Augustine Moshi
JF-Expert Member
- Apr 22, 2006
- 2,556
- 1,392
Ukificha ugonjwa, kifo kitakusema. Kutokana na kuwa katika kundi la mwisho katika vipengele mbalimbali vya maendeleo na utawala bora, ni sawa kusema nchi yetu ni ya mwisho. Kuwa katika kundi la wachache wa mwisho ni kuwa wa mwisho.
Kuna tatizo kubwa kwenye vita dhidi ya rushwa. Wanaotegemewa kuongoza hivyo vita, ni wale wale ambao wanapashwa kushambuliwa. Adui wa kweli katika vita dhidi ya rushwa hapa kwetu ni viongozi. Wataongozaje vita dhidi yao wenyewe? Ilibidi kuwe na chombo huru cha kupambana na rushwa. PCB iliyo ndani ya Ofisi ya Rais haiwezi kushutumu viongozi, hasa wale wakuu, kwani ni viongozi wao, na ni washirika wa wakubwa wao wa kazi.
Inatakiwa kuwe na chombo kinachoajibika kwa wananchi, kwa kupitia Bunge. Kuwe na kamati ya kikatiba ya uteuzi wa wakuu wa PCB (mpya), Polisi, Jeshi, Magereza na Mahakama. Viongozi hao wa kikatiba, wasiteuliwe na kufukuzwa kazi na Rais. Kwa njia hiyo wataweza kumchunguza hata Rais inapoonekana anavunja sheria.
Haiwezekani kuleta utawala bora wa kuridhisha na wa kisheria Tanzania bila kufanya mabadiliko makubwa katika katiba yetu. Bahati mbaya, wale tunaotegemea wakubali na kuongoza marekebisho hayo ya katiba wanapinga. Wanapenda tuendelee na hali ya sasa kwani wanafaidika nayo, na wanadiriki hata kuwadanganya wananchi kwamba tunafanya vizuri sana.
Wananchi waliosoma vizuri hawadanganyiki kiurahisi, lakini hali ya Elimu Tanzania ni duni sana. Ni rahisi sana kuudanganya umma wa Tanzania, na viongozi wetu wanaishi kwa hilo.
Waandishi wa habari waendelee kuwalimisha wananchi kwa kuandika ukweli, hata ule unaouma. Tuendelee kukazania Elimu kwa ujumla. Umma ulioelimika vizuri una nguvu za kujikomboa zisizo na kifani!