The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
GQ,

viongozi wa upinzani wameaanza long term plan na kama ulisoma ile thread ya Mnyika alikuwa anauliza maoni ya wana JF kwa chama ili ijulikane cha kufanya.

Kuna ile thread ya Rev Kishoka ya focus 2010 pia ilikuwa na very good insight ya what to do. Mambo mengine though yanafanyika in private na kuna wengi tu wamemtumia Mnyika mapendekezo yao kwenye PM.

Tusife moyo kwani nchi hii ni sisi ndio tutaingoa toka makucha ya mafisadi.

Kama ni hivyo MwK basi itakuwa vizuri sana kukabiliana na CCM na hii iende sambamba na kuwafahamisha Watanzania wote hasa wa vijijini juu ya uchafu unaoendelea kufanywa na CCM.
 
Nadhani wengi wetu mnalijua jina la Dr. Wilbroad Slaa Mbunge wa Karatu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA. Mimi ni Mtanzania ambaye sifungamani na chama chochote lakini mwenye kuamini kabisa ya kwamba, miongoni mwetu kuna Watanzania ambao wanaweza kuleta mabadiliko makubwa katika njanja mbalimbali kama za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Nchi yetu iko kwenye wakati mgumu sana hivi sasa na tunahijati kiongozi bora na sio bora kiongozi ambaye ataweza kuleta mabadiliko makubwa na ya kweli katika kuiendeleza nchi yetu kiuchumi.

Kama mjuavyo tatizo la ufisadi na rushwa limekithiri sana na imeshajionyesha wazi ya kwamba, Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameshindwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza majukumu yake aliyopewa na watanzania kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Naamini huu ni muda thabiti kabisa kumtafuta mtu atakayefaa kukichukua kiti chake itakapofika wakati wa Uchaguzi wa mwaka 2010. Binafsi ningependa Kikwete aondoke hata leo hii na arudi kijijini kwao Bagamoyo akalime Mananasi yake na huku akiendelea kujichekesha mbele ya ndugu zake. Naamini kabisa Dr. Slaa ndio mtu anaefaa kuwa Rais wa nchi yetu na mwenye uwezo mkubwa wa kulianzisha gurudumu la maendeleo nchini. Mimi niko tayari kulipia gharama zote za kutengeneza tovuti ya Dr. Slaa na kulipia hosting charges kutoka hivi sasa mpaka wakati wa uchaguzi mwaka 2010. Kwa hiyo ningeomba watanzania wenzangu tumhamasishe Dr. Slaa agombee hiki kiti cha Urais mwaka 2010. Tumebakisha miaka miwili na nadhani huu ni muda muafaka kuanza kujiandaa ili kuhakikisha Kikwete na CCM hawarudi tena kwenye uongozi.

Ahsanteni.

(Haya ni maoni yangu binafsi hayaingiliani kabisa na maamuzi ya CHADEMA) www.drwilbroadslaa2010.com

kwanini asiwe Zitto au Mbowe akaja kwa mara pili?
 
Geeque,

Leo ni 25/04/2008. Bado hapaonekani dalili zozote kwamba wapinzani wana(me)jiandaa kuikabili CCM hapo 2010.

Mawazo mengi na mazuri yamekwishachambuliwa hapa JF, katika mjadala huu, na ule wa Rev. Kishoka unaozungumzia kujiandaa kwa 2010.

Mimi ninapendekeza, kama inawezekana, (kwa hisani ya Invisible na wenzake) nakala za mijadala yote hii miwili, au zaidi ipelekwe kwenye ofisi za vyama vya upinzani ili yaliyomo humu yajadiliwe na kuchambuliwa huko na wanachama wao.

Zaidi ya hivyo, tujiandae tu kuendelea na CCM yetu na uozo wote tunaoupigia kelele hapa.


Mkuu Kalamu,

Conclusion yako ni nzuri ingawa bado wale walio na ushabiki wa kivyama badala ya kudadisi mielekeo ya matukio, bado hawataridhika nayo. It is time now for Chadema, NCCR, TLP, CUF & even UDP and other small parties, kuunganisha nguvu zao, kuondoa dosari ndani yao na kuanza kufanya kazi kwa pamoja kama chama kimoja ili wananchi wawaamini na kuelewa wanachopigania katika umoja wao.

