The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Mwanzo wa kila kitu ni Fikra, kisha maneno halafu vitendo. Bado tunajadiliana na kufundishana.

No! sasa nimechoka, and I am getting depressed to accept the fact that come 2010, it is another five years (of the same?).....Ah...Ah..., even worse. Those last five years of the fourth phase would be unimaginable!

Forum hii inayo mambo mengi mazuri tu yaliyozungumziwa, na ambayo wapinzani wangepashwa kuyafanyia kazi mapema kabisa kabla ya 2010! But, Alas, hakuna lolote wanalolifanya so far!

MODS na Invisible..... Jamani, inawezekana kuwagawia vyama vyote vya upinzani 'hard copy' ya michango ya mawazo yaliyotolewa katika mjadala huu? Hili niombi tu kama inawezekana.

Ninaelewa kwamba baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali katika vyama hivi hupitia humu mara kwa mara, lakini ninaelewa pia, wengi wao hawana muda wa kusoma michango yote inapokuwa katika mtandao kama hivi.

Baada ya Rev. Kishoka kuuopoa tena huu mjadala leo, nimeupitia tena upya tokea mwanzo kabisa. Nimegundua kwamba mambo yote muhimu tulishayaongelea huku, na sasa tunarudia hayo hayo katika mijadala mipya inayobandikwa - kama ule wa Dr. Slaa na Urais.

I am saying, at a minimum, let JF play its small part by conveying this information to vyama vya upinzani in a form of a 'hardcopy.' OR is this too much to ask for?

Just imagine another five years of CCM in everything....Gosh....it is intolerable!
 
Kwa vigezo vya nani unatumia kusema kuwa hapajawi kuwa na kiongozi kama Mrema peke yake? mtu mwenye chuki za kikabila na kidini kama wewe hufai kuweka viwango vya kugombea uraisi maana unaweza kuua watu kwa chuki zako.

Hayo ya ukabila na udini tunayaonea kwa wanaKilimanjaro ndani ya Chadema na CUF kwenye misikiti.

Tokea Mrema apate almost 30% ya kura mwaka 1995, hakujatokea mgombea mwingine aliyekaribia hata 20%. This is a fact.
 
Kweli kabisa Ngabu,

badala ya Kubwajinga kuanza kuwaambia wapinzani wawaachie ccm nafasi ya uraisi, inabidi aanze kuwaambia ccm kuacha kutoa mgombea wa urais maana kuanzia mwaka 95 ccm wanatoa mabomu tupu


Huu ni upupu mwingine. Sijasema wawaachie. Soma tena article yangu tena.
 
Tokea Mrema apate almost 30% ya kura mwaka 1995, hakujatokea mgombea mwingine aliyekaribia hata 20%. This is a fact.

Lakini still hakuna rais wa CCM aliyewahi kupata kura 100%, kwa hiyo the name of the game hapa ni kuendelea kujaribu lakini sio kuacha kabisa, how can you know your political strength bila ya kujaribu?

Hivi kweli Jaluo angefika hapo alipo bila ya kujaribu? Dr. Slaa naye anaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa siasa za taifa kama alivyokwisha fanya anyways kwenye ufisadi.
 
Kama uwezo wa chadema kifedha ni mdogo je nini kitawasaidia kwenye ubunge pekee badala ya kwenye uraisi pia. Inaonekana wewe una tatizo na CHADEMA kuweka mgombea wa uraisi na sio swala la upinzani.

Nina wasiwasi ungefurahi sana kama mgombea uraisi angekuwa yule rafiki yako mdini mwenzako ambaye ulikuwa unampigia debe kipindi kile.

Ingawa hii pia imejaa pumba, lakini nitakujibu sehemu isiyo pumba.

Hapa ni kutumia simple economics za wall street. You invest where you are likely to get returns/profit. Mwaka 2005, CHADEMA wali-invest pesa nyingi kwenye uraisi, wakashindwa lakini Mkenya mwenye kopta akatajirika. Wabumge wao walipewa only 7%. Kaborou kuona hivyo akakata deal na CCM akaachia ngazi.

