kinepi_nepi
JF-Expert Member
- Aug 16, 2007
- 869
- 239
oyaa!! Augustine Lyatonga Mrema atakumbukwa daima.
Ni wazi kila binadamu ana sehemu mbili chanya na hasi. Napenda kuongelea chanya za Lyatonga, huyu bwana ni mwanamageuzi wa kweli.wakati akiwa CCM na NCCR mageuzi niliwahi kuongea nae. Alikuwa na mipango madhubuti na alikuwa anajua anasema nini.Alifuata utashi wake na alitimiza wajibu wake.
Alipoingia NCCR alikuwa na mipango madhubuti ya kumkoma nyani, watu wa kulaumiwa ni akina Lamwai, Mabere na Ringo Tenga. Hawa watu walikuwa wasomi na ndio walikuwa wasanifu wa NCCR, niliwahi kuongea nao na nikiwauliza nini shida mnashindwa kuelewana marandu alinijibu kuwa Mrema anaakili nyingi sana huwezi cheza naye, nikimwuliza ninyi mlitengeza katiba kabla yake kwanini katiba yenu inawashinda, hakunijibu ila ukweli ni kwamba NCCR walitengeneza katiba ya kuwafaa viongozi ndio maana Mrema alipoanza kudili na katiba walishindwa kwani waanzilishi hawakuona mbali, kama vile itakavyotokea pale CCM itakaposhindwa na tume ya uchaguzi.
Mrema ana mengi sana ameyafanya ambayo hatuwezi kuyakataa, ni mwandemokrasia na mwana mapinduzi, alipigwa mishale mingi sana na CCM na kesi za kumwaga, alishaongelea sana matatizo ya tume ya uchaguzi, mgunduzi wa ufisadi wa serikali ya ccm ni chanzo cha kwanza cha kujiuzulu kwa mawaziri wa CCM, mbilinyi na mporogonyi. Mwiba wa mafisadi na wahamiaji maharamia. Mwiba kwa mama siti mwinyi kwenye wizi wa dhahabu. huyu jamaa alisaidia kupunguza wizi na ujambazi majambazi waliomba msamaha na kurjeesha silaha. ni huyu mrema aliye wahi kudhibiti matumizi mabovu ya magari ya serikali. ni huyu mrema aliyedhibiti unyanyasaji wa wanawake. Ni huyu mrema ambaye ameweza kuwa mbunge majimbo mawili moshi vijijini na temeke.
Hata kama kazeeka ni lazima akumbukwe kwa harakati zake za demokrasia tanzania, amepigwa mabomu ya machozi, amekamatwa na polisi na amefunguliwa kesi nyingi kuliko mtu yeyote. tutamkumbuka daima.
Mrema amekuwa mwiba tangia akiwa mbunge wa CCM amewahi kutishia kutoa shilingi kwenye mfumo wa chama kimoja alionyesha machungu na utetezi wa wanyonge hata pale ambapo alikuwa hana wala hapati umaarufu.
Ni lazima tukubali kujifunza kwa mashajaa wetu wa ukombozi wa demokrasia na watetezi wa wanyonge.