Bila ya hivyo wasitegemee watu wenye akili zao, no matter how ugly CCM looks like, wata-i-dampo CCM na kuwaamini Chadema, TLP, CUF n.k. kuwa watakuwa tofauti, hasa ukitilia maanani kuwa, wao nao wana dosari ambazo tayari zimo vichwani mwa baadhi ya wananchi.
 
Sawa sawa mkuu, hapa tupo ukurasa mmoja, kwamba tatizo lililopo kwa upinzani ni muungano, wakiungana na kuwapa wananchi chaguo la either CCM, au Dr. Slaaa basi kuna uwezekano mkubwa sana akafanya vizuri sana, kuliko akigombea kutoka chama kimoja cha upinzani. Hapa tupo wote the same page!


Mkuu FMES,

Hayo maneno ndio ya kuhimiza humu mtandoni. Wakiungana pia watapunguza gharama zinasojirudia katika kila chama.
 
Mkuu Kalamu,
Conclusion yako ni nzuri ingawa bado wale walio na ushabiki wa kivyama badala ya kudadisi mielekeo ya matukio, bado hawataridhika nayo. It is time now for Chadema, NCCR, TLP, CUF & even UDP and other small parties, kuunganisha nguvu zao, kuondoa dosari ndani yao na kuanza kufanya kazi kwa pamoja kama chama kimoja ili wananchi wawaamini na kuelewa wanachopigania katika umoja wao. Bila ya hivyo wasitegemee watu wenye akili zao, no matter how ugly CCM looks like, wata-i-dampo CCM na kuwaamini Chadema, TLP, CUF n.k. kuwa watakuwa tofauti, hasa ukitilia maanani kuwa, wao nao wana dosari ambazo tayari zimo vichwani mwa baadhi ya wananchi.

Angalau sasa unabadili tone na hupingi suala la CHADEMA au upinzani kugombea nafasi ya uraisi mwaka 2010. Punguza chuki za kidini na kikabila na utaishi maisha marefu.
 
Angalau sasa unabadili tone na hupingi suala la CHADEMA au upinzani kugombea nafasi ya uraisi mwaka 2010. Punguza chuki za kidini na kikabila na utaishi maisha marefu.

Mwafrika wK,

You seem to be angry each time you read my postings and causes your IQ to shoot down to earth. My position is always very clear and never change, read my first posting here. It is for you to adjust to realities that criticism is not enmity. I told your buddy Asha that when angry she should count to ten before posting anything, but if very angry, she should count to a thousand.

I would advise you to count to at least two thousands before responding to any of my comments. You tend to lose so much of your wits.
 
Hapa umethibitisha kweli wewe ni Kubwa Jinga Jinga, na kwa kweli sasa umeanza kujishushia hadhi yako ya uchangiaji humu. Nilisema awali kuwa wewe ni mtu wa propaganda za Chama Cha Mafisadi unayejifanya uko neutral na kuwaponda kidogo mafisadi wenzio ni kuwachafua wapinzani-UKANIBISHIA. Sasa hebu rudia mwenyewe kusoma upupu ulioandika(Neno UPUPU-umelitumia mwenyewe kukwepa kujibu hoja za Mwafrika wa Kike).

Kabarou hajahama kwa kuwa CHADEMA imetumia hela kwenye helikopta. Kaborou mwenyewe alihama kwa kusema kuwa ameridhishwa na CCM chini ya Kikwete. Lakini ukweli ni kuwa alihama kwa kuwa alishindwa ubunge na Chama CHa Mafisadi kikamuahidi ubunge wa Afrika Mashariki. Sasa kwako hili mentality hii ya kifisadi ya Kaborou na uamuzi CCM wa kuhonga wapinzani ni jambo la kuchekelea. Lakini ujue kwamba mikakati ya CHADEMA ya 2005 imesaidia CHADEMA kuongeza kura zaidi za Ubunge kwenye Mkoa wa Kigoma ukilinagnisha na mwaka 2005.

http://www.chadema.net/uchaguzi/matokeo/kigoma_1.php

Imesaidia pia CHADEMA kupata kura za Urais kule. Na Kigoma Mjini, pamoja na kuwa CHADEMA ilishindwa Ubunge, bado ilishinda madiwani wengi na hatimaye kuendelea kuwa chama tawala kwenye halmashauri. Hii inadhihirisha kuwa tatizo pale lilikuwa kaborou mwenyewe sio CHADEMA.

