The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

Umenikumbusha nihoji zaidi ile kauli aliyotoa Malecela kule Bariadi wakati wa Kampeni za Uchaguzi mdogo hadi akapelekea wana CCM kuwapiga wananchi na hadi leo sijasikia kesi ya Uchochezi kufunguliwa ila Mrema na Lissu pekee ndiyo wenye maneno ya uchochezi. Jamani CCM nyie kuweni na utu na Mahakama zenu .
 
Mrema amshangaa JK

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima


MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, amesema Rais Jakaya Kikwete amefanya makosa yanayoweza kuleta chuki na machafuko nchini kwa kuzungumzia suala la Mahakama ya Kadhi kanisani.

Mrema alisema kitendo hicho cha Rais kimelenga kumchonganisha yeye (Mrema) kwa wananchi, hasa Wakristo ambao wamembatiza, na kusema kuwa ataonekana amefanya jambo kubwa na baya nchini.

Alisema jana alipozungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho, Magomeni, Dar es Salaam.

Juzi, Rais Kikwete akiwa katika ibada ya kumsikika Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa, alisema hakuhusika kuliweka katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM suala la Mahakama ya Kadhi.

Rais Kikwete aliwaambia waumini wa kanisa hilo kuwa suala hilo kwa mara ya kwanza liliibuliwa bungeni na Mrema, wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

"Mimi sikatai kuwa hoja hiyo niliiibua bungeni, lakini kitendo cha Rais Kikwete kutumia jukwaa la dini kueleza suala hilo kunalenga kunichonganisha kwa wananchi hasa Wakristo, ambako mimi nimebatizwa," alisema Mrema.

Mrema alisema, yapo mambo mengi mazuri aliyoyafanya wakati huo, lakini hayatajwi, na kutoa mfano kuwa aliwahi kuzima mgogoro wa Kanisa la KKT Dayosisi ya Arumeru ambao ungeweza kuleta maafa.

Pia alisema aliwahi kuzima mgogoro ndani ya Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kuchangisha fedha za kufanya mkutano uliokuwa umeshindikana kutokana na ukata, lakini cha kushangaza, hayo yote hayasemwi.

Amemtuhumu Rais Kikwete kuzungumzia suala hilo kanisani, hali akijua ni kosa kuyapeleka mambo ya Waislamu kwa Wakristo, kwani linaweza kuibua mgogoro mkubwa au hata machafuko nchini.

Kutokana na hali hiyo, alisema hivi sasa ameshabaini sababu za kura zake kupungua wakati wa uchaguzi, na kusema kuwa hali hiyo inatokana na watu kuiba hoja zake.

"Hivi Rais Kikwete leo anaporuka na kusema suala la Mahakama ya Kadhi si ilani ya CCM na imewekwa na watu wengine… kama alikuwa halitaki kwanini hakulitoa?" alihoji Mrema.

Akieleza kilichomsukuma kuwasilisha hoja ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi bungeni, Mrema alisema akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani alikuwa akishughulikia migogoro ya ndoa na mirathi ya Waislamu, hivyo aliamua kufanya utafiti wa kuirejesha mahakama hiyo, ili iwasaidie.

Alisema katika uchunguzi wake alikwenda nchini Kenya ambako alijifunza jinsi mahakama hiyo inavyoweza kuendeshwa bila kuleta mifarakano katika nchi.

"….Baada ya kuhamia NCCR-Mageuzi nikiwa mgombea ubunge Jimbo la Temeke niliwaahidi wananchi nikishinda nitashughulikia siala hilo, ili mahakama hiyo irejeshwe.

"Kwa kuwa nilikuwa nimeliweka wazi kwa kila mwananchi, hakuna hata Mkristo aliyelipinga, kwani nilikuwa nimelifanyia utafiti wa kutosha na kila mmoja aliyelisikia aliridhika nalo, ndiyo maana mwaka 1996 nikalipeleka bungeni na likaungwa mkoni na wabunge wengi," alisema Mrema.

