The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Waungwana, kwa kweli today is a very sad day for our nascent democracy. Hivi jamani Tanzania tunaenda wapi? Kama hatutaki kukosolewa? hawa viongozi mbona wanatuchukulia raia million 37 (with exception ya million moja ya akina Mugongo mugongo) for granted?

Naomba nisitoe comment sasa hivi kuhusu hii issue ya Zitto mpaka nijiridhishe makosa aliyoadhibiwa nayo! Haiingii akilini wabunge kumsimamisha mwakilishi wa wananchi!! Hata kama ni kanuni au sheria za bunge, basi hizo sheria ni balaana za kizandiki, zifutwe haraka iwezekanavyo.

Jamani, Yaani sielewi kweli kama Tanzania kama familia yetu wote tunaelekea kwenye Neema. I very much doubt it. Kwa sababu akina Mugongo Mugongo wanakotupeleka ni kwingine kabisa, well tunaweza tukawa wajinga kizazi hiki, ila sina hakika kwamba vizazi vyote vitakuwa hopeless na mazezeta kama sisi! Mugongo alert your compatriots, Hali ni ngumu huko tuendako. Believe me you! Kwa mwendo huu, hatutakuwa wajinga forever.
 
Wale ambao mmemiss mchakato wa yote yaliyojiri Bungeni, ninawaletea taarifa ambayo baada ya kufupisha yote imebakia saa nzima. Nimezungumza na Zitto mara tu baada ya kikao na yuko kwenye good spirit na alikataa kumpa pole na badala yake alikubali kupokea pongezi. Kilichofanyika Bungeni ni jitihada ya kumnyamazisha na kumwadhibu kifedha. Maoni yangu ni kuwa kwa kumnyima kikao hiki na kile kinachokuja Zitto atapata mapungufu ya fedha ambayo yatamfanya afikiri mara mbili next time.

Suala la Mbunge kufungiwa siyo baya sana, tatizo ni utaratibu wa kumfungia Mbunge. Kama wangeunda kamati teule ambayo ingechunguza yote aliyoyadai zitto na baadaye kamati hiyo ingekuja na ripoti ya kusema kuwa Zitto alisema uongo basi hapo kufungiwa kwake kunakubalika. Sasa hivi kama alivyosema mtu mmoja CCM wanaweza kufanya lolote. Ukitaka documents ili kuthibitisha upande wako hawakupi ukitaka access nyingine ya information (kama utakavyomsikia spika) haupati hadi upitie kwa Spika.

Hivi sasa utaratibu ni kuwa ati mbunge akitaka information toka wizara yoyote au idara yoyote inabidi aandike kwa spika, ili ofisi ya spika iombe docs hizo kwa niaba yake. Kwa namna yoyote, hata kama hoja ilikuwa na nguvu kiasi gani ni vigumu kushinda kwani "the burden of proof" inaangukia upande wako kuthibitisha maneno yake, na siyo upande wa serikali kuthibitisha unasema uongo.

Hata hivyo, binafsi ningefurahi kama Zitto angeamua kurudi Kigoma for a "victory tour" akitoka huko aende Mwanza, Moshi, Karatu, Tarime, Karatu n.k ili kuwatia moyo wenzake na kuwapa CCM notice kwamba wamefanya uamuzi mbaya sana. Wangeamua kumkemea or lesser punishment watu wangeelewa lakini kumnyamazisha ndiyo yanakuwa yale yale ya rafiki yangu mmoja Mbunge ambaye alijikuta ananyamazishwa milele!

Akimaliza ziara hizo ndogo ndogo ndiyo aje na ziara kubwa ya kuwashukuru wananchi pale Jijini DAr. Atafanya vizuri kama hilo litatimilika kabla ya Mechi ya Taifa Stars na Msumbiji.
 
Star TV ni Obvious kufanya walichofanya kwa sababu mmiliki wake na serikali wana ajenda moja. Ni vizuri kama kungekuwa na televisheni ambayo iko independet ambayo ina-cover bunge lote non stop kama ilivyo BBC London, uchwara kama huu usingetokea!!!
 
