Mnyika,
Si lazima mtamke hadharani mipango ya utandawazi wenu kwa Taifa ili tujue mnafanya nini. Vitendo vyenu vitajitangaza.
Kinacho niudhi ni huku kukimbilia majukwaani kulaumu CCM na kuanika Uozo usiosafishika bila na kuwa na nguvu ya dola(majority rule)!
You (Chadema and alliance) are wasting time to keep up with headlines to air dirty laundry of CCM! What Slaa and Zitto have become is like tablid publicists!
What you need is to demonstrate effectivelly that your plans to lead the country can work even without being in power.
Je ni miradi gani ambayo mmekuwa mbele kusaidia kuvunja umasikini, ujinga na maradhi? are your plans and utendaji better than CCM?
You need to start preaching what you can activelly demonstrate to Wananchi to gain their trust and respect which will translate to acceptance when time comes!
As of now, you all look like Mtikila! Walalamishi wasio na mbele wala nyuma na mwasubiri 2009 kuamka ndipo taifa lijue kuwa Chadema ina sera kadhaa ambazo hazifanani na CCM na zinaweza kuaminika.
I can not stand the incompetence syndrome that is spreading in opposition taking great lessons from CCM.
Opposition needs to look and act differently from CCM. One step for them to achieve that is to be open minded to Ideas of new political structure that are in the world today.
Naomba uende kwenye mada yangu ya kuomba Chadema ifanye reform. Nia ya kuanzisha ule mjadala tofauti na huu ni kwa kuwa malengo ni tofauti na njia ni tofauti ingawa end result ni kuingoa CCM.
Hapa nawauliza, mnajiandaa vipi kuchukua uongozi wa Serikali (not Ikulu) 2010? Je mwaaminiana hata huko kuachiana majimbo? mna mtaji mkubwa kiasi gani?
Je sera zenu collectivelly ni kumkomboa Mtanzania na matatizo yake kwanza au ni Kuing'oa CCM tu?
Je wote mna msimamo gani kuhusu Zanzibar na hatima ya muungano?
Rev. Kishoka:
Kukimbilia majukwaani kukosoa si kupoteza muda-ni kutimiza wajibu wa upinzani wa kuwajibisha serikali iliyoko madarakani. It's a watch dog function. So far we have succecceded in being a party against, but we have to invest more into being a party for.
Ila ukisikiliza kwa makini utabaini nyuma ya kuwa 'dhidi ya' kuna kuwa kwa 'ajili ya'. Nichukulie mfano- Zitto alikuwa dhidi ya Karamagi kusaini mkataba wa Buzwagi bila kuzingatia maslahi ya taifa na kufanya hivyo kabla ya mabadiliko ya msingi ya kisheria na mazingira ya kuingia mikataba kufanyika.
Lakini kwa kufanya hivyo, Zitto amesimama pia kuwasilisha na kuwakilisha sera ya CHADEMA ya kutaka rasilimali za Tanzania zitumike kwa manufaa ya watanzania. Hatimaye serikali imeunda kamati ya kupitia sheria na mikataba(pamoja na mapungufu yake tuliyoyajadili) lakini kwa kiasi imetekeleza ilani ya CHADEMA (japo si kwa ukamilifu wake) maana sisi ndio tulisema tutapitia upya mikataba ya yenye utata ikiwemo katika madini.
Dr Slaa alipotaja orodha ya mafisadi alikuwa 'dhidi ya' lakini kwa kufanya hivyo ameweka bayana sera ya CHADEMA ya kuwa mfumo mpya wa utawala wenye serikali adilifu inayopambana na rushwa bila kutazama 'sura ya mtu'; hapa amebeba vizuri rangi nyeupe ya bendera ya CHADEMA inayowakilisha ukweli, uwazi na uadilifu.
Jambo moja nakubaliana nawe- bado hatujaweza kuhusisha vizuri kupanda kwa gharama za maisha, ukosefu wa huduma za msingi za kijamii na huu ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa ili watanzania wajue vizuri zaidi kwanini taifa letu liko lilivyo, na ni kwa vipi kwa sera yetu maisha yao yatakuwa bora zaidi.
Hii ni changamoto kwa kila kiongozi anavyopanda jukwaani.
Lakini kuna changamoto pia; kwa nyinyi ambao mnapata zaidi kusikia kutoka kwenye vyombo vya habari mnapata habari ambazo zimechujwa sana. Nikupe mfano- pale Jagwani, Zitto alizungumza uhusiaono baina ya madini na maisha ya watu- lakini kwa waandishi habari ilikuwa tu ni kusaini mkataba hotelini London ama nyumba ya Rais kuingiliwa, hayo mengine yote hawakuyaona kuwa ni habari.
Dr Slaa pale mwembeyanga alihusisha ufisadi na kukosekana na huduma muhimu za kijamii, lakini hili la huduma halikuwa sehemu ya habari. Nimefurahishwa na habari ya jana ya Tanzania Daima ya "Balali akamatwe" ilichanganya masuala mbalimbali kwa wakati mmoja. Iliweka bayana wakati mjamzito anajifungulia ofisi ya WEO kwa kukosa 20,000( infact ilikuwa ni elfu 20 za mchango wa MMES kwa hiyo ni kama aliwekwa rumande wakati anajifungua) huku Balali anatuhuma za mabilioni anaachwa mpaka sasa. Wakati watuhumiwa wadogo wanauguzwa wakiwa na pingu hospitali, watuhumiwa wakubwa wako huru. Uandishi wa namna hii unasaidia sana kufikisha ujumbe kwa undani wake.
Hili la kusaidia miradi ya kuthibiti umaskikini: Linahitaji mjadala zaidi, tujiulize- duniani kote, kazi ya vyama vya siasa ni nini? Imani yangu ni kuwa tumeweza kufanya vizuri katika miradi mbalimbali katika halmashauri ambazo tumeongoza Kigoma Ujiji, Hai na Karatu; na tuendelea katika halmashauri ambazo tumeanza kuongoza baada ya 2005, sasa tunaoongoza pia Halmashauri mpya moja ya Tarime.
Sidhani kama upinzani unatakiwa kugawa fedha za miradi ya kuondoa umasikin- kufanya hivyo, kuna vikwazo vifuatavyo: Mosi, tutakuwa tunatoa takrima ya maendeleo kwa wananchi toka mifukoni mwa chama ambayo kimsingi ni rushwa, Pili, tutatoa fursa kwa mafisadi nao kuanza kutoa michango hiyo kupitia vyama vyao- sasa mwenye kisu kikali ndio atakula nyama. Tatu, tutakuwa tumetoka katika malengo ya msingi ya chama cha siasa.
Kwa maoni yangu, chama cha siasa ni muunganiko wa watu wenye mawazo yanayoshabihiana kwa lengo la kuchukua dola ili kutekeleza mawazo hayo, na kabla ya kuchukua dola kuiwajibisha dola iliyoko madarakani kwa misingi ya mawazo hayo! Kwa hiyo bidhaa za vyama vya siasa ni 'uongozi', 'sera' na 'oganizesheni'. Kwa hiyo, tunaondoa umasikini kwa kutoa viongozi bora, sera bora na oganizesheni bora.
Kwa sasa pamoja na kuwa upinzani tumewatoa wakina Dr Slaa, Zitto nk ambao wanaiwajibisha serikali kwa sera zinazopinga ufisadi na kutetetea rasilimali za taifa, kwa kweli matokeo ya harakati zao ni fedha zetu za kodi kutumika vizuri zaidi katika miradi ya kuondoa umaskini. Naamini kabisa, serikali ya sasa(pamoja na ufisadi unaoendelea) kwa staili hii ya Orodha ya mafisadi kila mmoja yuko tumbo joto- hivyo, sidhani kama watakuwa na ari, nguvu na kasi mpya ya kufuja fedha za miradi ya kuondoa umaskini kama ilivyokuwa wakati wa Mkapa- sasa kama hali ikiwa nzuri kiasi nani atanufaika kama sio mwananchi? Nani amesababisha manufaa hayo kama si upinzani?
Na ikifika 2009 na 2010 changamoto kwetu ni kuwafanya watu waelewe kwamba wakituchagua sisi tutaingia wenyewe kutekeleza sera hizo vizuri zaidi tofauti na CCM inayofanya mambo machache tena baada ya shinikizo.
Umewahi kusoma mchango wangu kuhusu "Huduma za Kijamii zinazotolewa na Vyama vya Upinzani?", soma utapata mtizamo wangu kuhusu "Nini mchango wa upinzani katika kuleta maendeleo"
Kuhusu Muungano- sera za vyama karibu vyote vikubwa vya upinzani nchini vinataka Serikali tatu.....
JJ