Alisema hata alipohamia TLP alimtuma mbunge wake (Thomas Ngawaiya) kulikumbusha suala hilo bungeni ambapo tangu wakati huo tume iliundwa kwa ajili ya kulifanyia kazi, ingawa hawakumshirikisha kama muasisi wa jambo hilo.

Katika mkutano huo, Mrema alionyesha kitabu alichodai alikiandaa mwaka 1996 kikionyesha muundo wa mahakama hiyo utakavyokuwa bila kuathiri maisha ya Wakristo.

Hata hivyo, Mrema alimuonya Rais Kikwete kulipeleka suala hilo kwa wananchi, kwani linaweza kuleta machafuko na kusema kama ameapa kwa Msahafu kutafuta maoni kwa wananchi, kutakuwa ni kwenda kinyume na maagizo ya mtume, kujadili au kuyatolea maoni masuala ya Mwenyezi Mungu.

"Rais Kikwete anasema kuwa atalipeleka suala hilo kwa wananchi wakalitolee maoni, wananchi gani? Yaani unaweza kwenda kumuuliza Mkristo kuwa unaitaka Mahakama ya Kadhi….hii si ni sawa na kwenda kumuuliza Mwislamu akubali kuwa Yesu ni mwana wa Mungu wakati wao wanaamini kuwa Mungu hakuzaa," alionya Mrema.

Alisema kuwa hata huu unaoitwa mgogoro uliopo ni ufisadi unaochochewa na viongozi waliopo madarakani na jinsi viongozi wa CCM wanavyoitumia kwa kueneza propaganda kuwa italeta vurugu, kwani wakati anaiandaa hiyo mahakama hakukurupuka kama CCM walivyoirukia, sasa wanaonyesha kuwa wameshindwa kuitekeleza.


Wakati huohuo, Kaimu Meneja Elimu wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika, Gloria Mazoko, alisema anafurahishwa na kitendo cha Rais kuzungumzia suala hilo, kwani limetoa mwanga hasa kwa watu waliokuwa hawafahamu suala hilo lilikotokea.

Akizungumza na Tanzania Daima , Gloria alisema awali alidhani hoja ya kuwepo kwa mahakama hiyo kuliwekwa, ili kuwavutia wapiga kura hasa wa madhehebu ya Kiislamu.

"Awali nilikuwa na mtazamo tofauti kuhusu kuwepo kwa mahakama hiyo ya kadhi, kwa kweli kitendo cha rais kulizungumzia suala hilo kumenipa mwanga mkubwa na sasa nimeondokana na mtazamo wa awali niliokuwa nao juu ya kuwepo kwa kadhi," alisema Gloria.

Aliongeza kuwa pamoja na suala hilo kuzua mjadala mkubwa, haoni tatizo la kuwepo kwake. Hata hivyo, alishauri kuwa ikiwa kuwepo kwa suala hilo ni utaratibu na haliathiri, haoni sababu ya kutokuwepo.

Katika maoni yake mengine, kaimu meneja huyo alisema kutokana na suala hilo kuzungumzwa kwa kina na watu mbalimbali, kwa sasa limeanza kuleta mtafaruku katika madhehebu ya dini.

Alishauri taasisi za kidini kutofika mahali kusababisha mgawanyiko baina ya Wakristo na Waislamu, kwani inaweza kusababisha mshikamano na muungano uliopo nchini kupotea.

Naye Jerry Tillya, alisema kwa sasa wananchi wamechoshwa na uundwaji wa tume za kufuatilia masuala mbalimbali, akisema badala yake serikali ingetumia fedha hizo katika shughuli nyingine za maendeleo.

"Kila siku tume zinaundwa bila mpango huku wananchi wanataabika, hivi sasa kuna mfumuko wa bei ya vitu mbalimbali vikiwemo vyakula, kwa nini serikali isiunde tume kuchunguza suala hili ambalo lina masilahi makubwa kwa taifa?" alihoji Tillya.

Ofisa Ugavi wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika, Mteme Kungwe, alikubaliana na tamko la Rais Kikwete, alizishauri taasisi za kidini kuendesha mambo yake bila kuwepo kwa mkono (mchango) kutoka serikalini.

