Nilichosema bungeni kuhusu mpango wa taifa (2011-2016) na Bajeti (2011/2012) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nilichosema bungeni kuhusu mpango wa taifa (2011-2016) na Bajeti (2011/2012)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by John Mnyika, Jun 29, 2011.

 1. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  MHE. JOHN J. MNYIKA (14/06/2011): Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi hii ya kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya kwenye Mpango kwa mujibu wa Kanuni ya 57 na Kanuni ya 58 ya Bunge.Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Katiba yetu, Ibara ya 63, Bunge ndiyo chombo kikuu kwa niaba ya wananchi chenye wajibu wa kuishauri na kuisimamia Serikali na katika kutekeleza wajibu huu, Ibara ndogo ya (3) inatamka kwamba, kazi mojawapo ni kujadili na kupitisha mipango ya muda mfupi na muda mrefu na huu ndiyo wajibu tulionao mbele hivi sasa.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, nitajielekeza kwenye maeneo mahususi ambayo nimewasilisha mabadiliko ambayo nitaomba yazingatiwe kwa mujibu wa Kanuni ya 57 na 58 kwenye hoja iliyo mbele yetu. Kwanza ni eneo ambalo liko ukurasa wa 117 wa nyaraka hii wa mpango wa miaka mitano. Hili ni eneo linalohusu miradi ya maji, sababu ya kuwasilisha mabadiliko haya ni kwamba huko nyuma kumekuwepo na miradi ya maji ikiwemo miradi mbalimbali katika Jimbo ambalo wamenituma kuwawakilisha la Ubungo. Miradi ambayo ilihusisha ulazaji wa mabomba ambayo yanajulikana zaidi kama mabomba ya Wachina, lakini pamoja na mabomba kuwekwa kwa muda mrefu, wananchi wa maeneo mengi sana ukienda King'ong'o, Mbezi, Mavurunza, Makoka na kwingineko. Serikali imetumia pesa nyingi sana ikiwa kiasi kikubwa ni mkopo kutoka Benki ya Dunia, lakini maji hayatoki.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hapa kuna mpango ambao unalenga kuchangia katika kurekebisha kasoro zilizotokea kipindi cha nyuma, lakini mpango wenyewe kama ukiachwa kama ulivyo utarudia kasoro za kipindi cha nyuma na kasoro kubwa iliyoko kwenye mpango huu ni kwamba ukitazama kwenye hilo jedwali la miradi hii ya maji ya Ruvu juu, Ruvu chini pamoja na ujenzi wa mabwawa Kidunda na visima Kimbiji na Mpera ambayo yangeongeza vilevile uzalishaji wa maji Dar es Salaam, yamegawanywa rasilimali zake katika kipindi cha miaka mitano. Kwa hiyo, ukianza utekelezaji mpaka utakapokamilika, kitakachotokea ni kama kinachoendelea sasa Ubungo, mradi wa mabomba wa Benki ya Dunia umewekwa, maji hayafiki, mabomba yameanza kuharibika, miundombinu imeanza kuharibiwa kwelikweli.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nafahamu, ndani ya Baraza la Mawaziri, ndani ya Serikali, baada ya mijadala ya umma na sisi kule Ubungo tulifanya kongamano la wananchi la maji, Serikali ikaamua kwamba miradi hii ya Ruvu juu, Ruvu chini, ujenzi wa bwawa Kidunda na visima Kimbiji, Mpera ikamilike kwa ukamilifu wake ifikapo mwaka 2013 na Serikali kwa maana ya Rais akatoa kauli, Waziri wa Maji akatoa kauli hadharani, sasa kilichopo kwenye mpango, kinapingana na Kauli ya Waziri na Rais ya kumaliza miradi hii ifikapo mwaka 2013.Mheshimiwa Mwenyekiti, mapendekezo yangu ya mabadiliko kwenye kifungu hiki ili kurekebisha hii hali, rasilimali zilizotengwa hapa kwa mwaka wa fedha 2014/2015 na mwaka wa fedha 2015/2016 zipunguzwe bila kuathiri jumla, zirudishwe nyuma kwenye miaka mitatu ya kwanza na nimewaeleza kwenye mapendekezo ambayo Wabunge mnayo nakala yake, kiwango cha pesa kinachopaswa kuhamishwa ili miradi ikamilike kwa wakati kuepusha hasara kama iliyoko hivi sasa kutokana na mradi wa mabomba ya Wachina na ili kutimiza kauli ya Rais na Waziri.