The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Mnyika nimekupata, inatia moyo kwamba angalau mmeongea and I was wrong in my earlier analysis.I understand you may not want to go into bunge's technicalities for tactical reasons, but without even knowing the details I can tell the technicalities are unhealthy if they can be abused to silence genuine opposition.The question is, what is the opposition doing to adress this?

Bab kubwa, kuwa balozi wa mabadiliko vijijini huko na tupe ripoti ya maendeleo ya mwamko katika ngazi ya vijijini.

Pundit

Upinzani unamwaga yote kwa umma, kama wabunge wameshindwa kuwawakilisha wananchi basi tunayapeleka kwa wananchi wenyewe. Na wananchi wanaamua hatua gani za kuchukua.

Naona wameanza kwa kuwazomea na hakupunguza imani nao(mintaarafu ripoti ya REDET). Na naona bunge limeshtuka kwamba wanazidi kudharaulika, naamini kuundwa kwa haraka haraka kwa kamati teule ya Richmond katika suala ambalo Lowassa alikuwa akilizimia kwenye kamati ya Wabunge wa CCM kunaonyesha pengine wanajaribu kurejesha imani.

Pia wanajaribu kupiga baragumu kuwa kanuni za bunge zimebadilishwa, kwamba sasa wabunge watakuwa na uhuru zaidi wa kuikosoa serikali! Sisi tunaendelea kufuatilia tu; kadiri bunge linavyoshindwa kuiwajibisha serikali kwa sababu ya hodhi ya chama kimoja bungeni ndio kadiri wabunge wa CCM wanavyojichimbia kaburi la kisiasa. Sasa ikifika 2010 unatajua upinzani utafanya nini.

JJ
 
Rev. Kishoka
Kuhusu BOT, mkondo wa bunge ulijaribiwa na Dr Slaa alishaandika Hoja Binafsi lakini dalili zilionyesha wazi kabisa kwamba walitaka kuifanyia mizegwe isiingie, umesoma ripoti ya usalama wa taifa ikimshauri Waziri Mkuu Lowasa ahakikishe Kashfa ya BOT kama alivyoiandika Dr Slaa haiingii bungeni? Katika mazingira hayo, unaweza kumlaumu vipi Dr Slaa kuichomoa hoja yake na kuiwasilisha kwenye mahakama ya wananchi ama bunge la umma? Dr Slaa ni mbunge, kama angeiwasilisha ile hoja mule, kuna baadhi ya mambo angebanwa na kanuni za bunge(naomba niseseme kwa nini ingawa najua kwaninini). Kwa hiyo, alifanya uamuzi wa busara kabisa. JJ

Mnyika,

This is why I stated that on critical issues and smear campaigns,Opposiion should use other instruments (sisi, JF, Magazeti and spinmasters) to air the dirty laundry and let the people make descicion.

Naelewa sana ugumu wa tecnicalities ndio maana narudia kusema kuwa it is not about ownership of story or popularity, but how to capitalize on story.

Mfano, kama hiyo ripoti ya Waziri Mkuu na usalama ambayo Slaa alitaka kuileta hadhdarani lakini kwa ajili ya technicality hakuweza, kwa nini hakuleta kwa wavuja habari halafu akapata nguvu kushinikiza Bunge lifuatilie tuhuma?

This is why I said, "I am pissed off"! Opposition needs to have operatives who will stir the ship to break down the "technicalities" in place. haya ndiyo tunayoyaona huku kwingine tunakoishi iwe UK, USA, China au Venezuela. It is how to play the game to your advantage avoiding technicalities.

Ndio maana katika scandals za politics za Marekani, unasikia habari imechapwa gazetini, kwenye blogu na hata kumbi kama hizi, kisha mshike mshike huanza. Wabunge kuwasilisha petition, hoja ya kutaka uchunguzi na Bunge au serikali linakuwa halina njiya bali kuruhusu Uchnguzi ufanyike na ripoti kutoka hadharani.

CCM are great to contain that and to some extent to manipulate the public, mfano wa ile barua ya kijinga kuhusu Mbowe au Slaa!

Lakini you may have a different take kwa kuwa mandhari uliyoko ni tofauti na yangu, hivyo inawezekana kabisa maoni yangu kuhusiana na jinsi ya kupigana vita dhidi ya ufisadi ikawa ni upupu kwako huku mimi nikiona ndio njia bora ya kupigana!

Tuendelee..
 
Rev. Kishoka umeongea vizuri.I second that. Kumkoma nyani giladi, kama vipi ripoti ya "Usalama wa Taifa" imwagwe hapa watu tuichambue.
 
Kishoka,

Tulia kwanza! Mtu anayekusoma hapa ataona jinsi ulivyokasirika kweli kweli, na atakubaliana nawe kwamba unayozungumza mengi ni muhimu...

Na mimi nilipokuandikia mara ya kwanza nilitaka kukujulisha kuwa hayo unayosema hapa si mapya hata kidogo, baadhi yalishapatiw amajibu hapa hapa, na mengine yanaendelea kutekelezwa na wapinzani wenyewe katika mipango yao.

Kinachoonekana hapa ni kwamba hujui wapinzani wanafanya nini, na unadhani wanapaswa kuja hapa JF kuanika mipango yao. Kwa watu wanaojua mikakati makini waliyonayo wapinzani, ukizingatia pia uhuni wa serikali na CCM dhidi yao, kwa kutumia mfumo mbovu na kanuni zilizopo hasa Bungeni, mtu mwenye hasira kama wewe anagepaswa kuwa amechukua hatua muhimu ya kuwaunga mkono kwa vitendo badala ya kulalama kwenye mtandao na 'kuogopa' kuchukua hatua ambazo zingeongeza nguvu ya ziada unayoikosa kule.

Kwa sababu hiyo, nilikuwa na kila sababu ya kukushangaa kwamba umeganda tu kwenye mtandao...Ingia mitaani ufanye kazi...haya unayosema tumeyasema na yamefanyiwa kazi tayari....Na nidyo maana nilimsifu Mnyika kwa sababu yuko uwanjani anapambana si maneno matupu. Upo hapo?

Sisi wengine tunaona mabadiliko yameanza kuonekana, na upinzani umeanza kujifunza kutokana na makosa ya nyuma. Hatuwezi kurejea mambo ya Mrema bila kujifunza kwayo, wala hatuwezi kusahau kilichommaliza Mtikila...wakati huo tunampongeza kwa kazi anayoifanya mahakamani...Lakini yote hayo wapinzani wameyaona nawanayafanyia kazi. Waunge mkono, usilalame tu!
 
Kishoka,

Tulia kwanza! Mtu anayekusoma hapa ataona jinsi ulivyokasirika kweli kweli, na atakubaliana nawe kwamba unayozungumza mengi ni muhimu...

Kichwamaji,

I do not underestimate Wapinzani, however they are underestimating CCM and Wananchi.

Mfano, wakati listi ya mafisadi ilipotoka, jambo la Kwanza Serikali na CCM walilifanya ni kujiuliza, je jambo hili lafungika na laweza kufika mahakamani? Jibu likawa hapana (do not ask for my source on this!), next CCM wakaanza technical mashambulizi na kuzima moto baada ya Mafisadi watajwa kudai watakwenda mahakamani (Mgonja, Ruta, Karamagi). Ukiangalia majibu ya Mkono, yalikuwa tofauti sana na alitumia technicalities and absence of subsance materials kuhusiana na tuhuma hizo.

Kilichotokea ni kuwa ile "Sensetion" ya orodha na mikutano ya hadhara ikatapakaa, lakini hakuna lililofuata.

Sisi Watanzania, tumeanza kukosoana ni nani ana haki kukemea ufisadi, huku mafisadi wakipeta na mkuu wao akitangaza rasmi ana imani na serikali yake.

Suala la BOT lina pembe tatu. EPA, Majengo na pesa za Meremeta, Tangold, Deep Green and Mwananchi. Kama kawaida, politicians wa Upinzani wakakimbilia majukwaa wakiwa na facts nusu nusu zisizo na misuli, CAG na Meghji wakasema tunafanya uchunguzi wa BOT, kila mtu akakaa kimya kusubiri ripoti binafsi ya CAG ambayo haiwi a Public thing mpaka Meghji na Kikwete waipitie.

Ripoti ya EY kwa CAG kuhusu BOT ni kuhusiana na EPA pekee na si zile pembe mbili zilizobakia. Sasa kama Uinzani ulikuwa na nondo za kutosha na kutaka kufanya hili ni jambo la Taifa, wangekuwa wajanja kumwaga habari hizi kama Udako na ushahidi wote, waache CCM wakihangaika kutafuta mchawi (kama ile barua ya Jitu Patel), halafu Upinzani ukawasilisha hoja Bungeni kuchunguza hayo mambo matatu ya BOT!

Ninachojaribu kufanya ni kusaidia Upinzani kutumuia nguvu zake katika Bunge kushikisha adabu CCM na mafisadi na si kuuza magazeti halafu 2010 unasikia Chadema ina viti 6, CUF 20 (vyote vya Pemba), TLP, UDP na NCCR wana viti 2 kila mmoja jumla ya viti 32 katika Bunge la viti 250!

Kesi za Mtikila za Wagombea huru na hata hii ya sasa ya Kadhi, Serikali na CCM wanaziogopa. Infact alishinda kesi ya Wagombea Huru, Tume ya Uchaguzi ikakiuka uamuzi wa Mahakama (Uchaguzi Tunduru) na hakuna hata mmoja kwenye Upinzani ameshinikiza suala la Ugombea Huru kufuatilia tamko la Mahakama (ingawa bado si Sheria, lakini tamko la mahakama halifutiki)!

There are better ways to play the game, so if some of us see a better way to win why not share? We are not looking for methods on how Opposition gather the facts, but it is how to use those facts effectivelly to your advantage!
 
Turudi kwenye 2010, what is our analysis of majimbo ambayo ni sandakalawe? Katika viti 270+ (ondoa viti maalumu ambavyo ni kujaza chumba bila sababu) ni majimbo mangapi kukweli yanaweza kuchukulika na nguvu zetu zikahamia huko?
 
Kuiangusha CCM inawezekana kabisa kwa sababu ya makosa yao chungu nzima katika maamuzi mbali mbali waliyoyafanya katika miaka ya karibuni.

Kwa maoni yangu cha muhimu kufanya kwanza kabisa ni kuunda chama kimoja chenye nguvu kitakachojumuisha CHADEMA, CUF, TPL na vyama na vyama vingine vyote vyenye kupenda maendeleo ya kweli ya nchi yetu. Chama hiki kitumie muda uliopo mpaka hapo 2010 kujitangaza na kufungua matawi katika kila kona ya Tanzania na kuweka mikakati ya uchaguzi huo.

Kama viongozi wa vyama vya upinzani wakiamua kuuweka ubinafsi wao pembeni unaosababishwa na wasiwasi wao wakukosa madaraka katika chama kipya na kuangalia the big picture for the benefit of all Tanzanians, basi sioni kwanini CCM isianguke hapo 2010.

Katika Kampeni hizo za 2010 unatumia makosa mbali mbali ambayo yamefanywa na viongozi wa awamu ya tatu na ya nne. Na makosa hayo ni mengi tu. Wananchi wakiona kama upinzani una nia ya kweli ya kufanya maamuzi kwa manufaa ya Tanzania basi hata wizi wa kura unaofanywa na CCM hautafua dafu hapo 2010.
 
Kuiangusha CCM inawezekana kabisa kwa sababu ya makosa yao chungu nzima katika maamuzi mbali mbali waliyoyafanya katika miaka ya karibuni.

Kwa maoni yangu cha muhimu kufanya kwanza kabisa ni kuunga chama kimoja chenye nguvu kitakachojumuisha CHADEMA, CUF, na vyama vingine vyote. Chama hiki kitumie muda uliopo mpaka hapo 2010 kujitangaza na kufungua matawi katika kila kona ya Tanzania na kuweka mikakati ya uchaguzi huo.

Kama viongozi wa vyama vya upinzani wakiamua kuuweka ubinafsi wao pembeni unaosababishwa na wasiwasi wao wakukosa madaraka katika chama kipya na kuangalia the big picture for the benefit of all Tanzanians, basi sioni kwanini CCM isianguke hapo 2010.

Katika Kampeni hizo za 2010 unatumia makosa mbali mbali ambayo yamefanywa na viongozi wa awamu ya tatu na ya nne. Na makosa hayo ni mengi tu. Wananchi wakiona kama upinzani una nia ya kweli ya kufanya maamuzi kwa manufaa ya Tanzania basi hata wizi wa kura unaofanywa na CCM hautafua dafu hapo 2010.

Bubu

mawazo yako ni safi sana.
 
Bubu ataka Kusema,
[Kama viongozi wa vyama vya upinzani wakiamua kuuweka ubinafsi wao pembeni unaosababishwa na wasiwasi wao wakukosa madaraka katika chama kipya na kuangalia the big picture for the benefit of all Tanzanians, basi sioni kwanini CCM isianguke hapo 2010.

Ikiwa maneno yako kweli nadhani hii ni kazi moja kubwa sana inayotakiwa kutanguliwa na kila kitu. Na inatisha sana kuona kuwa viongozi wetu nje ya CCM nao wanakuwa na fikra za matumbo yao kwanza. Nina hakika Chadema wapo tayari kuungana isipokuwa matatizo makubwa yanatoka nje zaidi.

Hivi vyama vikiungana kuna majimbo ambayo kila chama kimekamata ama ni mshindani mkubwa dhidi ya CCM kwa hiyo kazi ni ndogo sana kupitia upya matokeo ya mwaka 2005 kisha kusimamisha wagombea hao ktk kamati husika kumtafuta finalist!.

Sehemu tulizoshindwa vibaya vibaya zinahitaji mgombea mpya kabisa na sehemu hizo zipewe nafasi kubwa kukitangaza chama kwani hiyo ni ishara kuwa habari mpya haijawafikia. Kumbukeni tu somo kubwa a uchaguzi wa Mdanganyika ni MTU, yaani nani mgombea sio sera za chama, mengine taratibu yatafuata baada ya ushindi.

Pili, ikiwa wapinzani watashindwa kujiunga nadhani tumaini linalobakia ni kuwepo na mabadiliko ya kweli ndani ya uongozi wa CCM yaani atokee nabii Daud ndani ya CCM yenyewe na kumshinda Golith kwani nina imani kuwa silaha ya kuangusha hili jitu mkoloni mweusi inakuwa na yule mwenye kulifahamu uzembe wa hili jitu...
 
Kazi nyingine ni kuwaelimisha umma. Huu ushindi wa tsunami umetokea kwa sababu wananchi walikubali kuhongwa vi-T-shirt na shilingi alfu mbili kwenye bahasha.

Tukifanikiwa kuwaelimisha raia hatari ya kukubali kuhongwa kuwa ni sawa na kumpa kura yako tapeli tutakuwa tumepiga hatua kidogo.
 
Kuunganisha vyama si kitu rahisi vile unavyoweza kufiri. kila chama ina interest zake kama ilivyo ccm. Leo CHADEMA ikiwa ikulu ccm nao tutawaita upinzani. Wapo wengine wanatumia vyama vyao kama ajira zao. kukivuja chama chake ni sawa na mtu kutangaza kampuni imefilisika.

Mimi siamini kwenye muungano wa vyama hasa vinapokuwa na interest tofauti. Wana upinzani wetu hivi sasa wanataka kuamini kwenye shirikisho la vyama vipindi vya uchaguzi lakini bado ni mfumo usio na mzuri hauwezi kutofautisha sana Serikali na siasa za kiitikadi. mfano mzuri kwa wenzetu wa kenya. Unaweza kuona uchaguzi wao ulivyo wa vurugu, hauna sera wala ilani zinazoeleweka.

Mimi naamini kuwa chama kama chama kikiwa serious hakiitaji muungano na wengine kufanikiwa. hao wengine wenye hekima wataona tu watoke waliko na wajiunge na hao walio serious. waswahili wanasema katika msafara wa mamba kenge nao watakuwepo tu.

Cha muhimu watanzania tuangalie chama kilicho serious tukiunge mkono kwa nguvu zote.

Vyama vyetu pia vimekuwa dhaifu sana katika kupata mawakala makini kwenye usimamizi wa kuhesabu kura. hilo sisi wananchi hatuna la kuwasaidia. vituo vingine havina mawakala kabisa vingine wanashea mawakala. hivyo wataendelea kuibiwa kura hadi watakapoamka na kujifunza kujipanga mapema.

Zaidi ya asilimia 60 ya watanzania wapo huko mikoani na vijijini ambapo hakuna hata kalamu ya upinzani sembuse ofisi. namna hiyo hata watangaze listi milioni za mafisadi hakuna kitu watafanya.

Upinzani unategemea sana magazeti ndo yawasaidie kuwapa umaarufu. wenzao wanakwenda front line kuutafuta huo umaarufu. CCM wamepandikiza watu hadi kwenye vijiwe vya kahawa [makada]kazi yao kubwa ni kuhakikisha watu hawamezi sumu za upinzani zinazowafikia kupitia vyombo vya habari. na ni wazuri sana wa kuziponda. Watanzania walio wengi wanaamini sana ya kusikia haswa kwa watu wanaoishi nao huko mitaani maana wengi wa watanzania si wasomaji au watafiti wa habari. kama huna watu walio karibu nao wa kuweza kuwaambia na kuwasisitizia mambo, upinzani mtahubiri sana kwenye majukwaa, siku mbili tu kila kitu ulichosema watu wanakuwa wamekisahau.

Huku mitaani tunaona CCM wanafanya kampeni nyumba kwa nyumba. Upinzani mnasubiri mtuite jangwani. Jangwani kwenyewe wala hatuji, hapo sasa....

Upinzani hanawa vikundi vya uhamasishaji. TOT inawabeba sana CCM, Redio Uhuru, na magazeti yao. vyombo hivyo ni kampeni tosha ya kuushinda upinzani kila mwaka. hilo upinzani haujajua namna ya kushindana nalo. Ushindi wa uchaguzi sio sera tu, uhamasishaji ndio siri ya ushindi. Mbowe aliweza kujikusanyia watu si kwa ajili wanaipenda sana chadema ila technic ya uhamasishaji aloitumia. kwanza ilikuwa surprise kwa CCM na pili watanzania wengi haswa huko ndani ndani helikopta lilikuwa kivutio tosha cha kuhamasisha watu kuja kumsilikiza lakini tatizo anapoondoka hapakuwepo na wa kuendelea kuhamasisha, wakija CCM wanafuta yote alosema Mbowe wanawajaza yao, makada wanaendeleza pale wakubwa wao walioachia mwisho wa siku uchaguzi wanashinda upinzani unabaki kulalama.

Kote kule upinzani ulipojijenga hadi chini utaona kweli CCM wanakuwa na wakati mgumu. Mfano Kwa Mzee Momose, maeneo ya Mara, Kigoma, karatu, kilimanjaro na pemba. wangekuwa wamefanya hiyo nchi nzima ungekuta wala CCM haiwapi taabu. Tatizo maeneo karibu yote hayo ni nguvu za watu binafsi ama kiuchumi na kimaarufu zinawawezesha kushinda, ama hao wasipogomea upinzani una nafasi kubwa ya kuyapoteza hayo maeneo na kibaya zaidi hao ambao tayari wamekubalika hawawaandai watakao warithi. Upinzani wa mtu mmoja mmoja hatutafika.

Vyama vianzishe vyombo ya uhamasishaji na habari. hivi vyombo huru haviwezi kuweka bayana kila kitu. lakini ukiwa na chombo chako unaweza kufanya achochote, haya mambo ya kusema jina limehifadhiwa yatakoma kama habari ni ya ukweli kila kitu kitakuwa bayana.

Bila uhamasishaji hakuna ushindi hata uwe mzuri kiasi gani. kwa wale mliosoma vyuo vikuu mnalijua hilo wakati wa uchaguzi wa uongozi wa wanafunzi.[huu ni mfano tu]

Pamoja tutashinda
 
La Muhimu jamani ni kwanza hivi vyama vyoote vya upinzani vidrop mawazo na madhumuni yao yoote ya kuhold power hence waungane woote wawe kitu kimoja wateuwe wagombea wanaoweza influence wananchi then wahelp kuelimisha jamii kuwa Tanzania sio ccm tuu as wengine wakigo kupiga kura watakwambia nachagua ccm kz toka 1961 ipo madarakani!halafuuuu rushwa idhibitiwe vilivyo n mwishoni kabsaaa watumie makosa ya ccm kipindi choote wakiwa madarakani kushindia uchaguzi!

lakini hofu yangu mie ni kuwa upinzani kwa hilo ndilo gumu watasema wanaungana lakini kila mtu atataka kugombea uraisi!sasa mimi huwa najiulizaga swali moja tuu kwa mfano hata mtu kama Mrema

akishinda...atatmteua nani kuwa waziri mkuu from his chama na kina nani wawe Mawaziriiii?atleast wakiwa woote chama kimoja utaona kutakua na angalau watu ambao wataweza msaidia raisi kuongoza nchi
 
Kuiangusha CCM inawezekana kabisa kwa sababu ya makosa yao chungu nzima katika maamuzi mbali mbali waliyoyafanya katika miaka ya karibuni.