Naye Emmanuel Richard, alisema ili kuondoa mvutano ulipo kati ya serikali na Waislamu kuhusu kuanzishwa kwa mahakam hiyo, ni bora pande zote mbili zikakaa pamoja na kujadili suala hilo, kuliko kukaa kimya, jambo ambalo amesema linaweza kuhatarisha amani ya nchi.

Juzi, Rais Kikwete alikaririwa akisema chimbuko kuhusu Mahakama ya Kadhi ni bungeni, na muasisi wake ni Mrema alipokuwa mbunge wa Temeke.

Alisema baadaye hoja hiyo iliwasilishwa na Ngawaiya kwa nguvu ya hoja binafsi na kwamba kwa busara za Spika wa kipindi hicho, Pius Msekwa na kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, Frederick Sumaye, alikataa hoja hiyo kujadiliwa bungeni moja kwa moja kutokana na kile alichokitaja kuwa ni unyeti wake na kuamua kuipeleka katika Kamati ya Katiba na Sheria.

Rais Kikwete alisema baada ya kamati hiyo kukamilisha utafiti na kukabidhi ripoti kwa Spika, alikabidhi serikalini ambako inafanyiwa kazi, ili kutoa ushauri unaofaa.

Taarifa hii imeandaliwa na Mobin Sarya, Hellen Ngoromera, Dauson Harold na Happiness Katabazi.
 
...hahah haha hahah hapo waswahili wanasema kichaka kimepata mnyaji,subirini muone mrema atakavyotumia hii issue kupata attention maana alikuwa hajaipata siku nyingi mzee wa kilalacha
 
Naona huyu mzee wa kiraracha ameelezea kwa utulivu mkubwa na pia amekuwa na falsafa fulani.Point muhimu sana ni kwamba sisiemu waliirukia issue bila maandalizi, na wakajisahau punde baada ya kutwaa dola.Ameendelea kusema hilo suala alikuwa analipeleka katika utaratibu fulani ambao haukuleta mikwaruzo kama ilivyo sasa.Mantiki nyingine ni kuzungumzia suala hilo kanisani,nami nadhani hapo kuna utata kwani ni uchonganishi fulani.Nilichogundua zaidi ni kwamba Mrema anaonyesha ukomavu katika mambo muhimu nilikinganisha na namna muungwana anavyotoka katika issue sensitive inayohusu imani za watu.
 
mrema kwa hili ana point kubwa tena.
kikwete anatafuta kupalilia moto kuni!
tayari ameshaona mvutano baina ya waislam na wakristo kwa nini akamtaje mrema kanisani kuwa yeye ndio mwanzilishi wa hoja hiyo kma si uchonganishi!.

this is also a part of dirty politics ambazo ccm wanatumia.
 
Kikwete siasa hawezi na wala uongozi hawezi. Amepata uraisi kwa pesa za wizi BOT, kwa kuchafua wapinzani wake ccm (Dr Salim), na kutumia pesa za magaidi wa Kiirani (kupitia kwa Rostam Aziz).

Kikwete uongozi pia umemshinda na ona anavyochemsha kwa kwenda kuongelea mambo ya uislam kwenye sherehe ya ukristo. Huyu baba sijui nani ni mshauri wake! Naona inabidi watu wafukuzwe kazi hapa.

Mrema hapa kampiga Kikwete bonge la bao... kisha watu wote weweeeeeeeeeeeeee
 
Mimi jana nilisema sasa kikwete na CCM yake kwanini waliirukia hiyo hoja? Yaani kisa uroho wa madaraka katamka vitu asivyoweza kusimamia.Je kwa maoni yake sasa yeye kama JK anadhani mahakama ya kadhi ina umuhimu au la? Ajibu bila kuweka sanaa

Kajidhalilisha sana kuja kudai hiyo ilikua si hoja yake eti ni ya Mrema.Ona sasa mzee wa kiraracha atakvyoitumia kishujaaa.

