Tundu Lissu: Mkataba wa bandari ni suala nyeti sana

Zawadi B Lupelo

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
2,549
3,722
Makamu mwenyekiti wa Chadema Tundu Antipas Lissu amesema mkataba wa kuwakabidhi bandari baina ya Tanzania na Dubai ni swala nyeti (very seriously) ndiyo maana limepelekwa bungeni.

Akiongea club house amesema kitendo cha mkataba huo kupelekwa bungeni kinaashiria unyeti wake na athari ya mkataba husika katika sheria za nchi. Mikataba ya kimataifa yenye athari ya kubadilisha sheria lazima ipite bungeni.

Kwa mujibu wa sheria Za kimataifa kwa mfumo wa Tanzania mikataba ya kimataifa (international treaties) haiwi na nguvu dhidi ya Tanzania mpaka ipitie bungeni na kutungiwa sheria ya bunge. Hatua hii ndiyo inayoitwa domestication /ratification, yaani bunge linapitia Masharti ya mkataba wa kimataifa na kuyapitisha upya kama sheria ya bunge na baada ya hapo mkataba husika unakuwa na nguvu nchini maana unakuwa ni sheria.

Kwa kawaida mikataba ya kibiashara (bilateral commercial agreements) huwa haipiti bungeni, ukiona umepita bungeni basi mkataba husika una athari kubwa Sana kwa sheria za nchi hivyo unahitaji kupita bungeni ili kubadilisha baadhi ya sheria za nchi kuendana na mkataba husika. Hivyo kwa mujibu wa Tundu Lissu mkataba huo ukiridhiwa na bunge unakuwa sheria na unakwenda kubadilisha sheria zetu.

Tundu Lissu ameeleza kuwa mkataba huo unaenda kukinzana na Sheria zetu za maliasili zilizopitishwa na Magufuli zinazolazimisha migogoro yote ya rasimali zetu baina ya serikali na wawekezaji iamriwe nchini na kwa sheria zetu, lakini mkataba wa bandari unataka migogoro yote iamriwe Johannesburg Afrika kusini kwa kutumia sheria za Uingereza

Kuhusu vipengele vya ukomo Tundu Lissu amesema mkataba huu hauna ukomo kwani unasema utakoma pale ambapo shughuli husika zilizomo kwenye mkataba zitakoma, shughuli za kuendeleza na kusimamia bandari hazina ukomo.

---
Akijibu maswali ya wananchi kuhusiana na mkataba huu. Lissu amesema kuwa huu ni mkataba mbaya zaidi tuliowahi kuingia ukilinganisha na mingine yote.

1. Anasema ubaya wa mktaba huu unaenda kubadili sheria za nchi. Akimaanisha kuwa hakuna sheria yeyote nchini ya masuala ya uendeshaji wa bandari itakayotungwa siku na miaka ijayo bila kwanza kuhakikisha haiendi kinyume na mkataba huu wa bandari kati yetu na Dubai. Anasema kwa muktadha huo , uhuru wetu wa kumaneuvre ktk ishu za bandari ndo umeshapigwa PINI na mkataba huu

2. Pili anasema mkataba wenyewe unaenda kinyume cha katiba. Anasema kwa mujibu wa katiba Bandari ni jambo la muungano. Anahoji kdma bandari ni jambo la muungano iweje DP world ihusike na bandari za Tanganyika huku za Zanzibar zikiwa huru nje ya Scope ya mkataba huu. Anauliza utakuwaje na sheria mbili tofauti kwa jambo lilelile la muungano.

3. Pia ameonya kuhusu Kampuni hiyo ya DP kuingilia siasa za Tanzania hasa uchaguzi mkuu, akijibu swali la mwananchi, amesema kuwa uzoefu wake ni makampuni haya ya uwekezaji kufanya michezo hiyo, akatolea mfano kwenye uchaguzi wa nwaka 2005, ambao licha ya CCM kuiba hela za EPA zaidi ya dola milioni 100 ili kuitumia kwenye kampeni za uchaguzi, Makampuni ya Madini yalichangia CCM zaidi ya dola milioni 30. Akaonya kuwa hata hii ksmpuni ya Dubai nayo inaweza kuendelea na mchezo huu maana ili ifanikiwe zaidi katika mkataba huu wa kuuza nchi, lazima CCM iendelee kubaki madarakani, maana serikali yake ndiyo iliyowauzia bandari kiubwete.

Unaweza kumsikiliza kiurefu hapa:

Huu mkataba una kila dalili ya umangungo ndani yake. Kwa nini migogoro ikaamuliwe, na kwa sheria za Uingereza!!

Yaani ni kwa sababu tunawahitaji sana hao Waarabu, au ni kwa sababu tayari rushwa imeshatembezwa kwa waganga njaa, na wachumia tumbo wetu?
 