Hilo la Zitto umeanza kuzusha, CCM inawezaje kuwaagiza US State Department imachague Zitto? Na hata kama ingekuwa kweli, Zitto atajuaje kwamba CCM ndio imemchagua wakati ambapo ni Wamarekani ndio wamempeleka? Walau ungesema kwamba wamarekani wanataka wame vi offer ili awe Mbunge wa Marekani ungeeleweka, lakini Wamerekani kumpa vi-offer ili awe Mbunge Wa CCM imedhihirisha uwezo wako mdogo wa kufikiri!

Sasa jua hawa wamerekani wanawachagua hawa vijana wa CHADEMA kwa capacity zao, hebu soma hapa maelezo ya kwanini Mnyika alichaguliwa wenye ziara kama hiyo:
http://www.chadema.net/habari/misc/misc_9.html

Wabunge walipewa 7% kwa kuwa CHADEMA ilimamisha wabunge wachache sana, kati ya wabunge zaidi ya 200 CHADEMA ilikuwa na wagombea 100+ hii inamaanisha kwamba toka wakati uchaguzi unaanza CHADEMA ilishaachia takribani 50% katika ubunge. Hata katika hiyo 50% ambayo wamesimamisha bado 3o% ya wagombea walikuwa wamejaza tu nafasi. Ukiangalia matokeo yao hapa utaona 10-20% ndio walikuwa wagombea wa kweli. Hii ni kwa kuwa 2005 chama hakikuwa kikubwa sana. Sasa subiri, wagombea wengi wameshaanza kujitokeza kuanzia 2006 na hasa 2008 na wameanza kupalilia maeneo. Tena wengine wamejitaja kabisa humu JF ni wanachama wenzetu humu, wenye hoja makini.

Asha

My Dear Kubwa Jinga

Any comment on this?

Asha
 
Hoja yako haina uzito. Mrema alipata kura hizo wakati huo kwa kuwa CCM ilikuwa haijajiandaa kikamilifu kuiba na kulikuwa na wave kubwa ya upinzani nchi nzima. Mwaka 2000 Mkapa alikuwa amejizatiti wakati huo huo NCCR ilikuwa imeanguka, mwaka 2005 kulikuwa na ujio wa Kikwete kama Tumaini lililorejea wakati huo huo TLP na CUF zilikuwa zinaelekea kushuka. Mwaka 2010 Kikwete atakuwa ameporomoka wakati huo huo hamasa ya upinzani na CHADEMA inazidi kuendelea nchi nzima na kuna ushirikiano wa vyama. Ufisadi umetamalaki na watanzania wameelewa zaidi. Sasa unategemea nini?

Siasa ni kitu cha ajabu, lolote laweza kutokea wakati wowote. Kwa hiyo usijidanyanye eti kwa kuwa Kikwete amepata 80 ya kura upinzani 20 basi kibao hakiwezi kugeuka upinzani ukapata 80 Kikwete 20!

Nikupe mfano mdogo tu, hebu angalia matokeo ya Urais Tarime na Karatu mwaka 2000 halafu angalia yalivyokuwa ghafla mwaka 2005 mpaka Mbowe amepata 30-40 percent! Kutokana na ufisadi uliokithiri, sitashangaa kama maeneo yote yakawa zaidi ya Tarime na Karatu mwaka 2010. Umeona jinsi watu wa Kiteto mijini walivyobadilika na kutoa kura nyingi kwa upinzani kuliko CCM. Umeona jinsi ambavyo CCM ilibidi ipeleke nguvu yote. Umeona yule mbunge wa Kiteto jinsi ambavyo anazomewa hivi sasa akipita kule. Sasa jua kwamba hataweza hayo nchi nzima, by election ni tofauti na election nchi nzima.

Halafu, kura za upinzani sivyo kama unavyoziona kwenye matokeo- CCM walijiokotea kura nyingi tu kama sio kuiba, tazama matokeo ya udiwani na ubunge. Utakufata maeneo mengi sasa CHADEMA haikuwa na wagombea hivyo hapakuwa na mtu wa kulinda kura ama palikuwa na wagombea dhaifu kupindukia ambao hawakuwa na mawakala. Lakini 2010 kwa muamka uliokuwepo hali itakuwa tofauti CCM itabanwa kila mahali. Pia jiulize 2005 CHADEMA ilikuwaje? Iliingia ikiwa haina nguvu, hata uchaguzi wa 2004 imeshinda vijiji na mitaa michache sana. Sasa subiri uone mwaka 2009 kabla ya kumaliza kazi 2010. CHADEMA kabla ya Mbowe kugombea Urais ilikuwa ni chama cha kawaida sana.Urais umesaidia sana kukiamsha chama. Mwaka 2003 CHADEMA haikuwa ikijadiliwa kama hivi, lakini sasa tunaanza kujadili toka 2008 kuhusu mgombea wa CHADEMA wa mwaka 2010 hii inamaanisha kuwa kuna watu wanafanya maamuzi leo ya kumpigia mgombea wa CHADEMA tofauti na Mbowe alivyoibuka kwa ghafla tu wakati wa uchaguzi 2010. Sasa Mbowe, Dr Slaa na wengine kama wanataka kugombea uchaguzi 2010 wataanza kuaandaa mazingira mapema kabla ya 2010 ikiwemo kujenga mtandao wa chama nchi nzima.

Sasa hiki ndicho kinachokuuma Kubwa Jinga Jinga, Chama Cha Mafisadi kuondoka katika Urais.

Hebu angalia haya matokeo ya Urais hapa linganisha na mwaka 2000 utoana jinsi ambavyo kuna maeneo yamebadilika ghafla ya kupigia upinzani na mengi ya majimbo hayo sio ya Kilimanjaro kabisa:
http://www.chadema.net/uchaguzi/matokeo/urais_1.php

Halafu urudi tena

Asha

Do you have any word on this as well? If not ask Mugongo Mugongo to come up

Asha
 
Ona Kubwa Jinga Jinga linavyojichanganya. Sasa kama uyasemayo unayaamini kwanini unataka Kikwete arudi tena 2010? Sio unajua kwa mtindo wa Chama Cha Mafisadi wa kuachiana terms mbili Salim na Mwandosya hawatagombea? Je, wewe ni sehemu ya mafisadi wanaotaka watanzania waendelea kubeba mzigo wa ufisadi kwa miaka mingine 5 baada ya 2010? Go away with your Kikwete please. I use to luv him in 2005 to 2006. Now he is a crap. Mchukue ukanywe naye chai

Asha

Do you agree with me on this? You seem to skip my post jamani. I am just reminding you to respond to the issues I have raised.

Asha
 
We Kubwa Jinga Jinga unakaa nchi gani? We hujui kwamba haya matokeo ya Ubunge ni pamoja na uwizi waliufanya kule kwa Balozi Ngaiza,Mbogoro, Pesha nk(CHADEMA); Lwakatare CUF nk, Lema(TLP Arusha) nk? Hivi CCM wasingeiba wangepoteza majimbo mangapi kwa staili hii?

Umetoa mfano wa Mnyika wa CHADEMA, si umeona hapa jinsi ambayo aliyalalamikia matokeo yake kwamba yamepikwa?
"Kwa hali iliyodhihirisha wazi kuwa matokeo yalipikwa, waliopiga kura za Ubunge walikuwa 185,684 wakati waliopiga kura za Rais walikuwa 152,525 na hivyo kufanya tofauti ya kura za Ubunge na urais kufikia 33,159. Katika hali ya kawaida na katika uchaguzi uliofanyika kwa wakati mmoja ilikuwa ni vigumu kwa tofauti kubwa ya kura kiasi hiki. Na hata kama wananchi wangekuwa hawapendi kupiga kura za rais kwa kuwa mpiga kura alikuwa akipewa karatasi zote tatu kura hizi zilipaswa kuwepo katika kura zilizoharibika kitu ambacho hakikutokea.
Kimsingi, hujuma za kimfumo na kimkakati za chama tawala ndiyo hasa vilivyofanya uchaguzi kutokuwa huru na haki. Kabla ya uchaguzi wajumbe wa nyumba kumi waliandikisha kadi za wapiga kura kwa lengo la kuwakosesha kupiga kura wale walioelekea kupigia kura upinzani na pia kuweza kuwapa rushwa wengine ili kupigia CCM.Wananchi wengi walizuiwa kupiga kura licha ya kuwa na kadi kutokana na ama majina yao kutoonekana kwenye orodha au kuwa tofauti na kwenye daftari. Kulikuwa na kampeni za vitisho kwa wapiga kura hususani katika kata za vijijini. Wananchi wengi walihongwa kukipigia kura chama tawala – hii ni pamoja na wengi kujifanya hawajui kusoma na kuandika ingawa baadhi yao vitambulisho vyao vya kupigia kura vilionekana kuwa na saini. Kulikuwa na mapungufu kadhaa katika mpangilio na idadi ya vituo vya kupigia kura. Halikadhalika, kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa kanuni na sheria katika ujumlishaji wa kura za ubunge. Kwa kiasi kidogo mtandao hafifu wa chama katika maeneo machache na udhaifu wa baadhi ya mawakala navyo vilichangia kushindwa katika vituo vichache ambavyo visingeathiri matokeo kwa kiasi kikubwa kwa ujumla. Na mwisho matokeo ya ubunge jimbo la Ubungo yakatangazwa kwa shuruti bila kutangaza na kujumlisha kwa pamoja matokeo ya kituo hadi kituo hali iliyoashiria kuwa matokeo ya Ubunge yalikuwa na utata. Kutangaza huku kwa nguvu ilikuwa ni mkakati wa kutaka matokeo hayo yasihojiwe kama ilivyokuwa katika matokeo ya urais ambayo yalichelewa kutangazwa kutokana na kukutwa na mapungufu mengi. Kwa hali iliyodhihirisha wazi kuwa matokeo yalipikwa, waliopiga kura za Ubunge walikuwa 185,684 wakati waliopiga kura za Rais walikuwa 152,525 na hivyo kufanya tofauti ya kura za Ubunge na urais kufikia 33,159. Katika hali ya kawaida na katika uchaguzi uliofanyika kwa wakati mmoja ilikuwa ni vigumu kwa tofauti kubwa ya kura kiasi hiki. Na hata kama wananchi wangekuwa hawapendi kupiga kura za rais kwa kuwa mpiga kura alikuwa akipewa karatasi zote tatu kura hizi zilipaswa kuwepo katika kura zilizoharibika kitu ambacho hakikutokea.

http://www.chadema.net/hotuba/mnyika/hotuba_4.html

Lakini unadhani wapinzani watakubali tena kuibiwa 2010? Wewe badala ya kujadili jinsi ya watu kulinda hizo kura za Urais wewe kazi yako ni kusema kwama wasigombee, amakweli ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni

Asha

Come on guy! Kama kimeeleweka niambie tu adios, otherwise- tuliendeleze

Asha
 
Mwafrika wK,
You seem to be angry each time you read my postings and causes your IQ to shoot down to earth. My position is always very clear and never change, read my first posting here. It is for you to adjust to realities that criticism is not enmity. I told your buddy Asha that when angry she should count to ten before posting anything, but if very angry, she should count to a thousand. I would advise you to count to at least two thousands before responding to any of my comments. You tend to lose so much of your wits.


Is it a sign of being provoked to the extent that you degrade her that her IQ is down, or are you losing your wits as well? Have you counted up to ten thousand before writing this? I think you should count and rewrite. Just be sober, there is nothing personal.

The main mjadala was Dr Slaa for Urais 2010, lets get back to the talk...

