Tazama baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza katika majina ya ajira za Ualimu yaliyotolewa. Jina la 'ABADALLAH LEONARD SHONDE lajirudia mara 196

"Najaribu kuwaza kwa sauti ,huyo muhusika anapoenda kureport kwa mkurugenzi wa halmashauri(sehemu kituo chake cha kazi kilipo ,kiutaratibu anatakiwa aende akiwa na vyeti vyake original kikiwemo cheti chake cha taaluma,,nawaza tu huyu mtu atasubmit nini???? Ukishafikiria kote huku hapa ndo utajua wala hayo sio makosa ,ni planned issue kabisa,,
 
Kakuambia NI YEYE.

Hayo majina hufanana na ndiyo maana tukiwa shuleni sekondaei mkuu wetu wa shule alilazimisha jina moja lazima liwe la KIBANTU kujitofautisha na wengine
Hapo kinachoongelewa sio Jina... Ni mwaka aliomaliza 2019
 
Mkuu uki resit index namba haibadiliki hata kidogo inabaki ileile kwa sababu hupewi index mpya ila matokeo ndo yatakayobadikika tu.

Ukiresit unapewa namba nyingine inayoanza na P, angalia hata Necta kwenye matokeo ya PC! Ukiangalia katika majina ya hizi ajira mpya utaona namba za pc nyingi tu, na ukifuatilia kwenye tovuta ya necta utazikuta zikiwa na matokeo yao!
Kuhusu huyu dada, naomba kwenye mwaka aliofanya pepa kama inavyoonyeshwa nisilisemee...
 
mi naona aliresit, huyo anaesema ukiresit unapewa index namba hiyo hiyo mbona mi zipo tofaut na nina vyet viwil vya four? tusichoshane mwachen akapige kaz
 
Madudu yaliyofanyika kwenye ajira za Ualimu zilizotangazwa.

Jina la 'ABADALLAH LEONARD SHONDE S3630-0099/2013' lajirudia mara 196

Kusema ukweli hizi ajira ni MAGUMASHI, hazina uhalisia wowote. Jina moja linajirudia mara nyngi na kituo ni kilekile.

Kuna wengine wamemaliza fom4 mwaka 2019 eti na wao wameajiriwa.

Swali: Kwanini hawajaandika vyuo walivyosomea? Kwanini hawajaweka serial number?

MUNGU TUNUSURU

Wakati kundi kubwa la vijana likiwa na nyuso za simanzi baada ya kukosa ajira, haya ni baadhi ya madudu yaliyofanywa na TAMISEMI na kupelekea vijana wengi kukosa ajira huku wakiwa na vigezo.

1. Serikali kupitia TAMISEMI imeajiri jumla ya walimu 28 waliomaliza kidato cha nne mwaka jana, 2019. Swali la kujiuliza kama hawa vijana walimaliza form four mwaka jana, chuo walienda lini na walimaliza lini mafunzo ya ualimu?. Huu ni mwendelezo wa TAMISEMI kuajiri walimu hewa serikalini.

2. Serikali imeajiri walimu wenye tahasusi zenye utata kwenye masomo yao. Mf. Mmoja kaajiriwa kama mwl wa mathematics, civics na mwingine ana masomo ya mathematics, history na kiswahili Wote wamepangiwa kufundisha sekondari. Je, walimu hawa walichukua tahasusi gani kidato cha sita?. Hawa nao ni hewa.

3. Kigezo cha umri kuajiriwa serikalini mwisho ni miaka 45. Lakini kwenye ajira zilizotangazwa na tamisemi wapo walimu walimaliza kidato cha nne kati ya 1994-1997. Ukipiga hesabu hawa walimu wana umri zaidi ya miaka 45. Swali la kujiuliza, hawa walimu walikuwa wapi miaka yote hiyo? na je, tamisemi hawakuligundua hilo?. Hawa inawezekana wana michongo na wakubwa kule tamisemi.

4. Katibu anasema ajira zilizotolewa ni 13000. Uongo mtupu. Kuna page zina walimu 48, 38, 37, 42, n.k. Ambapo kwa uwiano wa walimu 41 × idadi ya page 197 utapata jumla ya walimu 8077 ndio walioajiriwa. Je hiyo 13000 ya katibu mkuu inakujaje?. Hewa hewa kwa kwenda mbele.

5. Walimu wengi wamepangiwa sehemu ambazo hawakuchagua. Hapa inaonyesha machaguo hayakuzingatiwa kwahiyo hapakuwepo haja ya watu kuchagua shule kama serikali ilikuwa inajua pa kuwapeleka.

