilituvifanyie marekebisho kidogo na kuwa Mwongozo kamili:

Najua hapa simahala pake, wataalamu mtanipa mwogozo tuiweke wapi hii thread ilituanze kuifanyia marekebisho. Lakini ni kwa wale tu wenye mapenzi mema na Nchi hii, na wala siyo ushabiki wa Kivyama

Post halisi inasomeka kama ifuatavyo

Mimi napingana na hilo wazo la kumpendekeza Dr. Slaa kuwa mgombea uraisi. Ku-focus kwenye uraisi pekee ni moja ya sababu kubwa ya wapinzani kushindwa kwenye kila uchaguzi. Ufumbuzi wa matatizo ya mtanzania hautatokana na upinzani kuingia ikulu, bali kwa kubadilisha mfumo mzima wa kiutawala. Ni vema tukaelewa yafuatayo;
  1. Nchi haijengwi na mtu mmoja na ndio maana Nyerere yalimshinda. Kwa hiyo kama mfumo wa kiutawala hautabadilishwa na kuondoa madaraka makubwa aliyonayo raisi na serikali yake hivi sasa, na kuyahamishia bungeni, mahakamani na kwa wananchi, yeyote yule atakayeingia anaweza akaifuja nchi bila kipingamizi.
  2. Hadi hivi sasa hakuna dalili zozote zinazoonyesha uwezekano wa CCM kushindwa kwenye kinyang'anyiro cha uraisi 2010, hata baada ya kulipuliwa kwa mafisadi wote wakiwa wanaCCM. Uchaguzi wa hivi karibuni Kiteto inatoa picha ya ugumu uliopo.
  3. Mgawanyiko na tamaa katika kambi ya upinzani ni kikwazo kikubwa sana kwao kupata ushindi. Hata kama Nyerere angefufuka na kuwa mgombea wa chama kimojawapo cha upinzani, bado ingekuwa vigumu kwao kuunganisha nguvu zao kuing'oa CCM.
  4. Uongozi mbovu ndani ya vyama vya upinzani nao ni kikwazo kikubwa katika kuwavutia wasomi na wafanyabiashara wengi ambao wanakerwa na CCM. Ni muhimu kutatua masuala kama ya udini, ukabila na umungu-mtu ndani ya vyama ili kuondoa hali ya hivi vyama kuwa na ushabiki wa kimajimbo na wenye upeo mwembamba.
  5. Nyerere alisema upinzani wa kiukweli TZ utatoka ndani ya CCM, na mimi nakubaliana naye kabisaa hata baada ya kufariki. Hili litawezekana kwa CCM wenyewe kupingana au kwa wapinzani kuwa na vyama ambavyo vitawavutia walioCCM kuhamia kwao. Hivi sasa la awali la CCM kupingana linakaribia linalohitajika ni kwa wapinzani kuunda mazingira yatakayoweza kuwavutia wanaCCM kuhamia kwao.
  6. Msisitizo kwa upinzani uwe katika kuandaa wabunge wengi iwezekanavyo. Na hii ndio sababu kubwa ya kupinga kumuingiza Dr. Slaa kwenye kinyang'anyiro cha uraisi. Uwezekano wa yeye kushinda ubunge ni mkubwa kuliko uraisi na isingekuwa vema akakosekana kwenye ulingo wa kisiasa kwa miaka 5, kama ilivyokuwa kwa Mrema, na kushindwa kufanya yale tuliyoona anaweza kuyafanya akiwa bungeni. Kila mpinzani aliye na uwezo wa kushinda ubunge, aanze kujengwa hivi sasa kwenye majimbo yao ili agombee ubunge na kuimarisha upinzani bungeni.
  7. Upinzani wapunguze hili la ku-focus zaidi kwenye uraisi, na kutumia rasilimali zao kwenye ubunge. Kwa mfano CHADEMA walitumia zaidi ya TShs 220millioni (30% ya pesa waliyokuwa nayo) kwenye kukodisha helicopter tu. Lakini jumla ya pesa yote walizowapa wagombea wa ubunge wao ilikuwa ni TShs. 59 millioni tu (8% tu). Kama wangewekeza zaidi kwenye wabunge labda watu kama Bob Makani wangekuwa wabunge hivi sasa.
Changamoto langu kwa vyama vya upinzani ni kuungana na kuwekeza zaidi kwenye ubunge maana kwa hali ilivyo hivi sasa, sio rahisi kuing'oa CCM in 2010.

Mimi Bila hata ya kupata idhini toka kwa KJ, naanza kwa kubadili sehemu chache kama kutia chachu!

MAMBO 7 YA KUZINGATIWA NA VYAMA VYA UPINZANI KUELEKEA IKULU 2015-2020.
Wapinzani Ku-focus kwenye uraisi pekee ni moja ya sababu kubwa ya kushindwa kwenye kila uchaguzi. Ufumbuzi wa matatizo ya mtanzania hautatokana na upinzani kuingia Ikulu, bali kwa kubadilisha mfumo mzima wa kiutawala. Ni vema tukaelewa yafuatayo;

1: Nchi haijengwi na mtu mmoja na ndio maana Nyerere yalimshinda. Kwa hiyo kama mfumo wa kiutawala hautabadilishwa na kuondoa madaraka makubwa aliyonayo raisi na serikali yake hivi sasa, na kuyahamishia Bungeni, Mahakamani na kwa Wananchi, yeyote yule atakayeingia anaweza akaifuja nchi bila kipingamizi.

2: Hadi hivi sasa hakuna dalili zozote zinazoonyesha uwezekano wa CCM kushindwa kwenye kinyang'anyiro cha uraisi 2010, hata baada ya kulipuliwa kwa mafisadi wote wakiwa wanaCCM. Bado haitoshi kupelekea vyama vya Upinzani Kuingia Ikulu 2010.

3: Mgawanyiko na tamaa katika kambi ya upinzani ni kikwazo kikubwa sana kwao kupata ushindi. Hata kama Nyerere angefufuka na kuwa mgombea wa chama kimojawapo cha upinzani, bado ingekuwa vigumu kwao kuunganisha nguvu zao kuing'oa CCM.

4: Uongozi mbovu ndani ya Vyama vya upinzani ni kikwazo kikubwa katika kuwavutia wasomi na wafanyabiashara wengi ambao wanakerwa na CCM. Ni muhimu kutatua masuala kama ya udini, ukabila na umungu-mtu ndani ya vyama ili kuondoa hali ya hivi vyama kuwa na ushabiki wa kimajimbo na wenye upeo mwembamba.

5: Upinzani wa kiukweli TZ utatoka ndani ya CCM. Hili litawezekana kwa CCM wenyewe kupingana au kwa wapinzani kuwa na vyama ambavyo vitawavutia walioCCM kuhamia kwao. Hivi sasa la awali la CCM kupingana linakaribia linalohitajika ni kwa wapinzani kuunda mazingira yatakayoweza kuwavutia wanaCCM kuhamia kwao.

6: Msisitizo kwa upinzani uwe katika kuandaa wabunge wengi iwezekanavyo. Kila mpinzani aliye na uwezo wa kushinda ubunge, aanze kujengwa hivi sasa kwenye majimbo yao ili agombee ubunge na kuimarisha upinzani bungeni.

7: Vyama vya Upinzani wapunguze ku-focus zaidi kwenye uraisi, na kutumia rasilimali zao kwenye Ubunge, maana kwa hali ilivyo hivi sasa, sio rahisi kuing'oa CCM in 2010.

Ah! unaweza ukaandika hayo tena! nawewe ukaitwa ni mwanamtandao..kumbe unaitakia mema Jamhuri ya Muungano ya Watu wa Tanzania.
 
Kweli JF hapo ndipo ninapoiona umuhimu wake ni kama Osama na Marekani kwani Osama hajulikani aliko, lakini huzungumza. Ama Joseph Kony na Serikali ya Mseveni, mashambulizi bila kumuona adui: Twendeni kazi.

Kwa Mujibu wa taratibu za kutumia kazi ya mtu lazima upate kibali toka kwa mhusika Mkuu.(All rights reserved; No part of this post may be sold or hired, without the written permission of the publisher/ Writter). Hivyo ninaomba nipate Kibali kwa Mh. KJ ilikutumia Vigezo 7 alivyoviorodhesha hapo chini vitakavyo pelekea Ushindi kwa vyama vya upinzania kuelekea Ikulu 2015-2020, ilituvifanyie marekebisho kidogo na kuwa Mwongozo kamili:

Najua hapa simahala pake, wataalamu mtanipa mwogozo tuiweke wapi hii thread ilituanze kuifanyia marekebisho. Lakini ni kwa wale tu wenye mapenzi mema na Nchi hii, na wala siyo ushabiki wa Kivyama

Post halisi inasomeka kama ifuatavyo

Mimi Bila hata ya kupata idhini toka kwa KJ, naanza kwa kubadili sehemu chache kama kutia chachu!

