The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Posted Date::5/8/2008
Chenge: Siwezi kujiua niache visenti vyangu

* Atamba akiwahutubia wananchi wa Bariadi

* Vigogo wa CCM Mwanza, Shinyanga wamsindikiza

* Mkuu wa Wilaya aongoza mapokezi mjini

* Makada Bariadi wapinga tamko la UVCCM Tanga


Frederick Katulanda, Bariadi


LICHA ya aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge kuwaomba radhi Watanzania kwa kudai kuwa Sh1.2bilioni anazodaiwa kuzificha katika Kisiwa cha Jersey ni vijisenti, jana alirudia tena usemi huo wakati akihutubia mamia ya wakazi wa Bariadi mjini.


Chenge aliwaambia wananchi waliofika kumsikiliza kuwa hawezi kunywa sumu na kuacha vijisenti vyake nyuma.


"Mnyantuzu, kamwe siwezi kunywa sumu ili nife na kuacha vijisenti vyangu nyuma..." alisema Chenge.


Akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Bariadi jana, Chenge alisema kuwa amesikitishwa sana kuzushiwa kuwa amefariki dunia na kusema kwamba hawezi kujiua na kuviacha vijisenti vyake.


Akizungumza kwa Lugha ya Kisukuma Chenge alisema: "Bhadugu bhane wakayomba niachile olwa sumu, bhadugu Mnyantuzu ong'wa sumu, oleka vijisenti byakwe?". Alikuwa ana maanisha kuwa, akiwa kama Msukuma Mnyantuzu hawezi kufa kwa kujiua na kuacha vijisenti vyake.


Wakati Chenge akirejea kutoka safari ya China, alisema kwamba amesikia kuna watu wanalalamikia vijisenti na alipobanwa na waandishi wa habari kuwa bilioni moja ni vijisenti, alisema kwamba kila mtu ana viwango vyake.


Mara baada ya kutoa matamshi hayo, watu mbalimbali wakiwamo wanasiasa walijitokeza kulaani matamshi hayo na kumtaka aeleze alivyopata hizo fedha, ikiwa ni pamoja na kuachia madaraka ya uwaziri.


Baada ya hali hiyo kuwa tete, Chenge kupitia vyombo vya habari aliomba msamaha Watanzania kwamba, kwa Wasukuma vijisenti ni neno la kawaida na kwamba yeye si mjuzi wa Kiswahili kama ilivyo kwa Wazaramo.


Pamoja na hayo, mamia ya wananchi wa Wilaya ya Bariadi wakiwamo viongozi wa CCM, walijitokeza kumpokea Chenge ambaye alihutubia mkutano wa hadhara mjini humo.


Akisoma risala ya chama, Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Bariadi, Masunga Lyabuyenze alisema wao kama wana-CCM na viongozi wa chama, wanapinga na kulaani tamko la kikao cha Baraza la Vijana wa CCM Mkoa wa Tanga kuwa waliokumbwa na tuhuma za ufisadi waachie ngazi.


Alidai tamko hilo lilipaswa kungoja uchunguzi ukamilike kwanza kwa vile Chenge anatuhumiwa tu na kwamba hazijathibitika kama ni kweli.



Katika hatua nyingine, viongozi waandamizi wa CCM wa mikoa ya Mwanza na Shinyanga jana waliongoza maandamano na mapokezi 'ya kishindo' ya Chenge ambaye alirejea kwa mara ya kwanza jimboni kwake Bariadi Magharibi, baada ya kulazimika kujiuzulu kwa kashfa ya kujilimbikizia fedha za kigeni dola milioni moja (Sh1.2bilioni) huko Uingereza zinazodaiwa kuhusika na malipo ya rada.


Viongozi walioshiriki katika maandamano yaliyoanzia Mwanza hadi Bariadi ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza,Clement Mabina na makada mbalimbali wa mkoa huo, na alipofika Bariadi alipokelewa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja.


Mbali na viongozi wa chama, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Baraka Konisaga aliongoza magari kutoka Bariadi kwenda kumpokea Chenge na msafara wake kutoka Mwanza.


Safari ya Chenge kujisafisha ilianzia jijini Mwanza juzi jioni, ambako mara baada ya kupokelewa alipelekwa katika ofisi ya CCM mkoa na kusaini kitabu cha wageni.


