The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Utawala wa sheria vipi wakati dola na mahamana ndio wanaongoza kwa rushwa?
maneno yako kweli na kwa sababu vyombo hivyo viko - Above the law...wakati sheria inasema no one is above the law.
Tunarudi pale pale kwamba kusimamisha sheria na sioo maandishi matupu haiwezi kuleta mabadiliko..
 
Correct Assesment of Tanzanians from ES,

Tukubaliane. Haya huwa yana matokeo yake. Historia ni mwalimu mzuri sana. Nchi zote zilizofikia hapa tulipofikia (kwenye rule of the jungle) ziliishia kwenye migogoro na umwagaji damu. Hayo ndo matokeo ya taifa lililosemwa na ES.

Hatuna haja wala sababu ya kujipa moyo!! We are in bad shape morally and something radical must happen. Kwa kupangwa au bila kupangwa.

Cha kupangwa ni kuwa aingie Ikulu mtu anaye dare. Afanye yale kila mtu anaona hayawezekani. Afunge wale wanaoonekana hawafungiki. Afukuze kazi wale wanaoonekana hawafukuziki.

Cha kutopangwa, ni vurugu na umwagaji damu, kwani mwisho wa yote ni kukata tamaa na kutojali. Haya mambo yanaonekana ila tunayafumbia macho.

Wezi waliokubuhu wanatanua na kuvinjari kila sehemu. Tusubiri tutaona!!!
 
Sasa hivi Bongo wapo watu wanaosema ikiwa watanzania wamekosa sembe, wapeni pilao. Hao wapo na wapo kila mahali.
 
- Huu ni wakati muafaka kwa wasomi, wana-dini, na viongozi wetu wa siasa kukaa chini na kujaribu kutafakari kwa makini, kwa sababu sio siri kwamba taifa letu limekumbwa na crisis kubwa sana ya character, Mwalimu alitupatia national ID basi lakini nationally kwenye character kwa maoni yangu tume-fail miserably.

- Sisi wananchi ni waongo, I mean taifa zima ni waongo, wezi, waumini wa uchawi, wanafiki, halafu masikini ya Mungu tunategemea viongozi wetu wa siasa wawe tofauti na sisi wananchi, it does not work tumekwama maana sasa nani wa kumfunga kengele paka?

- Hili ni taifa gani ambalo wote tumeharibikiwa?

Mkuu FMES, yaani umegusa sehemu ambayo hata mimi nimeiona siku nyingi ndo imeoza, ndo maana imepelekea kuzaliwa kizazi chenye tabia ya namna hii. Siwezi kuzungumzia kuhusu misikitini kwa kuwa sihudhurii huko. Lakini huko makanisani ni uozo mtupu. Dini zimetaifishwa,yaani watu wameona ndo sehemu rahisi ya kumtumia Mungu kujitajirisha na kuisha maisha ya anasa.

Inashangaza unaingia kwenye misa ya masaa 3 au 4 ukitegemea kwenda kusikia mahubiri ya biblia in comparison with our daily life,unakuta masaa mawili na nusu au matatu na nusu wanazungumzia kuhusu sadaka na zaka. Nusu saaa tu ndo utasikia juu ya biblia tena kwa kubabia. Makanisa yameingia kwenye mashindano na biashara na si kuhubiri neno la Mwenyezi Mungu ili kujenga maadili katika jamii. Jamii haijengwi kiroho unategemea nini! Huko makanisani ndo Maafisadi wamefanya kimbilio! Yaani aibu tupu. Unasikia Askofu mzima akimtetea mtu ambaye ushahidi wake wa wizi uko wazi. nadhani hizi ndo dalili za siku za mwisho.
 
Bila kumung'unya maneno, nchi hii mwaka 2005 tulibahatika sana kumpata Raisi aliyepata mandate ya asilimia 80% ya wapiga kura. Kwa kufanya hivyo wapiga kura walimpa uwezo mkubwa na uthubutu usio wa kawaida wa kuikwamua nchi hii kama angeamua kufanya hivyo. Hata hivyo hilo lingewezekana tu kama huyo Raisi angekuwa na nia ya dhati ya kulikwamua taifa kutoka mikononi mwa wezi na wabadhirifu, uwezo wa kusimamia kikamilifu mabadiliko ambayo yangeendana na nia hiyo na ujasiri wa kupambana na visiki ambavyo vingejaribu kukwamisha nia hiyo. Sadly this was not to be na sijui kama tutapata tena fursa kama hiyo bila kufanya maamuzi mazito yanayoendana na mabadiliko.