Mimi niliangalia kiasi fulani ( ilibidi niwahi kazini ) hoja za hawa wakubwa kupinga kauli ya Zito na niliziweza kujifunza vitu vichache. Kwanza CCM walikaa as a team kabla ya kikao cha jana kuhakikisha ya kuwa wanampunish Zito kwa ili kusend message kwa wabunge wengine wa upinzani ya kuwa usipingane na serikali kwani matokeo yake yatakuwa the same .

Pili yule jamaa mwenye koti jeupe , sijui ndio waziri au nani aliposema sheria hazikuvunjwa kwa kusaini mkataba nje amekosea ...simply kwa kuwa sheria hazikuvunjwa aimaanishi ya kuwa ni sawa, kuna tofauti kati ya sheria kuvunjwa na taratibu , ninachojaribu kusema inawezekana sheria za nchi hazikuvunjwa lakini kitendo kilikuwa unethical .

Halafu kuna yule bwana mwingine aliyesema Tanzania ni mjumbe wa MIGA , kwa hiyo hawawezi kuchange mikataba . This is totally contrary to what the President has been preaching , si alisema watareview mikataba mara tuu alipochaguliwa ...
 
Na mimi naona ni comedy tu. Na tena mwakani tutaanza kuwapa mamilioni ya Constituency Development Fund! Bunge livunjwe?

MugongoMungongo, kama kweli yanatoka moyoni mwako, naona umenena maana hawa wabunge wengi ambao wanatoka CCM wameshindwa kutetea wananachi wao na badala yake wanaangalia matumbo yao... Wanaogopa yasiwakute ya kina Tom Nyimbo, Njelu Kasaka, Simpasa, Derefa na kadhalika ambao walikua wakiishambulia serikali ya chama chao kwa yale waliyoyaamini... Hebu angalia ni aibu iliyoje kwa watu wote waliochangia kuchangia wakielemea kusema tu, "Waziri Karamagi kajibu vizuri sana" bila kuwa na angalau maneno ya kuonyesha wanafikiri kwa vichwa vyao... Hivi mbona wakati wa Bunge la chama kimoja mambo yalikua magumu kwa mawaziri? Hivi hawa wabunge wanamuwakilisha nani? Hivi Karamagi anawasilisha maslahi ya nani? Lakini naamini kwa hili kuna mambo mazito kuliko Zito alivyoyawasilisha na ndio maana VITA DHIDI YA ZITTO ilikua kubwa kupita kiasi na CCM ilijipanga hadi kumfanya Spika Sitta, kumeza WEMBE bila kupenda,, hata Mbunge Stela Manyanya (CCM), yeye alitaka Zitto asiadhibiwe, hata Adam Malima (CCM) pamoja na kumshambulia ZItto alijiuma uma katika kujenga hoja kutaka kuonyesha naye anamheshimu Zitto, hata Mbunge MAnju Msambya (CCM), alionekana kumsaidia Zitto bila kujijua aliposema Zitto angepewa mkataba auone ili ajiridhishe, lakini akazungumzia kwamba eti ingekua hoja kama mkataba ule ungesainiwa na NAibu Waziri, Ngeleja lakini Karamagi ilikua ni sawa. Kwa ujumla hakuna mbunge wa CCM aliyechangia kwa dhati ya moyo wake na ndio maana hata Chacha Wangwe, alisema MUNGU ANAWAONA WANAVYOZISALITI NAFSI ZAO.. Hata hivyo Chacha aliifanya hoja iwe nzito kwa Zitto alipotaka mikataba yote ichunguzwe ikiwamo ile ya miaka ya 80, kipindi ambacho aliyekua waziri kwa sasa ana madaraka ya juu.. hapo kuna waliomuona kuwa alimlenga JK alipokuwa Waziri wa Nishati na Madini ambako alitoa leseni kadhaa za madini katika migodi mikubwa... Hapo alizidisha maadui ndani ya CCM na kuwapa nguvu Karamagi na kundi lake dogo linaloongozwa na UTATU MTAKATIFU... (EL, Karamagi, Rostam).

