The Radar Scandal: Investigation & Progress

kumekucha! kujadili tu hakutoshi, kama watajadili na kuchukua hatua madhubuti watapata tano zangu, lakini isije ikawa wanajadili ili kumsafisha na kumpongeza eti kwa kujiuzulu
 
MBUNGE wa Buchosa, Samwel Chitalilo ameibuka bungeni na kumtetea aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge kuwa si mwizi kwa kuwa hajawahi kuvunja nyumba ya mtu.

Mbunge huyo alisema hayo jana bungeni wakati akichangia katika hotuba ya Waziri Mkuu, kuwa Chenge si mwizi na hajawahi kuvunja nyumba ya mtu ili kuiba hivyo aachwe bila kusakamwa.

Chenge alijiuzulu baada ya kudaiwa kuweka kiasi kikubwa cha fedha huko Kisiwa cha Jersey ambazo alikiri kwamba ni zake, lakini hazihusiani na ununuzi wa rada.

Mbunge huyo alisema kwamba, alizingaliza benki ambazo zimekuwa na tabia ya kutoa siri za wateja kuacha kufanya hivyo.

Sambamba na kumkingia kifua Chenge, mbunge huyo pia alidai kuwa ni jambo la kushangaza kuona kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakimzungumza vibaya Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wakimhusisha na masuala ya ukiukwaji wa maadili.

Vilevile, Mbunge huyo alipongeza juhudi za aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa ambaye

alijuzulu kutokana na sakata la Richmond, akidai kuwa kuwajibika kwake kulikuwa ni

kwa kisiasa.

Hata hivyo, wakati akiendelea na mchango akidai kuwa tabia ya wabunge kuingiza ushirikina na kutuhumiana kwa uchawi haifai, kwa sababu wataanza kutajana ovyo, Spika wa Bunge, Samwel Sitta aliingilia kati na kumtaka mbunge huyo kurudi kwenye hoja na kumuangaliza kuwa angalizo kuwa kila mbunge ana uhuru wa kuongea katika jumba hilo.

Aliporejeshwa katika hoja, Mbunge huyo aliamua kuikalia kooni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akidai kuwa imekuwa ikiwaonea wafanyabiashara kwa kuwabambikia kodi zaidi, hususani katika bidhaa zinazonunuliwa kutoka nje ya nchi.

Alisema kuwa wataalam wa TRA, wanajikita katika bei wanazoziona katika mtandao wa

kompyuta na kusahau kuwa biashara hufanywa ikitegemea nguvu ya mapatano.

Mbunge huyo alishauri kuwa katika wakati huu,Tanzania inapaswa kuepuka kuchanganya

masuala ya uchumi na siasa.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Severina Mwijage alisema kuwa ahadi ya

posho za madiwani itekelezeke sanjari utekelezaji wa miradi usimamiwe ipasavyo kwa kuimarisha ufuatiliaji.

Mbunge Mwijage akizungumzia mwafaka wa Zanzibar Zanzibar, alimtaka Rais Jakaya

Kikwete kutowasikiliza wasaidizi wake ambao alidai kuwa wanamdanganya.

Mbunge huyo alisema kuwa ni muhimu kwa Rais Kikwete yeye mwenyewe kuingia katika

mazungumzo hayo ili kupata ufumbuzi wa kina wa jambo hilo, ambalo limekuwa kero

kwa wananchi wa Zanzibar.

Naye Mbunge wa Gando(CUF), ambaye ni mnadhimu wa upinzani bungeni alisema kuwa

inaelekea Rais anapata shida juu ya mgogoro wa Zanzibar na akamtaka kufika bungeni

ili wabunge wampatie msaada.

Mbunge huyo alimweleza Waziri Mkuu, kumwambia Rais kuwa anahitajika kufika bungeni

akiwa ni sehemu mojawapo ya Bunge ili aweze kupewa msaada unaostahili kutoka kwa

wabunge.