MAMBO 7 YA KUZINGATIWA NA VYAMA VYA UPINZANI KUELEKEA IKULU 2015-2020.
Wapinzani Ku-focus kwenye uraisi pekee ni moja ya sababu kubwa ya kushindwa kwenye kila uchaguzi. Ufumbuzi wa matatizo ya mtanzania hautatokana na upinzani kuingia Ikulu, bali kwa kubadilisha mfumo mzima wa kiutawala. Ni vema tukaelewa yafuatayo;
Sidhani kwamba kuna mtu amesema hapa wapinzani wa-focus kuingia Ikulu pekee, mabadiliko yanayotakiwa kufanywa na upinzani ni katika ngazi zote za uongozi. Kuna umuhimu mkubwa kwa wapinzani kuweka watu wanaokubalika na wengi kuanzia kwenye Urais mpaka ubunge.

1: Nchi haijengwi na mtu mmoja na ndio maana Nyerere yalimshinda. Kwa hiyo kama mfumo wa kiutawala hautabadilishwa na kuondoa madaraka makubwa aliyonayo raisi na serikali yake hivi sasa, na kuyahamishia Bungeni, Mahakamani na kwa Wananchi, yeyote yule atakayeingia anaweza akaifuja nchi bila kipingamizi.
Ndio maana wapinzani wanaomba mabadiliko ya Katiba ili iendane na mfumo wa sasa wa vyama vingi na kuongeza ufanisi na uwazi katika utendaji wa Viongozi.

2: Hadi hivi sasa hakuna dalili zozote zinazoonyesha uwezekano wa CCM kushindwa kwenye kinyang'anyiro cha uraisi 2010, hata baada ya kulipuliwa kwa mafisadi wote wakiwa wanaCCM. Bado haitoshi kupelekea vyama vya Upinzani Kuingia Ikulu 2010.
Ndio maana hili vuguvugu la kumchagua mtu atayefaa kukichukua kiti cha uRais linaanza sasa na sio kuongojea mpaka karibia na uchaguzi. Kikwete hafai kuiongoza nchi kwa sababu ni Rais alieshindwa kabisa kuwatumikia watanzania na pia kutekeleza majukumu aliyopewa na watanzania.

3: Mgawanyiko na tamaa katika kambi ya upinzani ni kikwazo kikubwa sana kwao kupata ushindi. Hata kama Nyerere angefufuka na kuwa mgombea wa chama kimojawapo cha upinzani, bado ingekuwa vigumu kwao kuunganisha nguvu zao kuing'oa CCM.
Ni kweli kuna umuhimu mkubwa kwa vyama vya upinzani kuweka mgombea mmoja.

4: Uongozi mbovu ndani ya Vyama vya upinzani ni kikwazo kikubwa katika kuwavutia wasomi na wafanyabiashara wengi ambao wanakerwa na CCM. Ni muhimu kutatua masuala kama ya udini, ukabila na umungu-mtu ndani ya vyama ili kuondoa hali ya hivi vyama kuwa na ushabiki wa kimajimbo na wenye upeo mwembamba.
actually ukiniuliza mimi na watanzania wengi uongozi mbovu na unaonuka ni ule wa ndani ya CCM.

5: Upinzani wa kiukweli TZ utatoka ndani ya CCM. Hili litawezekana kwa CCM wenyewe kupingana au kwa wapinzani kuwa na vyama ambavyo vitawavutia walioCCM kuhamia kwao. Hivi sasa la awali la CCM kupingana linakaribia linalohitajika ni kwa wapinzani kuunda mazingira yatakayoweza kuwavutia wanaCCM kuhamia kwao.
Hii ni dhana potofu na sikubaliani nayo kabisa. Pia hii ni dharau kubwa kwa watanzania wengine ambao wanataka kuleta mabadiliko, kuonyesha kana kwamba ni CCM pekee yenye hadhi ya kutoa Viongozi nchini Tanzania ni upotofu wa kimawazo. Naona na wewe umekuwa brain-washed kuamini Tanzania ni CCM na CCM ni Tanzania. Unapokuwa na mawazo kama haya inatufanya wengi tujiulize kama ni kweli ulikaa chini na ukatafakari kabla ya kuandika.

