The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Invisible,
Mkuu unganisha hii na ile ya Chenge na Dr. Idrissa wanangojea nini?
 
..inawezekana Dr.Rashidi na Chenge ni wanamtandao. ikiwa hivyo Raisi huyu tuliyenaye hawezi kuwachukulia hatua.

..halafu na sisi wananchi tukubali kwamba tulichukuliwa msukule na wanamtandao.

..kinachotokea sasa hivi ni sawa na mtu anayekurupa kutafuta shuka wakati majogoo yanawika.
 
Duhhh,

.....kweli kabisa sijui Chenge na Rashidi kwa nini mpaka sasa hivi ni viongozi.......tunataka kusikia nao wamefikishwa Kisutu kwa Hakimu Hezron.........
 
swali langu ni kuwa tuhuma dhidi ya Chenge na Dr. Idris ni kubwa mno. Ni kubwa kiasi cha kutisha. Sasa kinachongojewa ni nini?

Hivi SFO wakisema hawawashtaki na sisi tusiwashtaki?

Kwanini tusiamue kufuta tu makosa yote ya nyuma tuanze na ukurasa mpya?
 
swali langu ni kuwa tuhuma dhidi ya Chenge na Dr. Idris ni kubwa mno. Ni kubwa kiasi cha kutisha. Sasa kinachongojewa ni nini?

Hivi SFO wakisema hawawashtaki na sisi tusiwashtaki?

Kwanini tusiamue kufuta tu makosa yote ya nyuma tuanze na ukurasa mpya?

Mwanakijiji,

Muamue na nani?au waamue wao..Mara ngapi tumewaeleza hawataki kusikia..

Tatizo ni viongozi wengi tulionao wameingia madarakani kwa pesa ya Rushwa hivyo hawawezi kuwafunga wenzao kwa kesi ya Rushwa
 
Invisible,
Mkuu unganisha hii na ile ya Chenge na Dr. Idrissa wanangojea nini?
Yap mkuu Mkandara, ni lengo langu kuwa hizi mbili ziunganishwe lakini target kubwa ilikuwa nianze kuiweka hii kando ili wenye uhitaji wa kung'amua wang'amue mapema baadae mjadala uendelee.

They'll be merged after 3hrs (from now).

Thanks...
 
Wapo kwa sababu watawala wengine wanafanana nao.Huwezi kuchukuliana na mwovu kama wewe sio mwovu!

toleola25.jpg
 
Kinachoweza kuwabadilisha watu ni kusimamisha sheria...
Sisi sote ni reflection ya viongozi wetu kwa sababu sheria zetu ni butu, lakini kama tunaweza kuchukia Ufisadi kama tunavyochukia vibaka wa Kariakoo basi bila shaka wananchi wote kwa ujumla tutabadilika...
Ni kweli kabisa kuwa hujuma yoyote dhidi ya uchumi wa Taifa huitwa ujanja..ni sifa kubwa kuvuta deal serikalini ukifahamu kwamba nyayo zako ziko covered na sheria butu.

Mimi nina hakika kabisa kusimamisha sheria ndio msingi wa mienendo ya binadamu wote..maneno matupu na viapo kuwa rushwa ni adui wa haki - sintatoa wala sintapokea rushwa ni hadithi tupu kama hakuna sheria na utamaduni unaofikisha ujumbe huu kwa wananchi wote...Na kwa bahati mbaya CCM wamekuwa mbele kuweka ubani kufukiza azimio lao la Zanzibar...

Mnategemea nini kama kiongozi wa chama mtu kama Makamba anayekuja wambia wananchi wake kwa ujeuri na majigambo kuwa chama ni safi isipokuwa kuna baadhi ya watu ndio wachafu wakati mwongozo wa chama chake unasisitiza kuwa:-

"Kiongozi wa CCM katika kukijenga na kukilinda Chama ni kubwa. Athari katika Chama za Kiongozi kutenda maovu, au kutotimiza wajibu, ni kubwa kiasi kwamba Maadili yake yakitetereka Chama kitavurugika; na nchi itakwenda mrama."

Umeongea Mkandara, nchi tunaweza kuimba sana kuwa tunafuata utawala wa sheria lakini ni usanii mtupu. Mifano, ikionekana sheria itamuumiza mkubwa ndio unasikia statement za "leteni ushahidi", hivi Chenge alipotuhumiwa tu kuwa ana mamilioni ameficha nje sijui kama kuna wahusika walienda hata kuchungulia tume ya maadili kama ame-declare utajiri wake.

Mfano mwingine ambao huwa unachochea sheria kuwekwa kando na maslahi ya wakati kuwa muhimu ni wakati wa kukaribia uchaguzi utasikia viongozi wa CCM wakikemea viongozi serikalini wasije wakatekeleza wajibu wao kama kuhamisha machinga etc...wakiongopa kukosa kura. Kwa maslahi ya chama na watu wachache ni bora hata kama sheria zitapindwa. Hii imejijenga sana kwa wananchi kiasi kwamba sasa mtu ukisimamia sheria unaonekana mbaya na una roho mbaya tu.