Asha
 
Hapa umethibitisha kweli wewe ni Kubwa Jinga Jinga, na kwa kweli sasa umeanza kujishushia hadhi yako ya uchangiaji humu. Nilisema awali kuwa wewe ni mtu wa propaganda za Chama Cha Mafisadi unayejifanya uko neutral na kuwaponda kidogo mafisadi wenzio ni kuwachafua wapinzani-UKANIBISHIA. Sasa hebu rudia mwenyewe kusoma upupu ulioandika(Neno UPUPU-umelitumia mwenyewe kukwepa kujibu hoja za Mwafrika wa Kike).

Kabarou hajahama kwa kuwa CHADEMA imetumia hela kwenye helikopta. Kaborou mwenyewe alihama kwa kusema kuwa ameridhishwa na CCM chini ya Kikwete. Lakini ukweli ni kuwa alihama kwa kuwa alishindwa ubunge na Chama CHa Mafisadi kikamuahidi ubunge wa Afrika Mashariki. Sasa kwako hili mentality hii ya kifisadi ya Kaborou na uamuzi CCM wa kuhonga wapinzani ni jambo la kuchekelea. Lakini ujue kwamba mikakati ya CHADEMA ya 2005 imesaidia CHADEMA kuongeza kura zaidi za Ubunge kwenye Mkoa wa Kigoma ukilinagnisha na mwaka 2005.


Imesaidia pia CHADEMA kupata kura za Urais kule. Na Kigoma Mjini, pamoja na kuwa CHADEMA ilishindwa Ubunge, bado ilishinda madiwani wengi na hatimaye kuendelea kuwa chama tawala kwenye halmashauri. Hii inadhihirisha kuwa tatizo pale lilikuwa kaborou mwenyewe sio CHADEMA.

Hilo la Zitto umeanza kuzusha, CCM inawezaje kuwaagiza US State Department imachague Zitto? Na hata kama ingekuwa kweli, Zitto atajuaje kwamba CCM ndio imemchagua wakati ambapo ni Wamarekani ndio wamempeleka? Walau ungesema kwamba wamarekani wanataka wame vi offer ili awe Mbunge wa Marekani ungeeleweka, lakini Wamerekani kumpa vi-offer ili awe Mbunge Wa CCM imedhihirisha uwezo wako mdogo wa kufikiri!

Sasa jua hawa wamerekani wanawachagua hawa vijana wa CHADEMA kwa capacity zao, hebu soma hapa maelezo ya kwanini Mnyika alichaguliwa wenye ziara kama hiyo:

Wabunge walipewa 7% kwa kuwa CHADEMA ilimamisha wabunge wachache sana, kati ya wabunge zaidi ya 200 CHADEMA ilikuwa na wagombea 100+ hii inamaanisha kwamba toka wakati uchaguzi unaanza CHADEMA ilishaachia takribani 50% katika ubunge. Hata katika hiyo 50% ambayo wamesimamisha bado 3o% ya wagombea walikuwa wamejaza tu nafasi. Ukiangalia matokeo yao hapa utaona 10-20% ndio walikuwa wagombea wa kweli. Hii ni kwa kuwa 2005 chama hakikuwa kikubwa sana. Sasa subiri, wagombea wengi wameshaanza kujitokeza kuanzia 2006 na hasa 2008 na wameanza kupalilia maeneo. Tena wengine wamejitaja kabisa humu JF ni wanachama wenzetu humu, wenye hoja makini.

Asha



My Dear Kubwa Jinga

Any comment on this?

Asha

Asha, No comments. Sikuzijibu postings zako maana zimejaa speculations na ushabiki wakati mimi napendelea kufanyia kazi facts. Ndio maana sikuona sababu ya kupoteza muda kujibu ushabiki.

Hii ni pamoja na hizo nyingine zilizofuata. Wakati tunajibizana hapa, sio ajabu Zitto akawa yupo nyumbani kwa balozi wa TZ, DC, kwa mwaliko wa maongezi ya 'kawaida'.
 
Do you agree with me on this? You seem to skip my post jamani. I am just reminding you to respond to the issues I have raised.

Asha

Yaah! Nazi-skip message ambazo ni miningless. Kikwete kurudi 2010 huwezi kuipinga hapa na ikawa hivyo.

