Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

Baraza la Mawaziri latupa muswada wa...

2006-12-29 10:02:24
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Baraza la Mapinduzi Zanzibar (BLM), limekataa kupitisha rasimu ya muswada wa sheria ya kuanzisha mamlaka ya kupambana na rushwa na maadili ya viongozi.

Rasimu hiyo iliwasilishwa katika Baraza hilo na Katibu Mkuu katika Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba na Utawala Bora Zanzibar, Bw. Mahadhi Juma Maalim.

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Bw. Omar Makungu, alisema awali muswada huo ulikuwa uwasilishwe katika kikao cha Baraza la Wawakilishi cha Oktoba mwaka huu.

Alisema sababu kubwa iliyotolewa na Baraza la Mawaziri ni kwamba waandaaji wa muswada huo, lazima kwanza wakachukue uzoefu wa sheria kama hizo zinavyotumika katika nchi za Jumuiya ya Madola.

Hata hivyo, Naibu Mwanasheria Mkuu huyo alisema muswada huo uliandikwa kwa kutumia uzoefu wa sheria zinazotumika katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mshariki, ikiwemo Uganda, Tanzania Bara na Kenya.

Bw. Makungu alisema kwa mara ya mwisho mwaka 2005, walishindwa kuwasilisha muswada huo kutokana na harakati za uchaguzi mkuu.

”Sheria hii ya kupambana na rushwa na kuweka maadili ya viongozi haitakwenda tena Januari, kwa vile Baraza la Mawaziri wametutaka tuchukue uzoefu katika nchi za Jumuiya ya Madola,”, alisema Naibu Mwanasheria Mkuu.

Hata hivyo, alisema mswada huo umekusanya mambo mbalimbali ikiwemo viongozi kutangaza mali zao katika kipindi cha mwezi mmoja tangu kuteuliwa katika nyadhifa zao.

Alisema pia sheria hiyo inapiga marufuku wanasiasa kutoa sadaka au takrima katika harakati za uchaguzi na itakuwa ni kosa kwa kiongozi atakayethibitishwa kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa Ibara ya 68 (1) ya rasimu ya muswada huo, itakuwa ni makosa kwa mtu kutoa fedha, chakula viburudisho na huduma za malazi katika kipindi cha uchaguzi.

Katika rasimu ya muswada huo, Ibara ya 35 (1) inasema kila kiongozi wa serikali atatangaza mali yake, mke na watoto wake baada ya kupata wadhifa.

Kwa mujibu wa rasimu hiyo, mtu yeyote atakayekwenda kinyume na sheria hizo, ikiwemo kujihusisha na rushwa adhabu yake ni faini ya Sh. zisizozidi milioni 10 au kutumikia adhabu ya miaka isiyozidi 10 jela, au adhabu zote kwa pamoja.

Naibu Mwanasheria Mkuu huyo alisema kazi ya kuuboresha mswada huo imekwishakamilika ikiwemo kukusanya maoni ya wanasheria na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kufanyiwa semina na kuijadili rasimu hiyo.

Alieleza kuwa mpango wa kuanzishwa sheria hiyo unafadhiliwa na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

”Hatufahamu ni lini muswada huu utakwenda na sasa tunazingatia kupata uzoefu wa kutosha kwa nchi za Jumuiya ya Madola,” alisema Bw. Makungu.

Walipokuwa wakijadili rasimu ya muswada huo katika semina waliyoandaliwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi baadhi ya wajumbe kutoka CCM walisema kutokana na mazingira ya kisiasa ya Zanzibar wana wasiwasi sheria hiyo itatumika vibaya kwa kukomoana.

Kikao cha Baraza la Wawakilishi kinatarajiwa kuendelea tena mwezi ujao kujadili miswada mbalimbali ya sheria.

* SOURCE: Nipashe 29/12/2006
 
Hivi kuruhusu TAKRIMA wakati ule walichukua uzoefu nchi gani ? Au mkuki kwa nguruwe ? Wanajua kuwa Norway na Sweden wamechomoa misaada katika bajeti ? Au wanategemea kodi kutoka kwa machinga waliowakusanya mchikichini kuziba pengo la bajeti ? mimi siwaelewi.
 