This is a warning, mambo yakiendelea hivi, sitashangaa Zitto naye akafanya kama Kaborou na ndio maana CCM wanampa vi-offer hivi sasa. I am even curious about hii trip yake. CCM wanaweza wakawa wameongea na balozi wa US na kumuunganishia kitrip.
 
Lakini still hakuna rais wa CCM aliyewahi kupata kura 100%, kwa hiyo the name of the game hapa ni kuendelea kujaribu lakini sio kuacha kabisa, how can you know your political strength bila ya kujaribu?

Hivi kweli Jaluo angefika hapo alipo bila ya kujaribu? Dr. Slaa naye anaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa siasa za taifa kama alivyokwisha fanya anyways kwenye ufisadi.

Mkuu FMES,
Kujaribu ni sawa kabisa, kibaya ni kutumia nguvu zote na kuwatoa mhanga wenye nafasi nzuri za kushinda ubunge kwa ajili ya experiment ambayo ina dalili zote za kufeli.

Ngoja niiandike hii kwa kirefu.
 
Kujaribu ni sawa kabisa, kibaya ni kutumia nguvu zote na kuwatoa mhanga wenye nafasi nzuri za kushinda ubunge kwa ajili ya experiment ambayo ina dalili zote za kufeli. Ngoja niiandike hii kwa kirefu.

Unajua mkuu KJ, sio kwamba huna point, lakini tatizo ni kwamba historia ya siasa ambayo ni muhimu sana kwenye kuamua haya maamuzi haiko upande wako, lakini ngoja nisubiri maelezo yako kwa kirefu!
 
nadhani makosa tuliyoyafanya kwa Kikwete kwa kuchanganya umaarufu na uwezo wa uongozi yanatugharimu sana, watanzania. Tanzania tunatakiwa tuombe Mungu atusaidie kutoka kwenye hili shimo kwanza. Hii habari ya kukurupuka itatupeleka Zimbabwe na Kenya na Congo na sehemu zingine ambazo tumeshuhudia mambo ya ajabu.
Tofauti pekee ni kwamba wenzetu wanaweza kuingia kwenye matatizo na kisha kutoka, watanzania kamwe hatutaweza kutoka kwenye matatizo kama tukiingia. Salama yetu ni kukwepa matatizo.

Kikwete alijulikana tokea awali kuwa hafai. Kama isingekuwa wana mtandao na msaada wa Mkapa, labda tungekuwa na Salm au Prof.

Hata utumishi walishamshauri Mkapa kumuondoa JK MOFA, Mkapa akafyata. Ndio maana JK alipoingia tu akawatimua utumishi.
 
Ahsante mkuu, CV inaonekana kuwa ni nzito maana sijui kama CV ya Kawawa aliyewahi kuwa waziri wetu mkuu inaweza fikia hii,

wakuu ninaomba kusema hivi msiongelee Tanzania kama Ulaya, Tanzania ni Tanzania, mambo yetu bado ni yale yale ya pole pole huwezi kujua uwezo wako on anything bila ya kujaribu, na kuhsindwa na kawaida katika mchezo wowote ule, wakali wa siasa hawahitaji kuingia bungeni kuonyesha ukali wao, kwa sababu ni wakali ukali wao huo upo hata wakiwa nje ya bunge, sasa hakuna tatizo lolote kwa Dr. Slaa kugombea urais, agombee ili aweze kuchomeka agenda nzito kwa taifa kwenye malumbano ya uchaguzi na ninaamini kuwa anyo nafasi kubwa ya kushinda, na hata akishindwa yeye ni mkali tu ataendeleza ukali hata akiwa pembeni, lakini kutojaribu kabisa eti kwa kuogopa CCM kuwa ni imara zaidi ni mawazo ya Mwalimu hayo yamepitwa na wakati!

Mkuu FMES et al,
Nakubaliana na wewe kuwa bila kujaribu huwezi kujua matokeo. Lakini ni vema kutumia uzoefu wa awali na data zilizopo kujaribu kuangalia future (forecasting) na sio kufanya mambo kienyeji-enyeji au kwa jazba kama watu wasioenda shule au kwa ushabiki kama Mwafrika wa Kike na bibie Asha.

URAISI
Katika uchaguzi uliopita, Kikwete alipata 80.3% (9,123,952), Lipumba 11.7% (1,327,125) na Mbowe alipata 5.9% (668,756). Kwa Chadema ni mikoa 4 ambayo walipata zaidi ya 10%, Kilimanjaro, Arusha, Mara na Manyara. Kigoma walikaribia kidogo na kupata 9.4%. Kilimanjaro peke yake ndio walipata zaidi ya 20% (ambayo ilikuwa 20.6%). Kwenye hizo kura alizopata Mbowe, karibu 40% zimetoka mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Mara with Kilimanjaro having almost 25%. Kwa hiyo kwa mtu mwenye akili yake, hata ukiweka factor za EPA, Chenge, Richmond, Mkapa n.k., unless kama JK naye akaguswa moja kwa moja kama Chenge, sidhani kama huku kuzomea kunakoongelewa kuna ukubwa wa kutosha kubadilisha mawazo ya hata say 20% ya waliompigia JK kura. Tusisahau pia kuwa, hawa wanaojiuzulu bado waTZ wengi wanaona kama vile Kikwete ndie anayewashughulikia.

Unaweza kukagua matokeo ya uchagusi kwenye attachment, Nimeyatoa NEC website au www ya Chadema
To be Contd.....
 

Attachments

Contd.....

UBUNGE
Lakini ukiangalia kwenye ubunge, zaidi ya wagombea 20 wa Chadema walipata zaidi ya 30% ya kura. CUF wao wanao wagombea wengi zaidi waliopata zaidi ya 30%. That means, with additional efforts na mazingira ya sasa ya siasa TZ yaliyo mazuri kwa wapinzani, sehemu kubwa ya hawa wagombea, kama wakipewa resources zaidi wanaweza wakawa wabunge. Ukiongezea majimbo ya mafisadi kama akina Basil Mramba, Chenge n.k., uwezekano wa kuibuka na wabunge wengine say 10-40 kutoka kwenye hii mizoga unaongezeka.

Then kuna kundi la akina Mnyika n.k., ambao walipata between 10% to 20%. Hawa nao wako wengi sana. Chadema peke yake ina kama 17 hivi. Hawa watahitaji mtaji mkubwa zaidi kuwafanya wawe competitive. Lakini kwa vile hawatakuwa wanashindana na JK, bado nguvu ya ushindani watakuwa nayo na wanaweza wakashinda.
 
Contd.....
MUUNGANIKO WA VYAMA
Pia **** maeneo ambayo wapinzani walipigana wenyewe kwa wenyewe ngwara wakawaachia CCM ubunge. Kwa mfano jimbo la Vunjo, Chadema ilipata kura (11.9%), TLP (31.2%), NCCR (11.5%) jumla 54.6%. Halafu CCM wakapata 43.8% tu, kwa hiyo kwa rule ya simple majority wakajichukulia ubunge kiulaini.

Ndio maana nasisitiza kuwa, kama wapinzani wanataka ushindi wa maana, na hata kumtoa mtu ambaye angeshinda ubunge kafara, say Dr.Slaa, ni vema wakafanya hivyo tu baada ya kuungana na wala sio kama walivyo vipande-vipande hivi sasa, maana odds za ushindi as Chadema au CUF hazipo.


To be Contd.....
 
Contd.....

UMAARUFU WA MGOMBEA
Mbowe alipoacha jimbo lake na kugombea uraisi, jimbo likachukuliwa na CCM, licha ya kuwa yeye, ambaye ni mgombea uraisi wa Chadema, alikuwa maarufu sana hapo awali. Baada ya kushindwa uraisi, umaarufu wake nje ya Chadema nao ukapungua kitu ambacho kinaweza kikawa tatizo kwake kama akiamua kurudi kugombea ubunge Hai.

Hivyo ni wazi kuwa, kama ilivyokuwa kwa Mbowe, wapiga kura wengi wanapopiga kura hutofautisha kura za ubunge na uraisi. Ndio maana vyama vya upinzani vilipata kura nyingi kwenye ubunge kuliko uraisi.