''Rais anaelekea anapata shida juu ya mgogoro wa Zanzibar, ninamwomba aje bungeni

akiwa ni sehemu ya bunge tumsaidie, Waziri Mkuu naomba umwambie Rais, aje

tumsaidie ili apate msaada,'' alisema Mbunge huyo wa Gando.

source; http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=6365
 
Statement ya kitoto sana sijui kama mheshimiwa huyu hata anastahili kuwa mbunge. Nafahamu kuwa General Abacha hakuwahi kuvunja nyumba ya mtu wa kudokoa naira moja, lakini huenda alikuwa mwizi mkubwa. Marcel Mobutu hakuwahi kudokoa hata Faranga moja lakini ni mwizi mkubwa sana. Kwa hiyo mheshimiwa anasema nini labda sielewi.
 
Huyu chitalilo naye hana akili ndo maana alifoji vyeti!Badala ya kuzungumzia mambo ya jimbo lake na maendeleo kwa ujumla anabwabwaja bungeni eti "Chenge hakuvunja nyumba ya mtu"Kwanza wizi wa viongozi serikalini ni wa kwenye makaratasi na si wa kuvunja nyumba!Kama ndo wabunge wetu hawa i mean Chitalilo type basi hatuna wabunge tuna figures tu kwa ajili ya kukuza vitambi vyao!
Chitalilo unawaabisha wana Bushosa!Hawakukutuma kwenda kuwasafisha kina Mkapa,Chenge,Lowasa n;k!
Asante
Hollo
 
Hawa akina Chitalilo ni vivuli vya akina chenge,EL, na mafisadi wengi bado vinatembea.
Bado tutatisikia mengi,tegeni masikio na macho elekezeni kwenye mjengo hapo.
Kwa akili hii ya akina Chitalilo utapata cheti shule gani hiyo?Hata kwenye shule ya matahaira hawezi mtu kama huyu kupewa cheti.
Narudia tena hata kwa magadi na Gwanji hawatatakasika?Labda kwa maamuma na mapunguani wasiojua wajibu wao.
Kwa akili zao wakisema hivyo wanadhani ndipo wamemaliza tatizo,This is BS
 
Lakini wakuu mkuumbuke huyu jamaa aliwahi lalamikiwa na wapiga kura wake kuwa aligushi vyeti.Hii inadhihilisha rasmi kuwa jamaa uwezo wake wa kifkra ni mdogo sana kumbukeni vigogo wa CCM ndio walio mkingia kifua huyu mbunge kuwa hajagushi vyeti.
Sasa amevuka mipaka na kuanza kuwatetea wala rushwa kama Chenge lazima huyu mbunge apime uzito wa kauli aliyo itoa na vile vile awajibike kwa matamshi yake.
 
MBUNGE wa Buchosa, Samwel Chitalilo ameibuka bungeni na kumtetea aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge kuwa si mwizi kwa kuwa hajawahi kuvunja nyumba ya mtu.

Mbunge huyo alisema hayo jana bungeni wakati akichangia katika hotuba ya Waziri Mkuu, kuwa Chenge si mwizi na hajawahi kuvunja nyumba ya mtu ili kuiba hivyo aachwe bila kusakamwa.

Chenge alijiuzulu baada ya kudaiwa kuweka kiasi kikubwa cha fedha huko Kisiwa cha Jersey ambazo alikiri kwamba ni zake, lakini hazihusiani na ununuzi wa rada.

Mbunge huyo alisema kwamba, alizingaliza benki ambazo zimekuwa na tabia ya kutoa siri za wateja kuacha kufanya hivyo.

Sambamba na kumkingia kifua Chenge, mbunge huyo pia alidai kuwa ni jambo la kushangaza kuona kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakimzungumza vibaya Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wakimhusisha na masuala ya ukiukwaji wa maadili.

Vilevile, Mbunge huyo alipongeza juhudi za aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa ambaye

alijuzulu kutokana na sakata la Richmond, akidai kuwa kuwajibika kwake kulikuwa ni

kwa kisiasa.

Hata hivyo, wakati akiendelea na mchango akidai kuwa tabia ya wabunge kuingiza ushirikina na kutuhumiana kwa uchawi haifai, kwa sababu wataanza kutajana ovyo, Spika wa Bunge, Samwel Sitta aliingilia kati na kumtaka mbunge huyo kurudi kwenye hoja na kumuangaliza kuwa angalizo kuwa kila mbunge ana uhuru wa kuongea katika jumba hilo.

