Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

JK cant be serious kumteua Hosea kuwa chief wa PCB.Huyo jamaa mwenyewe alikuwa under investigation chini ya Kamazima baada ya hsady deals flani za magari (hosea aliingiza kitu kilichotikisa mji na kuzua maswali yalopelekea Kamazima kuanza kudadisi).Labda JK ameamua kufuata "busara" za wahenga to use of a thief to catch a thief...but i doubt it.

Timu ya vyombo vya dola ya JK "imekamilika."Usalama kuna mshkaji wake Othman,polisi kuna shemeji yake Mwema,na PCB kuna swahiba wake Hosea.Ni huko JWTZ ambako nadhani anavutia subira kumweka chekibobu mwenzie.Kwa asiyemjua Hosea,huyo jamaa ni mtu wa totoz sana,bishoo flani na "anafit ktk sifa za uongozi wa TZ:ulevi au ufuska,affinity (or addiction) to corruption na having the i-dont-give-a-f@@ck-attitude" pale watu wanapohoji.
 
Matokeo ya kuendekeza longolongo badala ya vitendo!

Denmark yaichapa kiboko Tanzania

Na Mwandishi Wetu

DENMARK imesema itapunguza Sh4.1 bilioni sawa na asilimia 20 ya fedha za msaada katika bajeti kuu ya Tanzania mwakani, baada ya serikali kushindwa kutimiza ahadi yake ya kupeleka bungeni muswada wa sheria mpya ya kupambana na rushwa katika mkutano wa Novemba mwaka huu.

Nchi hiyo iliweka sharti la kutoa msaada kutunisha bajeti kuu ya serikali na asilimia 20 ya fedha zilizoahidiwa zilihusishwa na kurekebisha sheria ya kupambana na rushwa kwa sharti kwamba muswada huo upelekwe bungeni Novemba 2006.

Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Denmark nchini imesema kuwa kuwasilishwa kwa sheria mpya ya kupambana na rushwa bungeni ilikuwa ni mojawapo ya kipimo cha utekelezaji, kilichokubaliwa na serikali ya Tanzania na washirika wa maendeleo wanaoichangia bajeti ya serikali mwanzoni mwa mwaka huu.

Taarifa hiyo iliyotiwa saini na Katibu wa Kwanza wa Ubalozi huo, Jacob Dal Winther, imeeleza kuwa sheria mpya ya kupambana na rushwa inatarajiwa kuwa ni nyenzo muhimu katika kuimarisha vita dhidi ya rushwa.

Alisema sheria hiyo inaweka mazingira ya kupata taarifa na inatoa uwezekano wa kuwaadhibu watu wanaothibitika kuwa ni wala rushwa na pia inalinda watu wanaotoa taarifa za vitendo vya rushwa.

"Kutokana na umuhimu wa sheria hii kwa Tanzania, Denmark ilikubaliana na serikali ya Tanzania kuwa asilimia 20 ya fedha za msaada itakazotoa kwa ajili ya bajeti ziunganishwe na kipimo hiki maalum. Hata hivyo sheria hii haikuweza kuwasilishwa bungeni mwezi Novemba kama ilivyokubaliwa," inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Wakati huo huo, Denmark imekubali kuipatia Tanzania msaada wa bajeti wa Sh109 bilioni wa kipindi cha miaka 2006-2010. Sambamba na msaada huo, Denmark inatoa kiasi cha Sh22 bilioni kusaidia kuboresha sekta ya umma katika maeneo ya utumishi wa umma, usimamizi wa fedha za umma na maboresho ya sekta ya sheria.
http://www.mwananchi.co.tz/mwananchisite/Mwananchi/Habari/Habari1.asp
 
Nawapongeza sana PCB kwa kukamata virushwa vidogovidogo ambavyo ninaweza kuviita jamaa wanaganga njaa tu. Kukiri kwa mkuu wa PCB kuwa hawezi kuwachukulia hatua vigogo wanaokula rushwa ni sawa na kusema uwepo wa PCB ni sawa na kutokuwepo. Sasa kwa nini serikali iendelee kulipa watu mishahara kwa kazi wasioiweza? Dawa ipitishwe sheria ya kuifuta hii PCB. Na nafikiri itapita haraka sana kwa sababu wapitishaji watakuwa ni haohao walarushwa. La sivyo kuwepo kwake lazima ipimwe perfomance ya miaka ya nyuma na iweke strategy za kuiangamiza kabisa rushwa. Otherwise haina maana.
 