Hoja ya MSINGI ilikua ni kwanini Waziri alisaini mkataba wa Buzwagi London, na kwamba Waziri alidanganya Bunge kwa kusema kwamba alikwenda huko kwa kuwa alikua anatoka sekta binafsi na kuonyesha kwamba ilikua ni suala la haraka na ghafla wakati mchakato wa mkataba huo ulianza mapema na Waziri alifahamu kuwa atasafiri kwenda nje ya nchi na kwamba ni lazima angerudi.. lakini pia Waziri alisema mgodi wa Buzwagi ni kamgodi kadogo, leo anasema ni mgodi utakoliingizia Taifa fedha nyingi na kwamba utatoa ajira.. Sasa hapo aliyedanganya Bunge ni nani?

Lakini mapema habari za UHAKIKA zilisema kwamba Baraza la Mawaziri na Rais hawakua na taarifa, kabla ya Zitto kuzungumzia mkataba huo bungeni na waziri kukiri...Lakini leo tunaona watu wanakurupuka na kutetea kwa misingi ya U-CCM...

JAMANI HII NI HATARI SANA, TUNAKOELEKEA NI KUBAYA KUPITA KIASI.. SIJAPATA USINGIZI NA SAA HIZI NAANDIKA NI SAA 10 ALFAJIRI ZA TANZANIA (04.05) NAONA UCHUNGU SIASA ZINAVYOTUMIKA KUTUMALIZA. SIASA ZIMEJAA MATAPELI NA WANAFIKI WA AJABU.. NASEMA NINA USHAHIDI NITAUTOA SIKU SI NYINGI JINSI MADIWANI NA WABUNGE AMBAO WANA HISTORIA YA UHALIFU.. WAKO AMBAO WAMEKWISHAKAMATWA NA KULALA GEREZANI MARA NYINGI, BAADHI HUMU NCHINI NA NJE YA NCHI, BAADHI NI WEZI WANAOJULIKANA WAZIWAZI, LEO NI VIONGOZI NDANI YA CCM NA WANATETEA WAOVU WENZAO. HAO NI WALE NINAOWAJUA KWA USHAHIDI WA WAZI, JE, NI WANGAPI NISIOKUA NA USHAHIDI NAO?
 
Msikate tamaa enyi wana na mabinti wa Tanzania, ninyi muiwaziayo nchi yetu mema, msifumbe macho yenu. Ninyi ambao kila kukicha mnaamka na kuuliza habari za nchi yenu, msishike tama. Msitikise vichwa vyenu enyi wana mapinduzi wa karne mpya! Mnachokishuhudia sasa ni kutapatapa kwa mfa maji, mnachokiona ni jitihada za nyani kung'ang'ania tawi litelezalo, kwani siku yake ya kufa imefika.

CCM haina budi kujitutumua sasa, wabunge wake lazima washikane pamoja, kwani wakidondoka mmoja mmoja haiwastahili. Wameamua kula njama kuanguka pamoja, na pamoja wataanguka! Siku yao yaja, shujaa huanguka akasimama, hodari husukumwa akatikisika, lakini waoga wakianguka hulala chini, na wakisukumwa hupukutika! Wamezoea vile vya kunyonga, leo hivi ni vya kuchinja, hawaviwezi!
 