Well, huu ni mzizi uliopandwa kwa muda mrefu na itahitaji kujitoa kweli kweli ili watu wanyoke.
 
swali langu ni kuwa tuhuma dhidi ya Chenge na Dr. Idris ni kubwa mno. Ni kubwa kiasi cha kutisha. Sasa kinachongojewa ni nini?

Hivi SFO wakisema hawawashtaki na sisi tusiwashtaki?

Kwanini tusiamue kufuta tu makosa yote ya nyuma tuanze na ukurasa mpya?

Ajali kazini. Uongozi wa wa JUU WA serikali ya CCM na CCM yenyewe kwa kua kwa ujumla wao karibu wote wameoza wanaona kama walichofanya Chenge na Rashidi ni halali, lakini imetokea ajali ndogo - yaani bahati mbaya.
Kuiangusha CCM ndio itakua hatua ya kwanza kubadili yote haya. CCM wana kiburi cha kutawala muda mrefu kiasi kwamba hawaoni mbali na pua yao. Inawezekana hata chama KITACHOCHUKUA MADARAKA kimeambukizwa ugonjwa wa CCM, lakini tutaendelea kubadili chama tawala mpaka tutapata chama SAFI.
CCM walipata ridhaa ya kutawala kwa 80%, kimsingi ina maana wanapendwa sana hata tukidai waliiba kura wala haisaidii. Njoo tushirikiane kung'oa CCM, hio ndio dawa. Njia zingine km kupindua, ama Jeshi kuingilia nk zimepitwa na wakati na zinaleta mateso zaidi kwa raia. Usikose kupiga kura.
 
Mkuu Mwenzangu FMES,

Nchii ilianza kuangakuka Pale viongozi walipoamua kuwa matajiri kupitia Vyeo vyao walivyopewa. Dhambi hii ilianzishwa na wachache na wengine wakaamua kuifuata kwa kuogopa kuchekwa wakimaliza uongozi wao serikalini. Serikalini hakuna Maadili hata kidogo, kila mtu anajiona yeye ana uwezo wa kimaamuzi kuliko mtu yeyote.

Nchi ilianza kupotea pale Wafanyakazi wa Umma waliopoanza kuajiriana kutokana na ukabila,Udini na ukanda. Hii ilichangai kuvunja maadili na miiko ya Uongozi sababu kila mtu ana mtu nyuma yake... Hata Masha ana mtu nyuma yake kwa sasa!

Watu wa kulaumiwa katika hili,mmoja wapo na Mamvi nd ndiyo maana Mwalimu alikuwa akimpinga,Huyu ndiye aliyeonesha kuwa unaweza ukawa Tajiri kupitia Uongozi.Kinachoniuma ni hawa wachungaji na maaskofu kumkumbatia huyu mwenye historia chafu na asliyeshindwa kujisafisha mbele ya Mwalimu na waumini wote wa kitanzania.

Nakubaliana na maneno ya Zitto Kabwe kuwa Kunahitajika suluhisho la kitaifa katika mambo yahusuyo Nchi hii na wala siyo chama cha siasa.

Mzee Mwanakijiji umenena!
Kwa hali ilivyo hapa nchini kuna haja ya kutathmini role ya Moral institutions katika kujenga jamii staarabu nchini kwetu, hasa kwa kuangalia dini zetu kuu yaani ukristo na uislamu.
Katika ukristo nchi hii ina madhehebu makubwa mawili, wakatoliki na walutheri, kwa kifupi madhehebu haya yameshindwa vibaya ktk kuandaa watu wzr kwa jumuia zetu, wote wanaotuhumiwa kwa wizi na matumizi mabaya ya madaraka ni wakatoliki na walutheri, ni aibu kwa makanisa haya!!!! ndio maana wengine wanaona heri kusimama kuwatetea, inakuwaje muumini wenu anakuwa mwizi wa mali ya umma tena akiwa kiongozi??????
Kwa upande wa waislamu kwa kweli wanashika kile wanachokiamin vzr, ndio maana si rahis kukuta viongozi toka zanzibar wanatuhumiwa kwa wizi!!! ni watu wanyenyekevu wasio na tamaa, waangalie kina dk Shein, Salmin, marehemu dk. omar ali juma nk
Yapo madhehebu mengine ya kilokole (Pentecostals) hawa ni wazuri pia.pengine ipo haja ya kuwauliza walutheri na wakatoliki kuwa kwa nini wanaendelea kukumbatia watu wanaotuhumiwa kwa wizi makanisani kwao???
Labda wakifanya kama wpentecoste wanaowatenga waumini pale anapotuhumiwa kwa kosa lolote inaweza kusaidia kuwa na watu wema ktk jamii yetu, hasa viongozi!!
 
nilikuwa najiuliza tu,hivi kizazi hiki chote kitakuja kutoweka? halafu tutaacha wengine nyuma? nao watakuwa hivihivi? basi hii biashara kichaa kabisa. Ukianza biashara ukaproject hasara, kuna sababu ya kufanya hiyo biashara? labda kama mtaji ni wa EPA, kwa hiyo unazuga tu. Mimi sijui tunavumiliana saaaana mpaka lini? Chenge na mwenzake wameiba? sasa tatizo nini? mahakama kumbe ni kwa ajili yetu sisi tu, na jela je? Sijui kizazi kijacho kitarithi nini, kama kabla ya kufa ni lazima tuiharibu kabisa Tanzania ili watakaokuja wasiikute, Mungu atusamehe.. labda hatujui tutendalo? sote tuone aibuuuuuuuu, kama hatufanyi lolote, shame, shame on us all, kwani jk ni nani, na huyu Lowasa ndio nani? kwani wao ni watz kuliko sisi wengine wote, kwa kuwa wanamimvi kichwani? tusibabaishane bwana,wote ni watanzania, ila wametuona sisi wadanganyika eeh, wakija tunawekenulia meno kama vile hakuna kilichotokea tuone aibuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu.
 
nilikuwa najiuliza tu,hivi kizazi hiki chote kitakuja kutoweka? halafu tutaacha wengine nyuma? nao watakuwa hivihivi? basi hii biashara kichaa kabisa.

- Sawa sawa, hapa tupo pamoja sana, hili nalo ni swali la msingi sana tutaacha nini nyuma yetu? Eti watoto wetu watakuwa tofauti na sisi?

- Wasomi na wanadini, ni wakati muafaka sasa wakatafakari na kutuelimisha ni wapi tulikose akwenye hili, kwa sababu tabia zote nzuri za Mwalimu tunazo, kuanzia umasikini jeuri mpaka elimu za kubobea,

Sasa hizi tabia tabia tumeziota wapi mbona Mwalimu hakuwa nazo?


?
 
Kama kuna vikundi ambavyo vinatuangusha kwenye hii vita - ni vikundi vya dini. Inakatisha tamaa viongozi fulani fulani wa dini wanapojitokeza mbele ya hadhara na bila aibu kuyakumbatia na kuyatetea haya majizi - eti mradi wanachangia mifuko yao ya ulaji.

Sasa ni wakati muafaka tuanze kwa kuwaelekezea vidole na bila kumun'gunya maneno kuwaambia waache mara moja kutumia dini kama sabuni ya kuyafulia haya majambazi. Hii vita lazima ipigwe kwa kutumia zana na mbinu zote kama tunataka kufanikiwa.

Kamwe tusikubali hawa wezi watumie makanisa ama misikiti kama viwanda vya kusafisha (launder) pesa zao chafu. Tumeshuhudia wengi wakienda kutafuta hifadhi huko baada ya umma kuamua kuwazomea na kuwatenga. This has to stop now.
 
Radar deal`s top 10

2009-02-08 11:28:27
By Staff Writer​

After nearly three years of investigation, the UK`s Serious Fraud Office has implicated at least 10 top officials in Tanzania and Britain in the trumped up radar deal that cost the country $40m, The Guardian on Sunday can reveal.

The SFO has evidence that the officials were involved in the key negotiation stages that led Tanzania to purchase the military radar at an inflated price.

The top ten include former Attorney General Andrew Chenge, Sailesh Pragji Vithlani, Tanil Kumar Chandulal Somaiya, and Dr Idriss Rashidi.

Other players from the UK are Michael Peter Rouse, Sir Richard Harry Evans, Michael John Turner, Julia Adgridge and two senior officials from the British Aero Space Engineering (BAE System), the arms dealer that manufactured the radar.

It is believed that there are still more names from the previous regime that were part of the team that pocketed $12m in kickbacks from the deal.

According to reliable sources inside the SFO, the kickbacks were paid to Tanzania`s top officials in advance to move the negotiation process along smoothly.

Chenge`s role
The UK investigators believe the former Minister for Infrastructure Chenge was just `a conduit` through which the radar billions were distributed to selected top government officials whose decisions were crucial to the deal.

The SFO established that Chenge received $1.5m (2.1bn/-) from the deal through a slush fund he set up in the UK island of Jersey.

According to a draft report written by the UK`s Serious Fraud Office and seen by The Guardian on Sunday, Chenge received payments through six credit transfers between June 19, 1997, and April 17, 1998, while he was serving as Attorney General.

The billions were paid to account No.59662999 owned by Franton Investment Limited through Bank Code No 204505 of Barclays Bank Plc, according to the draft report, a final version of which has reportedly already been sent to the Director of Public Prosecutions.

The SFO has established that Chenge owns Franton Investment, a registered company that appears to have been established primarily to enable the transfer of the dirty money.

According to information provided by the Jersey Authority, the $1.5m was transferred from a Frankfurt branch of Barclays Bank to Chenge`s account at a Jersey branch.

But aside from the money Chenge pocketed himself, he also used the Franton account to dish out the money to others involved in the radar deal.

For example, the SFO established that on September 20, 1999, Chenge personally authorised the transfer of $1.2m from the Franton account to Royal Bank of Scotland International in Jersey.

In May 1998, Chenge also authorised the transfer of $600,000 to an account owned and operated by Langley Investments Ltd. The account was officially operated by former Central Bank Governor Dr Idrissa Rashidi.

Rashidi is currently the managing director of the troubled Tanzania Electric Supply Company Ltd (Tanesco).

The SFO report concluded that both Rashidi and Chenge were key figures in the corrupt radar deal, but they were acting with the full support of top officials from the third phase regime.

Hiding the facts
Details made available to The Guardian on Sunday show that Chenge, alarmed by the possibility of being detected, directed his financial advisors abroad not to use his Tanzania address for any correspondence concerning the offshore bank account.

``Instead Chenge asked his financial advisors to send all documentation to C/o 11 Sid Mouth Road, London this is the current address for JO Humbros used during their communication with Chenge,`` reads part of the SFO investigation report, compiled by lawyer Mathew Cowie.

The London address was the subject of a search operation conducted on March 26, last year.

Mr Fat from Tanzania
The SFO investigation established that, to avoid being caught, the facilitators of the radar deal gave Vithlani the codename `Mr Fat`, while any mention of bribing or corruption was replaced with the euphemism `commitments`.

``I had an extensive discussion with our friend and I have this morning had a meeting with the AG to go through outstanding contractual issues,`` reads part of the fax message from a Mr Simpkins confiscated by SFO investigators early last year.

``The fat man having, as I stipulated, now resolved all the issues, is keen to sign an addendum to his agreement and argues he has a lot of commitments to a lot of old and new players as the project has taken considerable period to effect.``

``In addition he has stated to achieve the above compromises, new promises have had to have been made,`` the fax reads.

Again in September 1997, Simpkins wrote a fax message to a BAE official using more code language. ``Also over the weekend our fat friend has been working to resolve the outstanding commercial issues,`` he wrote.

``This morning he informed me that all issues are now resolved as follows: They [the government] have accepted English Law with arbitration in London.``

Registered a front company in Panama
In what is believed to have been a tactic to obscure the deal`s corruption, Vithlani and his partners registered a front company in Panama called Envers Trading Co Ltd.

The company, according to SFO records, received $8m in kickbacks between 2000 and 2005.

The payments came from Red Diamond Trading Co Ltd a front company of BAE System until December 2005 when it was terminated at a settlement of $3.36m.

In 1999 BAE System, through Red Diamond, registered in the British Virgin Islands and entered into an agreement with Envers Trading Co.

The Panamanian company was identified as a consultant working in Tanzania, which acted for Siemens Plessey System (SPS) in 1992/93 when the government was considering purchasing the radar for $88m.

SPS was acquired by BAE System in 1995, according to available details.

UK investigators have established that Tanil Somaiya and Vithlani held a power of attorney over Envers for six years, until December 2006.

Somaiya had earlier told the SFO that he wasn`t involved directly in the radar deal, but that everything had been under the control of his partner, Vithlani.

SOURCE: Sunday Observer
 
SFO watoa tuhuma tisa dhidi ya Chenge

2009-02-09 10:07:58
Na Mwandishi Wetu


Makachero wa Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) wa Uingereza waliokuwa wanachunguza tuhuma za mlungula uliotolewa kwa aliyekuwa Waziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Andrew Chenge, ili kuruhusu ununuzi wa rada ya bei mbaya, wamejenga tuhuma kuu tisa ambazo zinaweza kumfikisha mwanasiasa huyo kizimbani.

Tuhuma hizo zimo kwenye ripoti ya SFO ambayo vyombo vya kisheria vya serikali ya Tanzania vilikabidhiwa tangu Machi mwaka jana, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya Chenge na mshirika wake wa karibu katika sakata hili, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Dk Idriss Rashidi.

Tuhuma ambazo zimetajwa na SFO dhidi ya watuhumiwa hao wawili, wakiwa ni miongoni mwa watuhumiwa 10 wanaochunguzwa katika kashfa ya rada iliyoigharimu Tanzania Dola za Marekani milioni 40, ni kwamba Chenge na Dk Rashidi walikuwa ni watu muhimu katika kufikiwa kwa mkataba wa ununuzi wa rada hiyo iliyouzwa kwa serikali na shirika la kuuza vifaa vya kijeshi la Uingereza, BAE System.

