The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Right to the point! Bila mikakati mathubuti, yatakuwa yale yale ya NARC baada ya kuibwaga KANU. Hakuna cha maana kimefanyika Kenya.

Yaleyale ya kudai talaka halafu unapata mume "bomu" kuliko wa awali!

Bahati mbaya mfano huu hauwezi kutumika katika suala la uongozi wa nchi, maana kwenye ndoa mtu anaweza kusema atabakia "single" kuliko kuolewa na mume "bomu". Kwenye nchi lazima uongozi uwepo.

Kabla hatujadhamiria kwa dhati kuiondoa CCM madarakani, lazima tutafakari kwa kina madaraka hayo tunataka kumpa nani? Kwa nafuu ipi aliyo nayo kulinganisha na CCM? Kabla ya kuipua chungu cha moto jikoni lazima uandae kwanza "kikalio", mahali pa kukiweka, vinginevyo utamwaga mboga yote na itakuwa hasara! Pengine kweli tumeichoka CCM, lakini hao wa kuwapa madaraka haya wako wapi?

Je hatuoni ni busara kuwajenga kwanza, wawepo wazuri na wa kutosha, na wenye uwezo na mtandao wa kitaifa na sura ya kitaifa, ndipo tuwape madaraka kwa kujiamini kabisa?
 
Mkatakati unaweza ukawa bora,ila wanaotaka kuufanikisha wakawa sio bora.Cha msingi ni kuwa na watendaji wanaofanya kazi kwa maslahi ya nchi,Watendaji waliotayari kukataa mabaya wanayoambiwa na wakubwa wao .rejea bwana githongo wa kenya aliyesimama hadharani na kusema Viongozi wanokula Rushwa.
 
Ni vipengele gani vya katiba vinahitajika kufanyiwa marekebisho kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2009 na Uchaguzi Mkuu 2010? kwa manufaa ya nani?
 
Turudi kwenye 2010, what is our analysis of majimbo ambayo ni sandakalawe? Katika viti 270+ (ondoa viti maalumu ambavyo ni kujaza chumba bila sababu) ni majimbo mangapi kukweli yanaweza kuchukulika na nguvu zetu zikahamia huko?


Tuwasikilize nyinyi wenyeji wa majimbo mbalimbali. Sisi tunayo tathmini yetu ya ndani ya wapi na wapi tuweke nguvu zaidi kwa nini; hii hatuwezi kuisema hadharani. Lakini ni wajibu wenu nyinyi wananchi kutoa maoni yenu na kujadili- wapi na wapi vyama viongeze nguvu, kwa nini na namna gani.

Tuko tayari kusikiliza na tukishawishika tunaweza kuboresha zaidi mikakati yetu. Tuendelee na mjadala
 
Ni vipengele gani vya katiba vinahitajika kufanyiwa marekebisho kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2009 na Uchaguzi Mkuu 2010? kwa manufaa ya nani?

Kwanza ieleweke wazi, kwa katiba yetu ilivyo na mapungufu mengi inahitajika katiba mpya- ambayo itaandaliwa pia kwa kuwashirikisha wananchi kikamilifu tofauti na katiba iliyoko sasa.

Lakini hata kama tunataka kufanya marekebisho tu kwa ajili ya kuboresha mfumo wa uchaguzi na kufanya chaguzi ziwe huru na haki. kwa maoni yangu yafuatayo yafanyike mwaka 2008.

1. Lazima uchaguzi wa serikali za mitaa uwe chini ya Tume ya uchaguzi badala ya hivi sasa ambapo uchaguzi huu upo chini ya serikali kuu! Haiwezekani serikali ya chama tawala ikajisimamia yenyewe katika uchaguzi. Rekebisho hili lazima lifanyike kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2009.

2. Tume ya uchaguzi iwe huru zaidi- watendaji wake lazima wawe na security of tenure, bajeti yake lazima iwe bajeti huru, na tume isitumie maofisa wa serikali kama wakurugenzi wa halmashauri na maafisa watendaji wa kata kusimamia uchaguzi katika ngazi za chini; tume itafute watendaji huru wa tume katika ngazi hizo.

3. Katiba iruhusu mfumo wa uwakilishi wa uwiano mpaka zaidi- badala ya kwa viti maalumu vya wanawake pekee.

4. Sheria ziwekwe bayana za kuthibiti kiasi cha matumizi katika kampeni na kulazimisha kutangaza wazi vyanzo na matumizi wakati wa kampeni za uchaguzi

5.Daftari la Kudumu la Wapiga Kura(DWKW) liboreshwe, kuanzia mfumo wake mpaka hatua zake za kuliboresha; kitovu cha daftari cha kwanza kabisa kiwe ni kituo cha kupigia kura, mtaa/kijiji na kuendelea ili daftari liweze kutumika hata kwenye chaguzi za mitaa. Bahati mbaya serikali imeshaanza tayari kuboresha daftari bila kuzingatia masuala haya. Kwa hiyo its another Garbage In Garbage Out(GIGO) na matumizi mabaya tu ya mabilioni ya walipa kodi! Pamoja na kuwa daftari limeanza kuboreshwa suala la wapiga kura walioko nje ya Tanzania halijazingatiwa hii inaonyesha kwamba mwaka 2010 walioko nje wanaweza wasiweze tena kupiga kura kama hawatarejea nyumbani na kujiandikisha.

