The Interview: mshana Jr.

The Interview: mshana Jr.

Kwako mshana, nina maswali kadhaa hapa.

1. Ni kitu gani haswa unajutia maishani.?
2. Elimu yako ya mambo ya kiroho imekusaidiaje wewe binafsi na watu wanaokuzunguka.?
3. Je ushawahi kupata woga.? Ilikuwa ni wakati gani na nini kilipelekea wewe kuogopa.?
4. Haya unayoshare nasi jukwaani, je familia yako inajua kuwa unajua.? Wanakuchukuliaje juu ya hilo.?

5. Umeshawahi kuona visivyooneka kwa macho ya kawaida.? Vipoje.?
6. Nakumbuka katika thread mojawapo inayozungumzia budhist college, ulsema kuwa ushawahi shuhudia kafara ya mtu toka kwa waabudu shetani, na ulipewa offer ya kujiunga nao. Je ulifikia nao wapi.?

Tuanze na hayo kisha nitarejea na mengine ninayohitaji kujua toka kwako.

Aisee mshana sijaona majibu ya hii post.
 
Kaka Mshana Jr,vp ile safari ya mafia ulirudi na mafanikio kwa kiwango gani?lini tena utaandaa safari ya kwenda huko maana ilinivutia sana, natamani kwenda kuonana na yule Rasta,anipatie mautundu ya baharini,yan ni kruz kwa ile boti yake.
 
Kaka Mshana Jr,vp ile safari ya mafia ulirudi na mafanikio kwa kiwango gani?lini tena utaandaa safari ya kwenda huko maana ilinivutia sana, natamani kwenda kuonana na yule Rasta,anipatie mautundu ya baharini,yan ni kruz kwa ile boti yake.
siendi kwa boat tena
 
5f4c16259cc7e1a3ceb6c27b617dffc9.gif
Zikiisha hizo ongezea na hizi
dd1f28444faf48271557796f7d913462.jpg

 
Asante nitautafuta siku moja.

Kuna watu hatujawahi kushuhudia uchawi na huwa hatuamini kama upo. Lakini hapa mjini kuna maonyesho ya hawa watu wa viini macho. Unakuta mtu amejipiga panga limemea kwenye kichwa kabisa na unaliona.

Wengine wanajivunja miguu na unaona kwa macho yako.

Haya mambo yanafanywaje hadi sisi tunayaona hivyo? Au huwa wanatuloga? Wanafanyafanyaje
Ule si uchawi ni mazingaombwe na viini macho na wengi huingizwa mkenge kuwa ni uchawi
 
Habari Mshana. Karibia mwezi sasa nikiwa namfikiria mtu napokea simu yake. Inanitokea mara nyingi mpaka naanza kujiuliza ni kama ni coincidence. Naweza kumfikira mtu fulani ndani ya sekunde 4 hivi napokea simu yake. Hii imekaaje? Ina ubaya au kuna kitu inaweza kunisaidia?
 
Salaamu Kaka Mshana !...

Naomba nijibu maswali haya kadri uwezavyo japo ni mengi.... samahani lakini.

1.Pesa (Sarafu) za kale zina mahusiano gani na mambo ya kichawi.... kazi yake ni nini hasa?.

2.Je ni kweli mtu anaweza kuwekewa kinga ya mwili kumzuia kutodhurika na baya lolote lile litakalopangwa juu yake?.

3.Mchawi anaweza kuwa na vitu hivi viwili "uchawi na Imani ya Kiroho" je kama anaweza kuwa navyo anavitumia vipi?.

4.Waganga wanapokupa masharti pale unapoenda kuhitaji msaada wao huwa haiwezekani mtu kutatuliwa tatizo lake bila kupewa masharti?.

5. Unaweza kuona dalili gani ukatambua kuwa unatumiwa kichawi?.

6. Je wachawi wa Mataifa mbalimbali wakikutana hutumia lugha gani kwenye mawasiliano yao?.

7. Ikitokea mtu anataka kukudhuru wewe kwa uchawi utatumia njia ya uchawi kumdhibiti au utatumia imani?.

8. Je leo hii akija mtu kwako anahitaji msaada na kweli ukaona yupo kwenye tatizo kubwa (ulimwengu wa giza ) utakuwa tayari kumsaidia?.

9. Mshana uliwahi kujaribu kutumia usafiri wowote wa kichawi na kama bado je unaweza kunielezea kidogo hatari ya usafiri wowote wa kichawi na mwendo wake?.

10. Mchawi anapoamua kumchezea mtu huwa anatafuta mtu anaemjua au yeyote?.

11. Mtu anaweza kurithishwa uchawi akiwa na umri gani, (kwa mtoto na mtu mzima).

12. Je wachawi wenyewe huwa wanaogopa nani ( tukiacha watu wa kiroho).

13. Ni sehemu gani uchawi hauwezi kuingia (au unaingia kwa shida sana).

14. Kuna tofauti gani pale mchawi anapomchezea mtu aliyejikinga na dawa na yule ambaye hajajikinga?.

15. Kuna Pesa mtu anaweza kuwa nazo ndani ila hazitumii kichawi pesa hizi huwa zina matumizi gani?.

Mwisho......... Karibu Mashana Nakungojea kwa majibu yako Muruaaaaaaaa
 
Mshana Jr nafuatilia sana posts zako hususani ile ya Budha college, mengi unayoongelea inaonyesha yanatokana na experience either ya kazi au mapitio, naomba nikuulize yafuatayo 1.Nini imani yako ktk ukristo (umeokoka?)
2.Nini shughuli yako Kuu kwa sasa inayokufanya uishi mjini.
3.Unaonaje maandishi yako /elimu ukaiweka kwenye vitabu?
 
Uchawi ulitoka wapi? Au ulitokana na nini? Ni kweli mtu hawezi kurogwa mpaka Mungu mwenyewe aruhusu?
 
Back
Top Bottom