The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

....historia ya mrema kwenye siasa za nchi hii haipingiki...nadhani atakayekuja kuivunja ni yule atakayekuja kuiongoza kuiangusha ccm kutoka kwenye madaraka...nadhani tumtarajie kutoka kwenye rika jipya la viongozi au lijalo....

....mrema mwaka 1994 hadi 1999 ..ni mwanasiasa aliyeigharimu serikali ya ccm pesa nyingi sana ..na kuna maafisa wa usalama wengi sana wamekuwa mamilionia kwa kigezo cha vita ya kummaliza mrema.......bajeti ya kummaliza iliendelea hadi 2002..siku hizi sio tisho tena,,...na yeye anajuwa.kuna wengi wamepata uwaziri,ubunge ,ubalozi etc kama reward ya kummaliza mrema....

..kilichobakia kwa mrema sasa ni kuzeeka kwa heshima kulinda heshima yake kwenye mageuzi ..sidhani kama kurudi ccm, kutaponya majeraha aliyokwisha kuyapata kwa miaka yote hii...zaidi anasubiri kufikia mwisho wake kishujaa....ni wazi sasa anatakiwa kustaafu ..ili aweze kuwa mshauri kama kina edwin mtei,bob makani et al.......
 
Mrema alitisha Jukwaa la Wahariri

[Source Tanzania Daima]

na Mobini Sarya

MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, anakusudia kulishitaki Jukwaa la Wahariri na magazeti kadhaa ikiwa hataombwa radhi kwa kuchafuliwa jina lake, kwa kuhusishwa kutoa maneno ya uchochezi kwenye msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mrema alisema anataka magazeti na wahariri waliotumika kumchafua wamuombe radhi kwenye ukurasa wa mbele sambamba na kuambatanisha fidia ya sh bilioni mbili kila mmoja, vingenevyo atawafikisha mahakamani.

“Nataka Jukwaa la Wahariri waniombe radhi ukurasa wa mbele pamoja na magazeti yaliyohusika kunikashfu bila kujali kuwa mimi Mrema nimewahi kuwa Naibu Waziri Mkuu wa nchi hii, Waziri wa Mambo ya Ndani na mbunge wa muda mrefu, kiongozi niliyefanya kazi hiyo kwa uaminifu mkubwa,” alisema Mrema.

Alisema Oktoba 14 mwaka huu, bila kufuata haki, Jukwaa la Wahariri lilitoa taarifa ya upande mmoja iliyokuwa inalenga kumchafua na kukisambaratisha chama chake huku ikisafisha baadhi ya wanasiasa baada ya kudaiwa aligeuza kifo cha Wangwe ‘mradi wa kisiasa’.

Alisema taarifa hiyo ilitolewa baada ya kamati iliyoundwa kuchunguza kama kwenye kifo kile palitokea vitendo vilivyoashiria vurugu, katika ripoti hiyo watu 18 walihojiwa lakini yeye hakuwahi kupewa nafasi ya kusikilizwa licha ya kwamba wahusika wanajua ofisini kwake na namba yake ya simu.

Alinukuu ripoti hiyo pale inaposema ‘kwa mfano Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema, kamati ilielezwa kwamba alitumia msiba huo kuchonganisha familia ya Wangwe na CHADEMA kiasi cha kuwashawishi waishushe bendera ya CHADEMA na kupeperusha ya TLP. Alisema CHADEMA wamemuua Wangwe’.

Alidai licha ya taarifa hiyo kujionyesha kuwa ilikuwa na upungufu, ambayo hakidhi ripoti kamili, lakini viongozi wa jukwaa hilo waliisambaza kwenye vyombo vya habari kwa makusudi maalumu hata pale walipotahadharishwa kuwa inapendelea upande mmoja.

Aliongeza kuwa hata pale ilipofikishwa kwenye vyombo vya habari na ikaonekana kuwa taarifa hiyo inaegemea upande mmoja, wahariri wake walishindwa kujisumbua kuisoma zaidi ili wabaini upungufu wake kisha wamuulize, badala yake waliamua kuiandika hivyo hivyo.

Aidha, alisema katika kuonyesha kuwa ulikuwa mpango maalumu wa kuisambaratisha TLP, baada ya siku mbili alifanya mkutano na vyombo vya habari akaeleza athari za ripoti ile, lakini ni gazeti moja lililoandika habari yake na Jukwaa la Wahariri likishindwa kumuomba radhi hadharani na kumwalika kama walivyokuwa wamedai.

“Kwa kuwa wameamua kutumika kusambaratisha chama changu nimeamua kuwapa siku hadi Novemba 13 mwaka huu wakishindwa kuniomba radhi na kunipatia vibilioni mbili nitakwenda, tutakutana mahakamani wanieleza aliyewatuma wanichafue,” alisema.

