Tazama baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza katika majina ya ajira za Ualimu yaliyotolewa. Jina la 'ABADALLAH LEONARD SHONDE lajirudia mara 196

TAMISEMI, MNALITIA AIBU TAIFA HILI


Na MwL DOTTO

usipostaajabu ya Musa utayaona ya filauni, siku ya leo nimefuatilia ufafanuzi wa kina kutoka TAMISEMI juu ya ufafanuzi wa ajira za waalimu. Katibu wa wizara ametoa ufafanuzi dhaifu kinyume na alichokisema siku chache zilizopita.

Wahitimu wengi walitegemea kusikia kuhusu idadi ya ajira kama ilivyotangazwa ili kufahamu kama kuna nafasi zingine au la. Itakumbukwa kuwa TAMISEMI ilitangaza nafasi 13000 ambazo kati ya hizo 7800+ ndio zilizo tangazwa. je Tamisemi itatangaza majina mengine?

Aidha, Katika uchunguzi wangu BABU LEMBRICE PETER mwenye nambari ya kidato cha nne (S. 1802-0102/2010) ametumia namba ya kidato cha nne ya EMMANUEL MANEMBE MABHU aliyewahi kuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari BWERI ndiye mmiliki halali mwenye index number ( S.1802-0102/2010). Hii ni kwa mujibu wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne CSEE 2010. Pia unaweza kujiridhisha kwa kuangalia matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2010. Ukosefu wa taarifa sasa ni vigezo kilichotumiwa na mfumo uliotumika kuwaondoa waombaji kama ilivyotangazwa na TAMISEMI.

Kuna MTU ameajiriwa hapa amenitatanisha sana naomba tusaidiane kufatilia uhalisia wake

Aidha Mfumo umeajir waalimu wasio na sifa kama ndugu ABBDALLAH AHMED JIGWA No yake ya Mtihani ni S2732-0091/2019
MTU huyu amehitimu shule ya sekondari MNADANI mwaka 2019 licha ya kuwa katibu kakanusha kuwa hapakuwa na kosa hilo.

Niwakumbushe kuwa kukosea kujaza taarifa sahihi pamoja na uhalali wa nyaraka kilikuwa kigezo kilichowanyima fulsa baadhi ya wahitimu. Hapa swal linakuja, kwann walikosea kujaza taarifa kama ilivyotolewa ufafanuzi na bado wakapewa nafasi?

Kwa moyo mkunjufu nadeclare. Interest kuwa sina imani na TAMISEMI, hivyo natamani kuona hatua zaid juu yenu zikichukuliwa

Regard, Mwl Dotto
 
Nyie walimu ndio mnalitia aibu taifa kwa kuendelea kuikumbatia CCM.
CCM ni Chanzo Cha Matatizo
 

Uzi una toka huku unakuja huku.
 
 

Hapa kuna shida...

Tunawataka wasitishe zoezi lote na mchakato ufanyike upya...

Kuna vijana wengi wenye sifa wameachwa na TAMISEMI kuwapa ajira watu wasio na sifa wala kustahili...

Hii si haki. Hii haikubaliki hata kidogo...
 
NIA YA KULA PESA...yaliyojirudia yatakuwa replaced baadae na ghost names....let us magufulify TZ na sio kuikwetefy and ridhichinafy
 

'ABADALLAH LEONARD SHONDE alipwe mshahara mara 196!​

 
Watu mnasikitika kujirudia rudia jina la uyo mwamba , ila mnasahau kuangalia uchukuaji wa watu bila upendeleo, izi ajira zimejaa ukanda na ukabila. Juhudi za mwenda zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…