Akimkaribisha Mwanza Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Rajabu Kundya alisema mapokezi hayo kwao yamekuwa na maana mbili, ya kwanza ikiwa ni pole kutokana na misukosuko hiyo na pili ikiwa ni kumpongeza kwa ujasiri ambao aliuchukua kuamua kujiuzulu kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma kufanyika.


Chenge aliondoka jijini Mwanza asubihi ambako msafara wake ulipokelewa wilayani Magu katika ofisi ya CCM kwa magari 22 yakiwemo mabasi madogo matano, malori aina ya fuso saba na gari ndogo pamoja na pikipiki kumi ambazo ziliandaliwa na Mabina.


Hata hivyo, idadi ya magari iliongezeka katika mji mdogo wa Ramadi ambako timu ya wafanyabiashara wa Bariadi mjini wanaodaiwa kumuunga mkono Chenge walipofika kumpokea wakiwa na malori mengine sita na magari zaidi ya 15 wakiongozwa na Konisaga.


Akizungumza katika Vijiji vya Dutwa na Sapiwi akiwa njiani kuelekea Bariadi mjini, Chenge alisema baada ya kujiuzulu uwaziri na baadhi ya watu wa Dar es Salaam wamekuwa wakimsakama wakidai kuwa hafai kuwa mbunge.


Hata hivyo, alisema uamuzi wa kutofaa ama kufaa wanajua wananchi wa Bariadi ambao ndiyo wapiga kura wake.


"Mimi ninaamini niko safi, tungoje uchunguzi, lakini kuna watu Dar wanapiga kelele eti sifai kuwa mbunge, jamani kama sifai kuwa mbunge mnaojua sifai ni ninyi wananchi wa Bariadi wala siyo wao, lakini maandiko matakatifu yanasema mpende binadamu mwenzako, wao wamenizushia Chenge (kajiua kwa sumu) wamepata faida gani,"

alihoji.


Alisema kuwa lengo la safari yake si kujisafisha bali kuhimiza maendeleo na kuwaahidi wananchi wa Bariadi Magharibi kuwa, ahadi zake ziko pale pale ikiwemo ile ya kujenga barabara ya Shinyanga kwenda Musoma kupitia Bariadi, hadi Ramadi wilayani Magu kwa kiwango cha lami ambayo alidai inaendelea kushughulikiwa.


Chenge alijiuzulu uwaziri wa Miundombinu kuhusiana na kuficha Sh1.2 bilioni katika Kisiwa cha Jersey ambazo zinachunguzwa na Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai ya Uingereza (SFO) ili kubaini kama zina uhusiano na rushwa kwenye mchakato wa ununuzi wa rada.
 
Posted Date::5/8/2008
Katika hatua nyingine, viongozi waandamizi wa CCM wa mikoa ya Mwanza na Shinyanga jana waliongoza maandamano na mapokezi 'ya kishindo' ya Chenge ambaye alirejea kwa mara ya kwanza jimboni kwake Bariadi Magharibi, baada ya kulazimika kujiuzulu kwa kashfa ya kujilimbikizia fedha za kigeni dola milioni moja (Sh1.2bilioni) huko Uingereza zinazodaiwa kuhusika na malipo ya rada.


Viongozi walioshiriki katika maandamano yaliyoanzia Mwanza hadi Bariadi ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza,Clement Mabina na makada mbalimbali wa mkoa huo, na alipofika Bariadi alipokelewa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja.

NDIYO MAANA CCM INATAFSIRIWA KUWA NI CHAMA CHA MAFISADI, SASA UTAPINGA NINI KAMA MABO NDIYO HAYA? AIBU AIBU KWA CCM, AIBU KWA WATU WA MWANZA NA SHINYANGA, AIBU KWA VIJANA NA RISALA YAO, AIBU KWA TANZANIA YETU.

TUTAWASHANGILIA MAFISADI MPAKA LINI? TUWAZOMEE KAMA ALIVYOZOMEWA MKAPA HATA KAMA WATATUFUNGA JELA, TUNAHAKI YA KULINDA RASILIMALI ZETU.

