The Radar Scandal: Investigation & Progress

Wabongo Naomba Nichukue Muda Huu Kuongelea Upande Mwengine Wa Shilingi. Nafikiri Mimi Ni Mmoja Wa Watu Waliopata Nafasi Ya Kuangalia Huo Mjadala. Linalotokea Hapa Baada Ya Kusoma Michango Ya Waliotangulia Inaonyesha Wazi Kwamba Kuna Jjambo Kubwa Ambalo Maya Be Hamkulielewa Au Mmelielewa Na Kwamba Mnajifanya Kama Hamjaelewa.


Tuambie hilo ambalo hatukulielewa bwana/bibi maneno?

Kwanza, Suala La Siasa Ya Tanzania Ni La Watanzania Wenyewe Na Raisi Anapochukua Ridhaa Hiyo Basi Ni Kwamba Ufanya Kile Kilichobora Kwa Nchi Yake. Mkapa Amenunua Rada Sio Suala Baya. Suala Linalojadiliwa Na Waingereza Ni Kutaka Kuona Uwazi Wa Deal Lenyewe Lilivyofanyika. Namshukrur Mwana Kijiji Alipoeleza Kwamba Deal Lile Lilitakiwa Kuwa Na Sehemu Mbili. Kwa Hiyo Basi, Maswali Ya Kujiuliza Ni Kwamba Je Ni Vibaya Kwa Kununua Hiyo Rada Kwa Wakati Mmoja? Suala La Kamisheni Ni Suala Ambalo Halikuzungumzwa. Waingereza Walikuwa Wanalalamika Kwamba Nchi Kama Tanzania Imekuwa Maskini Na Kununua Rada Haikutakiwa.swali Ni Kwamba Usalama Wako Unaweza Jadiliwa Na Mtu Kweli, Hawa Waingereza Ni Wakina Nani Hadi Watuamulie Nini Cha Kufanya Au Tulalaje ?

Suala Jengine Ni Kuhusu Kauli Ya Mh.kikwete Akiwa Waziri Wa Mambo Ya Nje. Nafikiri Mtakubaliana Na Mimi Nitakjapo Sema Kwamba Ile Ni Kauli Ya Commitment Na Ndiyto Maana Hata Yule Mbunge Aliposema Yalke Maneno Alizomewa.

Wewe ni mgeni hapa katika kuchangia hoja, je umefuatilia hii saga ya Rada katika thread mama hizi hapa kutoka mwanzo? Hizi hapa
http://jamboforums.com/showthread.php?t=1473
http://jamboforums.com/showthread.php?t=1333
http://jamboforums.com/showthread.php?t=1444
http://jamboforums.com/showthread.php?t=1508

Watanzania ndio tutarudisha hiyo fedha habari ya kuzomewa huku Westminster ni jambo la kawaida kabisa katika nyanja ya politics jaribu kupanua mawazo yako.

Mimi Nafikiri Tuangalie Kwetu Sisi, Tuachane Na Hizi Siasa Za West Ambazo Zinaweza Kutugombanisha. Tony Blair Knows What He Was Doing, He Is There Kuhahakikisha Kwamba Usalama Duniani Unakaa Sawa, Hawa Conservative Sidhani Kama Wana Nia Hiyo. Naanza Kupata Wasiwasi Na Hii Siasa Yao Kama Kweli Itatusaidiia Sisi Walalahoi Pale Kipawa, Dar Es Salaam Mjini Au Wengine Uita Bongo.

Usijidanganye ndugu yangu Mwalimu Nyerere alisema hatuwezi kuwa kisiwa. Soma thread mama utaelewa nini tunachoongelea. Hapa hakuna ushabiki wa kijinga.
 
Hofu imetawala Tanzania, waandishi wetu wanaogopa kwani wakiandika habari ambazo sirikali hazipendi watafungia, hofu hofu hofu..........

kazi ya ziada inatakiwa ifanywe kuondoa hofu kwa watanzania, ndani ya vyama na serikali kuna mashupavu hawakubalini na ufedhuli ufanyikao, lakini wamejawa hofu, wakipinga wataonekani si wenzao watatengwa au watapigwa fitna.

tufanyejeje kuondokana na hofu?

wazo kila mtu atume email kwa rafiki yake ili ujumbe ufike kwa kila mtanzania
 
kamishen dola milioni 15!

hivi hao akina mwakitwange walikuwa wapi mpaka aje mdosi kuchukua dili hapo mjini?
 