6. Vituo vya kujiandikisha na kupigia kura viwe vya kudumu na vitangazwe rasmi kabisa kwa sheria ama gazette la serikali!

7. Chama tawala kitengenishwe na dola- Ma DC, Ma-RC kama watumishi wa umma wasiwe sehemu ya uongozi wa chama kinachotawala nk. Lazima sheria iwepo kuthibiti watumishi wa umma kama Rais, Mawaziri nk kutumia kofia zao za kiserikali na rasilimali za taifa kujenga vyama vyao. Najua sheria imegusia kidogo, lakini enforcement ni muhimu.

Haya ni baadhi ya mambo ya msingi lakini unaweza kupata mengi zaidi katika mada yangu ifuatayo kuhusu "Uzoefu katika uendeshaji wa uchaguzi Tanzania"- bonyeza hapa: http://www.chadema.net/habari/misc/misc_10.html

Cha msingi si kujadili tu haya mambo, ni kuchukua hatua! Kwa wale waandishi wa habari na waandishi wa makala- ombi langu kwenu ni kufanya suala la mabadiliko ya katiba na marekebebisho ya sheria za uchaguzi kuwa ajenda zenu za kudumu kwa mwaka 2008. Ni kwa kufanya hivyo tu ndipo mnaweza kusaidia mabadiliko Tanzania mwaka 2010. Hata kama uko serikali, mashirika ya hiyari na hata taasisi za kimataifa, angalia unawezaje kusukuma mbele haya masuala kwa maslahi ya taifa. Hatuwezi kuwa na uchaguzi ambao ni mnada wa gulio na kura la kaburi la ridhaa ya wananchi!

JJ
 
Yohana wa Mnyika,

Sasa naomba nitoe ombi rasmi.

Hayo mapungufu Saba (7) uliyoyataja, yawasilisheni Serikalini kupitia Bunge, Mahakama na zaid wasilisheni kwa Wananchi (na mkitoa sababu) kupitia Magazeti, Majarida na hata mabango ya barabarani.

Taifa (umma) ni lazima uwelewe na kuelimishwa kuwa haki zake za msingi, zinang'ananiwa na kutawalwa na kikundi kimoja ambacho kinang'angania madaraka na utawala na kutokujali maslahi ya Taifa, uwiano wa haki za Wananchi na hata Ubutu wa mfumo wa Vyama Vingi na Demokrasia.

Kazi hii ya kupaza sauti hii kutaka haya mapungufu yarekebishwe isisubiri 2009, ianze Kesho!
 
kinacho tuponza wa bongo.ni kuchagua kwa mtindo kijana, mzee, mwanamke, mwisho tutasema tuanataka kiongozi mtoto.

suala katika kuchagua kiongozi ni kutazama record ya utendaji kazi wake miaka ya nyuma.amefanya nini amebuni nini akalitekeleza.ni mtu wa aina gani.vinginevyo tutakuwa tukijifurahisha na kuweka viongozi kwa majaribio huku nchi ikiteketea.jambo lingine ni wapiga kura tuache uroho wa vijisenti ambavyo madhara yake makubwa katika kupata kiongozi bora.mathlan ndugu yetu kwabwe ni juzi tuu ametoka chuo kikuu haivi kweli anaweza kuwa kiongozi bora?au anaweza akawa ni aina ya akina wangwe ambaye hubisha mpaka maazimio yake mwenyewe.

Au aina ya bwana mrema ambayo majibu na maagizo ya kazi ya papo kwa papo.mimi naamini bado ccm inao uwezo wa kutoa viongozi wazuri isipokuwa nao wanamatatizo kama ya wana JF katika uteuzi wao.ni lazima awe mwenzao.

sifa za uchapakazi hawazihitaji wao wanavigezo vyao.halafu inafaa kutazama tnamlaum JK lakini makozsa mengi yamefanyika uongozi uliopita.aidha tumukuwa kitaka kiongozi kuleta maendeleo mara anapochaguliwa kama vile unaponunua kibriti na kukiwasha kinawaka mara moja jambo ambalo ni ndoto maendeleo ni mchakato huchukua miaka mingi.

Tangu JK ashike madaraka mambo yafuatayo ameweza kuyashughulikia. Kupambana na ujambazi,kupambana na uharifu wa mazingira.Kuanzisha na kutekeleza miradi ya elimu ya sekondari.kuboresha michezo.kuiweka tanzania machoni mwa jumuiya ya kimataifa na kukubalika.miji yetu kuborika kutokana na na uharabifu wa vibanda vya machinga.