Aliporejeshwa katika hoja, Mbunge huyo aliamua kuikalia kooni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akidai kuwa imekuwa ikiwaonea wafanyabiashara kwa kuwabambikia kodi zaidi, hususani katika bidhaa zinazonunuliwa kutoka nje ya nchi.

Alisema kuwa wataalam wa TRA, wanajikita katika bei wanazoziona katika mtandao wa

kompyuta na kusahau kuwa biashara hufanywa ikitegemea nguvu ya mapatano.

Mbunge huyo alishauri kuwa katika wakati huu,Tanzania inapaswa kuepuka kuchanganya

masuala ya uchumi na siasa.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Severina Mwijage alisema kuwa ahadi ya

posho za madiwani itekelezeke sanjari utekelezaji wa miradi usimamiwe ipasavyo kwa kuimarisha ufuatiliaji.

Mbunge Mwijage akizungumzia mwafaka wa Zanzibar Zanzibar, alimtaka Rais Jakaya

Kikwete kutowasikiliza wasaidizi wake ambao alidai kuwa wanamdanganya.

Mbunge huyo alisema kuwa ni muhimu kwa Rais Kikwete yeye mwenyewe kuingia katika

mazungumzo hayo ili kupata ufumbuzi wa kina wa jambo hilo, ambalo limekuwa kero

kwa wananchi wa Zanzibar.

Naye Mbunge wa Gando(CUF), ambaye ni mnadhimu wa upinzani bungeni alisema kuwa

inaelekea Rais anapata shida juu ya mgogoro wa Zanzibar na akamtaka kufika bungeni

ili wabunge wampatie msaada.

Mbunge huyo alimweleza Waziri Mkuu, kumwambia Rais kuwa anahitajika kufika bungeni

akiwa ni sehemu mojawapo ya Bunge ili aweze kupewa msaada unaostahili kutoka kwa

wabunge.

''Rais anaelekea anapata shida juu ya mgogoro wa Zanzibar, ninamwomba aje bungeni

akiwa ni sehemu ya bunge tumsaidie, Waziri Mkuu naomba umwambie Rais, aje

tumsaidie ili apate msaada,'' alisema Mbunge huyo wa Gando.

source; http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=6365

Hivi huyu si ndio yule mwenye vyeti vya Posta Mjini(Feki)? Kama ni yeye issue yake kwanza iliishia wapi kabla hatujaanza kuhoji hoja zake anazozitoa.

Pili suala la Chenge, nafikiri halimuhusu na kama hiyo hela aliyopewa ya bia itamtokea puani. Its better kukaa kimya kuliko kufungua mdomo na watu kuthibitisha upumbavu ulionao.
 
yule jamaa hana hata chembe ya akili kule kichwani. hastahili kuwa mbunge, hata diwani tu. jamaa ana upeo mdogo sana nilipomsikia akiongea, na jimbo lake wana hasara kubwa sana kuwa na mwakilishi kama yule. wawakilishi wa aina hii ndo mwamejaa mle ndani ya bunge, na wengi wao ni wa ccm kama yeye mwenyewe. hata mkulima asiyeenda shule hawezi kuwa na akili kama ya yule jamaa.
 
wajameni,

Huyu mtu ana akili nzuri tu isipokuwa hajawahi kuitumia bado mpya kabisa, muangalieni tu akija kuitumia bunge halitokalika,
 
MBUNGE wa Buchosa, Samwel Chitalilo ameibuka bungeni na kumtetea aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge kuwa si mwizi kwa kuwa hajawahi kuvunja nyumba ya mtu.

Mbunge huyo alisema hayo jana bungeni wakati akichangia katika hotuba ya Waziri Mkuu, kuwa Chenge si mwizi na hajawahi kuvunja nyumba ya mtu ili kuiba hivyo aachwe bila kusakamwa.

Chenge alijiuzulu baada ya kudaiwa kuweka kiasi kikubwa cha fedha huko Kisiwa cha Jersey ambazo alikiri kwamba ni zake, lakini hazihusiani na ununuzi wa rada.

Mbunge huyo alisema kwamba, alizingaliza benki ambazo zimekuwa na tabia ya kutoa siri za wateja kuacha kufanya hivyo.

Sambamba na kumkingia kifua Chenge, mbunge huyo pia alidai kuwa ni jambo la kushangaza kuona kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakimzungumza vibaya Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wakimhusisha na masuala ya ukiukwaji wa maadili.

Vilevile, Mbunge huyo alipongeza juhudi za aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa ambaye

alijuzulu kutokana na sakata la Richmond, akidai kuwa kuwajibika kwake kulikuwa ni

kwa kisiasa.

Hata hivyo, wakati akiendelea na mchango akidai kuwa tabia ya wabunge kuingiza ushirikina na kutuhumiana kwa uchawi haifai, kwa sababu wataanza kutajana ovyo, Spika wa Bunge, Samwel Sitta aliingilia kati na kumtaka mbunge huyo kurudi kwenye hoja na kumuangaliza kuwa angalizo kuwa kila mbunge ana uhuru wa kuongea katika jumba hilo.

Aliporejeshwa katika hoja, Mbunge huyo aliamua kuikalia kooni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akidai kuwa imekuwa ikiwaonea wafanyabiashara kwa kuwabambikia kodi zaidi, hususani katika bidhaa zinazonunuliwa kutoka nje ya nchi.

Alisema kuwa wataalam wa TRA, wanajikita katika bei wanazoziona katika mtandao wa

kompyuta na kusahau kuwa biashara hufanywa ikitegemea nguvu ya mapatano.

Mbunge huyo alishauri kuwa katika wakati huu,Tanzania inapaswa kuepuka kuchanganya

masuala ya uchumi na siasa.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Severina Mwijage alisema kuwa ahadi ya

posho za madiwani itekelezeke sanjari utekelezaji wa miradi usimamiwe ipasavyo kwa kuimarisha ufuatiliaji.

Mbunge Mwijage akizungumzia mwafaka wa Zanzibar Zanzibar, alimtaka Rais Jakaya

Kikwete kutowasikiliza wasaidizi wake ambao alidai kuwa wanamdanganya.

Mbunge huyo alisema kuwa ni muhimu kwa Rais Kikwete yeye mwenyewe kuingia katika

mazungumzo hayo ili kupata ufumbuzi wa kina wa jambo hilo, ambalo limekuwa kero

kwa wananchi wa Zanzibar.

Naye Mbunge wa Gando(CUF), ambaye ni mnadhimu wa upinzani bungeni alisema kuwa

inaelekea Rais anapata shida juu ya mgogoro wa Zanzibar na akamtaka kufika bungeni

ili wabunge wampatie msaada.

Mbunge huyo alimweleza Waziri Mkuu, kumwambia Rais kuwa anahitajika kufika bungeni

akiwa ni sehemu mojawapo ya Bunge ili aweze kupewa msaada unaostahili kutoka kwa

wabunge.

''Rais anaelekea anapata shida juu ya mgogoro wa Zanzibar, ninamwomba aje bungeni

akiwa ni sehemu ya bunge tumsaidie, Waziri Mkuu naomba umwambie Rais, aje

tumsaidie ili apate msaada,'' alisema Mbunge huyo wa Gando.

source; http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=6365
aAuonyeshe alipobomoa nyumba Chiluba, huko ni mbali sana atuonyesha nyumba iliyovunjwa na Pr Mahalu. Kweli huyo jamaa ni std VII
 
wajameni,

Huyu mtu ana akili nzuri tu isipokuwa hajawahi kuitumia bado mpya kabisa, muangalieni tu akija kuitumia bunge halitokalika,

Atakuwa amechelewa. Kwa matamshi ya jana; kichefuchefu kitupu. Bora angekaa kimya..
 
MBUNGE wa Buchosa, Samwel Chitalilo ameibuka bungeni na kumtetea aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge kuwa si mwizi kwa kuwa hajawahi kuvunja nyumba ya mtu.