Mbili, Chenge anatajwa kuwa karibu na wakala wa kampuni ya Siemens Plessey System (SPS) iliyokuwa ikisukuma mpango huo, Sailesh Vithlani na kwamba ukaribu wao ulijitokeza wazi wakati wa kumalizia makubaliano ya mkataba wa ununuzi wa rada hiyo.

Tatu, SFO wanadai kwamba uhusiano wa karibu kati ya Chenge na Vithlani ulikuja katika kipindi ambacho wakala huyo, (Vithlani) anadaiwa kuwaeleza wafanyakazi wa SPS kuwa alikuwa na makubaliano ya zamani na mapya, makubaliano hayo katika mawasiliano yao yalimaanisha rushwa.

Nne, makachero hao wanamtuhumu Chenge kuwa alifanya maamnuzi mengi ya kisheria ambayo yalionekana wazi kwa jinsi mkataba wa malipo ulivyofikiwa katika ununuzi wa rada hiyo.

Tano, SFO pia wanatuhumu kwamba maamuzi hayo kwa vyovyote vile yanaonyesha kwamba hayakuzingatia maslahi ya Tanzania katika ununuzi wa rada hiyo.

Kwa maana hiyo kulikuwa na kitu kilichomfanya Chenge asiweke maslahi ya taifa mbele katika kutoa maoni hayo ya kisheria ambayo yalichukuliwa katika kufikia maamuzi ya mkataba wa kununua rada.

Sita, makachero hao wanaunganisha matukio hayo hapo juu na mmiminiko wa ghafla wa fedha kwenye akaunti ya Chenge kisiwani Jersey zikitokea Frankfurt.

Saba, Chenge anatuhumiwa na makachero hao kwamba ili kuficha kujulikana kwa fedha hizo, alianzisha kampuni ya Franton ambayo inamiliki akaunti hiyo, lakini pia akaibua anwani mjini London ambayo ilitumika kwa mawasiliano, kuficha kuonekana kwake moja kwa moja katika miliki ya fedha hizo.

Nane, SFO wanamtuhumu Chenge kwamba kutokana na ujanjaujanja wa kuficha vyanzo vya fedha hizo, benki hiyo iliamua kuvunja mahusiano naye kama mteja kwa kuwa hakuwa tayari kutoa maelezo ya kina juu ya fedha hizo.

Tisa, makachero wanatuhumu kwamba malipo ya Dola za Marekani 600,000 kwa Rashidi yanaonyesha kwamba hakuwa mpokeaji pekee wa rushwa kutoka kwa BAE System, ila ni mtu muhimu katika kuisambaza kwa kuwa watuhumiwa hao wawili (Chenge na Rashidi) walikuwa watu muhimu katika ununuzi wa rada hiyo.

Tuhuma hizi dhidi ya Chenge zinajulikana kwa vyombo vya kisheria vya nchi, lakini hadi sasa hakuna hata chombo kimoja cha kiserikali kimefungua kinywa kueleza hatma ya uchunguzi wa mwanasiasa huyo.

Chenge mara kadhaa amekanusha kuchukua rushwa ya rada, na alisema fedha alizojiwekea benki kisiwani Jersey ni vijisenti, lakini mara mbili ametoa kauli za kutatanisha juu ya vyanzo wa Dola za Marekani milioni 1.5 katika akaunti yake akieleza ni malipo yake halali kwa kazi za uanasheria lakini mara nyingine akasema ni urithi na akiba ya familia.

Katika fedha hizo alidai mkewe anamiliki asilimia 25.

SFO wamekuwa wanachunguza sakata la rada kwa miaka mitatu sasa, na kuna kila dalili imekuwa ikipewa ushirikiano na serikali tofauti na Kenya ambako walitangaza wiki iliyopita kufunga uchunguzi wa wizi wa Aglo Leaseing kutokana na kutokuwapo kwa dalili za kufungua mashitaka dhidi ya watuhumiwa wa kashfa hiyo.

Hadi sasa ni Vithlani pekee amefunguliwa mashitaka rasmi mahakamani kutokana na kashfa ya rada, lakini wakati mashitaka hayo yanawasilishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mshitakiwa hakuwapo na tangu wakati huo anasakwa kuja kujibu mashitaka yake.

SOURCE: Nipashe
 
Jamani nilisisitiza kuwa SFO wamefanya uchunguzi kwa sababu kwa sheria ya Uingereza, kamisheni hairuhusiwi kuzidi 10%. Mkosaji wao mkuu ni BAE kwa nini alifanya biashara na TZ na kulipa kamisheni kubwa zaidi ya asilimia 10%.

Sheria za Tanzania hazijaweka ukomo wa kamisheni. Hivyo Vithlani bado hana hatia kutoza kamisheni ya asilimia 40% na hata mashitaka aliyofunguliwa sio wizi bali kutosema ukweli kwa PCCB.

Waingereza ndio wanamshupalia Chenge. Mimi naamini UWT wanajua kila kitu. Kuna uwezekano mkubwa mgawo ulifika mpaka kwa Mkulu wa Magogoni ndio maana serikali yetu sio haifanyi lolote, bali haitafanya lolote zaidi ya kumwacha Mzee wa Vijisenti astaafu ubunge mwakani na kuachwa akajipumzikie kwa amani na kujilia vijisenti vyake kwa taratibu kama anavyolindwa Mzee wa Kiwira.

Kwa mujibu wa tuhuma zote 9 za SFO, hakuna yenye criminal liabilty kwa viwango vya serikali yetu, not at least for now.
 
Tujikumbushe ya rada, tusijesahau

Mwandishi Wetu Machi 25, 2009

Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

SASA imedhihirika kwamba Mkataba wa Ununuzi wa Rada wa mwaka 1999, kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Uingereza ya BAE Systems, uligubikwa na rushwa kubwa, kwa mujibu wa Ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya nchini Uingereza – Serious Fraud Office (SFO).

Wapelelezi wa ofisi hiyo juu ya mkataba wa ununuzi wa chombo hicho kwa Sh. bilioni 40 wamekuwa wakipeleleza kampuni hiyo na washukiwa wanane, wakiwamo Waingereza wanne - Sir Richard Harry Evans (67), Michael Peter Rouse (61), Michael John Turner (61), John Aldridge (52), na Watanzania watatu (majina tunayo, umri miaka 63, 44 na 45).

Katika taarifa yao ya awali ya Machi 2008, walisema: "Kuna kila sababu kuamini kwamba watu wote hao na Kampuni ya BAE Systems walitenda makosa ya rushwa katika ununuzi wa rada hiyo".

Wakibainisha jinsi sehemu ya mavuno ya rushwa hiyo yalivyogawanywa kupitia benki mbili za kigeni, kati ya Juni 19, 1997 na April 17, 1998, taarifa hiyo inasema hivi kuhusu Wa/Mtanzania hao/huyo: "SFO inahitimisha kwamba kuna kila sababu na kwa ushahidi tosha kwamba kwa kufanya hivyo (watu/mtu hao/huyo) alikuwa akiuweka uchumi wa Tanzania hatarini".

Ni dhahiri pia kuwa Serikali inawajua watu hao nao wanajijua; na ingekuwa kwa Nchi Zilizoendelea, zenye kuheshimu dhana ya kuwajibika, wangekuwa wameachia ngazi zamani kuponya nyuso zao. Lakini si kwa Mtanzania, ambaye kwake wizi, ubadhirifu na ufisadi ni ushujaa wa kupokelewa kwa kutandikiwa zulia jekundu.

Ningekuwa mimi ndiye Rais, ningewashauri watu hao kuachia ngazi kiungwana ili kutoipaka tope serikali yangu. Ningekuwa mimi ndimi mshukiwa, nafsi yangu ingenisuta na kujiuzulu sawia. Huu ndio uungwana; huu ndio ustaarabu wa binadamu, wa kuweka mbele maslahi ya walio wengi, tofauti na wanyama kama Nyang'au, wanaoweka maslahi binafsi mbele kwa maana ya "Rule of the Jungle"- Kanuni za mwituni". Na haya yanapotokea, tuliowaweka kusimamia serikali, wako wapi?. Au wametusahau kwa kujichongea mzinga wa asali?

Tabia ya kikundi cha viongozi wachache ya kulishwa asali kidogo na wawekezaji kwa kutumia mamluki wa ndani, ili kutetea manunuzi na uwekezaji usio na maslahi kwa taifa, inaendelea kuitafuna nchi. Tumejionea hili kwa mradi wa IPTL, ununuzi wa ndege mbovu ya Rais, mbuga za wanyama (Ortello), Richmond, mikataba ya madini na sasa Dowans, bila kusahau sakata hili la Ununuzi wa Rada.

Miradi yote hii imethibitika kuwa bomu la maangamizi kwa Taifa kiuchumi na kijamii. Na kwa nguvu ya fedha ya kifisadi, imeweza kuingiza "wateule" Bungeni, Chama tawala, Taasisi nyeti za serikali na serikali kuu. Ndiyo maana kero za wananchi hazipati majibu kutokana na jeuri za kifisadi, eti kwamba "dua la kuku halimpati mwewe".