Jk tulia mzee, next time tusijeomba wataalamu kutoka nje waje wakupepee maanake hata hapa Tanzania inawezekana wataalamu hawapo pia
 
Mzee wa kiraracha hapa kaonyesha ukomavu kwenye masuala tete, na kamweka JK kwenye angle na naamini kwa jinsi ninavyomjua kwenye hili atalisimamia kwani ndio kapewa exit point .
 
jamani nilisema na narudia kusema,
Raisi wetu anahitaji kati ya mambo makuu mawili

(1) Apigwe msasa wa shule ajue ni wakati gani wa kuongea mambo serious na sensitive siyo muda wote kuleta uswahili swahili katika mambo makini ama

(2) kama ni washauri wake, basi wabadilishwe mara moja kwani hawamfai siku zote wanamrisha kasa na kutoka na maelezo yanayo ibua maswali zaidi ya majibu katika hoja mbali mbali nyeti!

Vinginevyo tukubali kuendelea kushuhudia aibu hii mpaka asubuhi!
Mara maziwa yanachuluzika wadada shule, mara kelele za malngo.. mara hii hoja ya kadhi ni ya mrema si yangu! yaani completely crazy!
 
Hivi inaonekana Mrema alifanya Research ya Kutosha Kikwete akarukia bila research- Hiki kituko kabisa.

Nilimshangaa kuona anaongea na kumweka Mrema kwenye hotuba yake. Hapa ndo kufirisika kisiasa kabisa.
 
Hivi inaonekana Mrema alifanya Research ya Kutosha Kikwete akarukia bila research- Hiki kituko kabisa.

Nilimshangaa kuona anaongea na kumweka Mrema kwenye hotuba yake. Hapa ndo kufirisika kisiasa kabisa.

Unajua lengo la sisiemu kuweka katika ilani suala la mahakama ya kadhi ilikuwa ni kuchota ujiko na kura, bila kutabiri athari za suala tata kama hilo ambalo liko kinyume cha katiba. Sasa muungwana baada ya kuona ahadi haitekelezeki anamsukumia Mrema suala hili. Mrema naye kawashushua kuwa walidandia sera yake bila kujua yeye alipanga kulipelekaje suala hilo kama angeshinda uraisi.

Muungwana awaambie tu Waislamu kuwa sera hiyo ya mahakama ya kadhi haitekelezeki. Mbona Mkapa alikiri kuwa ilani ya sisiemu ilikuwa haitekelezeki? Kwa nini yeye muungwana anaona soo kutamka wazi kuwa mambo ni magumu?

Unajua hii sio mara ya kwanza sisiemu kuiba sera za wapinzani. Kwanza waliiba sera ya chama cha wananchi ya kufuta kodi ya maendeleo ambayo ilikuwa kero kwa wananchi. CUF waliponadi sera hii kwa wananchi sisiemu waliwaponda sana CUF kuwa, iwapo wangeondoa kodi ya maendeleo pesa wangepata wapi za kuendeshea sirikali?

Kwani sasa wao sisiemu wanapata wapi pesa za kuendeshea sirikali? Kabla hatujakaa sawa, wakati wa kampeni za kumpigia Mkapa kura za kugombea kipindi cha pili tukasikia waziri wa fedha Mhe Mramba Basil akisema sirikali imefuta kodi ya maendeleo. Ina maana walikubaliana na sera za CUF. Pamoja na CUF kulalamika kuwa sera zake zimeibwa, nani aliwasikia? Sisiemu wakasema ni sera yao, kwa hiyo sishangai sana kama waliiba sera ya Mrema akiwa NCCR, na sasa inawatokea puani. Wakomae nayo na hiyo kama walikomalia suala la kodi ya maendeleo.

Muungwana anakwepa hoja, atekeleze kama walivyoondoa kodi ya maendeleo ambayo ilikuwa kero sana kwa wananchi.
 
Mimi nikiwaambieni kura yangu kwa Mrema, eti mnanishangaa? Si unaona mrema na research yake akaja na vitu vya uhakika?

Kati ya hawa wawili, naona JK ndio anajikanyaga.
 
Mahakama ya kadhi nadani ya uislamu ni sawa lakini si ndani ya katiba. Serikali ikilipia gharama za kuzindesha itaingilia pia kuchagua waendeshaji. He who pays the piper chooses the tune. Na hapo ndipo mkologanyo katika swala hili utakapokomaa. L a BAKWATA kuwa chombo cha serikal na sio waislamu bado halijasuluhishwa. Viongozi wa dini wasiingize serikali na wanasiasa katika maswala yao. Dini ya wanasiasa ni kura basi. Je mahakam hizi zikifunguliwa nani atakayelipa wafanyakazi na mahakimu? Angalia jinsi jumuia za kiisalamu na kikristo zilivyo nyingi, hazikubaliani kiuongozi japo kiimani wanakubaliana katika mambo kadhaa.
 
Mrema ataka Rais Kikwete kushtaki watuhumiwa wa EPA, Richmond

Na Ally Sonda, Moshi
Mwananchi
17th June 2008


MWENYEKITI wa Chama Cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, amemuomba Rais Jakaya Kikwete, kuwa mkweli na kuwashitaki mahakamani vigogo wote wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika katika kashfa za ufisadi kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na Richmond.

Mrema alitoa ombi hilo juzi mjini hapa , ikiwa ni siku chache tu tangu aruhusiwe kutoka Hospitali ya Rufaa ya KCMC, ambako alikuwa amelazwa kwa wiki moja akisumbuliwa na homa ya mapafu.

Alisema amelazimika kutoa ombi hilo baada ya kuhisi kuwa baadhi ya taarifa zinazotolewa na serikali zinataka kuficha ukweli kuhusiana na kashfa hizo, hivyo kuwaacha wananchi njia panda wasijue zimeishia au zitaishia wapi.

Kiongozi huyo wa TLP, ana wasiwasi na kigugumizi cha serikali kutowachukulia hatua watuhumiwa hao, akitolea mfano kuwa aliyekuwa Mbunge wa viti maalumu, marehemu Amina Chifupa, aliwahi kuhojiwa na vyombo vya dola na kuwataja baadhi ya vinara wa biashara ya dawa za kulevya, lakini hadi sasa hakuna kigogo aliyekamatwa na kufikishwa mahakamani.

''Yule mtoto wa watu (Amina Chifupa) amekufa akipigania nchi yake, sijui kilichomuua wote tunaamini ni kazi ya mungu, lakini wale aliowataja kuhusika na biashara ya dawa za kulevya mbona Rais Kikwete na vyombo vyake vya dola wamekaa kimya?, kama hakutajwa mtu si waelezwe basi ?'' alihoji Mrema.

Alisema watu waliohusika na mikataba feki ya kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond na wale waliohusika na upotevu wa fedha za EPA wanajulikana lakini hakuna hatua zozote za kisheria zinazochukuliwa dhidi yao na badala yake wanajigamba mitaani.

''Hawa wote waliohusika na mikataba mibovu ya Richmond na waliochota fedha za EPA,wasingetakiwa leo hii kuwa uraiani, hawa walitakiwa kuwa magerezani wakati uchunguzi dhidi yao ukiendelea, kuwaachia huru ni kuwaogopa na kuwagwaya,'' aliongeza kusema Mrema.

Alitahadharisha kuwa jinsi watuhumiwa wa kashfahizo wanavyoendelea kuwa huru, ndivyo wanavyojipanga kujiokoa na balaa hilo ambalo chimbuko lake ni kelele za wabunge wa upinzani bungeni.

Alimtaka Rais Kikwete kuchukua hatua sasa za kuwaburuza mahakamani wale wote wenye tuhuma za ufisadi ili sheria ichukue nafasi yake, badala ya kusububiri wananchi waanze kufanya maandamano ya kuwalaani na kuwazomea.

