The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
I agree. Yeyote yule, au the likeness ya Mrema inafaa, lazima mtu aje na ukichaa(sina maana ya ugonjwa). Tanzania hii haiendi popote mpaka aje mtu atayekuja (to say the least) kutandika viboko wabadhirifu makazini na kuuwa wahujumu uchumi! I am for a person with Machiavelli style! Other than that...ni maikidamakida tu!

Duh!!!
Leo Mrema anakumbukwa lakini is too late hawezi kuwa Rais .Alipotaka watu mlisema hana shule , anakurupuka, ana hasira nk .Mungu wangu weeeeeeeee.

Huyu Mathayo ama Kamala ama Masha ama Malima hawa wawe ma Rais wana tofauti na huyu JK ? Wamefanya nini tofauti na JK kwamba niwe na matumaini ?

Wewe Dar Es Salaam usitake kila saa utajwe kwa ubaya .Ongea hata moja la maana basi watu wasema leo kajitahidi kusema .Au ndiyo Kada Mpinzani smell ?
 
Warioba aendelee kula pensheni yake ya WM... Inatosha!
JK is the right man at the right time in the right place... wenye chuki mjinyonge... Chini ya JK GDP imepanda na kufikia 6.2% katika 2007 na this year itafika 7.3%. Mwendo mdundo hadi 2015

Kijana naona na ww ni fisadi kukua kwa uchumi kwa 6.2% kunaweza kuwa ni ktk makaratasi tu.inabidi tuangalie macro economic indicators zingine price levels, general welfare of da people to mention but a few. vilevile ni jinsi gani ongezeko hilo la GDP linamsaidia mtu wa kawaida kama mfumuko wa bei ndio kama sasa hivi kwa kweli tunahitaji watendaji wengine ambao wako clear na wanachopaswa kufanywa.

Tukija ktk sual la warioba huyu jamaa hafai. kwanza alishawai kuwa waziri mkuu lazima tujiulize alifanya nini wakati wa kipindi chake.mungu atatusaidia tutapata mtu mwenye clarity of concepts ambaye atatuongoza kwenye policy mix zilizo sahihi kitu ambacho ahtuna sasa.

mtu ambaye ataweka vipaumbele ktk utekelezaji wa mjukumu ya serikali, kama mdau hapo juu alipodokeza kuwa na mapinduzi ya kilimo, mapinduzi ya viwanda, miundo mbinu n.k
 
Duh!!!
Leo Mrema anakumbukwa lakini is too late hawezi kuwa Rais .Alipotaka watu mlisema hana shule , anakurupuka, ana hasira nk .Mungu wangu weeeeeeeee.

Speak for yourself Sir !
 
Mambo mengi yaliyotokea mikononi mwa JK lakini ni matunda yaliyo pandikizwa wkipindi cha maraisi waliopita na haswa kipindi cha Mkapa.

Nadhani JK kama raisi ni mtu mpya kabisa na hatuwezi mshirikisha sana kwenye yaliyo toke a hivi punde kwani uraisi wake ni wa sasa na napo awali walikuwa maraisi wengine. Nadhani pia ni mapema sana kwa JK kubadilisha nchi ndani ya miaka miwili, anahitaji muda wa kutosha ili maamuzi yawe yaliyofanyiwa kazi na yakudumu.

Kwa sisi wenye familia ni kazi ngumu sana kubadilisha mazingira, mwenendo na jinsi anavyoishi binadamu hata katika familia ya watu wachache inatakiwa utayarishe kamkakati ili mabadiliko yawe shwari na ya mafanikio, SEMBUSE NCHI?

Pamoja na hayo utaratibu wa kumchagua raisi wa Tanzania na nchi nyingi duniani hau support kumbadilisha kabla ya mwisho wa kikomo cha vipindi vyake.

Hivyo inawezekana ikawa ngumu sana kumwondoa JK 2010 hata kama akimpatia DITO uwaziri mkuu labda.