Kwa mjibu wa malalamiko yake, tayari ameshampatia kazi wakili, Dk. Sengondo Mvungi kupitia Kampuni ya South Law Chamber kuhakikisha inawafungulia mashitaka wahariri hao.

Wahariri hao ni Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Sakina Datoo, Mhariri wa gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu, Mhariri wa Mwananchi, Theofil Makunga na Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda na Muhingo Rweyemamu, ambaye alikuwa mjumbe wa kamati iliyotoa ripoti hiyo.

Wengine ni mwandishi wa Sauti ya Amerika (VOA) aliyemtaja kama mdhamini wa jukwaa hilo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Saed Kubenea, Katibu wa Jukwaa, Jamila Abdallah na mjumbe, Neville Meena.

MT TAKE: Mrema muda wake umepita hata mwenyewe analitambua hilo. Anaelezea mambo aliyofanya enzi hizo lakini hana la maana la kuonyesha alilofanya siku za karibuni. Katika kila chaguzi anazoshiriki mzee wetu ndivyo anavyozidi kupata uchache wa kura. Sasa anadiriki kutaka kwenda mahakamani kudai vibilioni kadha kutaka kuua magazeti ambayo yamekuwa mwiba kwa mafisadi. Ingefaa ajiuzulu siasa wakati watu bado wanakumbuka mema aliyofanya.

This time sijui kama utabiri wako utatimia lakini ni wazi kuna wapinzani wengi sana wanamletea madharau mzee wa Kiraracha. Hizi tuhuma kwamba ni pandikizi mimi haziingii akilini kabisa kutokana na logic....Hakuna logic kabisa kwasababu maisha yake ya kisiasa hayaonyeshi hilo....Hana kashfa ya ufisadi na upinzani kama si yeye husingekuwa hapa...Kama ni mapandikizi yaliletwa upinzani kwasababu yake huko siku za nyuma.

Naweza kusema ni mwanasiasa na wanasiasa huwa na mbinu zao pale inapokuja kwenye kusave maisha yao ya kisiasa.
Kwani hata hapa JF wanazi wengi sana tu si wanasema Mrema keshachoka na keshakufa kisiasa?Sasa kama thats the case tusubiri tuone.

Hay Mkuu,habari ndio hiyo hapo juu
Once again ushabiki tu...Humu ndani chadema wengi sana humu...Hivi Single D una guts za kumfananisha Mtikila na Mrema?
Unaweza kufanya hivyo kwa wale wageni wa siasa za bongo lakini si wote ndugu yangu...Wengine tuna memory safi sana kwenye issue kama hizi.
Hivi kuna tofauti gani kati ya Mrema na Mtikila katika habari hiyo hapo juu?Kwanza hawa wote ni populists na opportunists.Wanakerwa kuona majina yao yakififia kwa vile hakuna wanachofanya kama wapinzani,na ili kujiweka hai kisiasa wako radhi hata kuwasaliti wapinzani wenzao.

I hope magazeti yaliyoripoti habari hiyo nayo hayajajaa mashabiki wa chadema kama JF (according to wewe Mkuu Mushi).Kwa kifupi ni hivi,mchambuzi yeyote makini atabaini kwamba Mrema anasumbuliwa na njaa.TLP imebaki kuwa jina tu,ruzuku inayopatikana haitoshelezi mahitaji ya chama na Mrema mwenyewe.Nilishahisi Mrema is up to something aliposhikilia bango suala la kifo cha Wangwe.

Anyway,Mrema kishafilisika kisiasa.Pengine kabla ya kurejea CCM ni vema awaulize Ngawaiya na Tambwe,ilikuwaje wakabwagwa kwenye kugombea nafasi ndani ya CCM.Kama anaota kuachiwa jimbo asahau,hicho kinyang'anyiro cha kupitishwa ndani ya CCM hakiangalii cv bali pochi la mtu.To hell with him,amebaki as a dead politician hapo TLP,na akienda CCM wont make a difference except for a few headlines.
 
Alisema kitendo hicho, mbali ya kudhihirisha nia mbaya, ajenda ya siri ya kamati dhidi yake na kutaka kumchonganisha na Chadema na Mbowe, kimemdhalilisha na kumvunjia hadhi na heshima aliyoijenga kwa muda mrefu.

Single D ni vyema kufuatilia kwa makini na ndio maana nikasema ushabiki...Ndugu Mpita njia nakusikiliza ila uje na vigezo vyenye kuonyesha hilo unalosema Mrema kubadilika...Ninapomlaumu ama kuweka mashaka kidogo kwa Mrema ni pale alipo jia align na Mbatia.

Hata hivyo hapo juu kwenye red highlights mnaweza kuona kuwa Mrema anadai kuwa anachonganishwa...Angekuwa kweli ana uadui na Mbowe na CHADEMA basi asingesema kuwa anachonganishwa na kamati bali angesema CHADEMA na Mbowe ni maadui zake.
 