Mlalahoi,
Huyo jamaa mwadilifu kiasi kikubwa kadri ninavyofahamu na ukilinganisha na wenye madaraka kama yake. Kwenye sifa za ulevi hayumo (labda Usabato wake unasaidia!) na ni mchapakazi. Kwa nafasi hiyo kinachotakiwa ni kutoingiliwa na Prez, vinginevyo itakuwa hadithi zile zile. Najua kuna kesi nyingi alizokuwa anazishughulikia lakini zikifika kwa bosi aliyemaliza muda wake anaambiwa "Umefanya vizuri basi inatosha niachie..."
 
Yap,
Kama utani vile, mbele ya waandishi wa habari jana Hosea akasema: "Ninawapa muda kidogo wala rushwa wakamilishe sikukuu za X-mas na mwaka mpya..."

Mh, wasiwasi unanijia... Yani wezi mnawajua na mnawapa muda washerehekee kwa amani? Is the guy serious? Alikuwa anatania? Hii imekaa vibaya sana! Lakini, Januari si mbali... Tutabanana nae hadi kieleweke tu!
 
Nyerere aliimba rushwa ni adui wa haki, lakini wapi! Inabidi kuiongeza rushwa kwenye amri kumi za Mungu, yaani watoto kuanzia chekechekea na msingi wafundishwe rushwa nini na inakuwaje mtu anashawishika kutoa au kupokea rushwa hata kama alikuwa hataki (ripoti ya warioba wanaoisoma tayari wameshakuwa deformed). Itawaongezea kidogo nguvu ya kukataa kuwa deformed na adult society watakayoikuta

Jamii yote chafu ndio mana rushwa itazidi kuota mizizi. Nchi itaendelea kuliwa mpaka Watanzania watakapo achana na uoga, watakapoacha kushabikia uovu.
 
tunasubiri kuona kama juhudi za hosea zitamfiklisha costa muhalu mahakamani,na iwapo zole eoro milioni mbili alizoficha kwenye moja ya merchants banks kule visiwa vya ufalme wa MONACO zitarudi hazina.
 
Hili ni swali la msingi na jibu langu ni ndiyo. Yafuatayo ni maoni yangu ya jinsi gani tukidhamiria kwa kweli tutaweza kupunguza rushwa ndogondogo.

http://h1.ripway.com/Mwanakijiji/Maoni/kubadilishamfumo.pdf

Niliandika hoja hiyo hapo juu kabla ya kusoma habari hii hapa toka gazeti la "Mwananchi"

Dawa ya mishahara ya walimu yapatikana

Na Mwandishi Wetu

KERO ya kuchelewa kwa mishahara ya walimu wa shule za msingi inahitimishwa mwezi huu baada ya serikali kujitia kitanzi cha kuhakikisha walimu wote wanalipwa mishahara yao tarehe 23 ya kila mwezi.

Vile vile serikali imeingia mkataba wa kibashara na benki ya NMB ili kuiwezesha kulipa mishahara ya walimu na watumishi wengine wa halmashauri ifikapo kila tarehe 23, hata kama haijapata fedha kutoka serikalini.

Walimu wa shule za msingi ni kada ambayo licha ya kuchelewa kwa mishahara yao, pia wamekuwa wakisumbuka kulipwa, wanapokwenda benki huelezwa kuwa mishahara haijaingia kwenye akaunti zao.

Akitangaza uamuzi huo jana, Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, alisema baada ya kukutana na wakurugenzi wa halmashauri zote nchini, uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Menejimenti ya Utumishi na Benki ya Microfinance (NMB), wameamua mishahara ya watumishi wa halmashauri iwe inalipwa tarehe 23 kila mwezi.

Meghji alisema mshahara ni haki ya mtumishi, pia mi mkataba kati ya mwajiri na mwajiriwa na kuongeza kuwa ni haki ya mwajiriwa kulipwa kwa wakati.

Rais mstaafu, Benjamin Mkapa aliwahi kutoa agizo la mishahara ya watumishi kulipwa tarehe 25 ya kila mwezi, lakini limekuwa likitekelezwa kwa watumishi wa serikali kuu tu, huku watumishi wa halmashauri wakiteseka hadi mwezi mwingine.

Waziri Meghji, alisema katika kuondoa vikwazo na visingizio vya kuchelewesha mishahara, Hazina Makao Makuu watalazimika kufanya kazi hata siku za mwisho wa wiki na kwamba atakayesababisha mishahara kuchelewa atawajibishwa.