Bahati mbaya pamoja na maneno matamu na ya kutia moyo aliyoanza nayo haikuchukua muda wananchi wakaanza kuhisi mapungufu makubwa katika yote matatu - nia, uwezo na ujasiri. Tunayoyashuhudia leo ni matokeo ya kukata tamaa kwa walio wengi na wengine kudiriki kusema "ndivyo tulivyo" na kukubali bora tuzame wote. Mimi sikubali wote tumeoza ila naona jitihada za waliochafuka nazo zimepamba moto kujaribu kutupaka wote uchafu ili tufanane. Tunashindwa kuangalia tumefikaje hapa na tufanye nini tujikwamue - kwanza lazima tukubali tumefika hapa kwa matakwa yetu wenyewe halafu tujiulize nani huyo katuongoza kufika hapa. Baada ya hapo tukimtambua, tumkatae huyo na yeyote anayemuunga mkono kwa nguvu zetu zote.

Katika kipindi hiki tumeshuhudia sheria zikivunjwa na viongozi wetu wazi wazi na watuhumiwa wasichukuliwe hatua, eti ushahidi hautoshi. Raisi anapounda serikali na kuteua viongozi, sasa ikionekana dhahiri kabisa mbele ya umma kuwa wanaboronga - halafu asite kuwatimua, eti anasubiri ushahidi au uamuzi wa mahakama - kwani mahakama zilimshauri katika kuwateua ? Ni wazi hapa anasukumwa na dhamira moja tu nayo ni kulinda maslahi ya marafiki na wabia wake ndani ya chama na serikali - huu ni ukosefu wa nia na ujasiri. Tanzania inaangamia kwa kuwa maslahi ya wachache yamewekwa mbele ya maslahi ya taifa na watu wake. Chama chochote kile kinachoendeleza dhana hii ya kijinga, hakitufai.

Watanzania tuamke - we have been taken for a ride for too long !! Serikali inaonekana imeelemewa na inahitaji msaada wetu. Gari limekwama na dereva ujanja umemwishia, tushuke, tulisukume na tuliondoe kwenye tope.
 
Tatizo letu si Sheria. Tatizo letu ni nani wa ku-enforce hizo sheria?? Mfumo wa mahakama ukiufuatilia kwa undani ni maigizo ya ze-comedy. Mawakili maarufu zaidi ndo watu wa kuogopwa zaidi kuliko hata ukimwi. Polisi na majeshi yetu sasa hivi ni magenge ya wezi na wahuni. Benki kuu sasa hivi ndiyo inazungumzwa kwa sababu watu fulani wanataka tuzungumzie benki kuu. Daktari aliyezungumza kwenye TV akiwa chakari nani alifanya nini?? Kila kona kuna old boys networks za kulinda uovu na uchafu, si makanisani wala misikitini, kote.

Wapo watakao-sema hiki kipima pembe kimekata tamaa. Lakini kama umeshawahi kuona ordered societies unaweza kujua how deep in a shit we are. Nchi zote zilizoendelea waovu wamejazana na wako kila sehemu, always attempting to do something terrible. Ila hawafanikiwi kwa sababu kuna mifumo ya kuwa-expose na kuwa angamiza. Kwetu ndoo hao hao wanaoprosper. Waadilifu katika mifumo yetu ni viumbe walio katika hatari ya kutoweka na ndio wanaokuwa victims kimya kimya na waziwazi. Watu wanakaa semina ndani ya ofisi zao, wanalipana per diem za safari za Ulaya. Watu wanasafiri kwenda Ulaya kwa full board halafu na per-diem zinalipwa. Watu wana-attend makongamano mawili au matatu kwa wakati mmoja na kote wanalipwa haki zao (kule waliko enda na kule ambako majina yao tu ndo yalienda). Kiumbe aliye katika hatari ya kutoweka ni yule atakaye-sema huo ni wizi - atahamishiwa kusiko julikana na biashara itaendelea kama kawaida.

Budget zinazosomwa kila mwaka zinaishia mifukoni mwa watu. Wanaopata mishahara midogo ndio wenye kumiliki mimali ya mabilioni. Badala ya barabara kujengwa yanajengwa majumba vichakani kusiko na bara bara. Kwa nini wote tusitake kufanya hizo kazi wanazofanya wao?