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, kinyume cha mapendekezo haya ni kutengeneza bomu lingine la wakati la kutumia rasilimali nyingi sana, lakini mradi ukachukua miaka mingi kukamilika, miundombinu ikaanza kuharibiwa kabla hata maji kuanza kupatikana. Kwa hiyo, naomba Waheshimiwa Wabunge hii ni kauli ya Mheshimiwa Rais, Waziri na Wabunge. Humu kuna Wabunge wa Majimbo mbalimbali ili si kwa ajili ya Jimbo la Ubungo tu, kuna Wabunge wa Mkuranga, Kigamboni, Wabunge wote wa Dar es Salaam na Wabunge wa maeneo mbalimbali ambao wanaamini katika usimamiaji wa kauli hizi kwa ukamilifu wake. Kwenye eneo hili nitaomba niishie hapa nihamie eneo lingine la mabadiliko ninayoyapendekeza. Hili lilikuwa linahusu ukurasa wa 147 kifungu cha A.1.4 ambacho kinahusiana na Kifungu cha 3.4.4 cha Mpango.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili liko ukurasa wa 127 ambao ni kifungu cha A1.2.2 ambacho kinatokana na Kifungu cha 3.4.1.1 cha kuhusiana na kupunguza foleni Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Mpango huu, yale mapendekezo ambayo wadau wamekuwa wakiyatoa na tumekuwa tukiyatoa kwa muda mrefu kwamba ili kupunguza foleni Dar es Salaam, lazima kuwekeza sana kwenye barabara za pembezoni. Humu kuna barabara zimeingizwa, mapendekezo yale yamekubalika, barabara ya kutoka Goba mpaka Mbezi, Mbezi Malambo Mawili mpaka Kinyerezi, Changanyikeni kwenda Chuo Kikuu kupitia Msewe na nyinginezo. Kabla sijasema pendekezo mahususi ambalo liko hapa kuhusiana na hii barabara nyingine, niombe tu katika kutekeleza Mpango huu ili jambo liharakishwe kwa haraka sana.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna tatizo kubwa litalikumba jiji la Dar es Salaam wakati wa utekelezaji wa mradi wa mabasi yaendayo kasi utakapoanza. Barabara ya Morogoro itakapoanza kutengenezewa njia maalum ya mradi wa mabasi yaendayo kasi, foleni ambayo itakuwepo kwenye barabara ya Morogoro, itakuwa ni foleni ya kihistoria kwa sababu barabara ni nyembamba lakini kutaanza construction pale.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, maamuzi ya kujenga barabara za kuchuja magari, barabara ya kutoka External kupitia Kilungule mpaka Kimara na nyinginezo inabidi yaharakishwe, naelewa kwamba hizi barabara zote zimeshafanyiwa upembuzi yakinifu, nipendekeze katika utekelezaji tathmini ya fidia ufanyike haraka ili zoezi lifanyike haraka kabla ya kuanza kwa ujenzi wa mabasi yaendayo kasi. Lakini kuna hoja mahususi iko hapa mbele ya barabara hii ambayo naomba iingizwe kwenye schedule, barabara ya kutoka Kimara kwenda Mavurunza mpaka Bonyokwa mpaka Segerea. Hii barabara ni muhimu iingizwe kwenye schedule hii niliyoisema ya barabara, katika ukurasa wa 127, kuna orodha ya barabara na hii barabara haipo, iingizwe kwa sababu ni ahadi ya Rais ya tarehe 24 Mei 2010 alivyokwenda kutembelea Mavurunza na alisema kwamba barabara hii ndani ya miaka mitano itajengwa kwa kiwango cha lami ili kupunguza foleni.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa isipokuwepo kwenye mpango wa miaka mitano maana yake ni kwamba hii ahadi itakuwa ni ahadi hewa. Sasa ninachosema tu hapa ni kwamba, wengine wanachambua, wanasema ahadi zote za ujumla za Rais zinafikia takriban trilioni 95, sasa hizi za hapa jumla ni trilioni kama 42 plus. Sasa ili kupunguza ule mzigo wa lawama kwamba kuna ahadi nyingi ambazo haziko kwenye Mpango, naomba kutoa pendekezo hapa kwa mabadiliko kwamba barabara hii ya kutoka Kimara kupitia Bonyokwa mpaka Segerea ambayo itaunganisha Majimbo haya mawili na kupunguza foleni iingizwe kwenye hii orodha kama ambavyo nimewasilisha kwenye jedwali la mabadiliko.