Ungekuwa mmoja wa waliotetea ununuzi wa rada na ndege ya Rais kwa maneno makali ya kutunisha mishipa ya shingo; kisha unagundua kwamba kwa kufanya hivyo uliudanganya umma, ungefanyaje? Ungekuwa na ujasiri tena kusimama kadamnasini, macho makavu, na kuusalimia umma unaoteseka kiuchumi kwa ulaghai wako?.

Rais Richard Nixon wa Marekani, kwa ustaarabu, alijiuzulu urais kwa kashfa ya Watergate. Naye Waziri Mkuu wa Israeli, amejiuzulu hivi karibuni kwa kashfa ya rushwa; wengi walipita njia ulimwenguni, kwa ustaarabu wao; wewe je? Utetezi wa matusi kwa kujificha ndani ya mbawa za chama kinalisaidia nini Taifa lako?.

Rushwa ya mtu mmoja ni mbaya vya kutosha, lakini Serikali nzima inapohusishwa na rushwa kwa matendo ya wachache ndani yake wasioguswa, kwa sababu tu wanaonekana kukipenda chama tawala kuliko Taifa, hili si jambo la kufumbia macho.

Tuangalie mfano wa sakata la rada. Wakati hoja ya utapeli wa mkataba huo ilipoibuliwa na wapinzani, Naibu Waziri wa Fedha, Abdulsalaam Issa Khatibu; Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mark Mwandosya na Mkurugenzi Mkuu wa Kurugenzi ya Usafiri wa Anga, Margareth Munyangi, ndio waliokuwa wa kwanza kutetea mradi huo wakisema: "Rais hawezi kudiriki kamwe kuacha usalama wa wasafiri wa ndege, mikononi mwa bahati nasibu".


Hakuna aliyekuwa akipinga hili, bali kilichopingwa ni bei kubwa na ubora hafifu wa kifaa hicho mtumba, kwa sababu tayari jumuiya za kimataifa na Waziri Clare Short wa Uingereza, walikwishaonya na kuitahadharisha Serikali juu ya ulaghai wa dili hilo. Kwa nini hawakuamka kwa tahadhari hiyo?

Naye Rais Benjamin William Mkapa, kwa kuambukizwa na watu waliomzunguka, na pengine kwa kutumia Chama, akiwa ziarani Mbeya alitetea ufisadi huo akisema: "Wanaoikosoa Serikali si tu wanaibeza Serikali na Chama chake, bali wanawabeza Watanzania waliokipatia Chama cha Mapinduzi mamlaka ya kutawala kwa wingi wa kura (bila kujali zilivyopatikana) ili kiweze kutekeleza ilani na sera sahihi, zenye kulenga kumletea maendeleo mwananchi….. Hao ni vipofu na viziwi".

Baada ya kuthibitika kwamba ndege ya Rais na rada aliyokuwa akitetea ni mabomu na kikwazo kwa maendeleo ya mwananchi; kati ya yeye na hao aliowaita eti ni vipofu na viziwi, ni yupi aliyekuwa akiwabeza Watanzania?.

Tangu mwanzo, Baraza la Mawaziri la Uingereza lilikuwa limegawanyika juu ya Uingerza kuiuzia Tanzania ndege mbovu, licha ya kwamba zoezi zima lilikuwa la udanganyifu. Waziri wa Fedha, Gordon Brown (sasa ni PM) na Mama Clare Short, Waziri wa Ushirikiano na Misaada ya Kimataifa, Mashirika ya Oxfam, Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Shirika la Kimataifa la Usalama wa Anga (ICAO), Jane's Air Traffic Control na wengine, wote waliweza kubainisha mapema juu ya udanganyifu wa mkataba huo, kiasi kwamba Benki ya Dunia ikatishia kuzuia misaada kwa Tanzania.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, alijua yote haya; lakini aliishinikiza Kabineti yake imruhusu kutoa kibali cha mauzo kwa BAE Systems ili kuokoa ajira za Waingereza 280 wa Kampuni hiyo, iliyopo katika kisiwa cha Isle of Weight, ili Chama chake kisipoteze ushindi katika jimbo lililohusika. Rais Mkapa alipeleka salaam kwa Blair, kumshukuru kwa kuweza kuifanya Serikali yake iidhinishe mauzo ya mtambo huo mbovu chini ya mkataba wa kitapeli.

Juni 21, 2002 Waziri wetu wa Fedha wa wakati ule, Basil Pesambili Mramba, katika kauli iliyoonekana kutowakilisha maslahi ya Taifa, alitamka Bungeni maneno yafuatayo ambayo itawachukua Watanzania muda mrefu kuyasahau: "Tunakataa kuambiwa mambo yakufanya hata kama sisi ni masikini … Wanawezaje kuwa na ujasiri wa kutuambia kwamba rada hiyo ni aghali sana kwetu?... Tuko tayari kula majani, na kama wanataka, waache kutupa misaada yao".

Kuonyesha kwamba hoja za wananchi hazikuwa na uzito kwake, Mramba, kwa wakati tofauti, alisema: "Baadhi ya watu wanaokota okota maneno baa na kuyafanya wimbo rada … rada … rada kwa kujisumbua; hawajui kwamba Serikali ya Uingereza imekwishatoa leseni ya kuiuzia Tanzania rada; na kinachotokea Uingerza sasa ni mgogoro ndani ya Serikali ya huko ambayo wanataka kuuleta katika Serikali ya Tanzania".


Mramba na wenzake waliilewa vizuri Kampuni ya BAE Systems na malengo yake; kwani wakati huo ilikuwa imekumbwa na kashfa ya madai ya kutoa rushwa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, baada ya nchi hiyo kutiliana sahihi mkataba wa kampuni hiyo kuiuzia silaha za kijeshi. Na kufuatia upelelezi wa SFO, kama inavyofanya hapa kwetu kwa sakata la rada, ilibainika kuwa BAE Systems, iliweka Pauni za Kingereza milioni saba katika Akaunti ya Mifuko (Trusts) huko Jersey, katika Visiwa vya Channel, na kutokana na uchunguzi zilimilikiwa na Waziri huyo.

Baada ya kuonekana mambo yanamwendea vibaya, Waziri huyo aliutema mfupa, akalipa Pauni milioni sita kwa mamlaka za utawala wa visiwa hivyo kama fidia ya usumbufu walioupata kutokana na upelelezi huo, na kwa maelewano ya kusimamishwa kwa upelelezi.

Kwa kufanya hivyo, inaweza kutafsiriwa kuwa, ama Waziri huyo alikuwa anautema mlungula kwa nafsi yake kumsuta, au naye alikuwa anatoa rushwa ili upelelezi usitishwe.

Hakuna shaka yoyote sasa kwamba wabeba mikoba ya ufisadi wa rada ya Tanzania, wanafahamika kwa mujibu wa taarifa ya SFO kwamba: "There is every reasonable cause to believe that all the above named persons and Company have committed offences of corruption …. The SFO concludes to believe that in taking this stance….. (name/s) was putting the economic interest of Tanzania at risk", ni maneno ambayo tafsiri yake tumeitoa hapo mwanzo.

Je, kwa taarifa hii ya SFO, wahusika wa kashfa ya rada nao sasa wanaweza kuitema milungula kama alivyofanya Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar; au watazuia wasiwajibishwe, au Sheria kuchukua mkondo wake, kwa nguvu ya fedha walizo nazo? Hivi ni mpaka SFO waje Tanzania ndipo tubaini vitendo vya ufisadi vyenye kuangamiza uchumi wa nchi yetu?

Hii inadhihirisha aina ya viongozi tulio nao, ambao Shaaban Robert anawaelezea kwa maneno yafuatayo:

"Ni waledi wa kusema, watu wa leo,
Bali hawana huruma, katika moyo,
Tamthili ya Wanyama mfano wao,
Kisha waweza kuuma, sumu wanayo,
Mungu nilinde nao wanyama, wala wenzao.

Kwa mazingira yetu ya sasa, Shaaban Robert hakosei anaposema tumepungukiwa hekima na heshima, kwamba heri wanyama, ndege na wadudu:

Serikali za wanyama, na ndege au wadudu,
Ndani zina taadhima, kama kwamba maabudu,
Na watu wenye hekima, siku hizi hawamudu,
Madaraka na heshima, heri mnyama na dudu,
Na mambo haya si mema, watu wanayahusudu;
Hizi husemwa ni zama, za watu kufa kibudu,
Kufa wangali wazima, na nguvu za kusujudu,
Na maudhi na hasama, kwa kashata na ladu.
 
Duuu.....mimi nashindwa hata kuanza kujadili maana serikali hatabakia mtu yeyote maana kashfa. Ziko kama 15 ivi sasa hata JK anatakiwa ajiuzulu haraka... kwa kweli ni balaa sana na aibu watu wamo tuu...JK unafanya nini? Unatuuzia sura? Kuwa jasiri japo kidogo tu, ni aibu jamani...

Hadi tunafikiria kukufuru kutaka mapinduzi maana watu hao hao wanatufanya wengine wote wapumbavu alaaa!
 
Duuu.....mimi nashindwa hata kuanza kujadili maana serikali hatabakia mtu yeyote maana kashfa. Ziko kama 15 ivi sasa hata JK anatakiwa ajiuzulu haraka... kwa kweli ni balaa sana na aibu watu wamo tuu...JK unafanya nini? Unatuuzia sura? Kuwa jasiri japo kidogo tu, ni aibu jamani...

Hadi tunafikiria kukufuru kutaka mapinduzi maana watu hao hao wanatufanya wengine wote wapumbavu alaaa!
Oh,

Mapinduzi HAPANA...!
 
Back
Top Bottom