KATIKA HAYO YOTE, MKULLO AMESEMA TUNAKARIBIA (MAADA YA MIAKA 2 AU 3) KUONDOKA KATIKA KUNDI LA NCHI MASIKINI ZAIDIO DUNIANI SUBUTU.
 
Hana lolote mwizi mkubwa!sura yake ina nini mpaka watu wa Dar si salama tumchukie,tunachukia unafiki na wizi wa mali ya umma! mikataba mibofu imepitishwa wakati wake ina maana alikuwa amelala hakuwa akiiona!Mijitu sampuli hii huko CHINA huwa ni Risasi hadharani,hii demokrezia itatupotezea muda na wakati wetu wakati washenzi wachache waliosahau kwamba dunia tunapita wanajichotea vijisenti kwa visingizio vya oh sisi wasukuma tumezoea! kwani mila za kisukuma zinaruhusu kuiba mali ya Umma! hivi hakuna wajukuu wa Mwanamalundi watusaidie huko kupuruni makuti makuvu kama haya nadhani inaweza kuwa solusheni mara nyingine! Inaonekana kabisa utawala wa sheria hapa kwetu ni msamiati basi turudi kwenye enzi za decree na authoritariarism labda tutafika!
 
.....ukifanya uchambuzI WA haraka haraka ..hali ya kuangalia hapo na inayoashiria mpasuko chamani ni kitendo cha jamaa kulakiwa na baadhi ya viongozi wa juu wa ccm -mkoa...kama mwenyekiti wa ccm mkoa,wilaya ..na makada...

mkuu wa wilaya kuwepo pia imenishangaza...

hii inamaana wanaashiria udhaifu wa rais na mwenyekiti wa chama...isingetokea kama angekuwa na nguvu ...haiwezekani kiongozi amefukuzwa au kustaafichwa na rais na mwenyekiti wa chama alafu wewe kiongozi wa chini ...unaandaa mapokezi kumlaki....bora wasingeshiriki!!!

viongozi wa chama na serikali walioshiriki mapokezi wameonyesha dharau za hali ya juu kwa rais...na sisi waangalizi wa mambo tunaona kuwa rais anashindwa kudhibiti chama na serikali kwa matukio ya aina hii!!
 
We are good at agonizing not organizing and that is where the fisads get credited! They are good at organizing,look at how Lowassa's reception in Monduli was organized! even bishops participated! compared it with Mwakyembe and how mizengwe dominated the preparations for his reception! Tuache kulalamika tuamke tuwaelimishe wanavijiji na ndugu zetu mikoani! niliwahi muuliza jamaa yangu anayefanya kazi Igunga hali ikoje na shutuma dhidi ya Rostam,ni nini maoni ya wananchi huko! alichoniambia kilinifanya nijiulize mara mbili maana yeye kwa jinsi alivyokata tamaa hakusta kutukana kwamba baada ya akili za ng'ombe, zinafuata za wakazi wa Igunga,sasa sijui niamini kwamba baada ya akili za ng'ombe zinafuata za hawa jamaa wanaoandaa mareception ya kufa mtu kwa ajili ya mafisadi? Lakini pia wanafaidi kwa kuitetea jumuiya ya mafisadi bila shaka, taabu yangu ni kwa hawa wanavijiji wa kawaida ambao huduma za barabara,maji,umeme, zahanati,shule nk ni mbovu lakini utawakuta ndani ya kijani na njano wakipunga bendera na kushangilia hata kama jua linachoma kupita kiasi! TUTAFIKA HATA KAMA MABADILIKO YATAKUJA KIZAZI CHA TANO CHA WATANZANIA
 
CCM inatia aibu hizi pesa zote wanazo zichezea zingeweza kusaidia kwenye maendeleo ya taifa mfano madawa ktk mahospital zahanati, watoto wanakaa chini hawana madawati majengo ya udongo na utakuta shule nyingine zimeezekwa kwa manyasi. Hiyo haitoshi kijijini kwake kuna WATOTO YATIMA wangapi wanao hitaji msaada!! Je! amefanya nini kwasaidia hao yatima au watu wanao hitaji msaada.
Kinamama wanapata shita ya kutafuta maji wanatembea umbali mrefu.
WAKAZI WA BARIADI KWENYE JIMBO LA CHENGE HIVI MNAFIKIRIA KWA KUTUMIA AKILI ZENU KABLA YA KUFANYA HAYO MLIOYAFANYA YA MAPOKEZI YA KUFA MTU YA HUYO FISADI CHENGE?"
 
Mm Naweza Kusema Wakazi Wa Bariadi Bado Hawajui Haki Yao Na Hawana Elimu Ya Kutosha Kabisa Na Yawezekana Bado Ni Primitive Na Haswa Lile Janga Mwalimu Alilo Kuwa Akilikemea La Ujinga...natambua Hapo Si Bule Hawa Wakazi Bado Wajinga Kumpokea Fisadi Na Kumshabikia Kwa Msululu Mrefu Wa Magari 70 Huu Ni Ujinga Mtupu Tunatakiwa Kuwaelimisha Hawa Wenzetu.
 
Chenge: Nimezushiwa




na Jane Kajoki, Bariadi



MBUNGE wa Bariadi Magharibi aliyejiuzulu uwaziri hivi karibuni kwa kashfa ya kukutwa na fedha zinazohusishwa na ufisadi, Andrew Chenge amewataka wananchi wa jimbo lake kuendelea kumwamini kwa kuwa yeye ni mtu safi na asiye na hatia yoyote kwani tuhuma dhidi yake ni za kuzushwa.

Mbali ya hilo, Chenge alisema alifikia uamuzi wa kujiuzulu wadhifa wa Waziri wa Miundombinu zaidi ya wiki mbili zilizopita si kwa sababu ya kukiri makosa, bali ili kutoa fursa kwa taasisi zinazochunguza kashfa yake kufanya kazi yake kwa uwazi.

Chenge ambaye jana alihutubia mikutano ya hadhara katika maeneo ya Bariadi Mjini, Ramadi, Nyakabimbi na Kapiwi, alisema wakazi wa Dar es Salaam ndio ambao wamekuwa wakimuona kuwa mtu asiyefaa kutokana na kubebeshwa tuhuma zisizo za ukweli, ikiwa ni pamoja na kuzushiwa kifo.

"Dar es Salaam wanasema sifai labda kwa sababu ya sura yangu...Pamoja na watu wa Dar es Salaam kupiga kelele kuwa sifai, naamini sina hatia yoyote, na ndiyo maana nilijiuzulu. Ninyi wakazi wa jimboni kwangu ndio mnajua kama sifai au nafaa.

"Haya mambo yaliyotokea ni ajali ya kisiasa. Ni mambo ya kupikwa na watu, lakini kwa tuhuma hizi wacha tuwape nafasi waendelee na uchunguzi. Sitakiwi kuzungumzia hilo kwa sasa, nimekuja nyumbani kuhimiza shughuli za maendeleo katika jimbo letu katika nyanja zote za barabara, elimu, afya na maji," alisema Chenge ambaye alivuta umati mkubwa wa wananchi waliokuwa wakimshangilia kila alipokuwa akihutubia.

Alisema pamoja na kujiuzulu uwaziri, aliahidi kuendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo lake na akasema anaamini ifikapo mwaka 2010 atakuwa ametekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005-2010.

"Walio na ndoto za ubunge tukutane kwenye hoja za utekelezaji wa ilani mwaka 2010. Mmeona tulivyojenga shule za sekondari, barabara, mabwawa, visima, vituo vya afya vyote hivyo ni katika jimbo letu. Pamoja na habari ya kuzushiwa kifo, nawaomba mtulie, tushirikiane kwa kutembea kifua mbele kufanya kazi na kujiletea maendeleo," alisema Chenge ambaye anatembelea jimbo lake kwa mara ya kwanza tangu ajiuzulu.

Akiwa katika Kijiji cha Dutwa alisema alitaja vijisenti si kwa nia ya kukejeli bali akiwa na mtazamo wa Kisukuma ambao wao wanapoongelea ng'ombe 100 kwa mfano wanasema ‘vijing'ombe'.

Hii ni mara ya pili kwa Chenge kuzungumzia kauli yake ya vijisenti ambayo kwa kiwango kikubwa ndiyo inayoonekana kuwa iliyokuza tuhuma alizokuwa akihusishwa nazo.