Madudu yapo mengi tutaendelea kuyaibua kadri tutakavyo yabaini

"Everything happen for a reason" nilivoona hakuna serial number nilijiuliza sana(kwamba excel ya hao jamaa ilishindwa kabisa kuweka number jibu ni hapana haikushindwa then why?). Nikajipa kaz ya kuhesabu idadi kwa baadhi ya pages, wastani kila page ni kama watu 40,document ina page 196

40x196=7840( kumbuka kwenye kila page kuna jina moja limerudiwa ,haya twende, nacheka lakini naogopa)

7840-195(hizi ni nafasi hewa ambazo hazina watu ,mathematically)=7645

Ajira zilitangazwa 13,000(kama kumbukumbu zangu ziko sawa)

13000-7645=5355( sio mbaya eti hahaha)

5355 ,ni watu idadi kubwa(mathematically),,ila politically sio mbaya sana,,,,

Pengine wakuu kuna second batch (who knows).

Brothers and sisters outthere na wahusika wote wa kada husika waliopatana nafasi kongole kwao ,waliokosa msikate tamaa kesho yenu ipo hata kama sio kupitia taaluma zenu basi itapatikana kwa namna nyingine ,msichoke kupambana ndani na nje ya mfumo.asante

Ali Maulid Mtawatawa-1997

Beatrice Apolinary Lyimo -1999

Charles Nyagaya John -1995

Miaka 20+ iliyopita alikuwa wapi hadi mwaka huu ndio waajiriwe?

Kuna MTU ameajiriwa hapa amenitatanisha sana naomba tusaidiane kufatilia uhalisia wake

View attachment 1636505
Anaitwa ABBDALLAH AHMED JIGWA

No yake ya Mtihani ni S2732-0091/2019

MTU huyu amehitimu shule ya sekondari MNADANI mwaka 2019

Haya ndo matokeo ya ana division four ya Point 31 na ufaulu wake wa masomo ni huu hapa;-

Civ F Hist D Geo F Kisw C Engl D Lit Eng F Bio F B/Math F

Leo amechaguliwa kwenda kufundisha Leo Leo Primary.

Maswali ya kujiuliza

1. Amesoma chuo kwa muda gani kama amehitimu kidato cha NNE 2019?

2. Amechukuliwaje kwenda kusoma chuoni ile hali ana Division Four ya pont 31?

3. Kama alianza kusoma chuoni akiwa hana cheti cha Form four aliruhusiwaje kusoma chuoni?

Rais anajitahidi sana lakin kuna watu wanamuangusha
 
Tumeomba Takukuru ipelekewa majina yote yaliyopitishwa kuajiriwa kabla hawajaripoti kwenye vituo vya kazi. Tanzania Kuna watu wanatumia fursaya mfumo kupiga deal au kuiba.kuna ufisadi mkubwa Sana Tamisemi hasa kupitia ajira za wasalimu wapya 2020.

Mmeomba kwa nani
 
Nimepata references zaidi ya moja je ni kweli zimetoka kwa kujuana au serikalin hakuna kujuana? Tamisemi ijitazame
 
Mkuu uki resit index namba haibadiliki hata kidogo inabaki ileile kwa sababu hupewi index mpya ila matokeo ndo yatakayobadikika tu.
Sijui huyo jamaa naye anajielewa kweli? Eti alikuwa anaresit huku anaendelea na ualimu, sasa kama alikuwa tayari ni mwalimu huku wenye ajira mpya anatafuta nini?
 
Hakuna cha connection wala upendeleo; kwa mfano, nimekuwa najitolea shule moja hapa Dar tangu 2019 july, na majina yetu yalichukuliwa na taarifa zetu, lakini mpka sasa hivi ni 0-0 broo (sjui sister)

Komaaa tuu; paychek can be seld-made...
 
Hakuna cha connection wala upendeleo; kwa mfano, nimekuwa najitolea shule moja hapa Dar tangu 2019 july, na majina yetu yalichukuliwa na taarifa zetu, lakini mpka sasa hivi ni 0-0 broo (sjui sister)

Komaaa tuu; paychek can be seld-made...
Conection sizungumziii barua nazungumzia watu na watu wao! Hzo barua gersha ndugu!

Kuna mtu kanambia alikuwa na mtu tamisem

Sasa hzo barua ni nini

Mimi niliambiwa nikajitolee na mzee mmoja nikamwambia huo ujinga sifanyi kujitolea serikalin
 
Anarudia mtihani wa form four wa nini kama alishafika chuo na akasomea ualimu? How can people be this foolish hata kuchambua vitu virahisi? So kasomaje chuo hadi aje aresit saivi smh
Acha ujinga wewe sijui umesoma wapi wewe ? Yani umeshindwa hata kuelewa hapo juu. Ccm tawala milele.
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom