Tazama foleni hii ya wanunuzi wa sukari Morogoro. Juzi Waziri Bashungwa kapitishiwa bajeti ya hovyo iliyoungwa mkono na wanaccm wote Bungeni

Hii ni mara ya pili kutokea uhaba wa sukari ktk awamu hii ya viwanda (awamu ya tano)?? Hivi wahusika hawaoni aibu Uhaba wa sukari ni kwetu tu? Mbona majirani zetu hawapati adha hii? Ndugu zetu wanaoishi mipakani huko ndiyo kumekuwa kimbilio lao. Tatizo letu kubwa liko kwa Watawala. Hawana mbinu wala nia ya kutatua kero za wananchi. Kila kitu kimekuwa ni siasa tu. Tena siasa zenyewe za maji taka.

Kazi yao kubwa na nguvu zao wanaelekeza Chadema hawana habari na suala hili la sukari. Wanawaza uagizaji wa mabomu ya machozi na risasi za moto kuwadhibiti Wapinzani na sio sukari.

Ushahidi wa haya yote angalia yanayoendelea Bungeni. Wabunge wa ccm wamechoka hawana maarifa tena. Kila anaenyanyuka kushambulia Chadema na kusifu kusiposifika. Hakuna anaewafikiria wapiga kura.

Lakini pia siwezi kuwalaumu kwakuwa wamechoka hata kujijali wenyewe imekuwa tabu. Vipi kuhusu kuwajali wapiga kura wao wataweza kweli?

La hasha.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuadimika kwa bidhaa muhimu kama sukari ni moja ya viashiria vya mgogoro wa uchumi. Mgogoro huu unajitokeza mara kwa mara kwenye serikali ya awamu ya tano.

Wasije kusingizia mwezi mtukufu ndo unasababisha uhaba wa sukari wakati hali hii haikuwahi kutokea awamu zilizotangulia na mwezi mtukufu ulikuwepo.
Visingizio huwa havikosekani
 
Kuna kipindi wakati wa jk ,Kuna watu walianza kuhodhi mpunga,mchele ukafika mpaka 3000 kwa kilo,wakaambiwa achieni mcheke uingie sokoni,,kila mtu amekauka,,serikali ikawapa wafanyabiashara waingize mchele,ndani ya mwezi,Bei I karudi kuwa sawa,
Tatizo la sukari watu wamehodhi haki ya kuimport sukari na Ni Hawa ndo hayataki kupunguza Bei na hivyo wauzaji wa jumla Kati na wale wa rejareja kulalamika kuwa haiwalipi kwa kuuza Bei elekezi
 
Wewe mchochezi, hao wanapewa
bure sukari na Mbunge wao, hongera sana Mh Mbunge kwa kuwajali wananchi wako..

Awamu ya tano inapiga kazi sana, pato la Mtanzania limekua na uchumi unakua kwa zaidi ya 7%.. Soon Watanzania kama wa hapo Moro wataanza kupanga foleni wakipewa bidhaa bure na Serikali yao..Tuchape kazi..
 
Najiona nikikoroga chai kwa ndizi mbivu. Au nikichemsha coca au pepsi.
 
Hii ni foleni ya wanaonunua sukari Morogoro mjini ndani ya duka la mbunge wao.

Kinachonikera zaidi juzi waziri wa viwanda na biashara kapitishiwa bajeti mbovu sana huku wabunge wa CCM pamoja na spika wakijikita kuishambulia Chadema.

Aidha hawa ni wanunuzi wa jumla. Unapata Corona na sukari halafu ukitoka hapo wanakuja watu wa serikali za mitaa wanataifisha.

Kishindo cha awamu ya tano kwelikweli!

Wazalishaji, Waigizaji wakubwa na Wauzaji Wakubwa wa sukari wote ni Waislamu, LAKINI kila mfungo mtukufu wa Ramadhani ukifika lazima shida hii ya sukari iibuke.
SIWAELEWI.
 
Hii ni foleni ya wanaonunua sukari Morogoro mjini ndani ya duka la mbunge wao.

Kinachonikera zaidi juzi waziri wa viwanda na biashara kapitishiwa bajeti mbovu sana huku wabunge wa CCM pamoja na spika wakijikita kuishambulia Chadema.

Aidha hawa ni wanunuzi wa jumla. Unapata Corona na sukari halafu ukitoka hapo wanakuja watu wa serikali za mitaa wanataifisha.

Kishindo cha awamu ya tano kwelikweli!

Awamu ya 5 imewarudisha watu mwaka 1980 sukari na bidhaa nyingine vilitoweka madukani.
 
Tatizo la watanzania hawafuati maelezo ya viongozi wao mbona naibu waziri wa viwanda na biashara Stella Manyanya aliisema tutumie asali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Za kuambiwa changanya na zako,

bei ya asali inalingana na bei ya sukari? Licha ya kuwa asali ni nzuri kiafya lakini je ni watanzania wangapi watamudu kutumia asali kama mbadala wa sukari?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la watanzania hawafuati maelezo ya viongozi wao mbona naibu waziri wa viwanda na biashara Stella Manyanya aliisema tutumie asali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi wewe unajua bei ya asali ?
Hivi unajua upatikanaji wa asali?
Hivi unajua utofauti wa matumizi&ladha ya asali yalivyo tofauti na sukari?

Kamwe Asali haiwezi kuwa mbadala wa sukari.
 
Back
Top Bottom