Kwa mara ya kwanza, Chenge alizungumzia kauli yake hiyo jijini Dar es Salaam wakati alipofanya mahojiano kwa njia ya simu na gazeti hili, ambapo aliwaomba radhi Watanzania ambao walikwazika au kuumizwa na kauli yake hiyo ya vijisenti.

Alisema halikuwa lengo lake kuwakera wananchi kwa kauli hiyo iliyozua mjadala kiasi cha baadhi ya makundi ya watu wa kada tofauti kutoa maoni yao wakimtaka Rais Jakaya Kikwete amwajibishe.

"Mimi siyo Mzaramo. Hiki ni Kiswahili. Sisi wengine kule Usukumani kusema vijimambo, au vijisenti, vijitoto hivi ni kawaida kwa desturi zetu...ndiyo maana napenda kusema wazi kwamba iwapo kuna Watanzania niliwaumiza kwa kauli ile niliyoitoa kwa nia njema kabisa na wala si kwa lengo la kuwakejeli, naomba radhi kwa hilo," alisema Chenge wakati huo.

Tuhuma dhidi ya Chenge ziliandikwa kwa mara ya kwanza katika gazeti la The Guardian la nchini Uingereza likikariri taarifa kutoka Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Jinai ya nchini humo (SFO).

Gazeti hilo liliandika kuwa, uchunguzi wa SFO uligundua akaunti moja inayohusishwa na Chenge ikiwa na zaidi ya dola za Marekani milioni moja iliyopo kwenye kisiwa cha Jersey.

Gazeti hilo liliandika kwamba, SFO ilikuwa ikitarajia kuanza upya kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo ili kuangalia iwapo zilikuwa na uhusiano na zile zinazoaminika kuwa zilitolewa kwa njia ya rushwa wakati Tanzania iliponunua rada ya kijeshi kutoka nchini humo kwa paundi milioni 28 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 70, mwaka 2002.

The Guardian katika habari yake hiyo liliripoti kuwa, taarifa hizo zinakuja ikiwa ni miaka mitatu sasa tangu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kwa kushirikiana na SFO na taasisi za uchunguzi za Uswisi na Jersey zilipoanza kuchunguza kuhusu kashfa nzima ya ununuzi wa rada.

Gazeti hilo lilimkariri Waziri Chenge akikiri kwamba fedha hizo ni zake na akatumia fursa hiyo kukanusha kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha hizo na kashfa nzima ya ununuzi wa rada, uliofanywa wakati yeye akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

"Jambo la wazi linalotaka kuonekana hapa ni kwamba mimi nilipokea kwa lengo la kujinufaisha mwenyewe fedha za rushwa kutoka BAE. Huu ni uongo," alisema Chenge.

Aidha, gazeti hilo lilimkariri Chenge akisema kuwa, wakati rada hiyo ilipokuwa ikinunuliwa yeye alihusika kwa kiwango kidogo sana katika mchakato mzima, kwani jambo hilo lilishughulikiwa na wizara nyingine na uamuzi ukaidhinishwa na Baraza la Mawaziri.

Mbali ya hilo, gazeti hilo lilimkariri mwanasheria wa Chenge anayeishi Cleveland, Ohio, nchini Marekani, J Lewis Madorsky, akikanusha kwa niaba ya mteja wake huyo, kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha zake na tuhuma zozote.

"Wakati tukitambua kuwa masuala hayo yalitokea muda mrefu uliopita, tunaweza tu tukathibitisha kuwa, tuhuma zozote za ukiukwaji wa sheria, ukiukwaji wa maadili, kutenda isivyo sawa na mambo mengine ya hivyo dhidi ya mteja wetu ni mambo ambayo kimsingi tunayakanusha kwa nguvu kubwa," alisema mwanasheria huyo wa Chenge.

Hata hivyo, gazeti hilo liliandika uchunguzi huo dhidi ya Chenge unamfanya yeye kuwa tu shahidi muhimu, kwani wanaielenga zaidi BAE ambayo inadaiwa ilimlipa wakala mmoja wa Tanzania mamilioni ya fedha ili kujenga ushawishi wa rada iliyokuwa ikiiuza kununuliwa.

Wakala huyo ambaye amekuwa akitajwa kwa muda mrefu, na ambaye sasa anaaminika kukimbia nchini na kutafutwa na polisi wa kimataifa ni, Shailesh Vithlani.
 
