Makamba aipiga chini ETDCCo kusaini mkataba mpya wa Usambazaji Umeme Vijini (REA)

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Waziri wa Nishati Januari Makamba amezuia Kampuni ya Usambazaji umeme ya ETDCCo kusaini mkabata wa usambazaji umeme akitoa madai ya kuwepo kwa uzembe.

Makamba amezui mkataba huo leo Desemba 19, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba ya utekelezaji wa mradi wa kupeleka umeme katika maeneo yaliyopo pembezoni mwa miji (Awamu ya tatu).

ETDCo ilitakiwa kuwa miongoni mwa kampuni tano za kusaini mikataba hiyo na Wakala wa Umeme Vijijini (REA), ikitakiwa kusaini mkataba wa kusafirisha umeme wa msongo wa 33KV katika mtandao wa kilometa 102. 5 za msongo mdogo wa matumizi ya umeme wa kawaida kwa Mikoa ya Kigoma na Geita.

“Mfano ETDCo wa Mbeya, kazi ya Mbeya umefikia asilimia 28 na ulitakiwa kuwa asilimia 88, halafu leo unataka kusaini mkataba upeleke mikoa miwili, hautasaini, na iwe fundisho kwa wengine,” amesema Makamba wakati akikemea wakandarasi wanaotaka kazi mpya huku wakiwa na kasi ndogo.

Makamba amesema haiwezekani mkandarasi huyo kupokea mradi mwingine wa Sh18 bilioni unalenga kuwafikia wananchi 6,725 katika mikoa hiyo ya Kigoma na Geita wakati kashindwa mkoa mmoja.

Makamba ametengua mkataba huo mbele ya wakandarasi na watendaji wengine wa REA huku akitoa angalizo la kutotoa kazi kwa mkandarasi yeyote kwa kigezo cha uzawa endapo hatazingatia muda wa mkataba.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufundi wa Kampuni hiyo ya ETDCo, Mohamed Abdallah ameomba Serikali itazame upya uamuzi huo kutokana na changamoto alizokutana nazo.

“Kweli mradi wa Mbeya ulikuwa wa miezi 18, tulitakiwa kumaliza mwezi huu, changamoto ilikuwa upatikanaji wa vifaa. Viwanda vya China vilifungwa kutokana na ugonjwa wa Uviko-19.

“Baada ya kufungua, tayari tumeonyesha kasi ya kufunga transfoma 33 kati ya 114 zinazohitajika, tunaomba Serikali iendelee kutuamini.”

MWANANCHI
 
😂😂 futuhi ndio ni futuhi😂😂 eti na yeye anaona watu ni wazembe 😂😂
 
Athari za uviko 19 ni kubwa kila sekta, wangefikiriwa. Sijui wanaishirikisha serikali kunapokuwa na majanga ya dunia, au walikaa kimya.
 
Mbona wengine wamefanikisha pamoja na changamoto hiyo..hao wakae pembeni.

#MaendeleoHayanaChama
 
Huyu nasikia mzee wa fungu. Kuna kampuni imemmegea hapo tayari.
 
Waziri wa Nishati Januari Makamba amezuia Kampuni ya Usambazaji umeme ya ETDCCo kusaini mkabata wa usambazaji umeme akitoa madai ya kuwepo kwa uzembe.

Makamba amezui mkataba huo leo Desemba 19, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba ya utekelezaji wa mradi wa kupeleka umeme katika maeneo yaliyopo pembezoni mwa miji (Awamu ya tatu).

ETDCo ilitakiwa kuwa miongoni mwa kampuni tano za kusaini mikataba hiyo na Wakala wa Umeme Vijijini (REA), ikitakiwa kusaini mkataba wa kusafirisha umeme wa msongo wa 33KV katika mtandao wa kilometa 102. 5 za msongo mdogo wa matumizi ya umeme wa kawaida kwa Mikoa ya Kigoma na Geita.

“Mfano ETDCo wa Mbeya, kazi ya Mbeya umefikia asilimia 28 na ulitakiwa kuwa asilimia 88, halafu leo unataka kusaini mkataba upeleke mikoa miwili, hautasaini, na iwe fundisho kwa wengine,” amesema Makamba wakati akikemea wakandarasi wanaotaka kazi mpya huku wakiwa na kasi ndogo.

Makamba amesema haiwezekani mkandarasi huyo kupokea mradi mwingine wa Sh18 bilioni unalenga kuwafikia wananchi 6,725 katika mikoa hiyo ya Kigoma na Geita wakati kashindwa mkoa mmoja.

Makamba ametengua mkataba huo mbele ya wakandarasi na watendaji wengine wa REA huku akitoa angalizo la kutotoa kazi kwa mkandarasi yeyote kwa kigezo cha uzawa endapo hatazingatia muda wa mkataba.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufundi wa Kampuni hiyo ya ETDCo, Mohamed Abdallah ameomba Serikali itazame upya uamuzi huo kutokana na changamoto alizokutana nazo.

“Kweli mradi wa Mbeya ulikuwa wa miezi 18, tulitakiwa kumaliza mwezi huu, changamoto ilikuwa upatikanaji wa vifaa. Viwanda vya China vilifungwa kutokana na ugonjwa wa Uviko-19.

“Baada ya kufungua, tayari tumeonyesha kasi ya kufunga transfoma 33 kati ya 114 zinazohitajika, tunaomba Serikali iendelee kutuamini.”

MWANANCHI
Yuko sahihi
 
Safi kazi ya kwanza uko 22% unataka tena kazi mpya. Hapana.
Tena kama ugonjwa bado upo china si ndio kazi mpya itasimama kabisa.
 
Kazi za REA Zina changamoto sana , Serikali ifuate mfumo wa Rwanda ambako Serikali inanuinua vifaa Toka kwa manufacturers moja kwa moja makandarasi Wana labour charge/ cost pekee
 
Waziri wa Nishati Januari Makamba amezuia Kampuni ya Usambazaji umeme ya ETDCCo kusaini mkabata wa usambazaji umeme akitoa madai ya kuwepo kwa uzembe.

Makamba amezui mkataba huo leo Desemba 19, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba ya utekelezaji wa mradi wa kupeleka umeme katika maeneo yaliyopo pembezoni mwa miji (Awamu ya tatu).

ETDCo ilitakiwa kuwa miongoni mwa kampuni tano za kusaini mikataba hiyo na Wakala wa Umeme Vijijini (REA), ikitakiwa kusaini mkataba wa kusafirisha umeme wa msongo wa 33KV katika mtandao wa kilometa 102. 5 za msongo mdogo wa matumizi ya umeme wa kawaida kwa Mikoa ya Kigoma na Geita.

“Mfano ETDCo wa Mbeya, kazi ya Mbeya umefikia asilimia 28 na ulitakiwa kuwa asilimia 88, halafu leo unataka kusaini mkataba upeleke mikoa miwili, hautasaini, na iwe fundisho kwa wengine,” amesema Makamba wakati akikemea wakandarasi wanaotaka kazi mpya huku wakiwa na kasi ndogo.

Makamba amesema haiwezekani mkandarasi huyo kupokea mradi mwingine wa Sh18 bilioni unalenga kuwafikia wananchi 6,725 katika mikoa hiyo ya Kigoma na Geita wakati kashindwa mkoa mmoja.

Makamba ametengua mkataba huo mbele ya wakandarasi na watendaji wengine wa REA huku akitoa angalizo la kutotoa kazi kwa mkandarasi yeyote kwa kigezo cha uzawa endapo hatazingatia muda wa mkataba.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufundi wa Kampuni hiyo ya ETDCo, Mohamed Abdallah ameomba Serikali itazame upya uamuzi huo kutokana na changamoto alizokutana nazo.

“Kweli mradi wa Mbeya ulikuwa wa miezi 18, tulitakiwa kumaliza mwezi huu, changamoto ilikuwa upatikanaji wa vifaa. Viwanda vya China vilifungwa kutokana na ugonjwa wa Uviko-19.

“Baada ya kufungua, tayari tumeonyesha kasi ya kufunga transfoma 33 kati ya 114 zinazohitajika, tunaomba Serikali iendelee kutuamini.”

MWANANCHI
Sasa transformer si bongo zinazalishwa mpaka zinakosa wanunuzi?
 
Back
Top Bottom