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni suala la nishati, Kifungu cha 3.4.1, kuna mambo mengi ambayo tungeweza kuzungumza kuhusu nishati, lakini hapa kuna pendekezo mahususi sana kwenye ukurasa wa 135, kwenye ile miradi ya umeme. Kuna mradi mmoja ambao Mheshimiwa Rais aliuzungumza Bungeni na baadaye aliuzungumza alipotembelea Wizara na baadaye kukatangazwa kuundwa Kamati ya kushughulikia mradi huo, mradi wa Stigler's Gorge, lakini mradi huu pamoja na kutangazwa kwamba ndani ya miaka hii mitano utekelezaji wake unaanza, mradi huu kwenye miradi ya umeme inayozungumzwa haupo kwenye orodha ya miradi. Kwa hiyo, mabadiliko ninayoyapendekeza hapa ni kwamba, kwa ajili ya uzalishaji mwingi wa umeme wa Taifa letu na huu ni mradi mkubwa sana utekelezaji wa mradi huu, maandalizi yake ya kirasilimali na kifedha uingizwe ndani ya mpango huu wa miaka mitano ili tuweze kuhakikisha kwamba mradi huu unatekelezwa kwa wakati.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni ukurasa wa 112, mabadiliko mahususi yanahusiana na uzalishaji, manufacturing ya Kifungu 3.4.3, lakini hapa narejea kifungu 1.12, kwanza nashukuru kwamba concept ya Special Economic Zone imeingizwa kwenye Mpango. Nitaomba tu katika utekelezaji wake huko nyuma tumewahi kuwa na mipango ya kuanzisha viwanda, tukiondoa hivi viwanda ambavyo vina motisha maalum na Ubungo ni moja kati ya maeneo ambayo yalikuwa industrial area yaani ukizungumza kuhusu viwanda vya Dar es Salaam unazungumza UFI, uzalishaji wa Zana za Kilimo, unazungumza Ubungo Maziwa, uzalishaji wa maziwa, Ubungo Garment, Urafiki na kadhalika lakini viwanda vile vingi vimefungwa, vingine vinafanya biashara tofauti, hatimaye watu wanakosa ajira. Sasa wakati tunafufua vile viwanda tumeanzisha mkakati mwingine wa maeneo maalum ya viwanda likiwemo hili la Benjamin Mkapa Special Economic Zone lililopo pale Mabibo na kule kuna viwanda vinakusudiwa kuanzishwa. Sasa naomba, vitakapoanzishwa vichangie kwenye ajira lakini tufufue viwanda vile vile vilivyokufa ndani ya Jimbo la Ubungo.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hapa kuna hoja mahususi sana ambayo naomba izingatiwe ni sehemu ya 1.1.2 ambapo ndani ya Mpango huu inakusudiwa kama sehemu ya Benjamin William Mkapa Special Economic Zone kujenga bomba maalum la mtaro kutoka eneo la viwanda kupeleka kwenye mabwawa ya kumwaga uchafu yaliyoko pale Mabibo yanaitwa Mabibo oxidization ponds. Sasa naomba hili pendekezo lizingatiwe, hii hoja ni hoja hatari sana. Kwa sababu kwa mtu anayefahamu jiografia ya Dar es Salaam, mabwawa yale ya Mabibo yameshazusha zogo sana kutokana na uchafuzi wa mazingira usio wa kawaida. Sasa hii ni waste ya kawaida tu imezusha zogo, fikiria uwe na eneo la viwanda lenye viwanda zaidi ya kumi, halafu industrial sewage ijengewe bomba lipeleke kwenye mabwawa ambayo yako katikati ya community ya watu ni janga litakalokuja kutokea baadaye.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, Sasa hoja yangu ninayopendekeza hapa ni kwamba, mabadiliko yafanyike kwenye hiki kifungu na nimeandika text ya Kiingereza sitasoma kwa Kiingereza iingie kwenye rekodi rasmi kwa sababu ni nyaraka rasmi, lakini hoja yangu ni kwamba huu mtaro wa maji machafu uelekezwe, uungane na sewage system inayo-service viwanda badala ya kupelekwa Mabibo oxidization ponds na kwa kiwango cha pesa kilichotengwa technicalities, tutazungumza baadaye, ni jambo ambalo linawezekana ili kuepusha hiyo hatari ya baadaye.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kwenyewe kuna uchafuzi mkubwa wa mazingira kwenye mto unaoitwa Mto Ubungo pale eneo la Kisiwani kutokana na uchafu wa majitaka kutoka Hosteli za Mabibo kuishia njiani na kumwagwa mtoni badala ya kumwagwa kwenye mabwawa kwa sababu ya huo udhaifu wa mtandao wa sewage system. Kwa sasa kama hali iko hivyo, je, itakuwaje kama industrial waste ikienda kuelekezwa kwenye eneo kama hilo?Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya muda nimalizie rekebisho lililoko kwenye ukurasa wa 146, linahusu kifungu cha…(Hapa kengele ya pili ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