.....nafikiri ni bora wapinzani wote nao wakaungana na zitto ku walk out kwa hizo siku mbili ili na dunia ijue...........bunge limetekwa ..sio muhimili tena!!!!!!!!!!!!

na hii iwe kwa wapinzani wote wa Chadema, CUF etc. Lakini je wakitoka nje itabadilisha mwelekeo wa CCM? Hapana ni bora wabanane huko huko na hii wachukulie kama ushindi kwao na iwe ndio mwanzo tuu. Kuna uwezekano wa kuwa na nchi bila bunge? inasikitisha sana wabunge wanakula mabilion ya kodi za wananchi wakati ni wao ni wawakilishi wa chama na serikali. Inasikitisha wananchi wanalipia namilioni ya pesa kulipa deni la ujenzi wa bunge ambalo halina faida kwao, inasikitisha kuona rasilimali za nchi zinaibiwa na wawakilishi wawananchi wanasuport, Inasikitisha sana kumuona mzee kama Malecela anatoa kauli za vitisho kwa wawakilishi wa wananchi bila kuona haya. INASIKITISHA SANA. Nini kifanyike?

ZItto nenda jimboni kwako rudia wananchi wako waambie wasikate tamaa Aluta continue. Wapinzani shizikianeni ummoja ni nguvu CCM itawamaliza. Vyombo vya habari viacha uwakala wa CCM........
 
Kuna vifungu kadhaa kwenye mwenendo wa bunge ambavyo nimegundua kuwa vinaondoa demokrasi bungeni, na vinawanyima wananchi haki yao kusikilizwa serikalini kupitia kwa mbunge wao. Kimojawapo ni hiki cha kumfungia mbunge asihudhurie vikao vya bunge kwa njia ya simple majority vote. Adhabu hiyo haitolewi kwa mbunge tu bali ni adhabu kwa watu wa jimbo analowakilisha. Je adhabu hiyo inasaidia nini taifa hili? Kufanya hivyo kunakiweka chama chenye wabunge wengi bungeni kuzuia watu wanaowakilishwa na wabunge kutoka chama kidogo wasisikilizwe. Demokrasi ni utawala wa wengi lakini unajali pia hoja za wachache wanaopingana. Nchi hii siyo ya CCM ila ni yetu sote.
 
kazi ipo, nnaona ndugu yetu Kabwe tokea yale ayliomkuta hajui ni nini anafanya, bora apumzike kwanza na katika kupumzika akae na kutafakari, kisha ajisawazishe na kuanaglia wapi alipokosea.


huyu jamaa tokea kutokea msiba ambaop yeye anahusika amekuwa hajielewi, mara ooh rais kanizalilisha, mara ooo EAC kuwa EAF bomba, mara ooo karamagi hivi, kwa nini umekuwa kiromo romo?

umekuwa mtu wa kukurupuka tu, au ile halbadiri na ww imekupata?


sasa turudi kwenye mada ukiangalia kwa umakini utagundua kuwa zitto hajajipanga, kakurupuka, na haya ndio matatizo ya upinzani, kunahitajika mashambulizi ya uhakika na ya maana kabla ya kushambulia sio tetesi tu, au hisia maana sasa mnaotukanisha upinzani, kila siku nyie mnasema maneno halafu mnamalizia kushindwa kutetea hoja zenu.

demekrasia imefata mkondo wake kwa mujibu wa katiba tulio nayo, Kabwe kawakilisha hoja, waziri kajibu mapigo, wachangiaji wa pande zote mbili wamepata fursa za kuchangia.

michango ya wapinzani ilionekana wazi kuwa dhaifu, sasa tumlaumu nani? jamani yaani kwa kuwa wapinzani hata wakija na hoja dhaifu tuseme wameonewa na CCM hata wakija na hoja za msingi tuseme wameonea kwa kuwa wao wengi? nmo tuwe fair and balanced.


hili ni somo zuri, siasa ni mapambano kwa hiyo panga mashambulizi na pima uwezo wa unaepambana nae ili ujue ni nguvu gani ujtumie.
 
Leo Karamagi nami kanishangaza manake huwa hajui Kiswahili fasaha lakini leo kakomaa...na kum-reduce Zitto to almost nothing. Kachambua kipengele kimoja baada ya kingine, kwa data na kwa kujiamini. Kila mtu kaona kwamba Zitto alisema uongo ili kutaka umaarufu. Bado nadhani kumfungia sio jawabu, mimi nadhani ile aibu ya kwamba kadanganya, katoa data za uongo ingetosha (ingawa huyu bwana hana uso wa haya hata anapogundulika kasema uongo).

