KAHAMA : Afariki dunia masaa machache baada ya kuhesabiwa kwenye sensa ya Agosti 23

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,485
2,110

TAARIFA KWA WOTE,​

IELEWEKE SIO SENSA IMEMUUA ILA ALIKUWA HOSPITALI AKIJIUGUZA HAPO KABLA,​

KILA MMOJA AHESABIWE MIMI KAMA JABALI TAYARI NIMEHESABIWA LEO NAKUOMBA KAMA UMEKOSA NAFASI LEO SIKU BADO ZIPO KAHESABIWE.​

Hospitali-ya-Kahama-mkoani-Shinyanga-780x470.jpeg
Hospitali ya Kahama, mkoani Shinyanga

===
Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 60 mkazi wa kata ya Majengo manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga amefariki dunia saa chache baada ya kuhesabiwa na makarani wa sensa nyakati za usiku katika hospitali ya manispaa ya Kahama.

Pia mtu mwingine aliyekuwa amelazwa wodini katika hospitali hiyo alikataa kuhesabiwa mpaka awaone viongozi wa eneo lake.

Akiongea na HabariLEO, Karani wa Sensa aliyefanya zoezi hilo hospitalini hapo Robert Mayunga amesema kuwa zoezi limeenda vizuri kwani walianza majira ya saa sita usiku kwa kuanzia hospitalini hapo.

Mayunga amesema kuwa mgonjwa aliyekuwa akikataa kuhesabiwa tayari ameshahesabiwa baada ya kupata maelezo na kujiridhisha na zoezi zima. Vilevile amesema, Mzee aliyefariki alikuwa na kijana wake aliyetambulishwa kwa jina la Williams Shija ambaye pia alitoa maelezo kabla mzee hajafariki dunia.

HIVYO PUUZENI TAARIFA HII AFARIKI DUNIA BAADA YA KUMALIZA KUHESABIWA SENSA KAHAMA

#MIMI TAYARI NIMEHESABIWA WEWE JE?
 
Hakuna cha ajabu hapo kwani tutaendelea kufa mmoja mmoja kwa wakati wake hadi kurudi kwa Messiah mara ya pili. Mengine yote ni ubatili mtupu.
 
tufute kabisa
Huwezi kuifuta kwa maana saa 6 na dakika moja leo asubuhi alikuwa hai. Sensa ni kwa wale wote ambao walikuwa hai saa 5.59:59 usiku tarehe 22/08/2022 na wakafika saa 6:00:01 usiku tarehe 23/08/2022.
 
Kwani kuhesabiwa ni Kinga ya kifo hadi iwe habari ya kushangaza mtu kufa baada ya kuhesabiwa?
Hizi ndo Habari zisizo na maana
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom