The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Lakini hebu tutafakari. Nitoe hapo mfano tu, unajua kwamba vijana 4,000 kila mmoja akichangia walau elfu 10 tu kwa mwenzi(ambayo ni kama dola 100 kwa mwaka) ifikapo 2010 tutakuwa na bilioni moja za kuwawezesha vijana kuchukua majimbo? Unajua kwamba jimbo moja- kama hutoi rushwa linahitaji kati ya milioni 10 na 20 kushinda? Kwa kiasi hicho unadhani vijana tukiamua kuchukua hii nchi tunashindwa? Mimi naamini, tunaweza. Bila kuwategemea mafisadi kutuchangia mabilioni, tunaweza kwa umoja wetu, fedha zetu za kiadilifu tukiamua kujikamua kidogo tu kwa ajili ya mabadiliko. Tunaweza kabisa, tukiamini- Maneno matupu hayavunji mfupa! Tunaweza kabisa! Tunaweza kupunguza hodhi ya chama kimoja bungeni. Tunaweza, ni kiasi cha kuchukua hatua.

Nimetoa mfano tu- kama unaamini ni mfano ambao unaweza kuwekwa kwenye matendo tuwasiliane tafadhali kupitia mnyika@yahoo.com au 0754694553 tubadilishane mawazo zaidi kuhusu FOCUS 2010

JJ...Nimetafakari, naamini ni mfano mzuri au ni ajenda nzuri ya kuanzia.

Wembemkali
Sasa nini cha kufanya sasa hivi:
1) Ni lazima tuanze mara moja kuwaelimisha wananchi kwa sasa.
Na elimu yenyewe ilenge kwenye mapinduzi ya kuwakomboa wananchi.Ni lazima tuwafikie wapiga kura sasa hivi bila ya kusubiri eti mwaka au miezi kadhaa ndiyo tuanze.Halafu tuwaeleze kuwa Tanzania yenye neema inawezekana kabisa bila ya kusubiri ahadi za za uongo za CCM.Tutumie kila liwezekanalo kufikisha ujumbe huu.Kwa kupitia magazeti,radio binafsi,internet blogs,midahalo,fulana zenye kubeba ujumbe wa mapinduzi,kuongeza mikutano ya hadhara hasa vijijini na kadhalika!

Kwa wembe huo tutafika tick tack...

walakini...
2) Kufunua uozo ndani ya CCM.Wananchi siyo wajinga kama baadhi yetu wanavyofikiri.Zipo sehemu nyingi tu za Tanzania ambazo wananchi wake wameshaamka na huwezi kuenda na kuwapa ahadi za kusubiri ati 2010 mambo yatakuwa safi kama JK alivyosema huku wao wakifa sasa hivi.
Kwa hivyo tufanye kila namna kufichua uozo wote na vilevile kutoa solutions ya nini kingefanyika kama mbadala na siyo kulalamika tu kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu.

Karma hii nzito kujirudia hata vyama vya upinzani kuna uozo...hii hapo juu ndio italeta matokeo kama majungu,blah blah, 'pumba juu ya pumba', na matokeo yake tutabaki kutwapana madongo na kukosa kabisa focus.

Vilevile naamini wananchi siyo wajinga hivyo basi wameona ni nini na lini kutawafikisha 2010! Uozo uliopo watosha kuwafanya wananchi focused 2010! Na pale bin hapa nafikiri sasa liwe jukumu la waandishi wa habari (Investigative Journalism) na wanja la siasa liwe kama nyika!

Yaani tambarare
 
Mnyika,

Sikudhamiria hata kwa sekunde moja kuwa Chadema na Wapinzani watoboe mifuko yao kuanza kuendesha Taifa kwa niaba ya Serikali. Nafikiri hukunielewa.

Hazina kubwa ni mawazo na fikra zinazotekelezeka. Katika mada yangu ya Chadema must Reeform, nimekuuliza je mpo tayari kuweka nguvu zenu za kiutawala na utendaji katika kata, tarafa, wilaya na mikoa na si Kitaifa pekee? Ni yangu ni kuhakikisha kuwa msukumo wa maendeleo ambao utafanya wapinzani wauzike utaanzia kwenye mafungu madogo madog na mwishowe kutapakaa kama vilinge na kujenga umoja mkubwa. Jiulizeni CCM waliwezaje kuwa mashuhuru namna hiyo?

Wao walikuwa na ujamaa vijijini na siasa ya ujamaa na kujitegemea. Ndio mkono wa kiserikali ulitumika kuhakikisha njozi na fikra zinatumika.

Nikiuliza je msukumo wa Chadema ni nini kwa mtanzania wa kawaida, wengi hawajui na majibu mnayotoa ni njoo kwetu kwanza au nenda tembelea katiba na webusaiti!

Ni nani ambaye atataka kwenda kukaa na kupukunyua kurasa kujifunza Chadema yafanya nini badala ya kufanya utafutaji?

Ndio upinzani hauna rasilimali za kifedha za kutosha. Lakini unazembea rasilimali za kimawazo ambazo ni nyingi kupita kiasi.

Tatizo la Watanzania ni njaa na umasikini na hii watu huona suluhisho lake ni pesa pekee au msaada wa hali na mali. Lakini msaada wa kimawazo ambao Mwalimu Nyerere aliujenga katika akili na mioyo yetu haupo tena. Kujituma bila kusukumwa au kutegemea kugawiwa na kusaidiwa kumekuwa ni mwiko kuanzia ngazi ya mtu binafsi mpaka Taifa. Tumekuwa tegemezi wa msaada na kushindwa kutumia fikra na mawazo yetu kwa urahisi na kuyafanya yatumike (bongo lala).