Fedha za jk kupelekwa kupelekwa kwenye mikoa kukopesha wajasiriamali wadogo.sasa watanzania walitarajia nini katika kipindi cha miaka miwili wote tuwe na mali kama bakhresa?

Mimi naamini atafanya vizuri zaod katika kipindi kinachobaki na ikiwezekana tumpe miaka mingine mitano ijayo.vinginevyo tutajuta
 
kinacho tuponza wa bongo.ni kuchagua kwa mtindo kijana, mzee, mwanamke, mwisho tutasema tuanataka kiongozi mtoto.suala katika kuchagua kiongozi ni kutazama record ya utendaji kazi wake miaka ya nyuma.amefanya nini amebuni nini akalitekeleza.

ni mtu wa aina gani.vinginevyo tutakuwa tukijifurahisha na kuweka viongozi kwa majaribio huku nchi ikiteketea.jambo lingine ni wapiga kura tuache uroho wa vijisenti ambavyo madhara yake makubwa katika kupata kiongozi bora.mathlan ndugu yetu kwabwe ni juzi tuu ametoka chuo kikuu haivi kweli anaweza kuwa kiongozi bora?

au anaweza akawa ni aina ya akina wangwe ambaye hubisha mpaka maazimio yake mwenyewe.Au aina ya bwana mrema ambayo majibu na maagizo ya kazi ya papo kwa papo.mimi naamini bado ccm inao uwezo wa kutoa viongozi wazuri isipokuwa nao wanamatatizo kama ya wana JF katika uteuzi wao.

ni lazima awe mwenzao.sifa za uchapakazi hawazihitaji wao wanavigezo vyao.halafu inafaa kutazama tnamlaum JK lakini makozsa mengi yamefanyika uongozi uliopita.aidha tumukuwa kitaka kiongozi kuleta maendeleo mara anapochaguliwa kama vile unaponunua kibriti na kukiwasha kinawaka mara moja jambo ambalo ni ndoto maendeleo ni mchakato huchukua miaka mingi.

Tangu JK ashike madaraka mambo yafuatayo ameweza kuyashughulikia.Kupambana na ujambazi,kupambana na uharifu wa mazingira.Kuanzisha na kutekeleza miradi ya elimu ya sekondari.kuboresha michezo.kuiweka tanzania machoni mwa jumuiya ya kimataifa na kukubalika.miji yetu kuborika kutokana na na uharabifu wa vibanda vya machinga.

Fedha za jk kupelekwa kupelekwa kwenye mikoa kukopesha wajasiriamali wadogo.sasa watanzania walitarajia nini katika kipindi cha miaka miwili wote tuwe na mali kama bakhresa?

Mimi naamini atafanya vizuri zaid katika kipindi kinachobaki na ikiwezekana tumpe miaka mingine mitano ijayo.vinginevyo tutajuta
 
Kweli Mchungaji Kishoka ana hasira na Mnyika naye anampango/utaratibu mzuri.

Mnyika, nakubaliana nawe kabisa katika hayo mapungufu saba uliyoyataja. Lakini, mimi nina mtazamo mmoja tofauti kidogo. Ningependa kuona kwamba haya matatizo yanatafutiwa tiba na sio kufungwa plasta!! Hii namaanisha kuwa, inahitajika kuwepo suluhisho la kudumu. Kwa hilo, mimi nitaanzia na kitu kimoja: KATIBA.

Katiba ambayo Tanzania yetu tuipendayo, iliandikwa kwa kunufaisha CCM na sio Taifa. Katiba inapaswa kuchanganuliwa na kisha kuandikwa upya ili iweze kutumika leo, kesho na mwaka 2108. Vinginevyo, tutaendelea kulumbana kila leo na kubadilishana mawazo ya maana yasiyoweza kutekelezeka.

Kwa hali iliyopo sasa, kila move ambayo CCM inafanya, inalindwa kikatiba au watatumia katiba (kupitia nguvu ya idadi ya wabunge) kujilinda. Hali hii itaendelea hata upinzani wakiwa katika nafasi iliyo CCM leo hii. Tofauti itakayokuwepo ni kuwa CCM itakuwa kwenye upinzani ikikoromea chama kilichoshinda huku ikisahau kuwa nacho (CCM) kilikuwa kinaendeleza hatamu kwa staili hiyohiyo.

Sasa ni vipi katiba ibadilike? Yafuatayo ni baadhi ya mapendekezo ya utendaji wa serikali:

i) Kutenganishwa kwa serikali na siasa.
Hapa namaanisha kwamba mawaziri, manaibu waziri na watendaji wakuu wa serikali wasiwe wabunge. Wanaweza wakawa ni wameteuliwa kisiasa lakini wasiwe na nafasi katika sehemu mbili za mhimili wa serikali. Kwa mtaji huo pendekezo la pili linahusiana.

ii) Mihimili ya serikali itenganishwe na kutumika kuwekana sawa
Kipengele hiki kichukuliwe kwamba, serikali kuu, Bunge na Mahakama vyote viwe na uhuru wa kujiendesha na lengo lake ni kutunga sheria (Bunge), kutekeleza (enforce) sheria (Serikali kuu) na kuitafsiri sheria (Mahakama). Hali halisi ya sasa ni kuwa, Mahakama pekee ndio inayojitahidi (bahati mbaya inaingiliwa kila leo na Bunge) kufanya kazi jinsi inavyotakiwa. Bunge, hususan wabunge wa chama tawala wakiongozwa na Spika, limekuwa ni kibaraka wa Serikali kuu (kutokana na kuzidisha siasa badala ya utendaji). Hivi sasa hata kama kuna mbunge wa CCM anataka kuikosoa serikali bungeni, akikoromewa na Lowassa au Kingunge basi atafyata mkia for the sake of chama.

iii)Ugombea binafsi uruhusiwe
Kuna watu wengi wenye uwezo wa kuongoza lakini wanajikuta wakiingia CCM ili wapate nafasi ya kuchaguliwa, au kuogopa kujiunga na upinzani wasije wakasakamwa na serikali ya CCM. Matokeo yake watanzania hawapati watu wenye sifa zinazohitajika au fikra na mwelekeo utakaonufaisha taifa. Badala yake tunaendelea kupata vibaraka wapya wakiwarithi wale wa awali.

iv)Checks and balances
Huu ni utaratibu ambao utatoa changamoto kwa utawala wowote kutofanya kazi kienyeji. Rais asijiamulie kuongeza au kupunguza wizara kwa manufaa yake na washkaji zake. Bunge lazima liidhinishe teuzi hizi (mabalozi, mawaziri, majaji n.k.) ili wateuliwa wawe ni watu wenye ujuzi na uzoefu kwenye nyanja zao na sio kuteua vihio.

Labda niishie hapa kwa leo lakini kuna sehemu nyingi za katiba zinatakiwa ziangaliwe upya (udhibiti wa fedha za kampeni nk). Kikubwa, katiba hii iwe ni matokeo ya ridhaa ya watanzania na sio wanaCCM. Jambo hili, kiuhalisi, linaweza kuleta mafanikio makubwa kisiasa na kuwa na upinzani wenye afya kwa faida ya wote ikiwa litaanza kufanyiwa kazi sasa, kupata katiba mpya mwaka 2010 na kuona matunda mwaka 2015. Hatutaweza kuona matunda kesho wala kesho kutwa, na pengine baadhi yetu hatutakuwa hai kuona matunda hayo. Lakini ikumbukwe kuwa, tunafanya yote haya kwetu sisi na kwa kizazi kijacho ili watoto na wajukuu wetu wasitiane vidole vya machoni.
 
Mzee wa Merikebu,

Shukrani sana kwa nyongeza ya mawazo. Sijui Mnyika kapotelea wapi na hata Zitto sijamuona akichangia katika mjadala huu.

Lakini twaendelea na safari ya Mapinduzi!
 
..But democracy is about more than casting vote. It's about building lasting institutions such as a free press, an effetive legislature and,most important, an independent judiciary.
Aryn Baker, Time Magazine

Is freedom of press, effective legilature and independent judiciary body existing in Tanzania?

Safari ya 2010, iendane sambamba na hiyo quote hapo juu.
 
Wakuu Heshima Yenu,

Nimeanzisha huu mjadala ili kuchochea au kuhamasisha wanachama wa hapa mtandaoni kutenda kwa vitendo yale ambayo tumekua tukichangia hapa JF.Ni jambo liliko wazi kabisa JF imekua na watu wenye dira mbalimbali zenye mwelekeo mpya katika kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi kwa Taifa letu tukufu Tanzania.
Hapa namaanisha wale wanaochochewa na moyo wa kizalendo zaidi kuliko tamaa binafsi,yaani wale ambao watatea maslahi ya Taifa na wananchi zaidi ili kufikia kule ambako tumeshindwa miaka 46 iliyopita.


Ni jambo lililo wazi kabisa kwamba Tanzania tunahitaji Ukombozi wa pili "Secondary Liberation" kwani ukombozi wa kwanza ambao babu zetu walipigania kwa kumwaga damu zao umepuuzwa na watu wachache ndio maana leo hii tumekua maskini.Ni kama vile tunalaumu kwa nini tulipatiwa uhuru kwani hadi leo hii tumeamua kujirudisha kule kule kwa wale tuliowafukuza na kujipendekeza kwao ili kupata msaada.Bajeti yetu itanisaidia kushuhudia zaidi.