Vilevile, Mbunge huyo alipongeza juhudi za aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa ambaye

alijuzulu kutokana na sakata la Richmond, akidai kuwa kuwajibika kwake kulikuwa ni

kwa kisiasa.

source; http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=6365

Spika kama yuko makini maneno kama haya inatakiwa hayakemee kabisa au mbunge aseme haswa anamaanisha nini?
 
maana yake anapingana na ripoti aliyoipigia makofi ya kamati ya kina mwakembe,
ina maana hajijui anataka nini hana msimamo, ni wale wabunge ambao wanatumika na wenzao wenye agenda kuzipitisha, yani ataewahi kumpa chochote ndio atasimama upande wake.
yani hana issue, hana mwlekeo, hana kilichompeleka humo zaidi ya kukaa mkao wa kula vya wenye agenda
 
Huyu kihiyo Chitalilo si ndiye aliyewadanganya wapigakura wake kuwa alisomea form six Uganda?

Hiki ni kiti kingine ambacho wapinzani wanaweza wakaanza kukipigania hivi sasa wakati Chitalilo akiendelea kupayuka majongoo. Wamrekodi anayosema na kwenda kutawanya maneno yake, magazetini, video, audio n.k., jimboni kwake, ili wapiga kura wake wamjue kabla ya 2010 kuwa yeye ni mtumishi wa mafisadi.
 
masikini chitalilo anashindwa kujua kama kalamu inaweza kuiba zaidi kuliko huko kuvunja nyumba anakokusema.

kwa maana hiyo kiongozi yoyote hawezi kuambiwa kaiba kwa vile sidhani kama kuna kiongozi anayeweza kwenda kuvunja nyumba ya mtu.
 
Fisadi mwingine aendelea kuropoka

Date::6/30/2008
Chitalilo adai wananchi wamempongeza kumtetea Chenge
Na Frederick Katulanda, Mwanza
Mwananchi

MBUNGE wa Buchosa, Samwel Mchele Chitalilo, ameibuka upya na kudai kuwa maoni ya wananchi yaliyotolewa na wananchi wa kumpinga kumtetea aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Change bungeni ni mbinu za wapinzani wake kisiasa na si ya wananchi wake.

Akizungumza kwa simu kutoka mjini Dodoma, Chitalilo alisema kuwa anaamini sehemu kubwa ya maoni hayo imeandaliwa na wapinzani wake kisiasa na kumtaja Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Charles Tizeba kuhusika.

"Nasema hayo siyo maoni ya wananchi wangu, hayo ni maoni ya Tizeba na wenzake, wananchi wa Buchosa wanakubaliana na kauli yangu na mara baada ya kuongea bungeni kuomba Rais Mstaafu Benjamin Mkapa asisakamwe alinipongeza kwa kunipigia simu na kunitumia ujumbe wa maandishi," alieleza Chitalilo.

Alisema siku hiyo baada ya kuongea bungeni jioni yake alipokea ujumbe wa maandishi kutoka kwa wananchi wake na watu mbalimbali zaidi ya 200 na kuongeza kuwa anaaminiwa na watu wa Buchosa na hata kile anachokizungumza ni kwa ajili yao hivyo wanaopinga ni wapinzani wake kisiasa.

Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Charles Tizeba akiwa mhandisi wa Jiji la Mwanza mwaka 2005 alijitokeza kuombe uteuzi wa kugombea ubunge wa jimbo la Buchosa lakini aliangushwa na Chitalilo katika kura za maoni.

Kutokana na hatua ya kujitokeza kuwania ubunge wa jimbo hilo, ilimfanya Chitalilo kumchukulia Tizeba kama mpinzani wake kisiasa.

Hata hivyo, Tizeba alipoulizwa kwa njia ya simu jana kuhusiana na kauli ya Chitalilo, alisema madai ya Chitalilo ni kutapatapa na kueleza kuwa yeye hana muda wa kupoteza kuandaa watu wa kumshutumu na kusema kuwa Chitalilo anapaswa kutambua kuwa wananchi wa sasa wa Tanzania wamekwishaamka.