Mwiba katika hoja yake kumnadi Lipumba, anadai, umahiri wa kiuchumi wa Lipumba ni mkubwa sana kuwa hataweza kumsaidia mlima mchicha kujiendesha kwa ufanisi.

Sasa kama mawazo ya Wapinzani ni kuwa wao hawawezi kumfikia mtu wa kawaida in simple terms ili mtu huyu aimarike na wao (nyie) mnasubiri complex issues ndipo tuone utekelezaji wa Itikadi, falsafa na mipango mbinu yenu, basi kamwe hamtaweza kuwa na uwezo wa kuongoza nchi na kuleta mapinduzi.

Nafurahia ufasaha wako kujieleza hapa kwetu ukumbini, naamini wewe ni kijana mwenzangu ambaye katika safari yako ya kujifunza, pamoja na Kitila, mpo wazi kujielimisha kutokana na ubwabwaji wetu.

Je Elimu ya bure mnayoipata hapa natumikaje na vyama vyenu?

Je Vyama vyenu vina idara zilizoshiba ambazo zina wataalamu wa kila nyannja ambao wanaweza kujitolea kuelimisha umma jinsi ya kujitegemea na kuboresha maisha bila kutegemea msaada na kusukumwa na Serikali?

Jee Wapinzani wanafanya nini kuchukua tuzo ya Siasa ya Ujamaa(not communism like Russians but African Socialism) na Kujitegemea ambayo CCM imeacha kuinadi kwa nguvu za vitendo na kubakia kuwa maandishi katika makaratasi?

Tuendelee na shule!
 
JJ...Nimetafakari, naamini ni mfano mzuri au ni ajenda nzuri ya kuanzia.

Sura ya Kwanza

Nashukuru kwa kutafakari. Sasa chukua hatua, kuna mpango umeshaanza kutekelezwa na tayari unaoshabihiana kidogo na huo mfano ambao nimemutoa. Tuwasiliane chemba kama utahitaji maelezo zaidi.

JJ
 
Nafikiri focus ya vyama Tanzania inaweza kuwa sio sahihi kwa mawazo yangu kwa sababu yakutaka kwenda Ikulu mapema. Ikulu patawezekana tu wakati umeweka foundation nzuri. Swala liwe kupata wabunge wengi mengine yatafuata. Imagine kama tungekuwa na akina Zito, Slaa kama kumi tu katika bunge letu, ungeona moto unawaka bungeni. Iweje kiongozi anayevunja sheria alindwe na rais? (karamagi, Dito etc.)

Anyways 2010 inakuja tupo na tutaona jinsi tutakavyopelekana.
 
Mnyika,

Sikudhamiria hata kwa sekunde moja kuwa Chadema na Wapinzani watoboe mifuko yao kuanza kuendesha Taifa kwa niaba ya Serikali. Nafikiri hukunielewa.

Hazina kubwa ni mawazo na fikra zinazotekelezeka. Katika mada yangu ya Chadema must Reeform, nimekuuliza je mpo tayari kuweka nguvu zenu za kiutawala na utendaji katika kata, tarafa, wilaya na mikoa na si Kitaifa pekee? Ni yangu ni kuhakikisha kuwa msukumo wa maendeleo ambao utafanya wapinzani wauzike utaanzia kwenye mafungu madogo madog na mwishowe kutapakaa kama vilinge na kujenga umoja mkubwa. Jiulizeni CCM waliwezaje kuwa mashuhuru namna hiyo?

Wao walikuwa na ujamaa vijijini na siasa ya ujamaa na kujitegemea. Ndio mkono wa kiserikali ulitumika kuhakikisha njozi na fikra zinatumika.

Nikiuliza je msukumo wa Chadema ni nini kwa mtanzania wa kawaida, wengi hawajui na majibu mnayotoa ni njoo kwetu kwanza au nenda tembelea katiba na webusaiti!

Ni nani ambaye atataka kwenda kukaa na kupukunyua kurasa kujifunza Chadema yafanya nini badala ya kufanya utafutaji?

Ndio upinzani hauna rasilimali za kifedha za kutosha. Lakini unazembea rasilimali za kimawazo ambazo ni nyingi kupita kiasi.

Tatizo la Watanzania ni njaa na umasikini na hii watu huona suluhisho lake ni pesa pekee au msaada wa hali na mali. Lakini msaada wa kimawazo ambao Mwalimu Nyerere aliujenga katika akili na mioyo yetu haupo tena. Kujituma bila kusukumwa au kutegemea kugawiwa na kusaidiwa kumekuwa ni mwiko kuanzia ngazi ya mtu binafsi mpaka Taifa. Tumekuwa tegemezi wa msaada na kushindwa kutumia fikra na mawazo yetu kwa urahisi na kuyafanya yatumike (bongo lala).

Mwiba katika hoja yake kumnadi Lipumba, anadai, umahiri wa kiuchumi wa Lipumba ni mkubwa sana kuwa hataweza kumsaidia mlima mchicha kujiendesha kwa ufanisi.

Sasa kama mawazo ya Wapinzani ni kuwa wao hawawezi kumfikia mtu wa kawaida in simple terms ili mtu huyu aimarike na wao (nyie) mnasubiri complex issues ndipo tuone utekelezaji wa Itikadi, falsafa na mipango mbinu yenu, basi kamwe hamtaweza kuwa na uwezo wa kuongoza nchi na kuleta mapinduzi.

Nafurahia ufasaha wako kujieleza hapa kwetu ukumbini, naamini wewe ni kijana mwenzangu ambaye katika safari yako ya kujifunza, pamoja na Kitila, mpo wazi kujielimisha kutokana na ubwabwaji wetu.

Je Elimu ya bure mnayoipata hapa natumikaje na vyama vyenu?

Je Vyama vyenu vina idara zilizoshiba ambazo zina wataalamu wa kila nyannja ambao wanaweza kujitolea kuelimisha umma jinsi ya kujitegemea na kuboresha maisha bila kutegemea msaada na kusukumwa na Serikali?

Jee Wapinzani wanafanya nini kuchukua tuzo ya Siasa ya Ujamaa(not communism like Russians but African Socialism) na Kujitegemea ambayo CCM imeacha kuinadi kwa nguvu za vitendo na kubakia kuwa maandishi katika makaratasi?

Tuendelee na shule!

Rev. Kishoka

Samahani kwa kukuelewa vivyo sivyo.

Hayo mengine nimekupata, tuendelee kuyajadili kule kwenye "CHADEMA must reform"

Mtanzania wa kawaida anachojua tu ni kwamba waCHADEMA wanapinga ufisadi na kutetea rasilimali za Taifa; wanachojua ni Mbowe wa Helikopta anayekemea rushwa ya CCM kwa kuwaapiza, Zitto Kabwe aliyefukuzwa Bungeni kwa sababu ya Dili la Karamagi la Buzwagi, Dr Slaa ambaye ameshika pabaya Balali kwenye BOT na Tundu Lissu ambaye ameshirikiana na Slaa kutaja orodha ya mafisadi. Hizo ndio stori za vijiweni! Ukiwauliza kuhusu falsafa na itikadi hawayajui mambo hayo, changamoto ni CHADEMA kuweza kueleza zaidi sera zake mpaka watanzania wajue kwamba ni chama cha itikadi ya mrengo wa kati chini ya falsafa ya "Nguvu ya Umma", taratibu tutafika. Hatua ya kwanza ambayo tumeanza nayo ni kutoa mafunzo kwa viongozi wetu ngazi za chini, taratibu tutafika. Safari ya maili mia huanzia na moja!

Elimu ya bure tunayoipata hapa inapenya katika akili zetu na tunaitoa tunapokaa katika vikao vya chama ama vya ushirikiano wa vyama ama tunapoandaa rasimu ya nyaraka mbalimbali za kutoa mwelekeo. Tunaitumia pia tunavyopanda jukwaani kuhutubia wananchi ikiwemo huko vijijini. Kwa hiyo, chukulia kila unachoandika hapa kinasadia katika kujenga demokrasia na maendeleo nchini. Sisi ni watumishi na wawakilishi, vyama vya siasa ni taasisi za umma!

CHADEMA ina kurugenzi mbalimbali ambazo zinawataalamu wa fani mbalimbali, lakini hawa pekee hawawezi kutosha kusambaa maeneo mbalimbali nchini. Tunahitaji wataalamu mbalimbali, hata kama wanakazi zao huo mawilayani ama kwenye taasisi mbalimbali watenge japo siku moja kwa mwezi huko walipo kujitolea utaalamu wao kwa ajili ya kusaidia mikakati ya kuleta demokrasia na maendeleo nchini. Vinginevyo, usomi wao utakuwa ni wa kibinafsi kama yule aliyechangiwa chakula chote kijijini avuke jangwa akalete chakula kwa waliobaki wenye njaa, huyo asiporudi ni msaliti! Kadhalika, wasomi wetu wakishindwa kuchukua japo muda mchache kukumbuka wajibu wao kwa wasiosoma na taifa kwa ujumla, nao ni wasaliti. Kama tunaweza kukaa kwenye pub masaa kadhaa tukipiga soga, tujue kuwa tunaweza kabisa kuwa na muda kwa ajili ya hii noble course tukitaka.

Wapinzani wanafanya nini kuchukua tuzo za siasa na ujamaa na kujitegemea? Tunafanya. Mimi na Profesa Baregu tulikuwa kwenye kamati ya kufanya mapitio ya itikadi ya CHADEMA kutenganisha bayana itikadi na falsafa ya CHADEMA katika muktadha wa malengo, sera za CHADEMA na mwelekeo wa Taifa kwa ujumla. Hatimaye katiba ikafanyiwa mabadiliko 2006- nimeweka kwenye "CHADEMA must reform" nakala ya Katiba ya CHADEMA- ukisoma 'itikadi ya CHADEMA ya mrengo wa kati" na falsafa ya CHADEMA ya "Nguvu ya umma" utaona kwamba imechota baadhi ya tunu za Ujamaa na kujitegemea ikachanganya na baadhi ya manufaa ya ubepari. Mchanyato uliopatikana utawezesha CHADEMA ikichukua dola- kuendesha nchi bila dola kuhodhi nyanja zote, lakini kuhakikisha pia uchumi unamilikiwa na wananchi waliowengi na si uchumi unaomilikiwa na kunufaisha kwa kiasi kikubwa tabaka la watu wachache ama wawekezaji kutoka nje chini ya ubepari wa kimataifa wa ukoloni mamboleo.

JJ
 
Nafikiri focus ya vyama Tanzania inaweza kuwa sio sahihi kwa mawazo yangu kwa sababu yakutaka kwenda Ikulu mapema. Ikulu patawezekana tu wakati umeweka foundation nzuri. Swala liwe kupata wabunge wengi mengine yatafuata. Imagine kama tungekuwa na akina Zito, Slaa kama kumi tu katika bunge letu, ungeona moto unawaka bungeni. Iweje kiongozi anayevunja sheria alindwe na rais? (karamagi, Dito etc.)

Anyways 2010 inakuja tupo na tutaona jinsi tutakavyopelekana.

DUA

Nakubaliana nawe. Wabunge wengi ni suala kipaumbele. Na huo ndio mtazamo wetu vilevile, vijana wa CHADEMA tunahitaji vijana wengi zaidi wajitokeze kugombea ubunge 2010, uchaguzi huo ni wa kizazi kipya kwa kweli pamoja na kuwa kila kundi rika lina haki ya kugombea.

Lakini uchaguzi wa urais nao una umuhimu wake kisiasa- kwa kuwa macho na masikio, kwa kiasi kikubwa huelekezwa huko. Ukifutika kabisa katika siasa za urais, unapunguza pia msukumo wa kisiasa kwa wagombea ubunge na udiwani.

Kadhalika, kwa mwelekeo wa CCM wa kufumbia mambo ufisadi na kuwaenzi mafisadi-tegemea chochote 2010. Na kwa kweli, ushindi wa upinzani, pamoja na chama tawala kuwa chama dola na kuminya uchaguzi na huru na haki, bado unategemea pia ni kwa namna gani upinzani umejipanga hususani kwa kuwa na wagombea wenye haiba/uwezo unaostahili na kuwa na oganizesheni/mtandao wa nguvu.

Hii ni changamoto ambayo ushirikiano wa CHADEMA, CUF, TLP na NCCR Mageuzi unapaswa kuifanyia kazi kwa bidii zaidi.

JJ
 
Mnyika,
Ni nini kiliwafanya 2005 vijana kutojitokeza kugombea ubunge kwa wingi? Je wanakosa hamasa zaidi? Hawatambui wajibu na mchango ktk uongozi wa nchi? Ni waoga to take political risks? Lack of resources to mount effecive campaings? Au wazee hawawapi nafasi kugombea!

Unadhani 2010 vijana wengi watakuwa wamehamasika zaidi na kugombea?

Blair alikuwa mbunge by 30 and 15 years later- PM. Well changamoto wanazotoa Zitto Bungeni- it is a good start kwa vijana na inashiria vijana mna potential kubwa- taabu ni kujiamini na kupewa/kuchukua nafasi!
 
Nafurahi jinsi kijana Mnyika anavyojibu maswali anayoulizwa hapa; na kwa kiasi kikubwa nimegundua kwamba majibu mengi ya Mnyika na MAZURI kuliko maswali anayoulizwa. Wasioamini wazidi kuchunguza watatambua maana yangu.

Kikubwa ninachokiona hapa ni kwamba "wajuzi" wengi wanaojadili na "kuelimisha" wengine hapa hawajui siasa halisi. Mnyika anazungumza kutoka 'kazini' anasema anachofanya, watu wanaandika na kukejeli tu hapa kwa siasa za kompyuta, na bado wanataka Mnyika awaamini wao (ajifunze kwao) kuliko anavyojiamini yeye na wanasiasa wenzake mitaani.

Utawezaje kukejeli mchango wa mgombea urais katika kukusanya kura za wabunge wa chama chake? Hebu chunguza kinachoifanya kumshabikia Kibaki sasa - ndiye 'mgombea' wao wa urais, ingawa haitarajiwi KANU wapate wabunge wengi kuliko ODM.

Ukweli ni kwamba kwa mkakati wa sasa wa opposition Bongo, lazima awepo mgombea urais wa opposition kama uniting force, hata kama anajua atashindwa! Bila hiyo hata wabunge hapati. Kama Mbowe, Cheyo, Lipumba na Mrema watagombea ubunge watapata, lakini bado wanahitaji wabunge wengi zaidi ya hao wanne au watano, na nguvu ya kuwapata itatokana na hamasa itakayowekwa na mgombea urais, wapatikane hao 4, a mmoja wao akose kwa kugombea urais lakini aunganishe nguvu zao kitaifa. Kishoka hulioni hili? AU unadhani vyama vya upinzani vilipolisema vilikosea sasa wewe ukilirudia hapa ndipo linakuwa na maana?

Kumbuka pia kuwa ushindi unategemea factors nyingi, hasa unapopambana na chama kikongwe kilichojaa mafisadi...kinachopambana na watu wenye raslimali limited, na ambao wangpaswa kuungwa mkono na jamii lakini inaogopa kuonekana nao...hata hapa kwenye mtandao tunawaona watu wanabehave hivyo.

Mtu makini hawezi kuwalaumu wapinzani kwa kuanika ufisadi wa CCM, na hawezi kusema "I am pissed of" wakati kazi ndo imeanza na inapaswa ishinikizwe hadi mwisho! ndio hizo siasa za kompyuta...anataka walete jingine hilo waliache pale Jangwani au Mwembe Yanga! Lakini hatazami impact ya suala hilo kwa sasa kitaifa.

Ushauri kwa MNYIKA:

Mnyika umekuwa mkweli na muungwana sana hapa JF, lakini bahati mbaya unaozungumza nao huwajui, huwaoni... na wanatumia fursa hiyo kukuchokoza na kukuchota...Kama wanataka siasa kweli waingie, WATAJIFUNZA tofausti kati ya siasa za kweli na porojo za kwenye kompyuta.

Unapomwaga mikakati yenu hapa kwa MIZIMU ambayo huijui (mingine ni ya CCM) na ni mioga ya kufanya siasa, naamini kwamba huwatendei haki wapinzani wenzako wanaokaa kuweka mikakati hiyo na hawadhamirii kuianika hadharani kabla ya wakati wake. Ukitaka ku-argue, waambie wakutafute mfahamiane na mpeane hoja, la sivyo unaumia sana kujadili mambo haya na MASKS za watu waoga kama hawa ninaowaona hapa JF...
 
Kichwamaji

Nashukuru kwa ushauri wako. Ila niliwahi kusema, na narudia tena- tunaweza kujifunza toka kwa yoyote wakati wowote popote- unaweza kujifunza mazuri na mabaya. Cha msingi ni kufanya maamuzi sahihi. Kwa kweli, yahitaji ukomavu na stahamala kuweza kufanya mjadala mahala kama hapa, lakini najua kabisa kwamba muda haupotei bure. Hata kwa wanaouliza kwa nia iliyojificha, majibu yangu najua yanasomwa na watu wengi- najua wapo ambao yanawasaidia kuwafanya maamuzi sahihi na kama tayari wamashaamua basi kuwa na msimamo thabiti katika yale waliyoamua.

Lakini jambo moja siwezi kufanya, nalo ni kuanika mikakati yetu ya ndani- maadili ya uongozi na uwajibikaji wa pamoja hauruhusu hilo. Ndio maana kuna mengine nasema kabisa kwamba hilo siwezi kuanika. Hata ukinitafuta pembeni, bado siwezi kukupa mambo kwa kina kwa kweli- imani hujengwa kwa muda na hutegemea ngazi na kazi.

Cha msingi tu, ulewa kwamba kila nisimecho hapa ni kile ambacho najua mtu yoyote akifanya jitihada kidogo tu angeweza kukipata. Chama cha siasa ni mali ya umma, hivyo mawasiliano na umma kujulisha na kujua kinachoendelea ni nyanja muhimu ya kuongeza ushirikiano na ni daraja la msingi la kutaka kuungwa mkono au kukabalika.

Tuendelee na mjadala- FOCUS 2010

Nakushukuru kwa uelewa wako na ujasiri wako pia. Wengi wetu hapa tuna mengi ya kujifunza kutoka kwako kuliko kujidai tunakufundisha katika siasa - ingawa elimu haona mwisho na inaweza kupatikana kutoka popote. Lakini kwa aquality ninayoiona hapa, wewe ni mwalimu wa wengi wetu. Hongera sana, na asante kwa ukomavu huo.

Najua maneno mengine hayapendezi kwa wengine, lakini kama nao wanataka kujifunza na kuaminiwa hawana budi kuwayakubali haya tunayosema kuhusu quality...ili tuweze ku-improve mijadala ya hapa...
 
Unapomwaga mikakati yenu hapa kwa MIZIMU ambayo huijui (mingine ni ya CCM) na ni mioga ya kufanya siasa,

Ukitaka ku-argue, waambie wakutafute mfahamiane na mpeane hoja, la sivyo unaumia sana kujadili mambo haya na MASKS za watu waoga kama hawa ninaowaona hapa JF...

Kichwamaji

Naamini ujumbe umefika kwa wahusika. Kuna haja ya kuacha uoga na unafiki. Watu wengi wanasema hapa 2010 CCM basi! Lakini ukimuuliza kila mmoja ni wangapi wamechukua hatua zaidi ya kusema tu 2010 lazima CCM ishindwe ama hodhi ya chama kimoja bungeni ipungue- wengi watabaki kimya.

Kuna mambo nimeyasema hapa ili watu wasimame na kuhesabiwa, na nimetoa simu na anuani pepe yangu makusudi ili wale wenye kutaka mabadiliko ya kweli kwa vitendo tuwasiliane. Lakini mpaka sasa nimepokea simu moja tu na hakuna barua pepe hata moja. Ni ama watu hawataki kuwa wakala wa mabadiliko wanayotaka kuwaoga au ni waoga(Mwafrika wa Kike angekuwepo angewaita lile jina analolitumiaga!).

Na kwa kweli nimetumia muda leo kujadili hoja kwa hoja leo ili kuongea hofu na hisia za watu kwamba upinzani hauko makini. Sasa kama hofu zimeanza kuondoka(kama ambavyo baadhi ya waliyouliza wamekiri) lakini bado hakuna kuchukua hatua- lazima itafika hatua tuanze kuwajibishane sisi kwa sisi. Tutaulizana FOCUS 2010- ni dhamira ya kweli, kuchotana mawazo au kufurahisha baraza tu?

Nilitegemea kutokana na mjadala huu wengine tuwasiliane wenye dhamira ya kugombea, wengine tuwasiliane wenye dhamira ya kuwaunga mkono wagombea katika maeneo waliyotoka hususani vijana, wengine tuwasiliane kushirikiana kujenga vyama taasisi nk.

Kwa maneno mengine kichwa maji, naendelea kuhesabu masaa yaliyobaki leo- kama mjadala huu nao utaendelea kuwa ni 'kuuziana chai'; basi nitaacha rasmi kuchangia. Na naamini unakumbuka, nikipotea kama nilivyoaga hutaniona hapa nikichangia kwa muda mrefu sana.

Hivyo usiwe na shaka, leo nimeamua kuitumia siku kuzungumza na umma wa watanzania hapa. Kama ambavyo tunakwenda vile vile kwenye mikutano ya hadhara. Na katika mikutano yangu huwa naruhusu maswali toka kwa wananchi. Tuendelee kujadili- FOCUS 2010

JJ
 
Mnyika,
Unakata tamaa hivyo mapema mdogo wangu at your age?

Muhimu message imefika-sasa ndo kutangaza kususa? Kwa faida ya nani?

Adult human beings are rational beings in making decisions!

Tambua pia audience unayowasiliana nayo- na upeo waliokuwa nao!

Tusonge tu mbele!
 
Kichwamaji,

Ni mimi ambaye unaniandikia hasira yako na hitimisho lako ni kutamka maneno niliyosema "I am pissed off"! Sasa kama wafikiri nampotezea wakati Mnyika, unapotoka!

Mrema na Mtikila, walitumia "tabloid" politics 1995, 2000 na 2005, je Watanzania walichiukua hatua gani? Nothing they made CCM to be the party of choice.

Sijakataa kuanika mafisadi, lakini kutumia kutafuta uchafu na kuanika uozo wa CCM kama turufu ya kushinda uchaguzi si nja ya makini kushinda uchaguzi. Ndio maana nimesema kwa sisis tunaoelewa Siasa za Kitanganyika na uelewa wa Siasa kwenye Demokrasia ya kweli, political smear campaign inaachwa kwenye vijiwe na opposition kuweka nguvu zao katika mkondo wa kisheria unaofanya kazi (Bunge hata Mahakama).

Je ni wangapi wamejiunga na Mtikila katika kesi zake anazopeleka Mahakamani ambazo ni za msingi kabisa kuhusiana na Katiba na Utendaji (Wagombea Huru) ili kuonekana kuna mshikamano? Hakuna, sana sana tunamuona Mtikila ni taahira fulani wakati anayofanya, ndiyo yanayopaswa kufanywa na Wapinzani wote kwa pamja ili kuonyesha mshikamano wa kudai mambo ya msingi ingawa kila chama kina sera zake!

Suala la Muafaka Zanzibar, BOT, Madini, Kiwira, Richmond na ufisadi mwingine hata kama umepita mfano IPTL, Radar, Ndege na kadhalika ni masuala ambayo ni nyeti kuishia katika mikutano ya waandishi wa habari pekee!

Mambo kama haya yanapaswa yashinikizwe Bungeni na wapinzani kwa kupitia kanuni na sheria zilizopo. Kuwasilishwa kwa hoja za kudai kuundiwa kwa kamati za bunge za kuchunguza niliyoyataja hapo juu, ndiyo nja sahihi ya kujenga imani kwa watu, hata kama CCM na Bunge lao la kiimla watapinga (mfano wa Zitto na Karamagi)!

Suala la Zitto kuhusu Karamagi, lilipotea njia awali kutokana na udhaifu wa hoja na ushahidi kuwakilishwa Bungeni ambako kungeshinikiza uchunguzi wa Suala la Buzwagi ufanywe na Bunge na si kuundia Kamati Kibogoyo ya Rais ambayo haitakaa kamwe kutoa suluhisho na tathmini ya maana ambayo itapelekea watuhumiwa kushitakiwa.

Sawasawa na uchunguzi wa BOT, badala ya kushinikiza kuundwa kwa kamati ya Bunge au kuipa madaraka Kamati ya Fedha ya Bunge kupeleleza na kuchunguza ubadhirifu huu kwa kutumia mamlaka yake kisheria (Bunge), kazi imepewa kwa kampuni binafsi na matokeo yake yanaenda kwa Waziri na Ikulu kwanza, yafanyiwe uhariri ndipo Taifa lipewe nakala ambayo imechujwa!

Ndio maana, nimesema " I am pissed off" with technics ambazo zinatumika na wapinzani kuelimisha umma kutumia habari ambazo zinaonekana kuwa ni za udaku na si za kweli!

Solution ni kuongeza uwakilishi wa vyama hivi katika Bunge ili miswaada ya kuchunguza ishu ikifika, basi kura zao zitafanya kazi!

Kuhusiana na urais, nimeuliza, kwa nini wasitafute mtu mmoja mahiri na popular awawakilishe wapinzani wote? Jibu ni kuwa kila mmoja wao anautaka Urais na zaidi, wengine wao ni makuwadi wa CCM. Tayari kuna mgawanyiko katika upinzani ambao unaonyesha wazi kuwa kamwe ufa wao hautaweza kuzibika.

Ni kwa nini kina Shayo, Mtikila na Makaidi wamekimbilia mbali, Cheyo yupo pekee halafu Mbowe, Lipumba, Mrema na Marando upande mmoja?

Will this work?

My passion and opinions are for the sake of Taifa and I am not a stooge who is trying to figure the upinzani best next move. I learn by observation and reading simple details and analyze them and try to provide alternatives that can work on the best interest of opoosition to make sure that the Political Dominance and Un-Accountability of CCM comes to an end!

Hivyo basi kama waona nampotezea wakati Mnyika, huo ni uhuru wa maoni yako, na mtazamo wako na nitauheshimu kwa maana weye na mimi hatujuani!
 
Kuhusu BOT, mkondo wa bunge ulijaribiwa na Dr Slaa alishaandika Hoja Binafsi lakini dalili zilionyesha wazi kabisa kwamba walitaka kuifanyia mizegwe isiingie, umesoma ripoti ya usalama wa taifa ikimshauri Waziri Mkuu Lowasa ahakikishe Kashfa ya BOT kama alivyoiandika Dr Slaa haiingii bungeni?

Katika mazingira hayo, unaweza kumlaumu vipi Dr Slaa kuichomoa hoja yake na kuiwasilisha kwenye mahakama ya wananchi ama bunge la umma? Dr Slaa ni mbunge, kama angeiwasilisha ile hoja mule, kuna baadhi ya mambo angebanwa na kanuni za bunge(naomba niseseme kwa nini ingawa najua kwaninini). Kwa hiyo, alifanya uamuzi wa busara kabisa.

Kuhusu EPA, hili ni tone dogo sana kati ya bahari ya yanayohitaji kuchunguzwa kuhusu BOT na kwa maoni yangu mimi limefanyika ili watu waghilibike kwamba uchunguzi umeshafanyika.

Kura serikali duniani zimewahi kuanguka kwa sababu ya mambo ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka tu; kuna upinzani umewekwa madarakani kwa sababu ya chuki ya watawaliwa dhidi ya watawala wa kiimla fisadi!. Sisi hatujafika huko bado, ndio maana nimesema- tunafanya yote, tunaanika ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka, wakati huo huo, chini kwa chini tunaendelea kujijenga kama chama mbadala na kutoa sera mbadala. Bado tuna safari ndefu kutokana na ukubwa wa nchi.

Lakini watu kama wewe mkibadili mawazo yenu, mkawa na mtazamo chanya juu ya upinzani na kuchukua hatua- hakika tutafika.

Umetaja orodha ndefu ya viongozi wa upinzani! Kumbuka si kila anayesema bwana bwana bwana ndio atayeuona ufalme wa Mungu(natumai unaelewa mantiki ya maneno yangu).

Ndio maana kama ulitazama kipindi cha TVT This Week Perspective kuhusu utafiti wa REDET nimewakosoa sana kwa ku-lump vyama vyote pamoja na kuita upinzani badala ya pamoja na kufanya hivyo, walipaswa kutafuta pia maoni ya wananchi kuhusu Ushirikiano wa Vyama(CHADEMA, TLP, NCCR na CUF) kama entity, na pia walipaswa kutafuta maoni kuhusu individual parties!.

Hata huko ulaya, kuna vyama vingine ni vya kiunamazingira tu(the greens) sasa ulitika ajenda zao ziwe sawa na waende mkondo mmoja na wakue(kwa maana ya kiasi cha kukubalika) sawa sawa na social democrats, socialists, conservatives au liberals? Huwezi kuihukumu CHADEMA kwa yanayofanywa na kila chama kingine kimoja kimoja!

Hilo la kuiongeza wabunge nimeshalizungumza umuhimu wake bila kuondoa haja pia ya kuweka nguvu katika Urais. Kama kuna wanaona uongozi wa Kikwete una mapungufu, unadhani suluhisho litapatikana vipi bila kuigusa na taasisi ya Urais? Yes, wabunge ni priority, but Yes, Urais ni lazima pia.

Cha msingi ni kwamba, chini ya ushirikiano wa vyama- akipatikana mgombea mmoja wa Urais, naamini wengine watakwenda majimboni kuongeza nguvu zaidi.

Mimi nitaendelea kuwa nawe mpaka kieleweke ndugu yangu. Endeleeni na mjadala

JJ
 
Mnyika,
Unakata tamaa hivyo mapema mdogo wangu at your age?

Muhimu message imefika-sasa ndo kutangaza kususa? Kwa faida ya nani?

Adult human beings are rational beings in making decisions!

Tambua pia audience unayowasiliana nayo- na upeo waliokuwa nao!

Tusonge tu mbele!

Kaka Mzalendohalisi,

Tungekuwa wakukata tamaa tusingekuwa huku tulipo. The last thing I can do in struggle is losing hope, losing hope is an automatic defeat.

Nimetangaza kutoweka- majukumu yapo mengi ndugu yangu, hii hadhira ya JF ni punje tu ya haradali katika hadhara ya watanzania ambayo tunapaswa kuifikia na kuitumikia. Hivyo, nikiona ujumbe umefika lakini watu wameamua kwa hiyari yao wenyewe kutoelewa ama kutokukubali na kuendeleza mjadala kwa lengo tu la kubishana, basi unatoweka unawachia muda wa kutafuna ujumbe, unakwenda kwingine.

Na kwa kweli, leo ndio siku yangu ya mwisho hapa. Tutaonana tena hapa siku zijazo! Maneno ya kichwamaji, pamoja na kutoka nje ya mstari katika baadhi ya mambo ni muhimu sana yakatafakariwa.

Tuendelee na mjadala

JJ
 
Rev. Kishoka

umesoma ripoti ya usalama wa taifa ikimshauri Waziri Mkuu Lowasa ahakikishe Kashfa ya BOT kama alivyoiandika Dr Slaa haiingii bungeni?

Rev
Mimi hiyo imenishtua sana, sijui kama unaweza kuni PM hiyo ripoti napenda niisome. Sasa swali linakuja upi ni usalama wa taifa, kupambana na ufisadi au kuulinda ufisadi? Inasikitisha sana kama kweli usalama wa taifa walimtaka PM akandamize kashfa ya BOT, so sad.
 
Kuhusu BOT, mkondo wa bunge ulijaribiwa na Dr Slaa alishaandika Hoja Binafsi lakini dalili zilionyesha wazi kabisa kwamba walitaka kuifanyia mizegwe isiingie, umesoma ripoti ya usalama wa taifa ikimshauri Waziri Mkuu Lowasa ahakikishe Kashfa ya BOT kama alivyoiandika Dr Slaa haiingii bungeni? Katika mazingira hayo, unaweza kumlaumu vipi Dr Slaa kuichomoa hoja yake na kuiwasilisha kwenye mahakama ya wananchi ama bunge la umma? Dr Slaa ni mbunge, kama angeiwasilisha ile hoja mule, kuna baadhi ya mambo angebanwa na kanuni za bunge(naomba niseseme kwa nini ingawa najua kwaninini). Kwa hiyo, alifanya uamuzi wa busara kabisa. Kuhusu EPA, hili ni tone dogo sana kati ya bahari ya yanayohitaji kuchunguzwa kuhusu BOT na kwa maoni yangu mimi limefanyika ili watu waghilibike kwamba uchunguzi umeshafanyika.

It is very disappointing kuona sio tu kwamba "Usalama wa Taifa" (note the quotes) wanaingilia katika mambo ya siasa kiasi cha kumpangia priorities Waziri Mkuu on a purely tyrannical basis, but also kuona upinzani unajua hilo lakini they do not make that an issue.Mnaogopa usalama wa taifa? This is sheer cowardice na ndiyo maana hatuendelei kwa sababu kwa jinsi nchi yetu ilivyooza tunahitaji revolutionaries walio tayari kujitoa mhanga maisha yao na sio calculating politicians.

Sasa tumefikia point hata kuongelea technicalities zinazowafunga kusema ukweli bungeni wanaogopa, either they are too cowardice to be effective or they have awkward skeletons in their own closet.

Both options are dangerous indeed.

What happenned to "kumkoma nyani giladi"?
 
We made it an issue- soma list of shame between lines ama press statement yetu kutoa maelezo ya ziada kuhusu tuhuma za BOT. Dr Slaa made it an issue in Jangwani, perhaps ask the media if it is scared to the rib! Soma pia hoja ya mabilioni yachotwa BOT wakati wa uchaguzi(ile scandal ya Deep Green na wenzake); we categorigacally indicated how much was sent to TISS(Read Usalama wa Taifa) from the private company, this was after finnishing 'their work';

Tundu Lissu bluntly said usalama wa taifa umehongwa kwa kupewa kiinua mgongo!, na ikahojiwa kama ni usalama wa taifa ama usalama wa mafisadi. Changamoto ni kufanya yule mtu wa kijijini afahamu haya, lakini changamoto zaidi ni kufanya ajue kuwa yeye anapokosa hela ya matibabu au anapokamatwa kwa kushindwa kuchagia madarasa ya MMES kuna watu wanaongeza matundu kwenye mikanda kutokana na ufisadi kukuza matumbo yao.

Them belly full but the majority are hungry! The beautiful twin towers, in the beatiful city of the beggars. With the Balali's becoming Madalali wa ufisadi na hatimaye kuigeuza benki kuu kuwa dampo kuu la kashfa za ufisadi!

JJ
 
Mnyika,
Unakata tamaa hivyo mapema mdogo wangu at your age?

Muhimu message imefika-sasa ndo kutangaza kususa? Kwa faida ya nani?

Adult human beings are rational beings in making decisions!

Tambua pia audience unayowasiliana nayo- na upeo waliokuwa nao!

Tusonge tu mbele!

Ni mategemeo ndani ya jamvi hili, kama wanauelewa mpana. Hivyo inashangaza baadhi ya wachangiaji wanavyoleta hoja nyepesi kwa masuala mazito.

Mimi kwa sasa hivi niko kijijini lupaso-Kyela nathibitisha watu wanavyoitikia mwito wa kuchunguza masuala ya madini na masuala ya utawala bora.
 
Mnyika nimekupata, inatia moyo kwamba angalau mmeongea and I was wrong in my earlier analysis.

I understand you may not want to go into bunge's technicalities for tactical reasons, but without even knowing the details I can tell the technicalities are unhealthy if they can be abused to silence genuine opposition.The question is, what is the opposition doing to adress this?

Ni mategemeo ndani ya jamvi hili, kama wanauelewa mpana. Hivyo inashangaza baadhi ya wachangiaji wanavyoleta hoja nyepesi kwa masuala mazito.Mimi kwa sasa hivi niko kijijini lupaso-Kyela nathibitisha watu wanavyoitikia mwito wa kuchunguza masuala ya madini na masuala ya utawala bora.

Bab kubwa, kuwa balozi wa mabadiliko vijijini huko na tupe ripoti ya maendeleo ya mwamko katika ngazi ya vijijini.
 
Back
Top Bottom