Makamu mwenyekiti wa Chadema Tundu Antipas Lissu amesema mkataba wa kuwakabidhi bandari baina ya Tanzania na Dubai ni swala nyeti (very seriously) ndiyo maana limepelekwa bungeni. Akiongea club house amesema kitendo cha mkataba huo kupelekwa bungeni kinaashiria unyeti wake na athari ya mkataba husika katika sheria za nchi. Mikataba ya kimataifa yenye athari ya kubadilisha sheria lazima ipite bungeni.

Kwa mujibu wa sheria Za kimataifa kwa mfumo wa Tanzania mikataba ya kimataifa (international treaties) haiwi na nguvu dhidi ya Tanzania mpaka ipitie bungeni na kutungiwa sheria ya bunge. Hatua hii ndiyo inayoitwa domestication/ratification, yaani bunge linapitia Masharti ya mkataba wa kimataifa na kuyapitisha upya kama sheria ya bunge na baada ya hapo mkataba husika unakuwa na nguvu nchini maana unakuwa ni sheria.

Kwa kawaida mikataba ya kibiashara (bilateral commercial agreements) huwa haipiti bungeni, ukiona umepita bungeni basi mkataba husika una athari kubwa Sana kwa sheria za nchi hivyo unahitaji kupita bungeni ili kubadilisha baadhi ya sheria za nchi kuendana na mkataba husika. Hivyo kwa mujibu wa Tundu Lissu mkataba huo ukiridhiwa na bunge unakuwa sheria na unakwenda kubadilisha sheria zetu.

Tundu Lissu ameeleza kuwa mkataba huo unaenda kukinzana na Sheria zetu za madini zilizopitishwa na Magufuli zinazolazimisha migogoro yote ya rasimali zetu baina ya serikali na wawekezaji iamriwe nchini na kwa sheria zetu, lakini mkataba wa bandari unataka migogoro yote iamriwe Johannesburg Afrika kusini kwa kutumia sheria za Uingereza

Kuhusu vipengele vya ukomo Tundu Lissu amesema mkataba huu hauna ukomo kwani unasema utakoma pale ambapo shughuli husika zilizomo kwenye mkataba zitakoma, shughuli za kuendeleza na kusimamia bandari hazina ukomo.

Swali kwa tundu lissu Vipi hamtoki barabarani!
 
Swali kwa tundu lissu Vipi hamtoki barabarani!
Nadhani kila mtu ameona. Huyu Lissu ameongea tu taratibu zinazotakiwa bila kusema mkataba una madhara gani kwa taifa. Na asingeweza kuupinga. Ujue yuko huko. Halafu eti anaonyesha kudharau hatua ya serikali ya Magufuli kutaka migogoro iamuliwd TZ. Halafu mtu na akili yake anadai Lissu ni mtetezi wa maslahi ya waTZ.
 
Lisu alihongwa na Accacia hana Uzalendo wowote yule.
 
Tundu Lissu ameeleza kuwa mkataba huo unaenda kukinzana na Sheria zetu za madini zilizopitishwa na Magufuli zinazolazimisha migogoro yote ya rasimali zetu baina ya serikali na wawekezaji iamriwe nchini na kwa sheria zetu, lakini mkataba wa bandari unataka migogoro yote iamriwe Johannesburg Afrika kusini kwa kutumia sheria za Uingereza

Kuhusu vipengele vya ukomo Tundu Lissu amesema mkataba huu hauna ukomo kwani unasema utakoma pale ambapo shughuli husika zilizomo kwenye mkataba zitakoma, shughuli za kuendeleza na kusimamia bandari hazina ukomo.
Ona upumbavu huu!

Mtu na akili timamu, tena unajitambua wewe ni kiongozi wa nchi, unafanya kwa maksudi kabisa ujinga wa namna hii?
 
Lisu alihongwa na Accacia hana Uzalendo wowote yule.
Hapana.
Weka ushabiki pembeni.
Lissu anajulikana kuwa mpambanaji toka Bulyankhulu; hadi Nyamongo. Kachaniawa magwanda na polisi kabla hata Acacia hajazaliwa.
Huu ushabiki ndio wanaoutumia akina Samia sasa kutuuza kama punda. Unasahau kabisa adui wa nchi hii ni nani badala yake unatumia ushabki tu, uliouzoea na kuufanya kama utani wa Simba na Yanga.
 
Hapo kwenye mkataba hauna ukomo ndio wananishangaza aisee.

Sisi hao juzi juzi tumeangaika kupanua bandari ya Dar na ata zile za mkoani. Hao hao sisi tunakuja kumpa mwekezaji ni jambo zuri. Sasa kwa nini tusingempa mapema akafanya ayo maendeleo na maboresho.

CCM atawapewe miaka mingine 100 hawawezi tuvusha toka kwenye umasikini wa miundombinu, huduma bora za afya na kijamii ata utawala bora
 
Back
Top Bottom