.




Naanza Kupata Wasiwasi Na Hii Siasa Yao Kama Kweli Itatusaidiia Sisi Walalahoi Pale Kipawa, Dar Es Salaam Mjini Au Wengine Uita Bongo.


Kwa nini unataka watusaidie sisi walalahoi wa Kipawa, kwani hilo ni jukumu lao? Huoni kwamba hili ni jukumu la letu na serikali yetu?
 
Maneno,

Suala la kamisheni liliongelewa kama unavyoona hapa chini:


Mr. Mitchell: The hon. Gentleman may well be making an interesting point, but it is not relevant to the argument that we are exploring.

Despite the opposition of all the most informed, respected and qualified observers, approval for the licences was forced through a divided Cabinet by the Prime Minister. The licences were granted on 20 December 2001. Early last year, the Serious Fraud Office started investigating the deal for alleged corruption. On 15 January 2007, The Guardian reported that some $12 million had been secretly paid into the Swiss bank account of an agent with connections to senior military and Government officials in Tanzania.
 
Daniel Kawczynski: The question that the hon. Member for North Norfolk (Norman Lamb) posed is important, and with all respect to the Secretary of State, I do not think that he answered it. Will he ensure that the World Bank report is published, so that the House can see it?



Hilary Benn: As I said to the hon. Member for North Norfolk (Norman Lamb)—and I think that he was referring to the ICAO report, not the World Bank report, as the hon. Member for Shrewsbury and Atcham (Daniel Kawczynski) says—my understanding is that the Government of Tanzania did not agree the publication of the ICAO report, and we should respect the view that they took on the subject at the time.
 
DrWho, that is what I was talking about.. je wabunge wetu wanaweza kuitaka serikali yetu kuruhusu ICAO kuchapisha ripoti yao hiyo? Kwanini serikali iliwakatalia?
 
DrWho wacha kutuyumbisha kwa hili . Jambo la jana ni nguvu ya wana forum na kamanda Mzee MKJJ sasa Zitto anatokea wapi hapa ?
 
DrWho, Mzee Mwanakijiji,

You real deserve our hi5!!

Kazi nzuri kwelikweli kula leki....
 
Ndugu zangu ile barua ilitumwa kwa wajumbe wengi wa House of Commons, Mitchell, Lamb na Short wote walipata na kama mnaafuatilia ile barua ilihoji siyo tu matumizi ya kumlipa dalali bali maadili mazima ya ununuzi wa kifaa hicho. Na hicho ndicho haswa kilikuwa kinazungumziwa jana. Sasa nimejua ya kuwa hata wasio na sauti wanaweza kusikika kwa wakubwa, lakini kwanini nyumbani hawasikiki. Hii barua nilituma pia kwa wabunge kadhaa nyumbani, lakini hakuna anayethubutu kusema lolote.
 
Bravo MKJJ umekuwa hazina kubwa hapa! Kelele zako haziendi Bure,hata waweke Pamba masikioni watasikia tu!Hawa vilaza wetu wapo Dodoma,wakumbushe tena !kwa kuwasambazia barua hiyo na kuwataarifu kuwa haya yamezungumzwa UK,kwenye House of commons.Tunataka Bunge active sio watu wa kwenda kulala Bungeni!
 
Hivi wabunge wetu wakisimamisha masikio, Richmonduli atawafanya nini?
 
On a flip side

Je kuna mkono wa ZITO KABWE katika hili lilotokea jana?

SASA NAONA DR.WHO UMEKOSA LA KUONGEA. HUYO ZITO KABWE NDIYO NANI KATIKA HILI. MIE NAFIKIRI HUJUI UNACHOKISEMA. HUYU MWANAKIJIJI AMEFANIKIWA KUINGIZA UJUMBE NDANI YA PARLIAMENT UNAJADILIWA NA HAKUNA LOLOTE LA ZIADA. MIE NAFIKIRI ACHA SIASA ZAUJINGA., WEWE NI PANDIKIZI TUMESHAKUSHTUKIA...U MNAFIKI AMBAYE SIJUI UKAE WAPI. NAKUONEA HURUMA KWA SABABU NYINYI NDIYO WALE KAMA WAKINANANII WANAOJIFANYA KWAMBA NI WEMA KUMBE HAKUNA LOLOTE WANATUMIWA NA HAO MABWANA NIWAITE.TOA HABARI AMBAZO HAZIHUSU.

SHAME ON YOU FOR A POINTLESS.
 
Hapo Maneno umekuwa mkali mno bila sababu. Yaani, Dr WHO kuuliza kama kuna mkono wa Zitto kunamfanya vipi kuwa pandikizi? Naona tuheshimu kauli mbiu ya MMKJJ: "Hoja hujibiwa kwa hoja"! na wala sio kwa matusi!
 
Mie natoa hongera kwa Mwanakjj na wote wana JF kwa kumpa moyo Mwanakjj na kuandika barua hiyo.
Ila pia ni vizuri westerners tukawaambia wazi kuwa hatuoni haja wao kutuimbia mambo ya utawala bora na kutuondolea umasikini kama wameshindwa kuelewa umuhimu na kipaumbele katika matumizi bora ya pesa za masikini.Tanzania haikuwa na immediate threat au vita kutoka popote,lakini ina vita ya umasikini wa kupindukia.Vita ya umasikini haipiganwi kwa kutuuzia radar. Hii issue imeoneka ndogo kwa kuwa tu hii rada imetoka kwao.Ingekuwa inatoka Urusi moto wake Tanzania ingeuona.
Mwisho hawa vilaza wa Tanzania(wabunge),nao waambiwe kuacha ujinga na waone aibu.Inakuwaje watu ambao hatukuwachagua tumewalalamikia angalau wameweza kuzungumzia hilo suala na wao wanakaa kimya!!Watumiwe pia hayo mazungumzo na tuwaambie huo ni mwanzo wa mapambano yetu dhidi ya udhalimu wa serikali.Kama hawatakuwa tayari kutusemea tutatumia kila njia kuhakikisha ujinga unaofanyika unaanikwa hadharani.
 
vilaza wapo dodoma wanahemea per day,yaani inakatisha tamaa tulioibiwa hakuna hata mbunge mmoja ambaye angalau kachomekea neno hadi leo,wabunge wa uingereza wana uchungu utafikiri pesa iliyoibiwa ni yao wetu aah kimyaa wanaogopa kamati za chama na wale wa upinzani wanaogopa kunyimwa vitripu vya kuandamana na muungwana zomboka
 
Hongereni Wanabodi wote kwa mchango wenu na hususan Mzee wa Kijijini...

Nimejaribu kufuatilia mjadala nikajaribu kuelewa baadhi ya mambo. Mengine nimeshindwa. Nilipitia hoja kama ifuatavyo:

System use: Dual civilian-military (Watchman)

Coverage Capacity: One-third of territory

Price: USD 40m

Broker’s Commission: USD 12m


How much was to be paid for the remaining part of the system to cover the whole country?

Claim: Outdated; low capability

Response: Still used in 8 regional airports in the UK; Long-range military capability. Other countries have bought similar type, but at lower cost.

Observation: System four times larger the country’s needs!

Question: How could ICAO and WB then claim that the system was inadequate?

Observation: Purchase was through an open tender where 4 companies did bid.

Question: Were the ICAO and WB fighting for the lost bidders or was it a genuine concern?

Claim: Tanzania did not need the military system given its low military traffic (There are nine aeroplanes—six MiG-1s and three MiG-17s—and 10 Bell Huey helicopters).

Response: System in operation todate and has improved air traffic control and increased revenues

Claim: System was four times expensive

Response: ?

Claim: Sale approval did not follow procedure (system built even before UK cabinet approval

Response: ?

Prime suspect: Tony Blair!

Witnesses: Brokers, GoT officials, WB, ICAO

INVESTIGATION CONTINUES
 
Mwanagenzi, kazi nzuri hiyo... ila kuna ripoti ambayo serikali ya Tanzania haitaki iwekwe hadharani, ripoti hiyo ndiyo kiini kitakachofungua kama kweli tulihitaji rada hiyo na kama tulipata dili nzuri au ndio tuliingizwa mjini mchana kweupe.
 
Mwanagenzi, kazi nzuri hiyo... ila kuna ripoti ambayo serikali ya Tanzania haitaki iwekwe hadharani, ripoti hiyo ndiyo kiini kitakachofungua kama kweli tulihitaji rada hiyo na kama tulipata dili nzuri au ndio tuliingizwa mjini mchana kweupe.


Hii ripoti ndio inayoleta mzozo maana kwa nini ripoti iandaliwe na WB halafu Serikali y Tz iwe na sauti ya kusema itolewe au isitolewe...!!
 
Back
Top Bottom