Jafar,
Ule muswada wa takrima hauitaji uzoefu wowote kwani Chenge alisema ni desturi ya mwafrika kumkirimu mgeni. Kwi kwi kwi
 
Ama kweli Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina mambo .Ndiyo mapambano haya dhidi ya rushwa .
 
Is the noose finally tightening?

Faili la Mahalu lafika kwa DPP

na Mwandishi Wetu

MCHAKATO wa kushughulikia tuhuma na ubadhirifu zinazomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Costa Mahalu, upo katika hatua za mwisho.

Akizungumza na waandishi wa habari jana osifini kwake, Msaidizi wa Mkurugenzi wa Mashitaka, Augustine Shio, alisema tayari tume ya uchunguzi kutoka Taasisi ya Kuzuia Rushwa (PCB), imelifikisha faili lake kwa Mkurugenzi wa Mashitaka.

“Ni kweli faili hili lipo hapa, linafanyiwa kazi ili kuhakikisha kuwa tuhuma hizo ni za kweli, tunatarajia kulirudisha PCB mwishoni mwa wiki ijayo,” alisema Shio.

Alisema faili hilo linafanyiwa kazi na ofisi hiyo, ambapo itaangalia mambo matatu, la kwanza ni kuhakikisha tuhuma ni za kweli, ili liweze kurudishwa PCB kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka.

Pili, ni kuangalia ushahidi uliotolewa kuwa unaridhisha, ikiwa hauridhishi, litarudishwa PCB ili waweze kuleta unaotosheleza.

Tatu, ni kuona kuwa hana tuhuma na kulifunga.

Tume hiyo ilikwenda nchini Italia kwa ajili ya uchunguzi huo mwaka jana.

Mwaka jana Serikali ya Italia iligundua kuwa Mahalu alinunua nyumba kwa kupandisha bei baada ya kuambiwa atafute nyumba, hatimaye Serikali ya Tanzania iliingilia kati suala hilo na kuchukua hatua ya kumwita nyumbani.
 
Issue Ya Mahalu Ndio Hayo Mambo Ya Viini Macho Yanayosemwa Na Mazingaombwe,
Inasemekana Mahalu Hilo Saga Jk Analifahamu Vizuri Sana Pamoja Na Lumbanga.kuna Mnyetishaji Mmoja Anasema Saga Liko Hivi...mahalu Alivyomaliza Ile Nyumbakule Italy Jk Wakati Huo Akiwa W Nj Walipatana Kuwa Aende Kuifungua Yeye Ili Naye Apande Chati Kama Waziri Na Kukuza Jina Lake Manake Alikuwa Anajua Atapambana Awe Raisi Baada Ya Bm.

Sasa Wakati Huo Magufuli Ni Waziri Naye Na Ni Best Wa Bm Akawa Ameenda Italy Kutibiwa,kufika Kule Akamwambia Mahalu Achana Na Jk Mimi Nakuunganisha Na Bm Mwenyewe Yaani Raisi Ndio Aje Kufungua Jengo Ili Upate Ujiko.

Sasa Ndio Magufuli Akapindisha Mipango Ya Jk Na Mahali Na Bm Akafanikiwa Kwenda Kufungua Jengo.sasa Kimbembe Jk Alivyopata Uraisi Akamuita Mahalu Nyumbani Na Tuhuma Kibao Kwa Vile Alimgeuka Mapatano Yao Na Mahalu Akamwambia Jk Kuwa Magufuli Ndio Issue Yote Na Nisingeweza Kukataa.

Ila Nasikia Mahalu Na Jk Wanajuana Sana Issue Zao Kwa Hiyo Sidhani Kama Kuna La Zaidi Ambalo Watamfanyia Mahalu.sina Ushaidi Ila Nasikia Ndo Hivo......................
 
Issue Ya Mahalu Ndio Hayo Mambo Ya Viini Macho Yanayosemwa Na Mazingaombwe,
Inasemekana Mahalu Hilo Saga Jk Analifahamu Vizuri Sana Pamoja Na Lumbanga.kuna Mnyetishaji Mmoja Anasema Saga Liko Hivi...mahalu Alivyomaliza Ile Nyumbakule Italy Jk Wakati Huo Akiwa W Nj Walipatana Kuwa Aende Kuifungua Yeye Ili Naye Apande Chati Kama Waziri Na Kukuza Jina Lake Manake Alikuwa Anajua Atapambana Awe Raisi Baada Ya Bm.