CLOCK
 
Naomba nitoe hoja kwenye hii issue, nitawarudisha nyuma kidogo.

Huyu jamaa ameanzia mbali, attorney general, waziri..... lakini cha muhimu ni kuangalia amefanya nini mpaka sasa hivi sio urais peke yake.

Kumpiga madongo haisaidii. Tanzania or rather waTanzania tumefikia sehemu ya kuwa washabiki tu, someni habari mbalimbali hata kwenye hii forum, zote ni ushabiki mtupu. Kikwete hivi, Lowassa vile, mara Mwakyembe, ooh Mrema, jamani Zitto, sasa Bush, kesho Kenya... na tunajiita intellectuals! I wonder!!!

Nani anakumbuka kuwa alijiuzulu uwadhifa wa Uwaziri Mkuu? na kwa nini? Cabinet ilivunjwa na kuteuliwa upya

Hizo kashfa za hawa watu wote are they true or semi-fabricated? Mtu akikashfu upinzani si mzalendo, akikashfu chama tawala pia si mzalendo. Media ikisema imesema, hatujali kujua kama ukweli wote umesemwa.

Kama tunataka kuleta maendeleo inabidi tubadilishe mtazamo, tuache jazba

Nawasilisha
 
Yaani tunashindwa kuona ukweli? kwamba hakuna awamu iliyofichua mafisadi na kuonyesha nia ya kuwashughulikia kama hii ya nne.

Dar-es-salaam, awamu ya nne haijafichua fisadi hata mmoja ni sisi wananchi baada ya kupiga kelele weee basi ndio wanaamka,wana-act,kama sisi tukikaa kimya basi na wao kimyaa.

Yaani ni sawa na mbwa ambaye bwana wake asipokuwepo au hawako pamoja habweki lakini akimwona bwana wake tu anaaanza kubweka hata kama mgeni bwana wake kashamfungulia, sasa hapa swali linakuwa huyu mgeni angekuwa jambazi si inamaana mbwa asingebweka hadi jamaa anaondoka na tv?

Labda tunachoweza kusema katika awamu hii ya nne ni kwamba,tukipiga kelele sanaaaaaaaaaaaaaaa tunasikilizwa jamaa wanaona aibu wanafanyia kazi.

Kwa ufupi ni ngumu sana kufanya kazi na 70% ya wanasiasa ambao ni marafiki unaocheka nao kila siku kwani daima utawaonea aibu kuwakanya hata pale wanapokosea.Tunahitaji watu kama kina bingu wa mutharika, kwenye uongozi udikteta pia unatakiwa hasa kwenye maamuzi mazito ili mambo yaweze kwenda maneno bila actions hazitufikishi mbali.

Wee mtu gani tunakulazimisha kufua shati ulilovaa?kila tunapokuambia shati hilo chafu huko mgongoni tafadhali livue uliangalie vizuri hutaki, baadaye tunakulazimisha sana, unaamua kulivua na kuvaa lenye unafuu kidogo, halafu unaendelea kutulaumu "LAKINI SIKUPENDI KULIBADILI LILE SHATI,HIVI KWELI LILIKUWA CHAFU?ANYWAY,NIMEFANYA ILI KUWARIDHISHENI TU LAKINI SIKUWA TAYARI KULIVUA"
HIYO NDIYO AWAMU YA NNE.
 
Dar-es-salaam, awamu ya nne haijafichua fisadi hata mmoja ni sisi wananchi baada ya kupiga kelele weee basi ndio wanaamka,wana-act,kama sisi tukikaa kimya basi na wao kimyaa.Yaani ni sawa na mbwa ambaye bwana wake asipokuwepo au hawako pamoja habweki lakini akimwona bwana wake tu anaaanza kubweka hata kama mgeni bwana wake kashamfungulia,sasa hapa swali linakuwa huyu mgeni angekuwa jambazi si inamaana mbwa asingebweka hadi jamaa anaondoka na tv?Labda tunachoweza kusema katika awamu hii ya nne ni kwamba,tukipiga kelele sanaaaaaaaaaaaaaaa tunasikilizwa jamaa wanaona aibu wanafanyia kazi.
Kwa ufupi ni ngumu sana kufanya kazi na 70% ya wanasiasa ambao ni marafiki unaocheka nao kila siku kwani daima utawaonea aibu kuwakanya hata pale wanapokosea.Tunahitaji watu kama kina bingu wa mutharika,kwenye uongozi udikteta pia unatakiwa hasa kwenye maamuzi mazito ili mambo yaweze kwenda maneno bila actions hazitufikishi mbali.
Wee mtu gani tunakulazimisha kufua shati ulilovaa?kila tunapokuambia shati hilo chafu huko mgongoni tafadhali livue uliangalie vizuri hutaki,baadaye tunakulazimisha sana,unaamua kulivua na kuvaa lenye unafuu kidogo,halafu unaendelea kutulaumu "LAKINI SIKUPENDI KULIBADILI LILE SHATI,HIVI KWELI LILIKUWA CHAFU?ANYWAY,NIMEFANYA ILI KUWARIDHISHENI TU LAKINI SIKUWA TAYARI KULIVUA"
HIYO NDIYO AWAMU YA NNE.

debe tupu weeeeeeeee haliachi kupiga kelele!!!!
 
Ama kweli asie na macho haambiwi tazama na asie na masikio haambiwi sikia
 
Wapendwa mlipo jamvini tujadiliane masuala muhimu ya kitaifa anayopaswa kuyafanya na kuyachukulia umuhimu (priorities) Muungwana kabla ya uchaguzi wa 2010 mimi niliyoyaona ni haya:

1. Kusitisha mkataba wa TICS na kuandaa mkataba mpya wenye manufaa kwa Taifa.
2.kuuboresha mtihani wa darasa la nne wanafunzi wengi wapasi.
3.kuhakikisha barabara ya kati Singida-Manyoni-Dodoma inakamilika 2009 Dec
4.Daraja la Kigamboni linaanza kujegwa
5.Kupunguza kodi na kuongeza wigo pana zaidi wa mapato yatokanayo na kodi.

Tujadiliane
 
Kuhusu barabara kuna kipande cha kilometa 60 kwenye barabara iendayo mikoa ya Kusini. Sijui kama kimepata mkandarasi ( I assume the funds were there)

Pia, pesa za Millenium Challenge zitumike bila kuchelewa, kwani kazi ya ku appoint wakandarasi sioni ina haja gani ya kuchukua miaka miwili.
 
Kipande hicho kimeshapata mkandarasi ( Kharafi & sons) na ujenzi unaanza Terehe 1, Mwezi ujao
 
JK alitoa ahadi 60 critical kwenye kampeni zake; so far ameshatekeleza 8 tu tena partially, tunamsubiri!
 
JK alitoa ahadi 60 critical kwenye kampeni zake; so far ameshatekeleza 8 tu tena partially, tunamsubiri!

Kitila, can you please take trouble to mention them? Or you can just copy and paste them here if they are in electronic form.
 
Kitila, can you please take trouble to mention them? Or you can just copy and paste them here if they are in electronic form.

Wakati tunangoja Kitila aweke hapa mie nitaweka ya 6 kwamba issue ya BOT iwe na majibu sahihi wala si kucheza makidamakida.
 
bila kuwashughulikia kikamilifu mafisadi wa BOT, RICHMOND, ATCL nk atakuwa bado hajanishawishi.
 
bila kuwashughulikia kikamilifu mafisadi wa BOT, RICHMOND, ATCL nk atakuwa bado hajanishawishi.

Maongezi tu haya .Hawezi kuwagusa maana ni wenzake hawa na yeye ni mmoja wao .
 
Back
Top Bottom