Sol de Mayo
JF-Expert Member
- Sep 10, 2016
- 6,501
- 6,185
Mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar na Mwanasiasa ambaye aliwahi kuwa Mwakilishi Jimbo la Uzini Mkoa wa Kusini Unguja, Mohamed Raza amefariki leo hii wakati alipokuwa akipatiwa matibabu, Allah amrehemu ndugu yetu huyu, na amuingize katika pepo.
Itakumbukwa May 09,2023 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi alimtembelea Mohamed Raza baada ya kulazwa Hospitalini Jijini Dar es Salaam.
Allah amjaalie kauli thabit huyu ndugu yetu, Aamiin.
=======
Aliyekuwa muwakilishi jimbo la Mkunazini kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM), Mohamed Raza ameaga dunia leo Juni 08, 2023 wakati akitibiwa jijini Dar es Salaam. Mohamed Raza Hassanali Dharamsi alizaliwa Julai 18, 1962 eneo la Mkunazini, ni mfanyabiashara maarufu visiwani Zanzibar.
Raza alizaliwa Zanzibar kwa wazazi wenye asili ya kihindi na alisoma shule ya Shaaban Robert iliyopo Upanga, Dar es Salaam mwaka 1977 mpaka 1980.
Alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2012 kuliwakilisha jimbo la Uzini, nafasi ambayo ameweza kuihudumu kwa zaidi ya miaka 10. Februari mosi zilisambaa taarifa za kifo chake ambazo zilikanushwa na mwandishi maarufu wa Zanzibar, Farouk Karim na kusema anaumwa lakini alikuwa mzima.
Baada ya kuhitimu kidato cha nne shule ya Shaaban Robert, Raza aliingia kwenye biashara kwa kuungwa mkono na jamii ya Kishia kupitia jamii ya wahindi ya Ithhia Zanzibar na kuibuka kwake na fursa za kibiashara kukisaidiwa na mfanyabiashara maarufu Zanzibar, Naushad Mohamed Suleiman. Uhusiano wa wawili hao ulikuja kuyumba 2016 kutokana na kutoaminiana.