Kwa maoni yangu cha muhimu kufanya kwanza kabisa ni kuunda chama kimoja chenye nguvu kitakachojumuisha CHADEMA, CUF, TPL na vyama na vyama vingine vyote vyenye kupenda maendeleo ya kweli ya nchi yetu. Chama hiki kitumie muda uliopo mpaka hapo 2010 kujitangaza na kufungua matawi katika kila kona ya Tanzania na kuweka mikakati ya uchaguzi huo.

Kama viongozi wa vyama vya upinzani wakiamua kuuweka ubinafsi wao pembeni unaosababishwa na wasiwasi wao wakukosa madaraka katika chama kipya na kuangalia the big picture for the benefit of all Tanzanians, basi sioni kwanini CCM isianguke hapo 2010.

Katika Kampeni hizo za 2010 unatumia makosa mbali mbali ambayo yamefanywa na viongozi wa awamu ya tatu na ya nne. Na makosa hayo ni mengi tu. Wananchi wakiona kama upinzani una nia ya kweli ya kufanya maamuzi kwa manufaa ya Tanzania basi hata wizi wa kura unaofanywa na CCM hautafua dafu hapo 2010.

Mbinu yoyote ya kuiondoa CCM bila kuhakikisha CCM yenyewe inakatika vipande... Alafu kipande kimoja kiingie upinzani haisaidii!!!

Mpaka kesho mimi siamini tatizo ni kuitoa CCM na kuiingiza chama kingine tatizo ni kuwa na uwiano wa wabunge say 40% by 60% au 45% by 55% ukilifanya hili linamanufaa zaidi kwa taifa zaidi ya kuiondoa CCM, kwa kuwa waupinzani nao hawajajiandaa kuongoza Taifa... hali hii ikifikia sina wasiwasi na chama chochote kutawala hata cha mashetani,,, serikali itakuwa inaadabishwa kwenye bunge! Simple Rule... Haya mengine ni kugombea madaraka tu kama ajira nk.

Hii ndio mikakati naitamani kuisikia!!!
 
Good thread,

Technologia iko upande wetu. Ni kuwaandikia point viongozi wa upinzani na kuweka data zote nje nje. Play by numbers na sio porojo kwa wananchi. Wakijua JK au BALAA BALALI analipa dola ngapi kwa kulala usiku mmoja hotelini London, wataanza kuipata.

PILI ni mwendo wa "TEXT MESSAGE" mpaka unapiga kura. Message, "NO CCM THIS TIME"
 
Naungana na members wanaopinga kuviunganisha vyama vya upinzani, ila naamini katika kuuunganisha upinzani.

Tunaweza kuuunganisha upinzani kwa mikakati ya kuachiana majimbo kwa style ya kuhakikisha kila jimbo linakuwa linagombaniwa na vyama viwili tu, CCM na chama wakilishi cha wapinzani ambacho is most likely to succeeed. Hii ni njia moja tu ya kujenga alliance katika vita hii dhidi ya chama tawala.
 
1.Wapinzani watafute nafasi ya ubunge kwanza (ili wawe wengi).
2.Kuhimza wananchi kujitokeza kupiga kura siku ya uchaguzi.
3.Kuweka nguvu zaidi kwa 74% ya waliopo vijijini (ambao wao bado wanaimani na chama cha nyerere).
4.Bila kuwasahau hao wa mjini pia, (kwa kuongeza imani yao) na kuwafanya wawe kama kioo cha mabadiliko kwa wananchi wa vijijini.
 
kuiangusha CCM ili kiwe nini? na hawa wapinzani washinde halafu kiwe nini? Kushinda uchaguzi peke yake siyo tatizo kubwa sana nadhani tatizo liko kwenye nini kinafuata baada ya ushindi.
 
Je kama hata chama cha Tumaini Chadema kina mfurukuto, je kuna tumaini makini 2010?
 
kuiangusha CCM ili kiwe nini? na hawa wapinzani washinde halafu kiwe nini? Kushinda uchaguzi peke yake siyo tatizo kubwa sana nadhani tatizo liko kwenye nini kinafuata baada ya ushindi.

Right to the point! Bila mikakati mathubuti, yatakuwa yale yale ya NARC baada ya kuibwaga KANU. Hakuna cha maana kimefanyika Kenya.
 
Back
Top Bottom