Tatizo sio CCM bali jamii nzima ya mtu mweusi

ASIWAJU

JF-Expert Member
Nov 18, 2022
1,939
1,625
Historia ni nini?

- Historia ni somo lihusulo mambo/matukio yaliyopita[ kale ], yaliyopo na yajayo.

Kabla hatujawatupia mizigo yote ya lawama Chama cha Mapinduzi [CCM] kwa huu umasikini wa taifa hili, tuji ulize maswali haya kwanza.

Maswali
1. Kwanini mtu mweusi duniani kote ana dharaulika kwa kiasi kikubwa sana?

2. Kwanini bara la Afrika licha ya mali zote hizi tulizo nazo lakini bado sisi ni masikini na ombaomba wa kutupwa?

3. Je, ni nchi gani duniani yenye majority watu weusi walioshika shughuli zote za uchumi na imeendelea kwa kiwango kikubwa bila ya watu weupe kuhusika?

4. Mbona Wazungu, Wachina, Wakorea, Wajapan na sasa Waarabu wameendelea lakini sisi watu weusi tupo nyuma sana?

5. Je, tunazifahamu historia zetu watu weusi kabla ya uwepo wa watu weupe huku kwetu zinasemaje? Au ndio zina anzia baada ya uwepo wa watu weupe?

6. Kwanini mtu mweusi anaonekana mjinga na anakatalika duniani kote kwa mataifa yaliyoendelea kuwa hana faida yoyote?

Fikra na mawazo ya ngono yamejaa ndani ya vichwa vyetu kuliko vitu vya msingi, kutwa ni kuwaza kuridhishana vitanda mwetu na mitindo ya ngono.

Kutafuta maarifa hatutaki kabisa tume waachia wazungu na waasia.
 
Kama tunadhani matatizo yetu watu weusi yatatibiwa kwa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi itakayo ingiza wapinzani ikulu tutakuwa tuna jiongopea.

Tazama Kenya, Zambia, Malawi, Ghana kwa watu weusi nao wamepitia mabadiliko hayo lakini hamna kitu zaidi ya upumbavu na njaa kali.

KIHISTORIA TATIZO LETU HASA SISI WATU WEUSI NI NINI?
 
🤔🤔🤔Sawa tutajiongoza na kwa kwenda kuishi Ikulu za nchini
Kwa nini watu weusi tupo hivi, je tuna shida gani sisi ?

Je, hatupendi kuwa kama hao watu wengine wachina, wakorea, wazungu ?
 
Unalisimali ngapi? Twende Qatar pale wana kagesi ila angalia wanavofanya matusi.

Toa CCM ili kupunguza uzawa madarakani kama mtaani kwako
 
Imani za kishirikina zinatufanya tusiwe na akili ya kuchunguza matatizo na kuyasolve.
 
Unalisimali ngapi? Twende Qatar pale wana kagesi ila angalia wanavofanya matusi. Toa CCM ili kupunguza uzawa madarakani kama mtaani kwako
Qatar ina ongozwa kifalme kwa makarne ya miaka hadi sasa, umri ambao hata CCM haija fika lakini tazama waliopo na sisi tulipo.

Kuna shida mahali juu yetu sio bure hii hali sio ya kawaida kabisa.
 
Imani za kishirikina zinatufanya tusiwe na akili ya kuchunguza matatizo na kuyasolve.
Hili ni tatizo kubwa sana, linalo sumbua jamii hii.

Sielewi kwa nini bado tuna kumbatia hizi imani kwa kiasi kikubwa?
 
Back
Top Bottom