WaTZ wengi wako radhi kumpa ubunge mgombea wa upinzani kama anawavutia, lakini ni wagumu kufanya hivyo kwenye uraisi. Hii ina maana kuwa hata Slaa akigombea, umaarufu wake sio kweli kuwa utasaidia kuleta kura. Hivi ni nani maarufu zaidi, Dr. Slaa wa 2010 au Mrema wa 1995?? Mrema aliingia ulingoni, sio tu baada ya kulipua mabomu na kukamata dhahabu airport, bali nchi nzima ilikuwa inamtambua maana alikuwa kiongozi wa ngazi ya juu na maarufu zaidi ya wengine wote. Lakini bado alipigwa chini kiulaini na Mkapa. Hivi sasa sidhani kama Dr.Slaa ana even 1/2 ya umaarufu alioingia nao Mrema kwenye kinyang'anyiro.

Lakini nina uhakika hii inaweza kubadilika kama major oppostion parties zikiamua kuungana. Faida ziko wazi;
  1. Watakuwa na Resources nyingi zaidi kwenye ubunge, na kwenye uraisi.
  2. Wananchi watakuwa wanacompare qualities za watu wawili tu na sio utitiri.
  3. Hata kama hawatashinda uraisi, lakini bado wanaweza wakawa na majority bungeni, badala ya kupoteza wabunge, maana chaguo la wananchi litakuwa wazi either CCM au upinzani.
Lakini wakiendelea na huu mchezo wa kila mtu na vyake, au hata kushirikiana tu bila kuvivunja vyama, kama ilivyokuwa Vunjo,
  1. Watashindwa kushindana na CCM sababu ya mgawanyiko
  2. Overheads zao zitakuwa kubwa na
  3. Sio ajabu wataishia kutapanya vipesa vichache walivyo navyo kwenye uraisi, maana kila mmoja wao atakuwa na mgombea, badala ya kuzipeleka kwenye ubunge.
 
Kubwajinga,
Comparing Dr Slaa na Mrema wa 1995 kunathibitisha kuwa wewe kweli ni kubwajinga.
 
Contd.....
MUUNGANIKO WA VYAMA
say Dr.Slaa, ni vema wakafanya hivyo tu baada ya kuungana na wala sio kama walivyo vipande-vipande hivi sasa, .


To be Contd.....

Hapa nitakubaliana na wewe suala ni kuungana tu.

Tanzania tunachohitaji ni maendeleo siyo longo longo. Nafikiri hata Mweshimiwa JK naye anahitaji kuongoza nchi yenye kuwa na maendeleo pamoja na kwamba ameishanyosha mikono kuhusu watu wanaokwamisha maendeleo.

Ninachoona kwa sababu anaipenda nchi yake mwaka 2010 hatachukua fomu ya kugombea Urais, badala yake naye pia anaungana na sisi watanzania wapenda maendeleo katika kumuunga mkono mgombea wetu ambaye atakuwa anatufaa.

Nategemea pia kwa kuwa siku hizi hata ndani ya chama cha mapinduzi kuna wale wabunge ambao wanajaribu kuleta ushindani bungeni wataweza pia kuunga mkono kiongozi bora anayeweza kutuvusha ktk hili wimbi la UFISADI bila woga.

Tunategemea baada ya 2010, badala ya kurudi nyuma, nategemea Tanzania yenye neema si kwa maneno hila kwa vitendo.

Wakati mwingine tunatakiwa kuona aibu, kuna Balozi mmoja ktk nchi zinazotoa misaada alishawahi kutushushua kuwa hivi jamani wao hawana raslimali yoyote ya maana wanayoitegemea ktk nchi yao. Lakini wanaweza kujipanga vizuri hata kuweza kusaidia nchi zenye utajiri mkubwa kama Tanzania. Aliuliza swali hivi Tatizo lenu ni nini? Kwa kweli kila aliyekuwepo aliona aibu.

Kwa kifupi nafikiri siyo mimi tu watanzania tumechoka kuaibika, kuchekwa na kejeli huku viongozi wetu wakijiona wao wameukata.
 
Hayo ya ukabila na udini tunayaonea kwa wanaKilimanjaro ndani ya Chadema na CUF kwenye misikiti.

Tokea Mrema apate almost 30% ya kura mwaka 1995, hakujatokea mgombea mwingine aliyekaribia hata 20%. This is a fact.

Hoja yako haina uzito. Mrema alipata kura hizo wakati huo kwa kuwa CCM ilikuwa haijajiandaa kikamilifu kuiba na kulikuwa na wave kubwa ya upinzani nchi nzima.

Mwaka 2000 Mkapa alikuwa amejizatiti wakati huo huo NCCR ilikuwa imeanguka, mwaka 2005 kulikuwa na ujio wa Kikwete kama Tumaini lililorejea wakati huo huo TLP na CUF zilikuwa zinaelekea kushuka. Mwaka 2010 Kikwete atakuwa ameporomoka wakati huo huo hamasa ya upinzani na CHADEMA inazidi kuendelea nchi nzima na kuna ushirikiano wa vyama. Ufisadi umetamalaki na watanzania wameelewa zaidi. Sasa unategemea nini?

Siasa ni kitu cha ajabu, lolote laweza kutokea wakati wowote. Kwa hiyo usijidanyanye eti kwa kuwa Kikwete amepata 80 ya kura upinzani 20 basi kibao hakiwezi kugeuka upinzani ukapata 80 Kikwete 20!

Nikupe mfano mdogo tu, hebu angalia matokeo ya Urais Tarime na Karatu mwaka 2000 halafu angalia yalivyokuwa ghafla mwaka 2005 mpaka Mbowe amepata 30-40 percent! Kutokana na ufisadi uliokithiri, sitashangaa kama maeneo yote yakawa zaidi ya Tarime na Karatu mwaka 2010. Umeona jinsi watu wa Kiteto mijini walivyobadilika na kutoa kura nyingi kwa upinzani kuliko CCM. Umeona jinsi ambavyo CCM ilibidi ipeleke nguvu yote.

Umeona yule mbunge wa Kiteto jinsi ambavyo anazomewa hivi sasa akipita kule. Sasa jua kwamba hataweza hayo nchi nzima, by election ni tofauti na election nchi nzima.

Halafu, kura za upinzani sivyo kama unavyoziona kwenye matokeo- CCM walijiokotea kura nyingi tu kama sio kuiba, tazama matokeo ya udiwani na ubunge. Utakufata maeneo mengi sasa CHADEMA haikuwa na wagombea hivyo hapakuwa na mtu wa kulinda kura ama palikuwa na wagombea dhaifu kupindukia ambao hawakuwa na mawakala.

Lakini 2010 kwa muamka uliokuwepo hali itakuwa tofauti CCM itabanwa kila mahali. Pia jiulize 2005 CHADEMA ilikuwaje? Iliingia ikiwa haina nguvu, hata uchaguzi wa 2004 imeshinda vijiji na mitaa michache sana. Sasa subiri uone mwaka 2009 kabla ya kumaliza kazi 2010. CHADEMA kabla ya Mbowe kugombea Urais ilikuwa ni chama cha kawaida sana.Urais umesaidia sana kukiamsha chama.

Mwaka 2003 CHADEMA haikuwa ikijadiliwa kama hivi, lakini sasa tunaanza kujadili toka 2008 kuhusu mgombea wa CHADEMA wa mwaka 2010 hii inamaanisha kuwa kuna watu wanafanya maamuzi leo ya kumpigia mgombea wa CHADEMA tofauti na Mbowe alivyoibuka kwa ghafla tu wakati wa uchaguzi 2010. Sasa Mbowe, Dr Slaa na wengine kama wanataka kugombea uchaguzi 2010 wataanza kuaandaa mazingira mapema kabla ya 2010 ikiwemo kujenga mtandao wa chama nchi nzima.

Sasa hiki ndicho kinachokuuma Kubwa Jinga Jinga, Chama Cha Mafisadi kuondoka katika Urais.

Hebu angalia haya matokeo ya Urais hapa linganisha na mwaka 2000 utoana jinsi ambavyo kuna maeneo yamebadilika ghafla ya kupigia upinzani na mengi ya majimbo hayo sio ya Kilimanjaro kabisa:
http://www.chadema.net/uchaguzi/matokeo/urais_1.php

Halafu urudi tena

Asha
 
Ingawa hii pia imejaa pumba, lakini nitakujibu sehemu isiyo pumba.

Hapa ni kutumia simple economics za wall street. You invest where you are likely to get returns/profit. Mwaka 2005, CHADEMA wali-invest pesa nyingi kwenye uraisi, wakashindwa lakini Mkenya mwenye kopta akatajirika. Wabumge wao walipewa only 7%. Kaborou kuona hivyo akakata deal na CCM akaachia ngazi. This is a warning, mambo yakiendelea hivi, sitashangaa Zitto naye akafanya kama Kaborou na ndio maana CCM wanampa vi-offer hivi sasa. I am even curious about hii trip yake. CCM wanaweza wakawa wameongea na balozi wa US na kumuunganishia kitrip.


Hapa umethibitisha kweli wewe ni Kubwa Jinga Jinga, na kwa kweli sasa umeanza kujishushia hadhi yako ya uchangiaji humu. Nilisema awali kuwa wewe ni mtu wa propaganda za Chama Cha Mafisadi unayejifanya uko neutral na kuwaponda kidogo mafisadi wenzio ni kuwachafua wapinzani-UKANIBISHIA. Sasa hebu rudia mwenyewe kusoma upupu ulioandika(Neno UPUPU-umelitumia mwenyewe kukwepa kujibu hoja za Mwafrika wa Kike).

Kabarou hajahama kwa kuwa CHADEMA imetumia hela kwenye helikopta. Kaborou mwenyewe alihama kwa kusema kuwa ameridhishwa na CCM chini ya Kikwete. Lakini ukweli ni kuwa alihama kwa kuwa alishindwa ubunge na Chama CHa Mafisadi kikamuahidi ubunge wa Afrika Mashariki. Sasa kwako hili mentality hii ya kifisadi ya Kaborou na uamuzi CCM wa kuhonga wapinzani ni jambo la kuchekelea. Lakini ujue kwamba mikakati ya CHADEMA ya 2005 imesaidia CHADEMA kuongeza kura zaidi za Ubunge kwenye Mkoa wa Kigoma ukilinagnisha na mwaka 2005.

http://www.chadema.net/uchaguzi/matokeo/kigoma_1.php

Imesaidia pia CHADEMA kupata kura za Urais kule. Na Kigoma Mjini, pamoja na kuwa CHADEMA ilishindwa Ubunge, bado ilishinda madiwani wengi na hatimaye kuendelea kuwa chama tawala kwenye halmashauri. Hii inadhihirisha kuwa tatizo pale lilikuwa kaborou mwenyewe sio CHADEMA.

Hilo la Zitto umeanza kuzusha, CCM inawezaje kuwaagiza US State Department imachague Zitto? Na hata kama ingekuwa kweli, Zitto atajuaje kwamba CCM ndio imemchagua wakati ambapo ni Wamarekani ndio wamempeleka? Walau ungesema kwamba wamarekani wanataka wame vi offer ili awe Mbunge wa Marekani ungeeleweka, lakini Wamerekani kumpa vi-offer ili awe Mbunge Wa CCM imedhihirisha uwezo wako mdogo wa kufikiri!

Sasa jua hawa wamerekani wanawachagua hawa vijana wa CHADEMA kwa capacity zao, hebu soma hapa maelezo ya kwanini Mnyika alichaguliwa wenye ziara kama hiyo:
http://www.chadema.net/habari/misc/misc_9.html

Wabunge walipewa 7% kwa kuwa CHADEMA ilimamisha wabunge wachache sana, kati ya wabunge zaidi ya 200 CHADEMA ilikuwa na wagombea 100+ hii inamaanisha kwamba toka wakati uchaguzi unaanza CHADEMA ilishaachia takribani 50% katika ubunge. Hata katika hiyo 50% ambayo wamesimamisha bado 3o% ya wagombea walikuwa wamejaza tu nafasi. Ukiangalia matokeo yao hapa utaona 10-20% ndio walikuwa wagombea wa kweli. Hii ni kwa kuwa 2005 chama hakikuwa kikubwa sana. Sasa subiri, wagombea wengi wameshaanza kujitokeza kuanzia 2006 na hasa 2008 na wameanza kupalilia maeneo. Tena wengine wamejitaja kabisa humu JF ni wanachama wenzetu humu, wenye hoja makini.

Asha
 
Kikwete alijulikana tokea awali kuwa hafai. Kama isingekuwa wana mtandao na msaada wa Mkapa, labda tungekuwa na Salm au Prof. Hata utumishi walishamshauri Mkapa kumuondoa JK MOFA, Mkapa akafyata. Ndio maana JK alipoingia tu akawatimua utumishi.

Ona Kubwa Jinga Jinga linavyojichanganya. Sasa kama uyasemayo unayaamini kwanini unataka Kikwete arudi tena 2010? Sio unajua kwa mtindo wa Chama Cha Mafisadi wa kuachiana terms mbili Salim na Mwandosya hawatagombea?

Je, wewe ni sehemu ya mafisadi wanaotaka watanzania waendelea kubeba mzigo wa ufisadi kwa miaka mingine 5 baada ya 2010? Go away with your Kikwete please. I use to luv him in 2005 to 2006. Now he is a crap. Mchukue ukanywe naye chai

Asha
 
Mkuu FMES et al,
Nakubaliana na wewe kuwa bila kujaribu huwezi kujua matokeo. Lakini ni vema kutumia uzoefu wa awali na data zilizopo kujaribu kuangalia future (forecasting) na sio kufanya mambo kienyeji-enyeji au kwa jazba kama watu wasioenda shule au kwa ushabiki kama Mwafrika wa Kike na bibie Asha.

URAISI
Katika uchaguzi uliopita, Kikwete alipata 80.3% (9,123,952), Lipumba 11.7% (1,327,125) na Mbowe alipata 5.9% (668,756). Kwa Chadema ni mikoa 4 ambayo walipata zaidi ya 10%, Kilimanjaro, Arusha, Mara na Manyara. Kigoma walikaribia kidogo na kupata 9.4%. Kilimanjaro peke yake ndio walipata zaidi ya 20% (ambayo ilikuwa 20.6%). Kwenye hizo kura alizopata Mbowe, karibu 40% zimetoka mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Mara with Kilimanjaro having almost 25%. Kwa hiyo kwa mtu mwenye akili yake, hata ukiweka factor za EPA, Chenge, Richmond, Mkapa n.k., unless kama JK naye akaguswa moja kwa moja kama Chenge, sidhani kama huku kuzomea kunakoongelewa kuna ukubwa wa kutosha kubadilisha mawazo ya hata say 20% ya waliompigia JK kura. Tusisahau pia kuwa, hawa wanaojiuzulu bado waTZ wengi wanaona kama vile Kikwete ndie anayewashughulikia.

Unaweza kukagua matokeo ya uchagusi kwenye attachment, Nimeyatoa NEC website au www ya Chadema
To be Contd.....



Wewe unamlaumu Mbowe na CHADEMA kwa kutumia milioni 700(kati ya hizo milioni 200 kwa helikopta) na kupata kura hizo; unajua Lipumba na CUF walitumia kiasi gani kupata kura hizo? Si unakumbuka mwenyewe walisema wametumia takribani bilioni mbili?Hii ni sawa na milioni 2000. Sasa piga mahesabu, nani amemefanikiwa zaidi kwa fedha alizotumia.

Haya sasa sema Chama Cha Mafisadi kilitumia bei gani kutoka BOT, EPA nk kwenye hizo kampeni za 2005. Tshirt na Kofia pekee ziliwagharimu bilioni 20(milioni 20,000). Si ajabu nikaambiwa walitumia bilioni 200 kwenye zile kampeni kwa ujumla. Si ajabu kwa kuwa najua majimbo ambayo jimbo moja ilitumika bilioni 1(milioni 1000) Eti 'kulikomboa'. Sasa hao nao waliotumia mapesa yote hayo wakapata 80% nao utawesemaje?

Na kwa kuwa hawakufanya 'uamuzi wa kijinga' wa kutumia helikopta kama CHADEMA kwanini wasingepata 100% kwa mapesa yote hayo?


