Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 28,529
- 82,330
Chonde chonde Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Tanzania (TEC)! Jitokezeni mapema kutoa ufafanuzi juu ya kauli ya Papa ya kuwaruhusu Mapadre wetu kubariki watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Hiyo kauli yake pamoja na huo waraka wake alioutoa bila shaka mnafahamu ni kwa namna gani umeleta mtafaruku duniani kote. Na ndani ya nchi yetu mnaona ni kwa namna gani maadui wa Kanisa wanavyoitumia hiyo kauli yake kulichafua Kanisa la Mungu!
Rai yangu kwenu ni kuwaomba mjitokeze haraka na kutoa ufafanuzi wa kina. Maana mnatambua fika imani yetu, na pia mila na desturi zetu kwa ujumla wake; hazitambui vitendo vya aina hiyo.
Hivyo kama itabainika ni kweli Papa anahamasisha kuwatambua Mashoga na Wasagaji kwenye Kanisa Katoliki, ni bora tukajitenga tu na kuanzisha Kanisa letu; kama ilivyo kwa wenzetu wa KKKT.
Mwisho kabisa naamini hili ni jaribu dogo sana kwa Kanisa, ukikinganisha na majaribu mengine makubwa ambayo Kanisa lilipitia huko nyuma. Hivyo nikiwa kama muumini wa Kanisa, naamini tutalishinda.
Tumsifu Yesu Kristu.
Ni mimi Tate Mkuu, Padre niliyekimbia kiapo cha Useja. Naomba kuwasilisha.✍️🙏