Mrema haendi mahali...Nyie mnaosema muda wake umepita mnatumia vigezo gani?
Wale watu waliokuwa level yake si bado wanapeta tu ndani ya chama tawala? Kweli watu hamna huruma kabisa..Yani mtu aliyejitolea maisha yake kwa wananchi na Taifa lake na kukataa maslahi ya kifisadi mnakuja na maneno ya kebehi kiasi hiki na kudai eti amepitwa na wakati?
Kweli mashetani ni watu.
 
Hay Mkuu,habari ndio hiyo hapo juu

Hivi kuna tofauti gani kati ya Mrema na Mtikila katika habari hiyo hapo juu?Kwanza hawa wote ni populists na opportunists.Wanakerwa kuona majina yao yakififia kwa vile hakuna wanachofanya kama wapinzani,na ili kujiweka hai kisiasa wako radhi hata kuwasaliti wapinzani wenzao.

I hope magazeti yaliyoripoti habari hiyo nayo hayajajaa mashabiki wa chadema kama JF (according to wewe Mkuu Mushi).Kwa kifupi ni hivi,mchambuzi yeyote makini atabaini kwamba Mrema anasumbuliwa na njaa.TLP imebaki kuwa jina tu,ruzuku inayopatikana haitoshelezi mahitaji ya chama na Mrema mwenyewe.Nilishahisi Mrema is up to something aliposhikilia bango suala la kifo cha Wangwe.

Anyway,Mrema kishafilisika kisiasa.Pengine kabla ya kurejea CCM ni vema awaulize Ngawaiya na Tambwe,ilikuwaje wakabwagwa kwenye kugombea nafasi ndani ya CCM.Kama anaota kuachiwa jimbo asahau,hicho kinyang'anyiro cha kupitishwa ndani ya CCM hakiangalii cv bali pochi la mtu.To hell with him,amebaki as a dead politician hapo TLP,na akienda CCM wont make a difference except for a few headlines.

Huwezi kabisa kumfananisha Mrema na Mtikila...Hapo sikubaliaini kwasababu Mrema ana historia ya kulitumikia Taifa kwa uadilifu....Unamshusha sana Mzee wa watu.

Hapa tulipo ni baada ya Mkapa kushinda na ilikuwa Mrema ndio ashinde kama si mwalimu kuingilia kati na wananchi kunyanyaswa huku kura zikiporwa.

Ufisadi huu uliopo ni baada ya gharama kubwa sana iliyotumika na ccm kummaliza Mrema.

Mtu kama Mahita mwenyewe alipofikia ni kwasababu ya Mrema kwa jinsi alivyomdhibiti kwa mabomu kule Arusha na Kilimanjaro...Ndipo Mkapa akampa u IGP...Na wengineo wengi tu kama alivyosema Philemon Mikael.

Suala la Wangwe kila mtu alilishikia bango aliependa kujuwa ukweli...Lakini sijasikia Mrema akisema eti CHADEMA ndiyo walimwua Wangwe...Na Mrema mwenyewe keshasema anachonganishwa.

Wakati huu ambapo wananchi niwazi wamechoshwa na ufisadi...Unaweza kuona jinsi upinzani unavyoanza kupigania maslahi ya vyama vyao...Kila mtu ni mimi mimi na chama changu nk.

Siwezi kupingana na wananchi kama wakiamuwa kuwa Mrema astaafu...Na kuwa wanachama wa vyama vingine vya upinzani...Kwasababu hata nilipotembelea bongo nilikuta watu wakidai kuwa Mrema ni ccm.

Lakini ninavyojuwa siasa na ni jinsi gani Mrema alivyowahi kuwa mwiba mbaya kwa ccm na pia jinsi siasa zilivyo chafu...Basi siwezi kushangaa kwamba ni mbinu za kuchafuana ili kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu...Ndio mawazo ya typical politicians.

Juzi tu ndugu Zitto alitowa ushauri kuwa ni vyema na ccm nao wakapata baadhi ya wabunge ili kuweza kuweka balance...(Endapo CHADEMA itashinda kwa kishindo uchaguzi mkuu wa 2010 Kwa maana hiyo ni wazi kabisa kuwa wasiwasi wa ndugu Zitto ni kwamba kama ikiwa ni chama kimoja tu...Basi maslahi ya chama yatazidi yale ya Taifa humo bungeni...Hili lina ukweli lakini ninabaki na maswali kuwa ni maamuzi gani ambayo wanaCHADEMA wakiyafanya huko bungeni kama wao ni majority yatakuwa ni kinyume na maslahi ya Taifa.Wote tunaelewa kuwa maamuzi ya kifisadi hata wanayoyafanya humo bungeni si sera za chama chao bali ni maamuzi yao ya kimtandao ambayo ni kinyume kabisa na sera za chama chao na pia kinyume na yale waliyowaahidi wananchi na kuapa kwa katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzani kuwa watalitumikia Taifa hili kwa moyo mmoja na kwa uaminifu.

Hivyo ndivyo nilivyoelewa kwasababu sioni ni kivipi kama wabunge hata kama wakiwa wote CHADEMA watashindwa kufanya maamuzi ya muhimu yenye maslahi ya Taifa simply kwasababu wote ni CHADEMA na hakuna upinzani wa ccm....Hata ccm wenyewe si kweli kwamba chama ni kibaya..Ila ni viongozi na itikadi mbaya a kuweka maslaji ya chama mbele...Sasa inaonekana ni kweli kanisa hakuna ambaye hataweka maslahi ya chama kama akichukuwa dola....Huko ndipo hatutaki kurudi tena.

Cha muhimu ni uzalendo....Sasa ikija kwenye siasa uzalendo unawashinda watu....CHADEMA wako vijijini wanafanya kazi...Lakini sioni umuhimu wa kuanza migawanyiko kwasababu zao binafsi nk.

Mimi najadili hoja tu...Sijui msimamo wa wananchi, lakini naamini wananchi ni waelewa na watafanya maamuzi sahihi.

Na wanasiasa kama Zitto,Slaa,Mbowe,Mrema,Lipumba na wengineo ni watu wanaohitajika kuunda serikali na kufanya kazi pamoja kama kweli wanataka upinzani ushinde.

Siasa chafu ziwekwe kando.

Naomba kuwakilisha.
 
Mrema haendi mahali...Nyie mnaosema muda wake umepita mnatumia vigezo gani?
Wale watu waliokuwa level yake si bado wanapeta tu ndani ya chama tawala? Kweli watu hamna huruma kabisa..Yani mtu aliyejitolea maisha yake kwa wananchi na Taifa lake na kukataa maslahi ya kifisadi mnakuja na maneno ya kebehi kiasi hiki na kudai eti amepitwa na wakati?Kweli mashetani ni watu.

Wewe JMushi acha hizo.Yaani Mrema kutulaza nje na sungusungu zake sisi watu waziza ndo ilikuwa level gani ya utawala???Yaani mtu mzima tena mwanausalama wa taifa anashindwa mbinu za kupambana na majambazi anaamua kutulaza nje sisi na kweli utafikiri hapakuwa na polisi??unafikiri tumesahau karaha za huyu bwana Mrema???Mbona sasa hivi hatulindi sungusungu na hali ya amani inatia afadhali kulinganishwa na wakati wa uongozi wa Mrema??Mrema was a failure big time.Yeye mabavu tuu.

Kafungua mavituo meeeeeengi ya polisi yasiyo na kazi sasa kisa alikuwa anajengewa na Wachaga vituo hivyo alimradi wachaga hao wanataka wawe jirani na kituo cha polisi na kujilinda ama kuwasaidia ulinzi.Wewe acha kusema mtu aliyekuwa HANA mbinu yeyote ya kukabiliana na ujambazi.

Ni kiongozi pekee aliyetoa siku saba kwa watendaji wake wa chini na yeye kwenda kwao marangu.Wewe Mushi wewe marangu kuna ofisi gani ya wizara hadi wamfuate yeye huko kama siyo ufisadi wa madaraka.Ni nini ilikuwa agenda ya yeye kufuatwa moshi kisa eti kasema???huo so ndio udikteta????
Nanukuu kauli ya Mrema kwa wanamageuzi "Yeyote atakaejitoa CCM na kuanzisha mageuzi ana matatizo ya akili" Hiyo ilikuwa mwaka 1991.Acha bwana huyu jamaa katutesa saaaaaana.Tena mimi nikimuona namdai jasho langu.
 
N.

...hivi kwa nini mnapiga sana vita WACHAGGA ????..kwani sio watanzania hawa......hii mentality imejengwa kwa muda mrefu kwenye ranks..yet tunasema hakuna ubaguzi tanzania.....kwanini usimuhukumu mrema as mrema ...na sio kwa uchagga wake....there is a problem here ..hata tukijidai kulificha....hawa wachagga waba NO GO ZONE????

historia ipo wazi na chanzo cha hii chuki kujengwa kinajulikana ...tangu 1961..Tusirudi huko...ugomvi wa nyerere na paramount chief ..ni wao ...lakini propaganda zinaenda vizazi kwa vizazi na kuhusicha wasiojuwa chochote....

watanzania ..ni ndugu moja!
 
Mkuu hakuna anaepiga vita wachaga bali ni kutokana na ukweli kuwa Mrema wakati wa Mrema WACHAGA walijenga vituo viiiingi vya polisi.Huu ndo ukweli na hatuwezi kuubadilisha.Mfano mdogo tu mkoa wa singida Wilaya ya Singida mjini kipolisi vituo kama Kibaoni,Majengo,stendi na mitunduruni vyote vilijengwa na Wachaga.Na ni hivyo vituo vinne pekee vilivyokuwa out post.Sasa tusemeje hapo??

Mimi sina chuki na Wachaga.Ukifuatilia post zangu za nyuma kidogo utagundua kuwa hata mke wangu mimi ni Mchaga.So hapa tunaongea kweli bin haki na siyo tofauti.Hoja ni kuwa Mrema alizidiwa na kufunikwa na wachaga.Hakuna ubishi kwa hilo.
 
Si kweli kabisa Majita...Si kweli...Mrema hata baada ya kujitowa ccm alikuwa kipenzi cha watanzania wengi wa makabila tofauti.
 
Mrema haendi mahali...Nyie mnaosema muda wake umepita mnatumia vigezo gani?
Wale watu waliokuwa level yake si bado wanapeta tu ndani ya chama tawala? Kweli watu hamna huruma kabisa..Yani mtu aliyejitolea maisha yake kwa wananchi na Taifa lake na kukataa maslahi ya kifisadi mnakuja na maneno ya kebehi kiasi hiki na kudai eti amepitwa na wakati?
Kweli mashetani ni watu.

Mkuu jmushi1,

1.Tukianza na mapambano dhidi ya ufisadi, hebu nitajie kimojawapo tu ya mafanikio ya Augostine Lyatonga Mrema.
2. Tukirudi kwenye harakati za mageuzi nitajie angalau moja alilolifanya A. L. Mrema kufanikisha hayo mageuzi.

Mimi nimesema nina makovu ya marungu ya polisi dhidi ya wanamageuzi kati ya 1991 mpaka 1994 wakiongozwa na Mrema. Wakati Mrema anadandia hiyo meli, mageuzi yalishapatikana na vyama vya kumsetiri asibaki uchi alipoihama CCM vilishakuwapo. Na hapa naomba usiingize ukabila kwa sababu ni njia ya kukosa hoja.
 
Huwezi kabisa kumfananisha Mrema na Mtikila...Hapo sikubaliaini kwasababu Mrema ana historia ya kulitumikia Taifa kwa uadilifu....Unamshusha sana Mzee wa watu.

Hapa tulipo ni baada ya Mkapa kushinda na ilikuwa Mrema ndio ashinde kama si mwalimu kuingilia kati na wananchi kunyanyaswa huku kura zikiporwa.

Ufisadi huu uliopo ni baada ya gharama kubwa sana iliyotumika na ccm kummaliza Mrema.

Mtu kama Mahita mwenyewe alipofikia ni kwasababu ya Mrema kwa jinsi alivyomdhibiti kwa mabomu kule Arusha na Kilimanjaro...Ndipo Mkapa akampa u IGP...Na wengineo wengi tu kama alivyosema Philemon Mikael.

Suala la Wangwe kila mtu alilishikia bango aliependa kujuwa ukweli...Lakini sijasikia Mrema akisema eti CHADEMA ndiyo walimwua Wangwe...Na Mrema mwenyewe keshasema anachonganishwa.

Wakati huu ambapo wananchi niwazi wamechoshwa na ufisadi...Unaweza kuona jinsi upinzani unavyoanza kupigania maslahi ya vyama vyao...Kila mtu ni mimi mimi na chama changu nk.

Siwezi kupingana na wananchi kama wakiamuwa kuwa Mrema astaafu...Na kuwa wanachama wa vyama vingine vya upinzani...Kwasababu hata nilipotembelea bongo nilikuta watu wakidai kuwa Mrema ni ccm.

Lakini ninavyojuwa siasa na ni jinsi gani Mrema alivyowahi kuwa mwiba mbaya kwa ccm na pia jinsi siasa zilivyo chafu...Basi siwezi kushangaa kwamba ni mbinu za kuchafuana ili kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu...Ndio mawazo ya typical politicians.

Juzi tu ndugu Zitto alitowa ushauri kuwa ni vyema na ccm nao wakapata baadhi ya wabunge ili kuweza kuweka balance...(Endapo CHADEMA itashinda kwa kishindo uchaguzi mkuu wa 2010 Kwa maana hiyo ni wazi kabisa kuwa wasiwasi wa ndugu Zitto ni kwamba kama ikiwa ni chama kimoja tu...Basi maslahi ya chama yatazidi yale ya Taifa humo bungeni...Hili lina ukweli lakini ninabaki na maswali kuwa ni maamuzi gani ambayo wanaCHADEMA wakiyafanya huko bungeni kama wao ni majority yatakuwa ni kinyume na maslahi ya Taifa.Wote tunaelewa kuwa maamuzi ya kifisadi hata wanayoyafanya humo bungeni si sera za chama chao bali ni maamuzi yao ya kimtandao ambayo ni kinyume kabisa na sera za chama chao na pia kinyume na yale waliyowaahidi wananchi na kuapa kwa katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzani kuwa watalitumikia Taifa hili kwa moyo mmoja na kwa uaminifu.

Hivyo ndivyo nilivyoelewa kwasababu sioni ni kivipi kama wabunge hata kama wakiwa wote CHADEMA watashindwa kufanya maamuzi ya muhimu yenye maslahi ya Taifa simply kwasababu wote ni CHADEMA na hakuna upinzani wa ccm....Hata ccm wenyewe si kweli kwamba chama ni kibaya..Ila ni viongozi na itikadi mbaya a kuweka maslaji ya chama mbele...Sasa inaonekana ni kweli kanisa hakuna ambaye hataweka maslahi ya chama kama akichukuwa dola....Huko ndipo hatutaki kurudi tena.

Cha muhimu ni uzalendo....Sasa ikija kwenye siasa uzalendo unawashinda watu....CHADEMA wako vijijini wanafanya kazi...Lakini sioni umuhimu wa kuanza migawanyiko kwasababu zao binafsi nk.

Mimi najadili hoja tu...Sijui msimamo wa wananchi, lakini naamini wananchi ni waelewa na watafanya maamuzi sahihi.

Na wanasiasa kama Zitto,Slaa,Mbowe,Mrema,Lipumba na wengineo ni watu wanaohitajika kuunda serikali na kufanya kazi pamoja kama kweli wanataka upinzani ushinde.

Siasa chafu ziwekwe kando.

Naomba kuwakilisha.

JMushi asante endelea kumwaga dataz
 
Mchango wa Mrema kwa taifa hili ni uliotukuka kabisa. Tusisahau kwenye politics hakuna permanent friend or enemy kuna permanent interest tu. Tukianza kuwahukumu viongozi kwa kauli zao za zamani hatobaki mtu.

Kama ni kweli Mrema anataka kurudi CCM huo ni utashi wake na ni haki yake ya kidemokrasia binafsi sioni tatizo hapo.

Hili la kuwa anataka kuwagombanisha Chadema na CUF na kumkandia mbowe mikoani nipure political Mrema kama Mwenyekiti wa TLP ana haki ya kukulinda chama chake dhidi ya hii surge ya Chadema ya kupoka wanachama wake na ndio siasa mlitaka afanyeje akae na kuchekelea wanachama wake wanachukiliwa left and right no bana.....
 
Si kweli kabisa Majita...Si kweli...Mrema hata baada ya kujitowa ccm alikuwa kipenzi cha watanzania wengi wa makabila tofauti.

Ni kweli Mrema alipotoka CCM alikuwa mwanasiasa tishio.NCCR walifanikiwa sana kuhujumu umaarufu wa Mrema,na hapo TLP imekuwa ni kama sehemu yake ya kustaafu siasa.Mkuu Mushi,tuweke unazi kando,na naomba unjibu angalau moja ya maswali yafuatayo:

1.Ulijisikiaje Mrema alipoishikia bango CHADEMA kuhusiana na kifo cha Wangwe,ilhali alikuwa anafahamu kuwa kwa kufanya hivyo anahujumu upinzani ambao yeye ni mmoja wao.

2.Uliweza kumtofautisha Mrema na Mtikila katika suala hilohilo la kifo cha Wangwe?

3.Unaweza kum-convince mtu kuwa umaarufu wa Mrema haujaporomoka na hivyo haitaji "tukio kubwa" la kumrejesha kwenye chati?

4.Hudhani kwamba Mrema,ambaye licha ya kuwa mchapakazi anapenda umaarufu,anajisikiaje wakati huu ambapo suala la ufisadi linaelekea kufuta umaarufu wake (Mrema) na badala yake kuwaweka kwenye spotlight akina Zitto na Dr Slaa?

5.Mwisho,kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo mwanzo,unaweza kututajia jambo lolote la muhimu lililofanywa na Mrema tangu aingie upinzani?Au kama huko ni mbali sana,basi nini ameshafanya tangu vita dhidi ya ufisadi itangazwe rasmi pale Mwembeyanga?
 
Mimi wacha nikatae kwa nguvu hilo la kumfananisha mrema na Mtikila.Sikubaliani nalo
 
Mimi wacha nikatae kwa nguvu hilo la kumfananisha mrema na Mtikila.Sikubaliani nalo
Ben, kama watu wamefanya mambo yanayofanana ni dhahiri wanafanana kimatendo kama ilivyokuwa kwa Mrema na Mtikila kule Tarime.
 
Itabidi nijifunze kuhus uchaga na historia yake then i will be back. See you then
 
Mchango wa Mrema kwa taifa hili ni uliotukuka kabisa. Tusisahau kwenye politics hakuna permanent friend or enemy kuna permanent interest tu. Tukianza kuwahukumu viongozi kwa kauli zao za zamani hatobaki mtu.

Kama ni kweli Mrema anataka kurudi CCM huo ni utashi wake na ni haki yake ya kidemokrasia binafsi sioni tatizo hapo.

Hili la kuwa anataka kuwagombanisha Chadema na CUF na kumkandia mbowe mikoani nipure political Mrema kama Mwenyekiti wa TLP ana haki ya kukulinda chama chake dhidi ya hii surge ya Chadema ya kupoka wanachama wake na ndio siasa mlitaka afanyeje akae na kuchekelea wanachama wake wanachukiliwa left and right no bana.....
Maneno hayo mekundu yameandikwa na Masatu, Ingekuwa ni jioni ningedhani mvinyo unaharibu macho yangu,lakini muda huu nabakia kuguna tuu. Mhh!!
 
Once again ushabiki tu...Humu ndani chadema wengi sana humu...Hivi Single D una guts za kumfananisha Mtikila na Mrema?
Unaweza kufanya hivyo kwa wale wageni wa siasa za bongo lakini si wote ndugu yangu...Wengine tuna memory safi sana kwenye issue kama hizi.

Mushi,

Unaweza kuwa na kumbukumbu nzuri ya 'mazuri' aliyoyafanya Mrema. Naomba unikumbushe zile Dhahabu za kina Naoushad Mohamed walizokamatwa nazo pale Airport ishu ile iliishia wapi? Maana tuliambiwa Mrema aliwaambia wale Watuhumiwa wamfuate Kiraracha na baada ya hapo hatukusikia tena zaidi ya kwaona kina Mohamed wakipeta Mitaani! Nakubaliana Mrema alifanya mengi makubwa katika serikali ile ya awamu ya pili lakini naye HAKUWA msafi sana...... alikuwa ni Mzee wa Madili yule kwa sasa angeitwa FISADI.

Mimi bado naamini Mrema aliondoka CCM sio kwa kutumwa kama wengi wanavyotaka tuamini. Mrema aliondoka CCM kwa HASIRA baada ya kujua JAMAA wamempiga chini kugombea Urais (ambao aliona hakuna mtu wa kumzuia kwa Umaarufu aliokuwa nao wakati ule) baada ya kuweka kipengele cha Digrii kwenye katiba ya CCM kwa wagombea Urais! Alipoona hivyo ndipo alipoamua kuwa Mzee wa Mabomu kila kukicha anapasua Bomu! Ndipo Rais Mwinyi akamvua Uwaziri kama alivyosema yeye mwenyewe kwa kukosa 'collective responsibility'

Kwa siasa za Tanzania SITASHANGAA kusikia Mrema karudi CCM kwani wapo wengi walisharudi huko! Yuko wapo Lamwai? Yuko wapi Ngawaiya? Yuko wapi Njelu Kasaka? Yuko wapi Ndembela Ngunangwa, yuko wapi Stephen Wassira, ukiacha wale 'wapuuzi' wengine kama kina Hizaa Tambwe na kina Msabaha! Kwa siasa za Tanzania kuwa Mpinzani inahitaji 'msuli' wa nguvu! Wapo viongozi wakubwa kabisa wa Serikali walishatamka hadharani kwamba ukiwa mfanyabiashara ukitaka kufanikiwa ni lazima uwe shabiki/mkereketwa/mwanachama wa CCM. Inawezekana kabisa kwa sasa Mrema anapita kwenye kipindi kigumu cha maisha! Ukizingatia Chama chake hakina au kinaweza kuwa kinapata ruzuku kidogo sana kutoka serikalini. Sidhani kama TLP ina vyanzo vingine vya fedha ili KIJIENDESHE ikiwemo kuwalipa mishahara watendaji wake. NJAA kwa kawaida huwa haina ADABU! Mrema kwa sasa ana NJAA! Kwa njaa yake aliyonayo ni rahisi sana kutumiwa na MAFISADI ili ikifika jioni wawe wamekamilisha malengo yao! Na yeye angalau awe AMESHIBA! Tusubiri tuone maneno aliyoyasema yule Muheshimiwa kuhusu Mrema si ya KUPUUZWA ila tusubiri tu!

Nawakilisha
 
Njaakali nasema nina njaa kali kweli lakini kuna wengi wananizidi kwa njaa kali zaidi na wanaweza kufanya lolote hivi sasa. Kama Ngawaiya mtetemewa yuko kwenye kapu la CCM unategemea nini sasa?
 
Wewe JMushi acha hizo.Yaani Mrema kutulaza nje na sungusungu zake sisi watu waziza ndo ilikuwa level gani ya utawala???Yaani mtu mzima tena mwanausalama wa taifa anashindwa mbinu za kupambana na majambazi anaamua kutulaza nje sisi na kweli utafikiri hapakuwa na polisi??unafikiri tumesahau karaha za huyu bwana Mrema???Mbona sasa hivi hatulindi sungusungu na hali ya amani inatia afadhali kulinganishwa na wakati wa uongozi wa Mrema??Mrema was a failure big time.Yeye mabavu tuu.