  Mheshimiwa Mwenyekiti, iingie kwenye kumbukumbu rasmi kwa sababu nimeshawasilisha kuhusu Chuo cha Butiama ambacho kipo kwenye hotuba ya Waziri kwamba kitajengwa Chuo cha Butiama, lakini kwenye Mpango wa miaka mitano hakipo. Kwa hiyo, naomba kutoa hoja kwamba hicho Chuo nacho kiingizwe kwenye Mpango pamoja na maelezo mengine ambayo nimeyatoa:…JOHN MNYIKA: Mabadiliko ya Mbunge kuhusu Mpango wa Miaka MitanoMheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru.

  MHE. JOHN J. MNYIKA (16/06/2011) :
  Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Lakini kwanza niseme tu kwamba nimesikia michango humu Bungeni inayosema mambo mawili makubwa. Kwanza inasema Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani ameiga kutoka mawazo ya Serikali bila kuishukuru Serikali kwa mawazo yake, lakini pili mawazo kwamba CHADEMA kwenye hotuba ya Kambi ya Upinzani haikutekeleza ilani yake.Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba Serikali imeiga mawazo mengi sana kutoka kwa CHADEMA, ni jambo zuri na kwa sababu mawazo haya yako kwenye Ilani ya CHADEMA ya mwaka 2010 na hayapo kwenye ilani ya CCM. Serikali kwenye hotuba ya Waziri wa Bajeti imezungumza kuhusu mchakato wa Katiba mpya ambayo haipo kwenye Ilani ya CCM, bali iko kwenye Ilani ya CHADEMA na Serikali imeiga, ni vizuri. Serikali imezungumza kuhusu kupunguza gharama za maisha ambayo haijachambuliwa kwa kina kwenye Ilani ya CCM, lakini humu imechambuliwa na CHADEMA imeeleza ni namna gani ambavyo kuna haja ya kupunguza gharama za maisha kwa wananchi.Serikali imeiga wazo la wingi wa posho na CHADEMA ilizungumza kwa kina sana na kwa takwimu kuhusu ukubwa wa posho na haja ya kuunganisha posho, kupunguza posho na kadhalika ili kuboresha mishahara ya wafanyakazi na kusukuma mbele maisha na wakati huo huo kuweka uchumi sawa. Hili wazo nalo Serikali imelichukua, lakini imelichukua ndivyo sivyo. Sasa mimi niseme tu kwamba ni vizuri watu wakawa wanasoma ilani za vyama vingine ili kujua asili ya haya mawazo. (Makofi)

  Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kumekuwepo na wazo kwamba hotuba ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haikutekeleza ilani hii. Kuna mambo humu tumeyasema kwenye hotuba ya Kambi na ninaomba tu Serikali iyachukue kwenye bajeti ijayo kama haiingizi sasa ambayo yamo kwenye Ilani na ambayo ni mambo yanayotekelezeka japo awali walisema hayatekelezeki. Tulisema elimu bure na tulisema bure Kidato cha Kwanza mpaka Kidato cha Sita na tukasema elimu ya juu tunavunja Bodi ya Mikopo, tunatengeneza mamlaka nyingine ya ugharamiaji wa elimu kwa mfumo tofauti.Kwenye bajeti ya mwaka huu, Msemaji wa Kambi Rasmi ameeleza kwa kina ni namna gani ambavyo tutagharamia elimu kwenye shule za umma za kutwa, ni namna gani watoto wa kike watasoma bure na tumeeleza kwamba yanatekelezeka. Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu jambo lingine la msingi kwamba kuna mambo walikuwa wanasema hayatekelezeki kwamba huwezi kushusha Pay As You Earn kodi ya wafanyakazi mpaka 9%. Sisi tumeteremsha na tunaomba Serikali ikubali hili wazo na tumeonyesha jinsi gani ambavyo linatelekezeka kwa ajili ya kutetea maslahi ya wafanyakazi. Tumezungumza muda mrefu kwenye Ilani kuhusu haja ya kutoa pension kwa wazee ikasemekana kwamba wazo hili halitekelezeki. Tumeeleza jinsi gani ambavyo suala la kutoa pension kwa wazee wote inawezekana kabisa. (Makofi) Kwa hiyo, naiomba tu Serikali katika haya mawazo ambayo hayapo katika bajeti ya Serikali na yenyewe katika hitimisho la Waziri ayatolee kauli na kuyaingiza kwenye utekelezaji.

  Kuna wengine wamesema kwamba bajeti kivuli haijazungumza kuhusu suala la kupunguza gharama za vifaa vya ujenzi na kumwondolea mzigo Mtanzania maskini.
  Kuna mchumi mmoja anaitwa Rostow, tatizo ni kwamba bajeti hizi zinaweza zikawa zinasomwa kama vitabu vya A, E, I, O, U, tusome kiuchambuzi wa kiuchumi. Unapozungumza kuinua viwanda ni lazima utengeneze kitu kinachoitwa pre-conditions for take off, kwamba uweke msingi ili uwekezaji kwenye viwanda uende kwa nguvu kubwa zaidi. Ukiangalia falsafa ya bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani ambayo mimi naiunga mkono, kwa kweli imejikita katika kuhakikisha gharama za uzalishaji zinapungua. (Makofi

  )
  Mheshimiwa Mwenyekiti, mmezungumza kutaka uwekezaji mkubwa kwenye gesi na hili naomba Waziri katika majumuisho yake alitolee kauli kwa sababu kama Waziri Kivuli wa Nishati na Madini naelewa kwamba ujenzi wa bomba kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam na baadaye Tanga ambao ungepunguza sana gharama za uzalishaji ikiwemo kwenye viwanda hivi vya cement kama cha Wazo Hill pale Dar es Salaam na viwanda vingine, bomba hili Serikali ya China iko tayari kuingiza pesa kwa condition kwamba Serikali ya Tanzania iwekeze bilioni 181 kama 15% ya mtaji. Nimepitia Vitabu vyetu vyote hivi vya Bajeti ya Maendeleo na kadhalika, hiki kitu hakipo. Mimi niwaombe tu kwamba kama tunataka kupunguza gharama za uzalishaji, ikiwemo uzalishaji wa cement lazima tu-invest kwenye gesi na falsafa ya mchango wetu ambao mimi nauunga mkono ni kwamba tulinde viwanda vya ndani, hiyo ndiyo principle. Viwanda vyetu vya saruji, iwe ni Mbeya, Tanga au Dar es Salaam vingeweza kuwekewa mazingira ya kupunguza cost za uzalishaji na kulinda na kumsaidia Mtanzania kwenye ujenzi.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, nihamie eneo lingine, mimi siungi mkono bajeti hii iliyo mbele yetu mpaka Serikali itoe maelezo ya kina sana na siungi mkono siyo kwa sababu niko Upinzani, kwa sababu kuna hoja Serikali imeleta nyingi tu hapa katika Mikutano iliyopita nimeziunga mkono, Maazimio yale ya SADC, UNESCO na mambo mengine, lakini hili siungi mkono na siungi mkono kwa sababu wananchi wa Jimbo langu walionileta hapa, wamenituma nisiunge mkono.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya Waziri kusoma Hotuba ya Bajeti, mimi niliandika kwenye ukurasa wangu wa mtandao kwamba hotuba hii ya Waziri imejaa matumaini hewa na bajeti ni ya kiini macho na nilisema hivyo kutokana na takwimu za bajeti yenyewe. Ukichukua kwa mfano suala dogo tu la tozo la faini kwa Madereva kwa mfano kwa watu wanaoendesha vyombo vya usafiri, Waziri alisema kwamba faini inapanda mpaka shilingi 50,000, Muswada wa Sheria ya Fedha unasema faini inapanda mpaka shilingi 300,000, Kitabu cha Mapato ya Serikali, Kitabu cha Mapato ukiangalia faini sehemu ya Wizara husika inaonesha Serikali haikusudii kugeuza leseni na faini hizi kama chanzo cha mapato lakini mantiki ya kupandishwa kwa kiwango hiki iko wapi? Madereva wa pikipiki wa Mbezi, Madereva taxi wa Ubungo na watumiaji wengine wa vyombo vya usafiri wa daladala na kadhalika wamenituma katika hili nisiunge mkono bajeti kwa sababu hii unless hiki kitu kiondolewe. Tatizo siyo ukubwa wa faini, faini ya shilingi 20,000 tu sasa hivi iliyopo, ama 40,000 ama ngapi, tatizo ni enforcement ya Sheria, rushwa iliyotapakaa. Kwa hiyo, unapoongeza kiwango cha faini, unaongeza tu kiwango cha rushwa. (Makofi)

  Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hoja kwamba, kweli ajali ziko nyingi hata kwenye pikipiki kule Dar es Salaam ajali zinaongezeka sana lakini tufikirie zaidi. Mimi ningeshukuru kama Waziri angekuja na mkakati kwamba sasa tunahakikisha kupitia Chuo cha Usafirishaji pale Dar es Salaam tunatoa mafunzo kwa Madereva pikipiki, Idara yetu ya Traffic inakwenda kutoa mafunzo inafanyaje mambo kama haya, ningetarajia kwamba haya ndiyo yangekuwa kipaumbele. Kwa hiyo, katika hili siungi mkono kwa sababu hiyo niliyozungumza.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti hii inasema kwamba kipaumbele ni nishati na kadhalika, lakini ni maneno. Nimezungumza suala la bomba la gesi ambalo linahitaji investment ya bilioni 181 na ningeweza kuzungumza mengine lakini kwa sababu nina platform nyingine ya Uwaziri Kivuli nitazungumza.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, nihamie kwenye eneo lingine la msingi sana ambalo linafanya nisiunge mkono bajeti hii. Bajeti inasema principle kubwa tunakwenda kupunguza gharama za maisha kwa wananchi, tunapunguzaje kwa sababu gharama zetu zinapanda kwa sababu ya nishati ikiwemo mafuta na umeme, basi tunapunguza tozo kwenye mafuta. Kauli hiyo ni kauli ya kiini macho ndiyo maana Waziri alipotoa hoja yake akasema ufafanuzi atautoa tarehe 22 wakati tutakapojadili Muswada wa Sheria ya Fedha, nimeupitia huu Muswada tutakuja kuujadili baadaye, lakini principle ya kukuza tozo haiwezi kusaidia kushusha kwa kiwango kikubwa bei ya mafuta sababu tozo zote za taasisi hizi SUMATRA, TBS changanyanga na EWURA na kila kitu haifiki 3% ni 2.3% tu ya bei ya mafuta. Tozo za makampuni binafsi ya mafuta ni 2% jumla ya tozo zote hazifiki hata 5%. Sababu kubwa ya bei ya mafuta kuwa juu kwenye Taifa letu ni ukubwa wa kodi, asilimia 26 ya bei ya mafuta kwa lita ni kodi, ni takribani shilingi 600. Sasa Muswada huu haujagusa kodi, hotuba haijagusa kodi, vitabu vya mapato havijaigusa kodi kwa sababu hiyo bei ya mafuta itashuka hata Serikali ikijitahidi vipi kati ya shilingi 100 mpaka shilingi 200 ugumu wa maisha utaendelea kuwa pale pale kwa ari, kasi na nguvu zaidi. (Makofi)

  Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazungumza kuhusu nishati ya gesi ambayo ingetumika majumbani kama LPG, gesi hii kama watu wangeitumia ingepunguza bei ya nishati nyingine. Tunazungumzia kuhusu gesi kutumika kwenye magari ambayo ingeshusha nusu ya nauli Dar es Salaam au nusu ya gharama. Investment kwenye gesi na miundombinu ya gesi siyo bomba tu lile na mitandao ya gesi, vituo vya kujazia mafuta ya gesi na kadhalika ni kama vile imeachiwa TPDC tu peke yake na hiyo retention ya 50% kama tunataka kupunguza gharama za maisha lazima pamoja na kupunguza kodi kwenye mafuta twende kuwekeza kwa nguvu sana kwenye nishati mbadala.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inasema tutapunguza gharama za maisha kwa sababu tutapunguza bei ya chakula, tutafungua strategic grain reserve na mambo mengine yamezungumzwa sana humu kwenye hotuba, lakini ni matumaini hewa na kwa fact kama kwenye mwaka huu wa fedha uliomalizika, Serikali imefungua ghala, Serikali ikifungua ghala maana yake mimi na wewe na Mtanzania mwingine tunaingia loss kwa sababu yale mahindi tumeyaweka mle kwenye ghala kwa pesa zetu, ime-inject kwenye soko lakini bei haijashuka. Niwaeleze tu siri moja na Waziri ukitaka nitakuletea taarifa kimaandishi, bei haishuki Manzese pale kwa sababu chakula kinachotolewa hiki cha kutoka katika hii grain reserve watu wanabeba wanakwenda kuuza nje kwa bei kubwa zaidi, kwa hiyo haishushi sembe pale Dar es Salaam, sijui Makurumla sijui wapi sembe haishuki, enforcement iko weak. Kwa hiyo, nitaunga mkono hoja kama haya yatatolewa ufafanuzi wa kina sana.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye bajeti hii kuna mambo humu ya maji, barabara na kadhalika na kwa kwetu sisi Dar es Salaam mtu ukisikia maji, barabara na kwa Ubungo kulivyo na shida ya maji mtu anaweza kusema kwa nini huyu anakataa kuunga mkono bajeti wakati bajeti inazungumza kuhusu maji, barabara, tatizo ni matumaini hewa maana kuna tofauti kati ya maneno na matendo. Ukiingia sasa kwenye Kitabu cha Bajeti cha Maendeleo cha Wizara ya Maji, ile specific section ya Wizara ya Maji, ukiangalie investment ambayo imewekwa pale kwa ujenzi wa bwawa la Kidunda ambayo ingesaidia siyo watu wa Morogoro tu kwa sababu Kidunda iko Morogoro, ingeboresha flow ya maji kwenye Ruvu Juu ambayo inge-service watu wa Ubungo kuanzia Kiluvya, Kwembe na kwingineko, investment ni ndogo sana.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, ukija mradi wa Kimbiji na Mpera, Mkuranga na Kigamboni ambao utasaidia vilevile Ubungo na maeneo mengine ya Dar es Salaam, Serikali ilisema hata kwenye Baraza la Mawaziri najua Mheshimiwa Pinda atakubaliana na mimi walisema kwamba sasa tutaingiza pesa za ndani ili tatizo la maji Dar es Salaam liishe, lakini ukiangalia 35 bilioni ni expectation za pesa za nje. Mimi nitaunga mkono hoja tu kama kweli tukidhamiria kwa dhati kutenga rasilimali kwa ajili ya kuboresha hii miundombinu.

  Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri amesema kwenye hotuba yake kwamba sasa hii bajeti inakwenda kuondoa tatizo la foleni Dar es Salaam, lakini ukipitia bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwenye kifungu kinachohusika na decongestion of Dar es Salaam, kupunguza foleni Dar es Salaam, kimetengewa bilioni tano peke yake, sisi wa Dar es Salaam nikiwemo mimi wa Ubungo ambao takribani 80% ya mapato yanatoka kwetu five billion decongestion, 20 billion fly over, siungi mkono hoja mpaka tupate kwanza ufafanuzi wa kina kutoka kwenye Serikali, ahsante. (Makofi)
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,290
  Likes Received: 19,445
  Trophy Points: 280
  Mnyika hatuna umeme tangazeni maandamano.tunakufa aiseee
   
 3. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  tunazungumza kuhusu nishati ya gesi ambayo ingetumika majumbani kama

  hapo tuko pamojo ndg mbunge nchi zote zilizoendela zinatumia gesi majumbani maana umeme hauwezi kukidhimaitaji kama nchi inakua
   
 4. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa yaani hii battery power iliyobaki sasa sidhani hata kama naweza kumalizia kusoma hii document...
  Mwambieni Jamaa awajibike na aache usaniii
   
 5. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  nina hakika kama watu watapanga kuingia barabara kwa nia na nguvu ya asilimia 100% utashangaa umeme umekuja na mgao ukawa historia
  baadala ya kuhusu wawekezaji wao wanataka 10% ili kutoa miradi
   
 6. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kwa hali hii halafu eti tunajigamba kuwa nchi imepiga hatua!
  Mungu ibariki Tanzania
   
 7. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  SENEGAL wameshafungua njia tunaweza kuwa copy na paste kama sisi hatuna ubunifu serikali za kiafrika zimekaliwa na wazee ambao wanaitaji push kwenye kila kitu

  hali sasa ni tofauti jamaa ngereja hacha uzembe weka kambi tanesco hacha kula bata
   
 8. G

  GunzInTheAir JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  next time, summarize hii kitu Mheshimiwa mbunge
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  hebu acheni porojo huko bungeni
  tunataka maandamano ya umeme now..........
   
 10. G

  GunzInTheAir JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hata mimi nasubiria maandamano ya umeme kwa hamu. Maana ndio mtaji pekee wa chadema
   
 11. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri amesema kwenye hotuba yake kwamba sasa hii bajeti inakwenda kuondoa tatizo la foleni Dar es Salaam

  hiyo changa la macho
   
 12. g

  geophysics JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Excellent work sir...but who is going to read all book on the internet....can you make story shot mheshimiwa....?
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,290
  Likes Received: 19,445
  Trophy Points: 280
  najua hujaisoma...usingesema hivi
   
 14. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hii sio habari ya mtaji watu hatuna umeme wewe unaleta siasa

  taifa kwanza watu tunateshwa biashara zetu zinakufa
   
 15. e

  ebrah JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wewe ndo mzembe, sisi tulihitaji taarifa kwa kumukumbu zetu, kuja ku quote full content unatuboa na kutupotezea muda!
   