"Kuchukua payroll (orodha ya malipo) Hazina Makao Makuu na Hazina ndogo mikoani kutafanyika hata kama ni siku za mwisho wa wiki au sikukuu," alisema.

Alisema atakayesababisha kuchelewa kwa mishahara hiyo atawajibishwa hata kama serikali italazimika kulipa riba kwa NMB kwa sababu wana mkataba wa biashara.

Alisema utaratibu huo utaanza kwa watumishi wanaolipwa kupitia halmashauri za wilaya ambao wengi ni walimu wa shule za msingi na watumishi wa kada ya afya, lakini baadaye utahusisha walimu wa sekondari.

Waziri Meghji alibainisha sababu za kuchelewa kulipwa kwa wakati kuwa ni kuchelewa kuchukua orodha ya malipo (payroll) kutoka hazina, dhana ambayo imepitwa na wakati na kwamba serikali imeamua kutafuta njia muafaka kuondoa tatizo hilo.

Katika kufanikisha ulipaji mishahara mapema, serikali imekubaliana na NMB kuboresha huduma za malipo ya mishahara kwa kufungua vituo vya malipo ya mishahara nje ya makao makuu ya wilaya.

Meghji alisema NMB itasaidia kufungua akaunti benki hata kama mtumishi hana fedha za kufungulia na benki hiyo itaanzisha mfumo wa kutoa taarifa za mishahara kwenye akauti ya mtumishi kupitia ujumbe wa maandishi katika simu.

Alisema kuanzia sasa, orodha ya malipo itakuwa inaandaliwa Hazina tarehe 12 ya kila mwezi, kutumia huduma ya usambazaji vifurushi (courier) kupeleka kwenye hazina ndogo zilizoko kila mkoa na msambazaji anatakiwa kuchukua orodha hiyo bila kukosa saa 2.00 asubuhi tarehe 13 ya kila mwezi.

Meghji alisema hatua nyingine ni msambazaji kuwajibika kuwasilisha orodha hiyo hazina ndogo ya kila mkoa kabla ya saa 2.00 asubuhi ya tarehe 15 kila mwezi, wakurugenzi watendaji wanawajibika kuzichukua saa 2.00 terehe 15 ya kila mwezi na watatakiwa kuziwasilisha pamoja na hundi za malipo ya mishahara kwenye benki ifikapo tarehe 22 ya kila mwezi.

Katika kukabiliana na mabadiliko hayo, wakurgenzi wametakiwa kupunguza idadi ya siku za kushughulikia malipo ya mishahara kwa nia ya kuleta tija, kusimamia kwa karibu suala la mishahara, kuchukua orodha ya malipo kutoka Hazina ndogo kwa tarehe iliyopangwa na kuhakikisha wanawasilisha benki orodha pamoja na hundi ya malipo kabla ya tarehe 22 ya kila mwezi.
 
THE government has been dismayed by Denmark's decision to reduce its general budget support (GBS) to Tanzania by 20 per cent, terming it harsh and hurriedly taken.

The Permanent Secretary in the Ministry of Finance, Mr Gray Mgonja, told this paper yesterday that his ministry and the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation are liaising on what the government should do.


http://www.tzuk.com/index.php?option=com_content&task=view&id=2590&Itemid=39
 
Mambo haya yanachanganya, hizi rushwa kubwa tunakulaga na akina nani? Huu unafiki utaishaga lini wajameni?
 
Rushwa itatutokea puani.

Vile vile ni Lazima tujifunze kujitegemea; hii tabia ya kupanga bajeti tukitegemea misaada na mikopo kutoke mataifa ya nje haileti maana yoyote.

Nyerere aliwahi kusema "Kujitawala ni kuijtegemea; kujitawala kwa kweli hakuwezekani kama taifa moja linategemea misaada na mikopo ya taifa jingine kwa maendeleo yake"
 
Mzee Wooh,

hivi jamani huko majuu hebu waombeni hao wa-tishi watutajie majina ya wala rushwa jamani, lini watawasema tule nao sahani moja?
 