Sasa basi,kwa sababu jukwaa hili kwa vile limekua likipitiwa na watu mbalimbali na ambao mitazamo yao na michango yao imekua na manufaa makubwa kwa taifa basi ni wakati muafaka wa wanachama kutoa maoni yao,michango yao na ushauri kwa wale wenzetu watakaotaka kambao ni memba wa hapa watakaojianda kwa Uchaguzi wa miaka miwili ijayo 2010


Na nina imani kabisa,Vijana wengi wasomi ni member wa hapa na wangetaka kutoa mchango wao kwa taifa kwa kugombea nafasi kadhaa hapo baadae,pia wapo watu wa makamo ambao wamekaa nje ya mfumo wa utawala kwa muda mrefu na wangependa kuingia kwenye system ili kulitetea taifa lao.Lakini tukumbuke si kila mtu anaweza kuwa kiongozi mzuri.Pia Nchi yetu imekua na uhaba wa viongozi waadilifu,na hawa ndio ambao wanaoifanya nchi yetu idharaulike na hata Mtanzania kupoteza thamani ya Utanzania wake kwa umaskini uliopindukia.

Hivyo,itakua ni jambo la maana kama watu watajiandaa mapema kama kweli tunataka mabadiliko na au kama tunataka kuzalisha viongozi wazuri na wenye dhamira ya dhati ya kulitumikia taifa letu.Mapinduzi makubwa ya Kidemokrasia Tanzania 2010 yanawezekana.Tanzania inaweza kuandika historia mpya aidha katika kiti cha Urais au katika Bunge letu

Sasa huu ni Muda wa kujiandaa kukomesha vitendo vya ukatili,kukomesha Ufisadi,kukomesha dharau na kejeli kwa Watanzania,kukomesha Uzembe serikali na kujenga Nidhamu ya Taifa letu tukufu Tanzania ili Mtanzania aweze kusimama popote duniani kujivunia nchi yake.Tunahitaji viongozi makini hapo 2010 kwa sanduku la Kura


Nawasilisha!
 
Ben:

Sio kwamba napinga mawazo yako lakini ukweli wa mambo uhuru tulipewa kwa sababu hatukuwa koloni. Na hii ndio sababu ya watu kutothamini uhuru wenyewe.

Pili mtu anaweza kuwa na tamaa binafsi na akawa mzalendo. Kutamani ni tabia ya binadamu. Na tulidanganywa kwa miaka mingi ya uhuru wetu kuwa tunajenga taifa la watu wasio na tamaa, lakini ukweli wa mambo ni kuwa kufuta tamaa ni kitu kisichowezekana.

Na kwa mtaji wa vitu vilivyosema hapo juu, basi mageuzi hayo ni lazima yawe katika mabadiliko ya vitu vinavyowezekana.

Mabadiliko ni lazima yakubali kuwa tamaa binafsi zipo na mtu mwenye kutumia sheria za nchi na misingi inayokubalika kutafuta mali au kitu chochote kukidhi tamaa yake binafsi atambuliwe kama mzalendo.

Demokrasia nayo ina matatizo yake. Ufisadi na kashfa zinazotoka sasa zinawafawanya walipo madarakani kubadilika hili nao washinde 2010. Ningeomba Tanzania waangalie uwezekano wa watu KWENDA MSITUNI au kutumia mbinu kama za IRA.
 
Bin Maryam,

Umeongelea kitu kizuri sana mtu atafute mali kwa kuzingatia kanuni na sheria za nchi.Kwa hili nakubaliana nalo.

Lakini Hilo la kutafuta njia ya kwenda msituni ni primitive way of solving the problem.Tunataka tuanze kutumia nguvu ya Umma kupitia njia ya Demokrasia Kiduchu tuliyo nayo ili kuikuza ikiwa tutafanikiwa katika mageuzi makubwa yajayo.Kwa kweli na jinsi CCM ilivyo king'ang'anizi wa madaraka sidhani kama watakubali kuachia madaraka hapo ndipo balaa litakapoibuka.

Haya ya kujenga taifa lisilo na watu wasio na Tamaa ilikua Vision Mwalimu Myerere lakini hadi kifo chake alishaona jinsi kila mtu alivyokua mroho.Na hata wale wachache ambao alidhania ni wasafi Kama Mjomba wetu Mkapa hadi akamwita Mr.Clean kwenye kinyang'anyiro chao cha ndani leo hii ndiye aliyegeuka mbabe na kuwakejeli watanzania.Mr.Clean akageuka kuwa Mr.Entrepreneur huko ikulu.

Halafu suala la walioko madarakani kubadilika sio shida,kwani hata Kenya waliokua kwenye serikali yaani mawaziri achilia mbali wabunge walianguka vibaya pamoja na kujinasua.Cha msingi pia hawa watu wakijiandaa mapema na kujifunza kutoka source mbalimbali mbinu kadhaa zitakazoweza kujenga hoja za kuwashawishi wapiga kura yaani hoja ambazo zitageuka kuwa Promise itakua ni jambo la msingi.Ziwe hoja nzito na zinazotekelezeka baada ya Uchaguzi
 
Ben:

Kuna vitu viwili ambavyo wanaotaka kuleta mabadiliko Tanzania wanafanana navyo sana: kwanza wanapenda kuishi mjini na pili wanaogopa kwenda msituni.