6: Msisitizo kwa upinzani uwe katika kuandaa wabunge wengi iwezekanavyo. Kila mpinzani aliye na uwezo wa kushinda ubunge, aanze kujengwa hivi sasa kwenye majimbo yao ili agombee ubunge na kuimarisha upinzani bungeni.
Ni muhimu kwa upinzani kuweka wagombea mahiri katika njanja zote za uongozi.

7: Vyama vya Upinzani wapunguze ku-focus zaidi kwenye uraisi, na kutumia rasilimali zao kwenye Ubunge, maana kwa hali ilivyo hivi sasa, sio rahisi kuing'oa CCM in 2010.
Uchaguzi wa Rais huwa unaenda sambamba na uchaguzi wa wabunge kwa hiyo ni rahisi kwa pesa hizo kutumika kutangaza both Mgombea Urais na Ubunge wa eneo husika.

Bado naamini kama wengi walivyokubaliana nami umuhimu wa Dr. Slaa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakati ni huu na hakuna kuongoja. Dr. Slaaa For President 2010.
 
Tunasema Dr. slaa awe President, ok, lakini hata akiwa rais nani atakuwa prime min? nani atakuwa vise pre? bado tunahitaji kupeleka changamoto ndani ya chama cha CHADEMA, ULE UKABILA UTOWEKE KWANZA KISHA itawezekana.Sote tunajua CHADEMA ndiyo chama mbadara kama Asha anavyosema.

kwani umesikia kuwa Tanzania wanaofaa kuwa hao MaPM na wengine ni wana ccm peke yake?

nchi ile inaweza kuongozwa na mawaziri hata 8 tu na kila kitu kikawa bora kuliko ufisadi na wizi unaofanywa huko sisiemu
 
Unajua mwafrika wa kike kuna sehemu nilishasema serikali nzima ya jamhuri ya muungano wa Tanzania iwe na watu 15 tu. Mawaziri na manaibu wawe 10 halafu Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Waziri Kiongozi wa Zanzibar.

Yaani hii ingeleta ufanisi mkubwa kuliko lundo la mawaziri hivi sasa ambalo halina msaada wowote kwa watanzania.
 
Unajua mwafrika wa kike kuna sehemu nilishasema serikali nzima ya jamhuri ya muungano wa Tanzania iwe na watu 15 tu. Mawaziri na manaibu wawe 10 halafu Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Waziri Kiongozi wa Zanzibar. Yaani hii ingeleta ufanisi mkubwa kuliko lundo la mawaziri hivi sasa ambalo halina msaada wowote kwa watanzania.

Geeque,

Hili hata mimi nimelisema sana hapa esp baada ya lile baraza kubwa la mawaziri la Kikwete analoendelea kulikuuza kila siku.

Wakipungua wanasiasa kwenye uendeshaji wa nchi basi kutakuwa angalau na unafuu kwenye matumizi ya serikali.
 
Hebu weka bayana muundo wa serikali iliyopo mawazoni mwako badala ya kuzungukazunguka na maeneno tele..
 
Jamani bila Utani hapa Dr. Slaa akisimama na Kikwete 2010 ni kitu gani kinachompa Popular vote kwa wananchi.

Ningeomba data hata za waandishi wa mtaani ambao wanaweza kusema Dr. Slaa ni popular kuliko Kikwete ktk nafasi hiyo maanake Wabongo kama navyowafahamu itakapo fika 2010 watakuwa wamesha sahau mengi na pengine kutoona uhusiano wa Utawala wa Kikwete na mafisadi.

Kumbukeni kwamba tamaduni zetu zina vimila vya ajabu ajabu.. watu wanaweza ishi na jambazi na hata siku moja wasihofie maisha yao. Mzazi anaweza kuwa na mtoto muuza Unga na asikubali ubaya wake isipokuwa majirani ndio wanamwonea wivu.

Kifupi mtu mbaya kwa MTanzania (mdanganyika) ni yule anayefunga milango kwa majirani wasipate kufaidika lakini yule anayewapa chochote, mcheshi na mtu wa watu hata kama ni jamabazi hakuna anayemtazama undani wake.

Waswahili husema ukimchunguza kuku huwezi kumla na kweli KUKU ndio kitoweo chenye hadhi kubwa kuliko vyote kwa Mdanganyika.

Kikwete anaweza kuwa ndio huyo kuku, hata kama mtamgeuza nguruwe watamkataa waislaam tu wengine ndio kwanza watashangilia - Kitu Moto!
 
Sidhani kwamba kuna mtu amesema hapa wapinzani wa-focus kuingia Ikulu pekee, mabadiliko yanayotakiwa kufanywa na upinzani ni katika ngazi zote za uongozi. Kuna umuhimu mkubwa kwa wapinzani kuweka watu wanaokubalika na wengi kuanzia kwenye Urais mpaka ubunge.

Bado naamini kama wengi walivyokubaliana nami umuhimu wa Dr. Slaa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakati ni huu na hakuna kuongoja. Dr. Slaaa For President 2010.

Mheshimiwa Geeque, Amani iwe nawe!
Ninauhakika kama tunakaa meza moja ya mazungumzo tunaweza kufikia muafaka, maana hata kwenye bendera ya Jamhuri yetu hakuna rangi nyekundu, hata Uhuru wa Nchi hii ulikuwa ni wamazungumzo!

katika nukuu ya kipengele cha kwanza; hilo limeeleweka, lakini nukuu ya PILI! Mimi binafsi Sikubaliani na DR. SLAA for President TWENTY - TEN (Zingatia sizungumzii ushabiki wa kivyama, naangalia Maslahi ya Utaifa)

Sababu zinazonifanya Nipingane na Mh. Dr.Wilbroad Slaa (MB) Kugombea URAIS, ni hizi zifuatazo:-

1: Siyo kwamba Mh. Slaa hafai kugombea Urais,La! anafaa lakini uwezekano wa Kufikisha ile asilimia 50% ya kura zote zitakazo pigwa kwa Mwaka wa Uchaguzi 2010 haupo!

2: Kwa sasa Dr. Slaa ni nguzo ya CHADEMA, kubali ama kataa! na ndiye anayeifanya Chadema iendelee kufahamika ndani na Nje ya Nchi kutokana na kazi yake nzuri aifanyayo yeye pamoja na washirika wake AKIWA BUNGENI

3: Dr. Slaa atakapogombea Urais mwaka 2010 na kisha kushindwa ina maana hatakuwa Bungeni tena kwa mwaka huo wa 2010 labda 2015 ambapo tayari atakuwa amepoteza nguvu kisiasa.

4: Dr. Slaa anatakiwa aendelee kuwa Bungeni kama NGUZO ya Chama, na kama watahitaji kusimamisha Mgombea Urais 2010 basi watafute mtu mwingine lakini siyo Dr. Slaa(MB)!! Watu wote wenye uwezo wakuikosoa Serikali, wanatakiwa wawe Bungeni

5: Bungeni ndiyo sehemu pekee inayomuwezesha Kufichua maovu ya kifisadi yafanywayo! Kuna mifano, iliyo wazi, Mh. Mrema alikuwa msema kweli na mfichua maovu, lakini alivyogombea Urais na kushindwa, na kupoteza Ubunge pia, Nani anamsikiliza tena???? hata kama hoja yake ina nguvu hakuna anayemjali

6: Kubali ama kataa yote sawa! Mpaka sasa mkakati walionao SiSi-eM nikuondoa Bungeni Jamii ya akina Slaa...lakini ninyi wenyewe mnaanza kampeni ya kumng'oa Dr. Slaa Bungeni!

7: Mh. Mrema alikataa Ushauri wa Mzee haambiliki wa kubaki Bungeni, akiamini ataikwaa Ikulu matokeo yake ndiyo hayo! Japo kuwa watafiti wanadai kuwa Mrema ndiye Mgombea pekee toka Upande wa Upinzani aliyewahi kupata Ushundi wa Kishindo kama mgombea Urais tangu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi vya siasa kwa kupata asilimia 11 ya kura zote zilizopigwa, rekodi ambayo hakuna mgombea mwingine wa kutoka Upinzani ameifikia.