 16. e

  ebrah JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jaman tunahitaji mabadiliko, na kwa mifano timejifunza kuwa hawa magamba hawaelewi, ila wanahitaji kulazimishwa, Mh. Mnyika siumeona matokeo ya maandamano yaliyokwisha fanyika, ukiacha kisiasa, kimaendeleo yameleta changamotoo kwani wana magamba kidogo wameanza kufanya kazi na wananchi wananufaika kiasi, so tuwasukume sukume ili waogope kuiba sana, wafanye kazi, tuendelee na normal graph hadi tutakapochukua NCHI, tukiacha kufanya hivyo graph itashuka na itatuchukua muda kuanza kuipandisha!
   
 17. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Mkuu
  watanzania tuache tabia ya uvivu wa kusoma, ndo maana tuna maneneo mengi (vitendo haba).
   
 18. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #18
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mh Mnyika

  ktk swala la maji Dsm yaonekana kuna kitu chini kwa chini kinaendelea,hilo ni tatizo la mda mrefu sana Dsm na inavyo onekana kuna watendaji wa serikali wakishirikiana na wanasiasa vigogo walizitumia vibaya pesa zote zilizotolewa na Bank ya DUNIA,kwa hiyo mkuu inahitajika nguvu ya ziada kufanikisha swala hilo,

  Kuhusu viwanda ulivyo vitaja nadhani sera yetu ni ya kuuwa mashirika ya umma na sio kuyaendeleza na hicho ndicho Mh Zito anapingana nacho

  na hii inatokana na Viongozi wetu kujiingiza ktk biashara hivyo wanauwa viwanda alivyo anzisha baba wa taifa hili ili kuwawezesha wao kufanya biashara kiurahisi

  Tunahitaji nguvu ya ziada kupambana na hii serikali ili kuweza kuvirejesha viwanda hivyo ktk hali ya kawaida na kuendelea kuzalisha ajira kwa vijana

  Nchi bila viwanda itaendeleaje? tunakimbilia kuwekeza na hata hao tunao wapa viwanda hawana uwezo wakuviendesha

  viongozi wanacho kiangalia ni 10%

  Uchina wao hadi mabasi mijini ni ya umma,reli inaongozwa na umma,viwanja vya ndege ni vya umma,machimbo yote ya madini kule inner mongolia ni ya umma,yaani serikali inamilika zile sehemu nyeti

  lakini sisi hapa tunawekeza hadi ikulu tutafika kweli?

  Mh huu ni wakata wa kusema no

  hatutaki tena kubadilishana mali zetu kwa vyandaluwa,tunataka mali zetu zitufaidishe watz

  angalia bandali zetu,hakunha kitu urasimu,reli kufa viwanda kufa

  nyie ndio wakutufikishia ujumbe na kutuwakilisha kwa kile tutakacho watuma

  pamoja daima,kwa pamoja tutafika
   
 19. F

  FJM JF-Expert Member

  #19
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hoja zilizoko kwenye hii hotuba ya Ndugu Mnyika ni za muhimu sana. Lakini cha muhimu zaidi kwangu ni pale unapeleza wazi wazi ni kitu gani wananchi wa Ubungo wamekutama ukasimamie Bungeni. Jana tulimsikia Mh. Beatrice Shelukindo - Mbunge wa Kilindi CCM, akitumia muda wake mwingi bungeni kuongelea Jamii Forums. Leo, tena, tumemsikia Mh. Stella Manyanya -ccm special seat, akitumia muda wake Bungeni kueleza dunia nani anamtumia sms!

  Wapo wabunge wengi sana na kwa bahati mbaya wengi ni ccm wanaonekana kutumia muda wao bungeni kuongelea mambo ambayo hayausiani na wapi kura wao na wala hayana tija kwa wananchi. Hivi hata kama JF ingefungiwa, wananchi wa Kilindi wataidiake? Au kama Mh. Stella Manyanya hatopata tena sms toka kwa mtu yeyote ni kwa vipi 'special people' (huyu ni special seat) watanufaidikaje?. Naomba Ndugu JJ mkumbushane mara kwa mara kuwa mko bungeni kuwakilisha wananchi na hivyo hoja ziwe ni kwa manufaa ya watanzania waliowatuma.

  NB: Nimetumia kwa makusudi neno 'Ndugu' kwa John Mnyika badala ya 'Mheshimiwa. kama nilivyofanya kwa Mh. Stella Manyanya na Mh.Beatrice Shelukindo' kwa sababu ccm wameamuwa kuwa 'WAO'- WAKUBWA na sisi 'SISI'-WALALAHOI. Lakini tunajuwa ni nani yuko na SISI. Endeleeni Ndugu Mnyika.
   
 20. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,058
  Likes Received: 4,625
  Trophy Points: 280
  Look how u are, na ww next time stop ku reply kwa kucopy hii loong report unajaza server bure, kwani huwezi reply bila kucopy?
   
Loading...