Hakuna kisicho na matokeo na lazima tuwe tayari kwa matokeo. Tusipopanga matokeo tutapata matokeo yasiyopangwa.
 
Dawa ya moto ni moto. Kama mtu unajua kuwa ukiiba hamna yatakayokupata, lazima utaiba tu.

Lakini kama viongozi wote wala rushwa wakijua kuwa watafungwa, TRUST ME rushwa itapungua kwa kiasi kikubwa.

Kwa hiyo tuendelee kupeleka wala rushwa mahakamani na nidhamu itarejea polepole.
 
Dawa ya moto ni moto. Kama mtu unajua kuwa ukiiba hamna yatakayokupata, lazima utaiba tu.

Lakini kama viongozi wote wala rushwa wakijua kuwa watafungwa, TRUST ME rushwa itapungua kwa kiasi kikubwa.

Kwa hiyo tuendelee kupeleka wala rushwa mahakamani na nidhamu itarejea polepole.

moelex mbona hilo la 'kujua' wanajua? Tatizo ni kuwa hata Uchina ambako wala rushwa wanatwangwa risasi wenye kula rushwa wanakula tu.. So, nadhani tatizo kuhakikisha kuwa watu hao "wanafungwa" ..
 
Bila utawala wa sheria isiyomuagopa mtu, mbeba na kuacha uswahiba kazi ipo.
Sheria lazima ifutwe na kila mtu mwenye hatia lazima aende jela. Bila hayo hakuna kitakacho tokea mpaka siku wananchi watakapochukua sheria mkononi na kuanza kuwashughulikia wahalifu kama Chenge, Idrisa, mkapa, nk kwa mawe na moto.
 
- Huu ni wakati muafaka kwa wasomi, wana-dini, na viongozi wetu wa siasa kukaa chini na kujaribu kutafakari kwa makini, kwa sababu sio siri kwamba taifa letu limekumbwa na crisis kubwa sana ya character, Mwalimu alitupatia national ID basi lakini nationally kwenye character kwa maoni yangu tume-fail miserably.

- Sisi wananchi ni waongo, I mean taifa zima ni waongo, wezi, waumini wa uchawi, wanafiki, halafu masikini ya Mungu tunategemea viongozi wetu wa siasa wawe tofauti na sisi wananchi, it does not work tumekwama maana sasa nani wa kumfunga kengele paka?

- Hili ni taifa gani ambalo wote tumeharibikiwa?

I cosign you FMES...It's a vicious cycle! Maybe we need a Cultural Revoulution kama ya Mao..
 
- Sisi wananchi ni waongo, I mean taifa zima ni waongo, wezi, waumini wa uchawi, wanafiki, halafu masikini ya Mungu tunategemea viongozi wetu wa siasa wawe tofauti na sisi wananchi, it does not work tumekwama maana sasa nani wa kumfunga kengele paka?


Ni kweli kabisa mkuu, lakini swali hili ni kama lile la nani katangulia kuku au yai? Swali lingine la kujiuliza ni vipi tutavunja mzunguko huu? lets call it CYCLE OF NATIONAL SHAME, mzunguko wenyewe uko hivi, wananchi ni wavivu, wezi, waongo, wana tamaa ya utajiri wa harakaharaka, wanadai "chai" kabla ya kupiga kura ----- kutokana na wananchi hao anapatikana kiongozi----kiongozi huyu kwa sababu naye ametokana na sisi atakuwa na sifa zilezile.

Mwanasolojia Max Weber called it "organic society". Jamii imefungamana sana kuvunja mielekeo kama hii.
 
Japo kuna topic zinaendelea nimeonelea niiweke hii hapa ili kuona wadau kama inaweza kuwa na msaada kwenu. Hebu ipitieni kidogo tu.

Thanks
 

Attachments

Asante mkuu invisible. Huu ni ushahidi tosha kabisa wa kuwapandisha mahakamani wahusika.
 
Ahsante sana mkuu hapa naona Idriss hatakuwa na cha kujitetea maana kuna ushaidi wa kutosha sasa
 
Du mkuu Invisible hii si mchezo, ni kweli kuwa nchi inajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno a.k.a chenge & Co.
 
- Wakuu ahsanteni sana kwa hii response, Tanzania tumetokewa na nini hasa? I mean tumefikaje hapa jamani ambapo hakuna wa kumuamini? Mimi sasa nimefikia mahali mtu akitaka kunikopa na ni rafiki yangu wa karibu, kama anataka 100, nitampa 50 na kumuomba asinirudishie ili tuendelee na urafiki wetu maana nikimdai tutavunja urafiki.

- Kweli kiongozi mkubwa wa taifa anatafuta risiti za uongo ili akadai hela za wananchi, na huku akijua wazi kuwa anachokifanya ni uizi? Unajua tumefikia mahali huu sasa nationally ya kutafuta risiti yamekubalika kuwa ni tabia ya kawaida tu kwa sisi wafanyakazi wa serikali yetu, wakubwa kwa wadogo bila hata ya aibu kidogo!

- Hatuwezi kuaminiana tena, hatuwezi hata kujali time maana tutatafuta sababu za hapa na pale na kudai tulikuwa na shughuli zilizotufanya tuchelewe kumbe ni uongo uongo usio na mfano. Ninakumbuka nilipokuwa nchi moja majuu, ilikuwa mbongo ukitaka kununua tiketi ya ndege, mhindi mmoja alikuwa na tiketi za cheap kwa hiyo wabongo wengi tulikuwa tunajimwaga huko, sasa hata yule Mhindi alishatushitukia I mean mbongo anapiga simu kuwa anaondoka Jumapili kumbe hata hela hana anategemea kupata Ijumaa jioni, atamzungusha Mhindi mpaka mwisho ataanza kujizungusha mwenyewe, matokeo safari hakuna analaumu Mhindi kumbe ni uongo tu umemzidi!

- Unajua ninashukuru sana kwa wale wote mliolichukulia hili suala on a serious note, wakuu sisi tunao-deal na wabongo kila siku kwa kweli hamjui how bad this thing are, sasa ninajiuliza kama sisi wenyewe kwa wenyewe ni hivi mazishi mazishi hawa viongozi wetu itakuwaje na wako kwenye nafasi na wanaziona hela ziko nje nje?

Wakuuu solution nini hasa na hili tatizo na sisi wabongo? Tumefikaje hapa? Hili taifa letu litakombolewa na nani hasa jamani kama sisi wenyewe ndio hivi hivi? Something ni lazima kifanyike jamani ama sivyo tutacheza mzunguko mpaka mwisho wa dunia ndugu zangu! Unajua yanakatisha tamaa sana huko uongozi wa juu, maana tulisema wakiingia wapya na hasa vijana mambo yatabadilika, kumbe sasa ndio worse kuliko zamani, ni nini hasa sisi na hiii special Tanzania's character?

Ahsante Wakuu
!
 
1. Katika kipindi hiki tumeshuhudia sheria zikivunjwa na viongozi wetu wazi wazi na watuhumiwa wasichukuliwe hatua, eti ushahidi hautoshi.

2. Raisi anapounda serikali na kuteua viongozi, sasa ikionekana dhahiri kabisa mbele ya umma kuwa wanaboronga - halafu asite kuwatimua, eti anasubiri ushahidi au uamuzi wa mahakama - kwani mahakama zilimshauri katika kuwateua ?

3. Ni wazi hapa anasukumwa na dhamira moja tu nayo ni kulinda maslahi ya marafiki na wabia wake ndani ya chama na serikali - huu ni ukosefu wa nia na ujasiri.
4. Tanzania inaangamia kwa kuwa maslahi ya wachache yamewekwa mbele ya maslahi ya taifa na watu wake.

5. Chama chochote kile kinachoendeleza dhana hii ya kijinga, hakitufai.

6. Watanzania tuamke - we have been taken for a ride for too long !!

7. Serikali inaonekana imeelemewa na inahitaji msaada wetu. Gari limekwama na dereva ujanja umemwishia, tushuke, tulisukume na tuliondoe kwenye tope.

- Mkuu haya maneno ni mazito sana na hkuna ubishi kabisa, sawa sawa na tupo pamoja hapa.
 
Kinachokatisha tamaa zaidi ni kuwa hata wale wazalendo wachache waliopo........wanawekwa pembeni/kufukuzwa...........au wanapewa sehemu ambazo they can not perform............

Jambo la kufanya

.....kwa kuwa MAFISADI ni network.....na hata sasa hivi wanapandikiza watoto wao na ndugu zao.......cha msingi sisi tunaoona haya maovu......tujiunge na tu-form namna ya ku-fight na huu upuuzi........chombo kimojawapo cha kupambana nao tunavyo i.e. JF+ Cheche za Fikra........hivyo basi tuongeze nguvu
 
Last edited:
Back
Top Bottom