Waliopata ubunge kupitia CUF wamepata nje ya Unguja. Waliopata kupitia CHADEMA wamepata nje ys DSM.
 
Demokrasia nayo ina matatizo yake. Ufisadi na kashfa zinazotoka sasa zinawafawanya walipo madarakani kubadilika hili nao washinde 2010. Ningeomba Tanzania waangalie uwezekano wa watu KWENDA MSITUNI au kutumia mbinu kama za IRA.

Bin Maryam:

Honestly speaking, nimejaribu kuchambua kila kona ya hii dunia..kujaribu kuona katika situation ambayo inalikuta taifa letu..UFISADI...!!! Ni nini hasa ni utatuzi fair kabisa and reasonable..! Unajua tumechart na kublog mpaka vidole vinaota sugu..but nchi inateketea. Kila asubuhi new threads and posting zinatiririka hapa JF na kwingineko. Personaly Ni kama ninaona jibu la kweli..but ni kama napata kigugumizi...tena nafikiri kigumizi cha unafiki. Mimi Mnafiki? Yes nisemeje sasa. maana inawezekana ninawakilisha kundikubwa lakini bora mimi nimejiweka hadharani Dr anaweza kunipa dawa kama anayo. Maana moyoni jibu liko very clear! lakini hapo hapo ninapata picha ya umati wa watz wakinizomea kwa maamuzi yangu ya dhati kabisa.

Kufanya "ACTION" kama ya shujaa MKWAWA PALE LUGALO IRINGA. Ninawaona wakinizomea ..wakisema this is very primitive way etc...lakini moyoni naumia. Ukweli wa moyoni kwangu unapingana na wanaonizomea. Ingekuwa ni swala personal..FISADI anasumbua familia yangu. Jibu ni moja tena ..lisilo la kuyumba. Ninamalizia mbali si self defence? Nafanya KI_MKWAWA MKWAMKWA!!

Lakini inapokuwa ni swala la nchi..wenyewe wanasema collective sijui responsibilty sijui nini! Inanipa shida. Mimi sioni mawazo yako mabaya kabisa.!!! Tena unajua nini?. Watanzania wengi sana they r fade up!!! Lakini kusema kama ulivyosema..Mdomoni...wanaweweseka. Wako conditioned hivyo.

Lakini nafikiri nakosea..Watanzania wako conditioned hivyo? TIP TIP? alikuwa hivyo kweli, MIRABO? YULE MZEE WA ACTION YA MAJIMAJI alikuwa Conditoned hivyo.. No! siwatendei haki.

Nina withdraw' statment yangu.. Hawa Wazee walikuwa vichwa na mashujaa..sio kama sisi. Walipigania uhuru wa Bendera..Its our time to honour them Tupiganie uhuru wa uchumi. Yes hata ikibidi Kufanyiwa kama alivyofanyiwa Babu yetu MPENDWA MKWAWA WA KALENGA na The Rest OF THE STRONG and NOBLE PEOPLE OF THEIR TIME.
 
wazo zuri sana maana haya makelele humu bila kujaribu hata kugombea ukatibu kata ili ukatetee kidogo kilichopo tutaonekana wapiga kelele tuu na mwisho watatupuuza, mimi niko nje ya nchi kwa hiyo kugombea siwezi ila nasubiri mtu/watu serious ambao watakuwa wazi kutupa CV zao na nia zao na wawe nje ya CCM, hapo nitakuwa tayari kukata check na idea nini cha kufanya, wanaotaka kugombea waanze mapema kujitayarisha na waangalie majimbo ambayo yana uwezekano wa kushinda, kujiandaa mapema ni weapon kubwa sana katika uchaguzi wowote
 
Viongozi wa Afrika hawana utaratibu wa kukubali kushindwa chaguzi. Kila kiongozi anataka aendelee kuwapo madarakani ama mpaka mwisho wa maisha yake au pale katiba inapomzuia kuendelea na madaraka. Ni viongozi wachache sana waliaochia madaraka nje ya taratibu hizo mbili. Waliiondoka kwa hiari zao bila shinikizo lolote ni pamoja Nyerere(baada ya kuwa madarakani kwa takriban miaka 25), Abdul Wakil na Mandela (baada ya miaka mitano tu) na mwingine sikumbuki jina lake naye baada ya muda wa zaidi ya miaka 25. Ni kiongozi mmoja tu aliyeondoka madarakani kwa kukubali matokeao ya uchaguzi; huyu ni Dr. Kenneth Kaunda wa Zambia (sijui kwa nini Wazambia hawamtukuzi kwa uungwana wake ule). Viongozi wengine wote kama vile akina Kibaki, Salmin, Karume, Mugabe na wengine wote hutumia madaraka wanayokuwa nayo wakati wa uchaguzi ili kubadili matokeo ya uchaguzi ili waonekane wameshinda.