Kama alivyosema Maulida Komu, Mbunge mwenzake wa CHADEMA, anachohitaji Zitto ni kueleweshwa (ingawa shida yake ni kujifanya mjuaji).

Nani kathibitisha kuwa Zitto kasema UONGO? Yawezekana hata Mtoa hoja ya kumsimamisha Ubunge kwa mkutano mmoja wa Bunge na siku chache za Mkutano wa bajeti amesema uongo!!! Tuwe wa kweli katika kujadili masuala mbalimbali, hivi waweza thibitisha kuwa mtu kasema uongo kwa kujibu kisiasa suala lenye manufaa kwa TAIFA!! kwani Mkataba haukusainiwa nje ya nchi? Alichohitaji yeye ni KAMATI TEULE, kama kweli hakuna ufujaji na wizi ndani yake kwa nini wakatae KAMATI TEULE, **** Mbunge mmoja alisema jana katika mjadala huo kuwa kama wewe unahisi ni msafi na polisi wanataka kuja ku search nyumbani kwako, kwa nini uwe namashaka wakati unaamini kuwa wewe ni msafi? hapo kuna namna!Siku ya jana Zitto ameweka historia na naamini kuwa kuna baadhi ya wana sisiemu hawakuridhishwa na kitendo cha kumsimamisha. Kama wana JF mlifanikiwa kuona kipindi cha Bunge usiku kupitia Star Tv ukiangalia hata taswira za baadhi ya viongozi wa juu wa chama na serikali zilivyokuwa zimesawajika kwa aibu!!! Zitto amehukumiwa kwa kutetea wanyonge na si kwa kutaka umaarufu kupitia hoja binafsi!!!

Hongera Zitto wewe ni shujaa kati ya wabunge wa chache tulionao.
 
wabunge wa ccm dhambi wanayofanya ni kama kula damu ya mtu...kinna zitto ni wapinzani mtawafukuza..sasa kwa kauli ya malecela si ajabu nyie mnapokuwa mwiba..inabidi wawa kolimbanise..tunawaoneaga huruma mnapokutwa na mauti kumbe ni kwa kuwa mnakumbatia fikra za kizamani za kina malecela...na kwa kuwa nyie wanajua wakiwafukuza mtasema..dawa yenu wanawapa hiyohiyo.............wapinzani msikate tamaa..

USHAURI WANGU...WAPINZANI RALLY A SUPPORT BEHIND ZITTO COS MMESHAAMBIWA DAWA NI HIYO HIYO...KWA CHADEMA NA VYAMA RAFIKI ANDAENI MIKUTANO NA WANANCHI NCHI NZIMA ILI MUWAAMBIE UKWELI...HADI KWENYE MAENEO YA MIGONI NA KULE KIGOMA...MERERANI ETS..FANYENI HIVYO HARAKA ..ZITTO,MBOWE,SLAA,MNYIKA..MKUMBO MKO HAPA ..CHUKULIENI HILI KWA KINA...BAADA YA HAPO CHADEMA KAMA CHAMA KIMLIPIE KIJANA WAO ZITTO HOLIDAY HATA YA WIKI MBILI NJE...Zitto you also have to be very careful you dont know they may still come at your back want to see you drop dead...chadema mpeni protection..solidarity forever,..wish you good luck!!!
 
Hongera sana Zitto....
....Umesimama kidete...yaani umekandamiza kisawasawa!
....CCM they are making you more famous!!!!!!!!!!!
....Usikate tamaa....Kila mwenye akili timamu amekuelewa sana..tu
....Tuko nyuma yako.
 