Ukitaka asirudi shawishi wabunge wamuondoe kabla ya 2010. Lakini uwezekano wa kurudi ni mkubwa whether unapenda au la.
 
Naamini kabisa Dr. Slaa ndio mtu anaefaa kuwa Rais wa nchi yetu na mwenye uwezo mkubwa wa kulianzisha gurudumu la maendeleo nchini. Mimi niko tayari kulipia gharama zote za kutengeneza tovuti ya Dr. Slaa na kulipia hosting charges kutoka hivi sasa mpaka wakati wa uchaguzi mwaka 2010. Kwa hiyo ningeomba watanzania wenzangu tumhamasishe Dr. Slaa agombee hiki kiti cha Urais mwaka 2010. Tumebakisha miaka miwili na nadhani huu ni muda muafaka kuanza kujiandaa ili kuhakikisha Kikwete na CCM hawarudi tena kwenye uongozi.

2ep51n4.jpg
 
Yaah! Nazi-skip message ambazo ni miningless. Kikwete kurudi 2010 huwezi kuipinga hapa na ikawa hivyo. Ukitaka asirudi shawishi wabunge wamuondoe kabla ya 2010. Lakini uwezekano wa kurudi ni mkubwa whether unapenda au la.

Silence means YES. Ok

Asha
 
Asha,
No comments. Sikuzijibu postings zako maana zimejaa speculations na ushabiki wakati mimi napendelea kufanyia kazi facts. Ndio maana sikuona sababu ya kupoteza muda kujibu ushabiki. Hii ni pamoja na hizo nyingine zilizofuata. Wakati tunajibizana hapa, sio ajabu Zitto akawa yupo nyumbani kwa balozi wa TZ, DC, kwa mwaliko wa maongezi ya 'kawaida'.

Wasomaji ndio waamuzi basi.

Hilo la Zitto mbona umezusha tena? Zitto mbona hayuko Washington wala New York leo? Ratiba yake ya wiki hii si imetangazwa? Sasa inamaana huyo balozi wa tanzania anapatikana kila state. Mbona unapenda propaganda wewe? Unataka tuamini kwamba Zitto wetu amenunuliwa? Hutafanikiwa kwa kweli.

Ni rahisi kusema tu, 'sijibu kwa kuwa simejaa speculations na ushabiki', kama ndio hivyo basi, kwa nini usizichane chane hoja kwa hoja kama wanavyofanya wakina mwanakijiji, Mkandara, FMES, Kitila na wengine ili nionekane bayana kama usemavyo?

Jamani si ukiri tu kwamba yamekushinda? Hii sio mchezo wa lazima kushinda jamani. Hapa tunatoa mawazo tu. Kama umeona mawazo yangu yamekushawishi au umeyaelewa si useme tu!

Asha
 
Kubwa Jinga

Mi si mtaalamu wa kuweka hizo links, kwa hiyo ambayo imekataa kufungua-nilidhamiria kuweka links ya kwenye thread hii- http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=12123 eneo ambalo nilianza kukuuliza maswali ambayo mpaka sasa hujanijibu. Hebu ingia kwanza huko ujibu maswali yangu.

Kuhusiana na majibu ya Zitto na Mnyika kuhusu Viti Maalumu sijaweka link yoyote, nimekwambia ufanye searching. Lakini kama hujui pia, hebu mwambie Game Theory aweke hapa link za thread zote ambazo Zitto na Mnyika wamezungumzia suala la Viti Maalum kuanzia kwenye “Mbowe Vs Chifupa”, “The only thing to fear”, “Focus 2010”, “CHADEMA Must reform” na nyingine nyingi tu. Mi niliwahi kufanyiwa searching hapa nikaona kuwa suala hili Zitto na Mnyika wamelitolea maelezo hapa vizuri kabisa mwaka 2006, 2007 na hata 2008 mpaka wanachama wengine humu wakaridhika

Nijibu pia jamani, nimeuliza swali kama uliwahi kufukuzwa CUF kutokana na tabia yako ya kuwabagua watu kutokana na dini na makabila yao.

Asha
 
Back
Top Bottom