Mrema alisema kuwa wananchi hawapo tayari tena kuona kesi za mafisadi wa EPA na Richmond zinazimika kama zilivyozimika kesi za wauza dawa za kulevya, ambazo alisema hata hivyo wananchi bado wanazisubiri hadi dakika ya mwisho kujua hatma yake.
 
Kama Huyo Sio Fisadi Na Yeye Au Kama Hajawahi Kushiriki Ufisadi Basi Awe Wa Kwanza Kuwashitaki Hao Mafisadi Mbona Hata Siku Moja Hashitaki Yeye Huomba Tu
 
Kikwete Na Yeye Ni Fisadi Jamani Ama Hamuelewi?
 
Kama Huyo Sio Fisadi Na Yeye Au Kama Hajawahi Kushiriki Ufisadi Basi Awe Wa Kwanza Kuwashitaki Hao Mafisadi Mbona Hata Siku Moja Hashitaki Yeye Huomba Tu
\



plz shy jaribu kuwa serious kwenye ishuz za kitaifa.Mnazi mkubwa wewe!
 
Niliwahi kuandika huku nyuma kuhusu mafisadi kadhaa kujaribu kutumia makanisa wa wakristu, mkakati wao ukaja kuonekana wazi kupitia yale ya Rostam na KKKT. Na sasa mkakati huo unaendelea kwa kasi lakini kimya kimya bila vyombo vya habari kuandika ukiendelezwa na Lowassa.

Baadaye nikaandika kuhusu Rostam na wenzake wakina Manji kutakana kuwatumia waislamu, hatimaye ikaja kujulikana wazi na ITV wakaanika kuhusu mikakati hiyo. Baada ya kuanikwa huko, kikundi hicho kidogo cha waislam kimeamua kujitokeza wazi wazi na kueleza bayana dhamaria yao ya kueneza udini na ukabila kupitia mihadhara. Tayari kikundi hicho kimeanza kazi katika mikoa kadhaa.

Wakati Fulani nikawaeleza kuhusu mafisadi kumtumia Mbatia na ikaja kuonekana wazi katika uchaguzi Tarime. Na kiongozi mmoja wa NCCR alithibitisha kuwa fedha za kampeni walikuwa wakichukua kutoka kwa Makamba.

Sasa baada ya NCCR kuonekana imechafuka sana, sasa umepangwa mkakati mwingine wa kuitumia TLP hususani Mwenyekiti wake bwana Augustine Mrema. Mkakati huo utahusisha Mrema kupita katika mikoa mbalimbali kuisema CHADEMA, Mbowe na Reginald Mengi.

Bwana Mrema atakuwa akikosoa ripoti ya jukwaa la wahariri ambayo iliweka wazi jinsi alivyotumia msiba wa Wangwe kutaka kujinufaisha kisiasa. Chini ya mkakati huo Bwana Mrema atajifanya kuwa rafiiki wa karibu na CUF ili kuwatenga na CHADEMA. Vyama hivi viwili vina ushirikiano wa karibu sana bungeni. Duru za uchunguzi zinaonyesha kwamba Bwana Mrema aliwahi kutembelea kiongozi mmoja mkuu wa nchi na kumuomba amuhakikishie kuwa ataendelea kuwa Mwenyekiti wa TLP dhidi ya anaowaita mamluki ambao wanataka mkutano mkuu wa chama hicho uitishwe ili waweze kumng’oa.

Chanzo cha habari kinaeleza kuwa Bwana Mrema alihakikishiwa kuendelea kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa masharti kwamba atumie chama hicho kuwapoteza maboya CUF katika mazungumzo yao ya mwafaka baina ya vyama hivyo na CCM. Mara baada ya kikao hicho, Mrema alifanya kikao kingine na watuhumiwa wawili wa ufisadi kwa lengo la kujadiliana kuhusu kupata fedha ya kuendesha chama hicho baada ya ruzuku ya chama hicho kupungua kutokana na aliyekuwa Mbunge wake Phares Kabuye kuondolewa.

Watuhumiwa hao wawili walimpa sharti bwana Mrema kuwa chama chake na yeye mwenyewe wawe mstari wa mbele kumshambulia Mbowe, CHADEMA na Reginald Mengi. Mwandishi mmoja wa habari aliyepewa jukumu la kuratibu habari za Mrema ameeleza kuwa mkakati mzima kama ukifanikiwa unalengo la kuharibu na kupunguza imani ya upinzani kwa ujumla wake.

Baada ya kumaliza kuishambulia CHADEMA na Mbowe, Bwana Mrema atarejea CCM na kueleza kwamba anarejea CCM kwa sababu ushirikiano wa upinzani umekuvunjika na kwamba wapinzani ni wanafiki. Hata hivyo, Bwana Mrema anakibiliwa na upinzani mkali ndani ya chama chake kutoka kwa kundi la Vijana ambalo limejijenga chini ya aliyekuwa Mbunge bwana Benedict Ntungirehi ambaye analenga kumwondoa Mrema na kuleta mageuzi katika chama hicho.

Hali si shwari ndani ya chama hicho baada ya hivi karibuni, chama hicho kukiandikia barua Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD) na nakala kupeleka kwa Rais Kikwete kikimlaumu Mkurugenzi wa Kituo hicho kushindwa kumtetea Kikwete kama Mwenyekiti wa CCM ambaye ni mwanachama wa kituo hicho alipotajwa kwenye orodha ya mafisadi. TLP imeilalamikia TCD kwa kumtetea Mbowe ambaye alikuwa Mkuu wa Msafara wa safari iliyoandaliwa na kituo hicho ya mjini Afrika Kusini ambayo Naibu Katibu Mkuu wa TLP aliyekuwa kwenye msafara huo aliwahi kumtuhumu Mbowe kuwa alifanya sherehe alipopokea Taarifa ya Kifo cha Chacha Wangwe.

Kati ya makombora ambayo Bwana Mrema amejiandaa kuirushia CHADEMA ni tuhuma kuwa chama hicho kinachukua wanachama na viongozi toka TLP na kuwahamaishia CHADEMA. Kati ya viongozi wanaotajwa ni pamoja na aliyekuwa Diwani wa Kata ya Sombetini Bwana Mawazo na aliyekuwa mgombea ubunge wa chama hicho Arusha mjini Bwana Godbless Lema. Habari kutoka Arusha zinaeleza kuwa wakati Bwana Mawazo alitoka TLP na kujiunga na CCM, bwana Lema si ametangaza kwa waandishi wa habari kwamba si mwanachama wa chama chochote cha siasa kwa sasa.

Hata hivyo Bwana Mrema amesisitiza kuwa wanachama wake hao wasingeondoka chama hicho kama isingekuwa ushawishi kutoka CHADEMA. Mchambuzi mmoja anasema kwamba kama mkakati huo utafanikiwa basi unaweza kuwa mwanzo wa umaarufu wa CHADEMA kisiasa kuporomoka na ule wa Mrema kupanda na kumfanya apokelewe CCM kama shujaa aliyerejea baada ya kukamilisha kazi maalum.

PM
 
This time sijui kama utabiri wako utatimia lakini ni wazi kuna wapinzani wengi sana wanamletea madharau mzee wa Kiraracha. Hizi tuhuma kwamba ni pandikizi mimi haziingii akilini kabisa kutokana na logic....Hakuna logic kabisa kwasababu maisha yake ya kisiasa hayaonyeshi hilo....Hana kashfa ya ufisadi na upinzani kama si yeye husingekuwa hapa...Kama ni mapandikizi yaliletwa upinzani kwasababu yake huko siku za nyuma.

Naweza kusema ni mwanasiasa na wanasiasa huwa na mbinu zao pale inapokuja kwenye kusave maisha yao ya kisiasa.
Kwani hata hapa JF wanazi wengi sana tu si wanasema Mrema keshachoka na keshakufa kisiasa?
Sasa kama thats the case tusubiri tuone.
 
Asante kwa taarif Mkuu, lets wait and see. Itakuwa poa mno kama Mrema akirejea alikotoka maana vitabaki vyama makini tu vya siasa.
 
Back
Top Bottom