Sasa Wakati Huo Magufuli Ni Waziri Naye Na Ni Best Wa Bm Akawa Ameenda Italy Kutibiwa,kufika Kule Akamwambia Mahalu Achana Na Jk Mimi Nakuunganisha Na Bm Mwenyewe Yaani Raisi Ndio Aje Kufungua Jengo Ili Upate Ujiko.

Sasa Ndio Magufuli Akapindisha Mipango Ya Jk Na Mahali Na Bm Akafanikiwa Kwenda Kufungua Jengo.sasa Kimbembe Jk Alivyopata Uraisi Akamuita Mahalu Nyumbani Na Tuhuma Kibao Kwa Vile Alimgeuka Mapatano Yao Na Mahalu Akamwambia Jk Kuwa Magufuli Ndio Issue Yote Na Nisingeweza Kukataa.

Ila Nasikia Mahalu Na Jk Wanajuana Sana Issue Zao Kwa Hiyo Sidhani Kama Kuna La Zaidi Ambalo Watamfanyia Mahalu.sina Ushaidi Ila Nasikia Ndo Hivo......................

Mhhhh! You do sound like mzee ES!
 
hani pai
Maneno haya ni kweli na kweli tupu . Kiini macho hiki na faili litafungwa kwa kukosa supporting documents. Utasikia badaye
 
Mie naunga mkono uamuzi wa Denmark.Misaada inatakiwa kuwa supplement na si replacement.Kampu letu limetobolewa kwa rushwa na ubadhilifu na viongozi wetu. Hivyo misaada inakuwa replacement na si supplement, ndo maana effectiveness yake haionekani,kwani misaaada hiyo imekuwa motivation ya rushwa,wizi na matumizi mabaya ya pesa za umma. Itakuwa vizuri nchi zote za Scandinavia zikakata kabisa misaada yao ili kuilazimisha selikari kuziba matobo yake(kama ilivyokuwa 1985-1995 wakati bidhaa nyingi ziliruhusiwa kuingia nchini lakini kodi iliyokusanywa ilikuwa bilioni 25 tu kwa mwezi!!!).Kwanza tukusanye vizuri kutoka katika resources zote tulizonazo ikiwa ni pamoja na kutumia mbinu za Putin ktk kerekebisha mikataba isiyotunufaisha, then tutumie kwa hekima tulichokusanya na pale tunapopelea ndo tupewe misaada.
Ni kweli pia kuwa wananchi ndo watakaoumia, lakini ni njia nzuri ya kuwaamsha watanzania kutoka usingizi wa pono ili waweze kuwabana watu waliowapa madaraka, badala ya kukaa kimya.Watanzania ni vizuri waelewe kuwa maendeleo yetu yataletwa na watanzania wenyewe kwa kwenda nyayo kwa unyayo na viongozi tunaowachagua.Watanzania lazima tujifunze lugha ya migomo na maandamano ili kuwaelewesha viongozi kero zetu.
 
MWANAKIJIJI heb tazama kama unaweza pata mahojiano na balozi wa DENAMARK bongo ili aweke wazi hili
 
Tatizo, watanzania hatujagundua kuwa tunawapa madaraka watu walio katika kundi lililo katika mashindano ya nani tajiri kuliko mwingine.Hivyo kila wanapoingia madarakania,wao pamoja na wapambe wao wanafanya kila namna kuwapiku wenzao.Nakubaliana pia kuwa misaada tunayopewa kwa sehemu kubwa inamadhumuni ya kuwanufaisha walioitoa,directly au indirectly.Wao wamekuwa wakitumia ujinga,ulafi na ukosefu wa uzalendo wa viongozi wetu kwa kujipatia manufaa.Shughuli yeyote ambayo itakuwa na manufaa kwa mabeberu hawa hata kama inarushwa na haina manufaa kwetu watakaa kimya mfano ununuzi wa radar,ndege ya rais na biashara ndege za kivita baina ya England na Saudi.

Tusisahau kuwa "WAJINGA NDO WALIWAO"
 
FUKARA HANA HIARI!!!!!!!!! Sasa pesa si zao kama hawaridhiki na matumizi ,wafanyeje...wala tusiwalaumu miAKA yote scandinavian countries have been so helpful to us so we cant crisize them infact they were helpful to us when everybody was desertin us...
 
Nyangumi maneno yako mazito sana na nimeyakubali .
 
Tanzania yafanya vibaya utawala bora, rushwa

Na Mwandishi Wetu

TANZANIA imeshika nafasi ya mwisho kati ya mataifa 43 duniani katika masuala ya utawala bora na udhibiti fedha na rushwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la kimataifa la Global Integrity Jumatano iliyopita, Tanzania imeonyesha kushika nafasi ya mwisho kwa kila kigezo miongoni mwa vigezo sita vilivyoainishwa.

Vigezo vilivyotumika kupima ufanisi ni pamoja na ufanisi wa jumuiya za kiraia, utoaji taarifa kwa umma na vyombo vya habari, ufanyaji uchaguzi, uwajibikaji wa serikali , utawala na utumishi wa umma, utaratibu na usimamizi na vita dhidi ya rushwa na utawala wa sheria.

Jopo la waandishi wa habari na wachunguzi 200 kutoka mataifa mbalimbali duniani kote ambao walifanya utafiti kwa kuzingatia vigezo hivyo sita kwa kila nchi. Mataifa yalipata maksi kwa kutumia vigezo vipengele vingine vidogo vidogo 23 vilivyomo katika hivyo sita.

Kwa kila nchi, alama kwa kila kigezo zilijumlishwa na kupatikana alama za jumla ambapo ilionyesha Tanzania imefanya vibaya.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo inasema kuwa Tanzania ilikuwa ya mwisho kwa kupata alama za jumla 59 ambazo zilionekana kuwa ni alama dhaifu sana.

Tanzania pia ilionekana kufanya vibaya zaidi ya majirani zake wa Kenya ambayo ilikuwa na alama 71, Uganda alama 76.

Kwa mujibu wa alama za viwango za shirika hilo alama kati ya 60 na 70 ni dhaifu, alama kati ya 70 na 80 ni za wastani ambapo walieleza kuwa alama 80 na 90 ndio alama za kuridhisha na 90 na kuendelea ndiyo hasa zilizokuwa zikitakiwa.

Katika kuelezea ripoti hiyo watafiti hao walisema kuwa nchi hizi ambazo zilikuwa na nafasi za mwisho ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda .

Katika huduma za jamii na, Taarifa za jamii na vyombo vya habari Tanzania ilipata alama 63, Kenya 68 na Uganda .

Kwa upande wa uchaguzi ufanyaji uchaguzi Tanzania ilipata alama 56 Kenya 64 na Uganda ilipata alama 74, katika uwajibikaji Tanzania ilipata alama 48, Kenya 56 na Uganda 76, Utawala bora na shughuli za jamii Tanzania 55 Kenya 70 na Uganda 71, katka utaratibu na usimamizi na vita dhidi ya rushwa 67 Kenya 89 na Uganda 81, katika masuala ya rushwa na utawala wa sheria Tanzania 66, Kenya 79 na Uganda 72.

Katika matokeo ya jumla Tanzania ilionekana kushindwa zaidi hasa katika rushwa kutokana na kushwa kukita mizizi katika vyombo vya sheria uwekezaji katika mambo ya umeme .

Ripoti hiyo iliendelea kueleza kuwa Tanzania inaonekana kuwa na vyombo dhaifu vya kupambana na rushwa na na kutokuwa wazi katika mapambano hayo .



Source: Gazeti la Mwananchi 14 January 2007
 
Lunyungu,
nadhani sasa umeona kile nachokizungumzia siku zote!... RUSHWA!.. rushwa sio tu adui wa Haki ila rushwa ni kilema cha maendeleo ya jamii!.. Hapa hakuna cha majimbo wala mjomba wake... RUSHWA - Grand corruption inapoteza kabisa maana ya UWAJIBIKAJI!... 1. ustawi wa jamiii wetu ni rushwa mbele, 2. Uchaguzi wetu ulijaa rushwa mbele. No matter kama nchi hiyo ina majimbo ama haina muhimu kuponya donda hili linalosambaza cancer nzima mwilini. Ikibidi mguu ukatwe (CCM) basi hakuna budi kwa usalama wa maisha yetu.
 
Back
Top Bottom