Mkandara,
Frustration kama hizi ndizo zinanifanya nikimbie hili baraza. Maana mtu unapata pressure kwa hasira na disappointments pasi na kifani.
Vijana tunajiuliza hivi haya mauzauza yanayoendelea nchini kwetu tunayaona sisi tu, au hata wazee wetu waliobobea katika siasa nao pia wanayaona?? Eti" wapinzani watakaofuata nyayo za Zitto......" Ni nini hii sasa, ili kumaanisha nini jamani?????

Na hivi hao mabalozi waliopo nchi kwetu hawayaoni mambo haya jamani??? Au ndio ule usemi usemao: Alalaye usimuamshe, ukimuamsha utalala wewe??????


Mimi kwa maoni yangu wapinzani wote should walk out of the Parliament!...Maneno ya Malecela ni tishio kubwa ambalo linavunja kabisa demokrasia! His is out of line kabisaaa! sikutegemea hata kidogo, Duh!
Wapizani waondoke bungeni na wafanye kila njia kukutana na rais wa nchi..
Kitendo cha kumsimamisha Zitto ni kashfa kubwa kwa wananchi na sidhani kama Malecela anaweza kusimama mbele yetu kutuhakikishia kwamba Wabunge ni wawakilishi wa wananchi sio serikali wala chama tawala kuwajibisha mbunge wa upoinzani!.
Kifupi wanabodi nashindwa kabisa kuona logic ktk heria hii ambayo mbunge kiongozi wa chama tawala anaweza kumsimamisha mbunge wa Upinzani!.. Mimi nachofahamu ni Uongozi wa Chadema ambao unaweza kumsimamisha mbunge wake!..

Ndugu zangu bado naomba somo ktk hili
 
Mkandara,
Frustration kama hizi ndizo zinanifanya nikimbie hili baraza. Maana mtu unapata pressure kwa hasira na disappointments pasi na kifani.
Vijana tunajiuliza hivi haya mauzauza yanayoendelea nchini kwetu tunayaona sisi tu, au hata wazee wetu waliobobea katika siasa nao pia wanayaona?? Eti" wapinzani watakaofuata nyayo za Zitto......" Ni nini hii sasa, ili kumaanisha nini jamani?????

Na hivi hao mabalozi waliopo nchi kwetu hawayaoni mambo haya jamani??? Au ndio ule usemi usemao: Alalaye usimuamshe, ukimuamsha utalala wewe??????

Zinduka,

Mabalozi (wengi wao) hapo nchini wanafurahia kinachoendelea sasa hivi dhidi ya Zito kwa sababu mambo kama haya ndio hupelekea civil unrest katika nchi. wauza silaha wengi wamekuwa wakisubiri kwa hamu siku nchi yenye utajiri kama Tz itakapotumbukia kwenye civil war ili wajiuzie silaha kama hawana akili nzuri.

Kwa sasa usitegemee reaction kubwa toka kwao...

It's very sad but true.
 
Wake up guys, Tanzania politics is the worth less game that you don't want to play. Zito is amazing guy, very smart, intelligent and he have a brilliant brain. However the Tanzania system does not support this kind of people at all.

I feel very sorry for Zito, he try help the country that is not ready for any certain of changes. Tanzania is approaching slow death,and it will die no matter who does what.

Poor people in Tanzania are not ready for changes, they can't speak for themselves. There is no leaders any more in Tanzania government, there is copy cat.
It's shame to see CCM will support any stupidity agenda because their member present it. CCM will put Tanzania in the coma, if not on electrical chair ready for execution.

Where is the giant politician of those days, where is the wanamapinduzi? All this people who was fighting for Tanzania has either face political shamble or ended career.

I don't blame Zito, he tries and i always salute those who try to change unbelieveble to be believable, but it couldn't work as he predict. That is Tanzania, i hope his 2008 resolution will be politics basi, and just be a nice men for his family
 
wapi hizo hoja 11 za Mh Zitto na majibu yake Karamagi tuyachambue hapa......eti wanasema nini? EIA imefanya nini??
 
Back
Top Bottom