Kwa ujtaratibu huo, nina imani ndogo sana kama kweli kutakuwa na mabadiliko yoyote mwaka 2010 kwa vile Kikwete na CCM watakuwa bado wanadhani kuwa miaka mitano ijayo bado ni ya utawala wao; na kwa bahati mbaya watakuwa wana-control vyombo vya dola na tume ya uchaguzi.
 
Bin Maryam:

Honestly speaking, nimejaribu kuchambua kila kona ya hii dunia..kujaribu kuona katika situation ambayo inalikuta taifa letu..UFISADI...!!! Ni nini hasa ni utatuzi fair kabisa and reasonable..! Unajua tumechart na kublog mpaka vidole vinaota sugu..but nchi inateketea. Kila asubuhi new threads and posting zinatiririka hapa JF na kwingineko. Personaly Ni kama ninaona jibu la kweli..but ni kama napata kigugumizi...tena nafikiri kigumizi cha unafiki. Mimi Mnafiki? Yes nisemeje sasa. maana inawezekana ninawakilisha kundikubwa lakini bora mimi nimejiweka hadharani Dr anaweza kunipa dawa kama anayo. Maana moyoni jibu liko very clear! lakini hapo hapo ninapata picha ya umati wa watz wakinizomea kwa maamuzi yangu ya dhati kabisa.

Kufanya "ACTION" kama ya shujaa MKWAWA PALE LUGALO IRINGA. Ninawaona wakinizomea ..wakisema this is very primitive way etc...lakini moyoni naumia. Ukweli wa moyoni kwangu unapingana na wanaonizomea. Ingekuwa ni swala personal..FISADI anasumbua familia yangu. Jibu ni moja tena ..lisilo la kuyumba. Ninamalizia mbali si self defence? Nafanya KI_MKWAWA MKWAMKWA!!

Lakini inapokuwa ni swala la nchi..wenyewe wanasema collective sijui responsibilty sijui nini! Inanipa shida. Mimi sioni mawazo yako mabaya kabisa.!!! Tena unajua nini?. Watanzania wengi sana they r fade up!!! Lakini kusema kama ulivyosema..Mdomoni...wanaweweseka. Wako conditioned hivyo.

Lakini nafikiri nakosea..Watanzania wako conditioned hivyo? TIP TIP? alikuwa hivyo kweli, MIRABO? YULE MZEE WA ACTION YA MAJIMAJI alikuwa Conditoned hivyo.. No! siwatendei haki.

Nina withdraw' statment yangu.. Hawa Wazee walikuwa vichwa na mashujaa..sio kama sisi. Walipigania uhuru wa Bendera..Its our time to honour them Tupiganie uhuru wa uchumi. Yes hata ikibidi Kufanyiwa kama alivyofanyiwa Babu yetu MPENDWA MKWAWA WA KALENGA na The Rest OF THE STRONG and NOBLE PEOPLE OF THEIR TIME.


Respect mkuu wangu,
Kwa kweli ulichosema hapa ni mawazo ya watanzania walio wengi na hasa vijana ambao kila leo wamekua wamechoshwa na ukandamizaji wa viongozi wetu ambao walikua mstari wan mbele kuwaomba kura lakini leo hii wanawatreat kama vibaka.Si Wamachinga tu na hata Vijana wengi wasomi na hasa walioko mavyuoni.Angalia kadhia wanazopata kwenye bodi ya mikopo.Kusoma kwenye mazingira magumu na kutafuta ajira katika mazingira yasiyofaa hata kidogo.

Sasa ukisema kuchukua Action ya mtutu wa bunduki,utapata wafuasi wengi sana.Historia inaonyesha ni mashujaa wachache waliowhi kutumia mbinu hii wakafanikiwa kuingia kwenye system na kutimiza malengo ya taifa zima kama akina Fidel Castro wa Cuba na Muamar Ghadaffi wa Libya.Ndiyo,kwangu hao ni MASHUJAA ambao walisolve problem once and for all ingawa ilicost damu za wachache.

Ninachotaka kusema hapo juu ni kwamba tujaribu njia nzuri zaidi ambayo haijawahi kutumika,Yes,tuna demokrasia kiduchu lakini tujaribu kuitumia ikishindikana basi tutaangalia njia zingine.Zote ni njia za kutufikisha huko lakini tupime ni ipi ambayo itakua the best option.But all in all Mabadiliko ni Lazima KWA NJIA YOYOTE ILI KULIKOMBOA TAIFA LETU HATA KAMA KWA GHARAMA YA DAMU ZETU!

wazo zuri sana maana haya makelele humu bila kujaribu hata kugombea ukatibu kata ili ukatetee kidogo kilichopo tutaonekana wapiga kelele tuu na mwisho watatupuuza,mimi niko nje ya nchi kwa hiyo kugombea siwezi ila nasubiri mtu/watu serious ambao watakuwa wazi kutupa CV zao na nia zao na wawe nje ya CCM,hapo nitakuwa tayari kukata check na idea nini cha kufanya,wanaotaka kugombea waanze mapema kujitayarisha na waangalie majimbo ambayo yana uwezekano wa kushinda,kujiandaa mapema ni weapon kubwa sana katika uchaguzi wowote

Mkuu heshima yako,
Unajua CCM wanajua weakness ya wapinzani wao ni kwamba hawajiandai mapema.Kwa mfano kama mtu unataka kugombea 2010 ni muhimu ukaanza maandalizi mapema na kwa umakini mkubwa ili isije ikafika muda ule mtu ukaanza kuwa opportunist,huo ndio utakua mwanzo wa usaliti na Ufisadi ndiko utakapoanzia

Unajua kwa mfano hapo Kenya watu wa ODM tangu watengane na serikali ya Kibaki walianza immediatelly kuweka strategy zao mezani kujiandaa kwa election 2 years in advance.na walicholeta niTsunami.Hata baadhi ya mawzairi waliobakia kule wakaja kujiunga na ODM mwishoni walibaki huko strategically.Kama CCM wanavyolaumiwa kuingiza mamluki ndani ya Upinzani basi upinzani nao ndio muda wa kuingiza mamluki ndani ya CCM mapema ili iangushwe kutoka ndani.kwani baada ya mwaka huu opposition hawataweza kufanya hivyo tena maanake cCM ni wajanjauchaguzi ukikaribia hawawezi kuruhusu outsider kuwa na acces na semu zao sensitive ktk Chama
 
Viongozi wa Afrika hawana utaratibu wa kukubali kushindwa chaguzi. Kila kiongozi anataka aendelee kuwapo madarakani ama mpaka mwisho wa maisha yake au pale katiba inapomzuia kuendelea na madaraka. Ni viongozi wachache sana waliaochia madaraka nje ya taratibu hizo mbili. Waliiondoka kwa hiari zao bila shinikizo lolote ni pamoja Nyerere(baada ya kuwa madarakani kwa takriban miaka 25), Abdul Wakil na Mandela (baada ya miaka mitano tu) na mwingine sikumbuki jina lake naye baada ya muda wa zaidi ya miaka 25. Ni kiongozi mmoja tu aliyeondoka madarakani kwa kukubali matokeao ya uchaguzi; huyu ni Dr. Kenneth Kaunda wa Zambia (sijui kwa nini Wazambia hawamtukuzi kwa uungwana wake ule). Viongozi wengine wote kama vile akina Kibaki, Salmin, Karume, Mugabe na wengine wote hutumia madaraka wanayokuwa nayo wakati wa uchaguzi ili kubadili matokeo ya uchaguzi ili waonekane wameshinda.

Kwa ujtaratibu huo, nina imani ndogo sana kama kweli kutakuwa na mabadiliko yoyote mwaka 2010 kwa vile Kikwete na CCM watakuwa bado wanadhani kuwa miaka mitano ijayo bado ni ya utawala wao; na kwa bahati mbaya watakuwa wana-control vyombo vya dola na tume ya uchaguzi.


Mkuu Kichuguu,
kwa kweli tukifikia hpo ndipo suala la kulazimasha wakubali linapozuka.Majirani zetu Kenya waliona utamaduni huu Haramu ambao Kibaki alitaka kudumisha kwa kung'ang'ania madaraka.sasa tifikie mahali Tanzania na sisi tukatae kutumiwa kama door step.


Wakionekana kutumi utamaduni huo na sisi TUTUMIE NGUVU kukabiliana nayo.Ndiyo maana tuko maskini kwa sababu ya walioko madaraka kumisuse dola ambyo inalipwa kutokana na kodi za walalahoi.Cha msingi ni kujiandaa mapema ili kushinda kwa Kishindo na wakijaribu kuiba au kutenda kinyume,basi TUWALAZIMISHE KUTOKA kuliko kuwabembeleza.Miaka 50 ya sisi kuwa maskini hivi inatosha.

Itapendeza tukiadhimisha Jubilei ya miaka 50 huku mageuzi au mapinduzi makubwa ya kiutawala na kiuchumi kama yamekwishafanyika.Sasa tutakua tunaanzia hapo kujenga Taifa kubwa Duniani Kiuchumi na lililoweza kuinua maisha ya Wananchi wake.Yaani kuanzia mwaka wa 51 na kuendelea tutakua tunajenga taifa la kuelekea huko Malaysia,Korea na Brunei waliko
 
Back
Top Bottom