Chenge mbona hasemi nani kamzushia habari hizi ? Kama habari ni za uongo unaachia madaraka kweli ?
 
Hii haijatulia kabisa na nina shaka na mwandishi kwamba ana kusudio gani.

Mwandishi alitakiwa asimame na amhoji Chenge kwamba mbona anawazidi kuwazuga wananchi wasojua lolote.
 
wananchi hawakupewa nafasi ya kuuliza swali lolote? maana sioni dalili ya jibu bali maelezo tu. Vijisent bwana!
 
wananchi hawakupewa nafasi ya kuuliza swali lolote? maana sioni dalili ya jibu bali maelezo tu. Vijisent bwana!

viongozi wetu hawana huo utaratibu wa kuulizwa maswali.siku zote mkubwa hakosei ndio utamaduni wa mtanzania.
 
Nimegundua kuwa Mawaziri ambao wamebainika na wale ambao wataibainika kuwa na makosa ya ufisadi au kuhusishwa na dili chafu za wizi wa fedha za umma wataandaa maandamano ya ufisadi kama ya Lowasa na chenge.

Hivi haya maandamano huwa yanaruhusiwa na polisi ambao kisheria wamepewa jukumu la kuchunguza kesi za hawa mafisadi au wazee wa vijisenti wana madaraka yao mikononi kwa kuwa walipendekeza watu wao ngazi za juu huko polisi?Polisi wajue huu ni mkakati mbovu tena ambao unachochoea hasira kwa wananchi.

Karamagi na MSABAHA kwa mtazamo wa kashfa yao ilijikita hasa ktk uwajibikaji,wakaamua kutulia kwa kuwa ni kafara na bangusilo.

Kitambo atafuatia Mramba naye kuandaa maandamano kwenda Rombo baada ya mambo yake kuwekwa hadharani.

Mwishowe wananchi wataanda maandamano kwenda IKULU kuonana na Rais.HAYA KAZI KWENU WANA USALAMA kama mtatosha kuzima maandamano ya nchi nzima yatokeapo.
 
Naheshimu uhuru wa mtu kuandika na kutoa maoni yake, lakini pia nachoshwa na waandishi wa habari za aina hii. Sijui mwandishi alikuwa na maana gani kuandika "Atamba akiwahutubia wanachi wa Bariadi". Sielewi anafurahia, anashangaa kama ninavyoshangaa mpuuzi miye au vipi. Utatamba kweli mbele ya watu uliowaibia kama wewe si baradhuli. Au amewadharau sana wananchi wake kuelewa linaloendelea?

Kwa kweli napenda taarifa ila zingine zinanichosha na kuzidi kuniogopesha.
 
Am telling you watz tumelogwa seriously speaking.
Alafu hao watu wanaomshangilia na kumpokea ukifuatilia utagundua hawana mbele wala nyuma na hata hawafahamu kuwa uyo mtu amekwiba ela zao na ndo in one way or the other amesababisha umaskini wao
 
hilo kundi la hardcore,kada,s wa ccm bariadi pamoja na chenge.a.k.a'vijisenti"kamwe hawawezi kutuwakilisha wasukuma wa shinyanga na mwanza ktk kuutukuza "ufisadi"nyeusi ita bakia kuwa nyeusi. na kamwe haita kuwa nyeupe.huko ni kutapatapa kwa mfa maji.
 
ndio watu wakasema BADO ccm kutoka serikalini, kwa sababu kama hizi.

ccm inapigiwa kura na watu wa vijijini ambao wengi wao hawajasoma, na huamini maneno yoyote wanayoambiwa na ccm iliyowakomboa kutoka 'utumwa' na kumtoa 'mkoloni'. msishangae mkisikia watu vijijini hawajui hata kama nyerere amekwisha kufa
 
wananchi tunatakiwa kuelimika na kujua ukweli ni upi na uongo ni upi. Mtu hawezi kufanya madhambi yote hayo kuanzia madini, rada, etc etc halafu tumshangilie anapotudanganya kuwa ni msafi. shame on you people of Bariadi kwa kushindwa kutambua uongo wa mtu wa namna hiyo!! nimesikitika sana! kweli bado tuna safari ndefu
 
Back
Top Bottom