The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

mrema hana lolote...anaona uchaguzi umekaribia...
 
Mrema amefulia,anajipendekeza kwa JK ili amuunge mkono kwenye Ubunge Vunjo kama alivyowahi kunukunuliwa.Kama amefikia hali hii mi nadhani akapumzike tu ameshachoka siasa.
 
Goodnes gracious Tanzania!

Mrema anachekesha sana, tena sana tu.

Anasema kwa nini makada wa CCM wasihame CCM kama wanaona Kikwete hafai.

Na yeye angeulizwa, kwa kufuata logic yake hiyo hiyo, kama anaona Kikwete anafanya vizuri kwa nini asirudi CCM?

Au ndiyo anaanza kutoa overtures pole pole?
 
"lakini si kweli kwamba hajafanya maamuzi, tayari amekwisha fanya hivyo na ndiyo maana alivunja baraza lake la mawaziri mara baada tua kujiuzulu kwa aliyekuwa waziri Mkuu..."

Mungu wangu! Hii inaonyesha jinsi gani hata hawa wanaotaka kutuongoza wasivyo ijua katiba ya nchi. Kikatiba waziri mkuu akijiuzulu raisi ni lazima avunje baraza la mawaziri. Leo hii mtu ana kuja kusema Kikwete kuvunja baraza la mawaziri baada ya Lowasa kujiuzulu ulikua uamuzi wake? Halafu huyu mtu ndiye aliye taka kuwa raisi wa nchi na ndiye anaye taka ubunge?
 
mi nafikiri aliposema hivyo alimean kwamba lowasa alipojiuzuri alibadilisha mawaziri ndani ya baraza kwenye hali nyingine angeweza kuchakua tuu waziri mkuu mpya na waziri wa kumplace karamanji lakini hakufanya hivyo....
 
Mlitaka Mrema (SHUSHUSHU) aseme nini zaidi ya aliyoyasema??
muoneeni huruma kwa kuwatumikia mabwana wawili (upinzania na chama tawala)
 
- This is very interesting, maana sio muda mrefu sana hapa JF tuliambiwa kwamba huyu ndiye shujaa wa taifa naomba nisiwataje Members waliotuambia hivyo na kuturushia maneno mazito sana tuliposema kwamba huyu Mrema ni compromise na bado ni agent, maana wengine wanaheshimika sana humu JF.

- Ndio uzuri wa ukweli, huwezi kuuficha hata uukalie vipi utajitokeza tu!

Respect.

FMEs!
 
Mkuu hakuna wa kukuhukumu kwa kusema ukweli. lets truth prevail.
Wataje hao.... maana kuna tabia humu baadhi ya watu wanakuja na mabandiko wasiyoyafanyia uchunguzi.
Piga msumari mzee
 
"Wakati nilipokuwa serikalini mara tu nilipogundua kuwa sipewi ushirikiano wa kutosha na wenzangu katika kupamba na vitendo viovu, nilijiengua na kujiunga na upizani",

What a timely advice!
 
mrema hana lolote...anaona uchaguzi umekaribia...
Mrema amesoma alama za nyakati, ashagombea uraisi zaidi ya mara tatu, na ameona hawezi kushinda uraisi tena kwa udi na uvumba,So this is anotrher opportunity to him!
 
hapa hamjamwelewa Mrema.yeye anachosema hawa wana CCM wanaompinga badala ya kuongea poroo tu kama baadhi ya wana Jamii Forum wanaweza kutumia the right media ya kuukosoa uongozi wa Kikwete. wanaweza kutumia NEC ya CCM kumuondoa kama wanaona hafai. lakini wao ni kuropoka tu, kitu ambacho hakijengi bali kinawafanya watanzania wengi waendelee kumchukia raisi. ndio kila mtu anajua raisi kashindwa kazi yake. lakini wao ni CCM badala ya kumsema mwenzao hadharani inabidi watumie nafasi zao ndani ya CCM kumsema na kwenye vikao tu. wao wanaropoka tu kama wapinzani!!!!!!
 
Mzee Mrema nakuheshimu sana na bado nathamini mchango wako ktk inji hii. Nipo na wewe katika kukuunga mkono uamuzi wako wa kurudi bungeni, ila hili ulilolileta juzi la kujikomba ili usaidiwe hela za kampeni kweli umenichefua sana mzee wangu linakupunguzia heshima yako mbele yangu na watanzania kwa ujumla.

Wengine wamesema umeanza kupoteza kumbukumbu, ila mi najua unafanya kusudi tu ili ufaidike.

We njoo huku jimboni bila hata ndururu ubunge tumeshakupa wasiwasi wako wa nini kuwaangukia watu kwa nini mzee? Leo kiatu cha baniani kimekuwa kizuri?
 
Mrema amejichokea sasa. Kaishiwa kabisa. Nadhani hata vyombo vya habari havina appetite ya kumsikiliza. Kumsifu kikwete kwa uongozi wake mbovu kiasi hiki ni kujipendekeza tu. Ninachomshauri mrema ni kubwaga manyanga ya siasa ili alinde kiasi kidogo cha heshima alichobakiza. Vinginevyo, mwisho wake utakuwa mbaya sana.
 
.
Mhh.Pumba hizi .
hayo ni maoni yake.Njaa hapo imetoka wapi?.Tusiwe kama kasuku.

Naam ni maoni yake na kila mwananchi anayo haki ya kutoa maoni iwe ni ya kuunga mkono au kukosoa.

Mrema alionekana kwenye luninga akiwa ni mmojawapo wa waliopigapicha na Rais baada ya kupata mwaliko rasmi wa kuhudhuria sherehe za Uhuru 9 Desemba. Kupiga picha na Rais si mchezo! Lazima alipata hamasa fulani ya kutaka kumfagilia Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama anachopingana nacho hata kama yeye ni kiongozi wa chama cha upinzani! Mrema atakaposimama kwenye kampeni zake za kugombea Ubunge atakuwa na lipi atakalosema kuhusu CCM ili wananchi wampe kura je ataendelea kufagilia akisaidiana na wana-CCM kufagilia utendaji wa Mwenyekiti wa CCM?!!
 
Kama Mlimani TV na Mrema wote wamepikwa na CCM, na Mkandala anayo Control na influence juu ya Mlimani TV, ni wazi ni midomo ya JK!!. Hapo hakuna ubishi anayebishia ni mbishi tu!
 
mi nafikiri aliposema hivyo alimean kwamba lowasa alipojiuzuri alibadilisha mawaziri ndani ya baraza kwenye hali nyingine angeweza kuchakua tuu waziri mkuu mpya na waziri wa kumplace karamanji lakini hakufanya hivyo....

Katiba hairuhusu hivyo. Inapofika mahali Waziri Mkuu anajiuzuru ni kwamba baraza lote la Mawaziri linajiuzuru na Rais inabidi aunde Baraza jipya. ndicho kilichotokea kulikuwa hakuna alternative ya kuchagua Waziri Mkuu mpya na mawaziri kureplace wale waliowajibika. Hapo hakuchukua uamuzi wowote mgumu ama bora alikuwa anatekeleza wajibu na hilo lilijulikana.
 
Just last week nilikua naongea na UDSM graduate alienimbia kwamba Mrema si mpinzan na akanipa mifano ya maandamano ya wafunzi kupinga CCM ambayo Mrema alipinga vikali na akaenda kuwaomba wanafunzi wasifanye hivyo.
Leo nimeamini.
Mrema, naomba niazime neno kutoka kwa Makamba, ni mwehu!
 
Mkuu hakuna wa kukuhukumu kwa kusema ukweli. lets truth prevail.
Wataje hao.... maana kuna tabia humu baadhi ya watu wanakuja na mabandiko wasiyoyafanyia uchunguzi.
Piga msumari mzee

Baada ya kuandika waliyoandika kuhusu Mrema yawezekana wakawa 'wameokoka' na kuuona mwanga na kujua kwamba walikosea. FMEs peace brother hakuna haja ya kuwataja twende mbele maana wameishapata mwanga mpya na wamejidhihirishia mtu waliyekuwa wakimsupport ni wa aina gani.
 
Back
Top Bottom