poleni kwa kutangulia ila usiofu iyo ndo njia pekee wote tutaipitia, tofauti ni mishale ya saa na mwaka.
Msalimiu dr mvungi, mwambie mawazo yake yataishi milele, mwambie Chachage asiofu,mawazo yake bado yanaishi, mwambie mwalimu nyerere ile katiba yake sio muda mrefu tunaiweka kwenye makumbusho ila watu wate tumekengeuka, mwambie fr Mushi kuwa watu wa zanzibar waliua mwili ila imani yake bado inadumu visiwani,
Mwambie mzee Sykes kuwa ile nchi aliyojitoa kuikomboa inaenda vizuri ila watu wake ndo tunaichafua, mwambie mh balozi sepetu tumemmis sana , aburudike kwa sinema za kanumba na muziki wa mangwair.
Mwambie mzee Kawawa na Sokoine kuwa vijana mliowalea siku izi ndo wazee wenye hekima japo wengine wanabaka na kuua.
Mwambie yule J.Jamaldin Akikweti kuwa ile mbeya uliyoenda kusuluhisha kisha ndege ikakutoa uhai siku izi iko chini ya chadema. Mwambie mwangosi ile habari iliyokutoa roho ilimpa cheo mkuu,siku izi anakula bata.
Mwambie mzee karume sr, ile zanzibar yako siku izi tumeigawana CUF na CCM, ila uko bara 2010 kura zote hazikuhesabiwa ila tunaye rais, na rais uyo katoa uhuru, kila mtu sasa anaweza kuandika japo magazeti yanafungwa kila kukicha.
Usisahau kumwambia Yondo kuwa ule mziki bado uatamba, pia mzee bob malley kuwa kijana wako wa morogoro siku izi kahamia chadema,ila anaitwa afande suleiman,sasa sijui alikoenda watamuita afande-kamanda sele!!nasema sijui.
Mwambie kijana mmoja anafuatilia mahela uswizi ila dalili njema hazijaonekana na wenye nchi ndo wenye mahela ayo, na unga , ugolo, pipi,maharage na majani ya Bob malley wanauza wao....
Mwambie mwl kuwa ile wimbo wa taifa ukipigwa, hakuna anayesimama tena watu wanaendelea kuchapa mguu,na kusaka mahela, hata bendera ikipanda au kushuka hakuna anayeangalia, ile nidhani mwl uliondoka nayo....
Mwambie mwl nyerere , wale tembo/ndovu wetu uliowaacha wame..... dah kalamu nayo imeisha winooooo