Soma tena nilichokwambia mwanzo: Hoja yako haina uzito. Mrema alipata kura hizo wakati huo kwa kuwa CCM ilikuwa haijajiandaa kikamilifu kuiba na kulikuwa na wave kubwa ya upinzani nchi nzima. Mwaka 2000 Mkapa alikuwa amejizatiti wakati huo huo NCCR ilikuwa imeanguka, mwaka 2005 kulikuwa na ujio wa Kikwete kama Tumaini lililorejea wakati huo huo TLP na CUF zilikuwa zinaelekea kushuka.

Mwaka 2010 Kikwete atakuwa ameporomoka wakati huo huo hamasa ya upinzani na CHADEMA inazidi kuendelea nchi nzima na kuna ushirikiano wa vyama. Ufisadi umetamalaki na watanzania wameelewa zaidi. Sasa unategemea nini?

Siasa ni kitu cha ajabu, lolote laweza kutokea wakati wowote. Kwa hiyo usijidanyanye eti kwa kuwa Kikwete amepata 80 ya kura upinzani 20 basi kibao hakiwezi kugeuka upinzani ukapata 80 Kikwete 20!

Nikupe mfano mdogo tu, hebu angalia matokeo ya Urais Tarime na Karatu mwaka 2000 halafu angalia yalivyokuwa ghafla mwaka 2005 mpaka Mbowe amepata 30-40 percent! Kutokana na ufisadi uliokithiri, sitashangaa kama maeneo yote yakawa zaidi ya Tarime na Karatu mwaka 2010.

Umeona jinsi watu wa Kiteto mijini walivyobadilika na kutoa kura nyingi kwa upinzani kuliko CCM. Umeona jinsi ambavyo CCM ilibidi ipeleke nguvu yote. Umeona yule mbunge wa Kiteto jinsi ambavyo anazomewa hivi sasa akipita kule. Sasa jua kwamba hataweza hayo nchi nzima, by election ni tofauti na election nchi nzima.

Halafu, kura za upinzani sivyo kama unavyoziona kwenye matokeo- CCM walijiokotea kura nyingi tu kama sio kuiba, tazama matokeo ya udiwani na ubunge.

Utakufata maeneo mengi sasa CHADEMA haikuwa na wagombea hivyo hapakuwa na mtu wa kulinda kura ama palikuwa na wagombea dhaifu kupindukia ambao hawakuwa na mawakala. Lakini 2010 kwa muamka uliokuwepo hali itakuwa tofauti CCM itabanwa kila mahali. Pia jiulize 2005 CHADEMA ilikuwaje?

Iliingia ikiwa haina nguvu, hata uchaguzi wa 2004 imeshinda vijiji na mitaa michache sana. Sasa subiri uone mwaka 2009 kabla ya kumaliza kazi 2010. CHADEMA kabla ya Mbowe kugombea Urais ilikuwa ni chama cha kawaida sana.Urais umesaidia sana kukiamsha chama.

Mwaka 2003 CHADEMA haikuwa ikijadiliwa kama hivi, lakini sasa tunaanza kujadili toka 2008 kuhusu mgombea wa CHADEMA wa mwaka 2010 hii inamaanisha kuwa kuna watu wanafanya maamuzi leo ya kumpigia mgombea wa CHADEMA tofauti na Mbowe alivyoibuka kwa ghafla tu wakati wa uchaguzi 2010.

Sasa Mbowe, Dr Slaa na wengine kama wanataka kugombea uchaguzi 2010 wataanza kuaandaa mazingira mapema kabla ya 2010 ikiwemo kujenga mtandao wa chama nchi nzima.

Sasa hiki ndicho kinachokuuma Kubwa Jinga Jinga, Chama Cha Mafisadi kuondoka katika Urais.

Hebu angalia haya matokeo ya Urais hapa linganisha na mwaka 2000 utoana jinsi ambavyo kuna maeneo yamebadilika ghafla ya kupigia upinzani na mengi ya majimbo hayo sio ya Kilimanjaro kabisa:
http://www.chadema.net/uchaguzi/matokeo/urais_1.php

Halafu urudi tena

Asha
 
Back
Top Bottom