Kafungua mavituo meeeeeengi ya polisi yasiyo na kazi sasa kisa alikuwa anajengewa na Wachaga vituo hivyo alimradi wachaga hao wanataka wawe jirani na kituo cha polisi na kujilinda ama kuwasaidia ulinzi.Wewe acha kusema mtu aliyekuwa HANA mbinu yeyote ya kukabiliana na ujambazi.

Ni kiongozi pekee aliyetoa siku saba kwa watendaji wake wa chini na yeye kwenda kwao marangu.Wewe Mushi wewe marangu kuna ofisi gani ya wizara hadi wamfuate yeye huko kama siyo ufisadi wa madaraka.Ni nini ilikuwa agenda ya yeye kufuatwa moshi kisa eti kasema???huo so ndio udikteta????
Nanukuu kauli ya Mrema kwa wanamageuzi "Yeyote atakaejitoa CCM na kuanzisha mageuzi ana matatizo ya akili" Hiyo ilikuwa mwaka 1991.Acha bwana huyu jamaa katutesa saaaaaana.Tena mimi nikimuona namdai jasho langu.

Wewe Majita unaropoka na inelekea huijui Tanzania vizuri. Kwanza hizo habari za kusema eti alikuwa akiwapa watu siku saba waende Kiraracha Marangu whatever si za kweli kabisa..Hii inaonyesha wewe ni mtu uliyekulia kwenye inteligensia za chuki amabazo ni mbovu na si za kweli...Ni false intelligence....Perception mbovu.

Kipindi cha Mrema alipokuwa waziri wa mambo ya ndani ufisadi ndi ulikuwa unapamba moto...Kila mtu anajuwa kuwa kipindi cha Mwinyi kila fisadi na jambazi alichuma na matajiri wa kila aina waliibuka baada ya "RUKHSA"
Na ni kipindi hicho Mrema alipojitowa ccm na aliyapiga chini maslahi yake ya uwaziri na kubakiwa na ubunge kwasababu ya collective responsibility ya kifisadi.

Unapokuwa hukumbuki impact ya ujambazi na ufisadi kipindi kile inanishangaza sana.

Talking about sungu sungu...Hata mimi nililinda sungu sungu na mambo ambayo nilikuwa nikiyaona mimi mwenyewe licha ya kwamba nilikuwa bwana mdogo yalikuwa yakinitisha...Ujambazi na kila aina ya dili zilikuwa zikipigwa na saa nyingine sungusungu ilikuwa ni pingamizi kubwa sana kwa wahalifu wengi na jamii nyingi sana zilikaa kwa amani....Wewe ulikuwa unakaa kwenye jamii isiyokuwa na ujambazi ama uhalifu?

Nimeona mengi sana kipindi hicho cha sungu sungu...Na hiyo ilikuwa usiku...Sasa wewe Majita nakushangaa kwasababu sasa hivi ujambazi wenyewe ni mchana kweupe na ni kama vita kali kabisa ndani ya nchi kati ya majambazi na wananchi kwa kupitia polisi...Hata hapa JF zilikuwa breaking news kibao kuhusu ujambazi wa mchana kweupe....Ina maana hata haina haja ya sungu sungu mchana kwa kipindi hiki ambapo ufisadi juu na ujambazi juu hadi JK mwenyewe akagawa polisi kikanda.

Majita nimerudi hapo bongo na kukuta kumebadilika sana kila mtu ana militia yake.

Hata walinzi wana magobore yao na wao wanajiona kama ndiyo sheria...Polisi wamegeuka majambazi na pia traficks..Ni vurugu tupu tu na hakuna tena ile jamii iliyokuwepo miaka ya nyuma..Chuki nyingi migawanyiko, kutokujali nk.

Binafsi sikubaliani na kila kitu alichfanya Mrema isipokuwa ni mtu aliyekuwa akihitaji support kwani idea zilikuwa nzuri tu.

Unadai eti alikuwa hana mbinu yoyote ya kukabiliana na ujambazi...Wewe unawajuwa majambazi wangapi? Kwa taarifa yako majambazi yaliibuka upya baada ya Mahita ku take over kwa fadhila za Mkapa dhidi ya Mrema.

Kuanzia hapo wakawa wanasindikizwa kabisa na vipira.
Unajuwa ni silaha ngapi zilisalimishwa chini ya Mrema na ni majambazi mangapi yaligive up ujambazi ama kukamatwa?

Mtu aliyeukataa ufisadi kipindi ambacho ufisadi ulishamiri kama vile ni sheria halali ya nchi lakini unajaribu kumzungumzia kwa lugha ambazo si sahihi.

Hizo kauli unazosema za kisiasa niambie ni nani ni perfect halafu na mimi nitakuletea kauli hapa.
 
Back
Top Bottom