..MAISHA BORA KWA KILA MHESHIMIWA!...
 
Quote: Savimbi
5: Upinzani wa kiukweli TZ utatoka ndani ya CCM. Hili litawezekana kwa CCM wenyewe kupingana au kwa wapinzani kuwa na vyama ambavyo vitawavutia walioCCM kuhamia kwao. Hivi sasa la awali la CCM kupingana linakaribia linalohitajika ni kwa wapinzani kuunda mazingira yatakayoweza kuwavutia wanaCCM kuhamia kwao.

Hii ni dhana potofu na sikubaliani nayo kabisa. Pia hii ni dharau kubwa kwa watanzania wengine ambao wanataka kuleta mabadiliko, kuonyesha kana kwamba ni CCM pekee yenye hadhi ya kutoa Viongozi nchini Tanzania ni upotofu wa kimawazo. Naona na wewe umekuwa brain-washed kuamini Tanzania ni CCM na CCM ni Tanzania. Unapokuwa na mawazo kama haya inatufanya wengi tujiulize kama ni kweli ulikaa chini na ukatafakari kabla ya kuandika.

Sijui kama umekaa ukafikiria kwa namna ipi, inaonyesha jina SiSi-eM linakukera sana! ukiliona tu hutaki hatakufikiria nini kinazungumziwa hapo.

Ninaposema:Upinzani wa kiukweli TZ utatoka ndani ya CCM. Hili litawezekana kwa CCM wenyewe kupingana au kwa wapinzani kuwa na vyama ambavyo vitawavutia walioCCM kuhamia kwao.Ulielewa nini hapo?

Mpaka sasa hivi ninavyoandika, CCM ndiyo chama chenye wanachama wengi, sasa kama wanachama wa vyama vingine watatoka wapi?? kama siyo ndani ya CCM na kuhamia vyama vya upinzani? ama vyama vya upinzani vitahitaji wanachama wa kizazi kipya tu?

kwaswala la upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM ina maana kwamba, Wao ndiyo wamekuwa ndani ya Serikali kwa miaka mingi hivyo wanajua siri nyingi za uovu: Kama mwanaccm atakacha na kuhamia chama cha upinzani si'atakuja na siri zote za kifisadi na kisha kuzianika hadharani, ambapo tayari atakuwa amekipa nguvu za ziada chama alichojiunga nacho ilikuendeleza mapambano.

Mrema alitokea SiSi-eM akaja na mabomu yake aliyoyafahamu akiwa huko, nadhani pia hata Dr. Slaa alikuwa hukohuko SiSi-eM miaka hiyo! ndiyo maana anajitahidi kupambana na serekili ya SiSi-eM

Mseveni alipoona Col. Dr.Kiiza anagombea Urais, aliishiwa nguvu na kuanza kumfungulia kesi za ajabu-ajabu, mara ubakaji ilimradi tu kumdhoofisha kisiasa, na hii ilitokana na kwamba Kiiza alimfahamu vyema Mseveni kwa vile alikuwa Daktari wake. Mseveni aliamini kabisa Col.Dr. Kiiza atayaweka wazi mambo yake. Kwa maana hiyo Kiongozi kigogo wa CCM, akihamia Chama Kingine lazima CCM wahahe si wajua anakwenda kuwaanika! ndiyo sababu ya kusema Upinzani utatoka ndani ya CCM na wala sivinginevyo!

Sizungumzii kwa ajili ya ushabiki wa kivyama; nazungumzia hali halisi!

...........MAISHA BORA KWA KILA MHESHIMIWA!
 
Kwa kweli mtu kama slaa ni vyema angesubiri 2015 kwani hapo ndipo kutakua na changamoto kubwa na kama opposition wakielekeza nguvu zao bungeni kwa sasa itakua jambo bora zaidi.

Still we need him in the parliament.Pia kuhusu sula la elimu ya uraia opposition ndio wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kutoa sapoti kwa NGO mbalimbali kwani CCM hawatafanya hivyo kwani hicho ni kiama kwao.

Sasa hivi ni takribani mwaka na nusu umebaki.Ni muda mchache sana umebaki kwa upinzani kujipanga na masuala kama muafaka nk ni masuala ambayo CCM pia wanayafanya ili kupoteza muda wa opposition kujipanga for the forthcoming election.Shame on them!
 
Back
Top Bottom