"Mimi sina muda mchafu, hapa nilipo nina kazi nyingi za kuwatumikia wananchi wa Wilaya ya Sikonge na wala sijatia mguu wangu huko (Mwanza), lakini Chitalilo anapaswa kutambua kuwa kama aliropoka, aliropoka mambo yake na mimi sikumtuma,"alisema.

Nako Arusha, Hemed Kivuyo anaripoti kuwa baadhi ya wananchi wa Jimbo la Arusha Mjini wamemjia juu Mbunge wao, Felex Mrema kwa kumtaka kutowatetea baadhi ya viongozi wanaodaiwa kufuja fedha za wananchi.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wananchi hao walisema kuwa wamekerwa na kitendo cha Mrema kutoa kauli inayoonyesha kuwasafisha viongozi wanaodaiwa kuhusika moja kwa moja na tuhuma za ufisadi na kumtaka Mbunge huyo kukaa kimya bungeni.

Mmoja wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Hamisi Gaudhi (37), Mkazi wa katikati ya Jiji la Arusha,alisema kuwa mbunge wao Mrema ameshindwa kutimiza ahadi yake kwa wananchi na mara nyingi amekuwa kimya bungeni ila sasa anashangazwa na kauli ya Mbunge huyo aliyoiita ya `kukurupuka` ya kuwasafisha viongozi wabadhirifu. "Nashangaa sana kwa kuwa yeye mwenyewe ameshindwa kuonekana katika jimbo lake na tumezoea kumuona bungeni akiwa kimya, sasa badala ya kuongelea masuala ya matatizo ya jimbo lake, yeye anakurupuka na kauli mbovu," alisema Hamisi kwa ukali.

Mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Edward Kasano (46), akizungumza na gazeti hili alidai kuwa mbunge wao bado ana deni kubwa katika jimbo lake kwa kuwa hawakumuona toka wamchague na kumtaka aendelee kukaa kimya bungeni kwa kile alichokiita kawaida yake awapo bungeni kuliko kuongea maneno ya kutetea uzembe.

"Ni afadhali angekaa kimya kwa kuwa sisi ni kama hatuna mbunge, kuliko kuongea maneno kama hayo ya kutetea ufujaji wa fedha za wananchi. Yeye ameshindwa kuwatetea wananchi, akae kimya, asubiri miaka yake ikiisha aje kujibu tuhuma kwa wananchi wake,"alisema Edward.

Naye mkazi mwingine wa Kata ya Daraja Mbili, Peter Ndarvoi, alisema kuwa wananchi wa Mkoa wa Arusha wanapaswa kuandamana ili kumpinga mbunge wao aliyedai kuwa amewasaliti kwa kutotimiza ahadi zake na kutokuoneakana jimboni mwake na kisha kutoa kauli iliyoonekana kuwadhihaki Watanzania. "Mimi nawaomba wananchi wenzangu sote kwa pamoja tuandamane kupingana na kauli ya mbunge wetu ya kuwatetea wabadhirifu.
 
Ignorance stimulates poverty and so many other things.Inakuwaje watu wanapongeza pale ambapo mafisadi wanasafishana?Hii ina doubts sana probably ni family yake na lazima kuna vijisenti wana sogezeana wanapo teteana.They must be nuts.Anyways sishangai hawa watu kama ndio walewale waliomfanyia welcome party lazima watakuwa dakika kumi mbele.hawawezi kurote in poverty while their representatives are accumulating 'vijisenti'in offshore bank accounts and being driven around in poshy cars so called 'mashangingi' while wao wanasifia tu.Sio lazima ukwate kilimi ndio uwe ndondocha hao wananchi watakuwa mandondocha yao kama kweli wapo.
 
Chitalilo kweli unaonekana hujatulia kabisaa! Yaani wakupongeze kwa kusafisha wezi wa mali zao? ama kwei wewe uifoji vyeti, nina wasi wasi hata cha darasa la saba huna!

Anyway sihitaji kukulaumu wewe sana, bali ni sisi wananchi tunao endelea kuabudu chama kwa kumpigia kura mtu yeyote aliye letwa na chama mbele yetu hata kama hafai kabisa!
Na pengine jinsi unavo endelea kubofoa litakuwa ni fundisho kwetu.
 
Back
Top Bottom