Mzee Es,
hawa watish, inf tunawapa sisi wenyewe (hivyo majina tunayo sisi wenyewe na HOSEA wetu), some things are so obvious, e.g RDC contract, and so many other contracts za serikali.

jambo la msingi la kujiuliza, ni kuwa huo muswada uliotakiwa kupelekwa bungeni, kwanini haukupelekwa kulingana na makubaliano ya msaada?, majibu yote viongozi wetu wanayo
 
Lecturer wa zamani pale UDSM Dr Fr John Sivalon aliwahi kusema kuwa maeneo mawili yanayoweza kuilzamisha serikali yetu ibadilike na kuwatumikia wananchi ipasavyo badala ya kuendekeza matumbo yao na vimada wao ni (a) vikundi vya kidini (b) nchi/mashirika wahisani.Kwa bahati mbaya vikundi vya kidini vimekuwa compromised na system hivyo vinalazimika kunyamaza hata pale vinapoona kuwa serikali inatenda kinyume na moral obligations zake kwa wananchi wake.Ushamsikia Mufti au Kardinali Pengo wakimpa chngamoto JK au Lowassa kuhusu,say,suala la Richmond?Hawa ni watu wanaoheshimika sana hasa kwa vile mambo ya kiroho yanawagusa waadilifu na wasio waadilifu.
Walichofanya Wadenishi kinaweza kuonekana kuwa ni jambo dogo tu lakini yatupasa kufahamu kuwa hawa waskandinavia wamekuwa wakitusaidia sana katika almost kila eneo la nchi yetu.Wakiamua kuwa serious na kuibana serikali naamini kabisa tutaanza kuona mabadiliko.Na haitonishangaza nikiona huo muswada wa anti-corruption unakuwa fast-tracked ili kuinusuru bajeti yetu ambayo tayari ishaathiriwa sana na tatizo la umeme.
Nafahamu kuwa kutunyima misaada kunawaathiri zaidi wananchi wa kawaida lakini wakati mwingine inabidi umezeshwe dawa chungu ili ugonjwa upone.Trust me,zikijitokeza nchi nyingine zaidi kufanya walichofanya wadenish,ni lazima JK atapata akili kwamba hawa watu hawawezi kuendelea kusikia porojo za kila siku kuwa "tumedhamiria kupambana na rushwa" huku mikataba ya kilevi kama huo wa richmond inaendelea kusainiwa.
 
Mh!

JK na serikali yake wameshashtukiwa. Porojo zimezidi, kama ulivyosema Mlalahoi walahoi ndo wataumia zaidi, wala-nchi wala hawaumii kiasi hicho. Kinachotakiwa ni movement yenye kuishinikiza serikali kuwa serious na issues zinazolipeleka taifa pabaya.

Viongozi wa dini na wadhamini wanaweza kubadili sana kama ulivyosema, huu ni mfano tu. Kama kuna mataifa ambayo hayataleta mambo ya kusifia uozo (kama walivyosifu uchaguzi wa Zanzibar wakti ulitawaliwa na usanii mtupu) basi serikali inaweza kuamka kwenye huu usingizi wa kuwa sisi ni wadanganyika. Mlalahoi hataongea, lakini wa kumwongelea ni kama wadanish hawa!

Inauma lakini ni nzuri kwa maendeleo!
 
Hapa jamani kuna mambo mawili katikati ya hilo moja.

Serikali ya JK inafakamia rushwa mpaka aibu. JK sasa hivi hajui amuamini nani. Maanake wazaramo wenzake (Msabaha) ndiyo hivyo washachukua chao mapema na umeme ni kitendawili. PM anasema matatizo wamerithi kwa hiyo wataendeleza urithi. Hivi nani atakata huu mnyororo.

Serikali ya JK haijaonyesha nia ya kushirikisha nchi za SCANDINAVIA kwenye kuimarisha uchumi na huduma za jamii. Yeye rafiki yake ni Kichaka (Bush), Waarabu na Wakorea. Amesahau 40% ya bajeti inategemea SCANDINAVIA. Si ajabu ukasikia baada ya baridi hii kali JK akatembelea hizo nchi kuomba msamaha. Maana akijitia kiburi atakwama.

Mwiso wake ni kukatiwa mirija
 
Hao wote, iwe Waskandinavia au Wakanada, Waingereza au Wamarekani, ni wale wale tu! Wanakupa na mkono wa kushoto kisha wanachukua na mkono wa kulia na wewe unabaki na umaskini wako.

Waingereza: angalia sakata la rada ya Tanzania na sasa mambo yao na Saudi Arabia. Ni hao hao ndiyo wanatuuzia silaha, tunauana, wanakuja kuamua vita na kulinda amani, wanatupa misaada ya kibinadamu, katika mchakato huo wanapata faida kubwa. Ni biashara, ni biashara...
Angalia biashara ya maji waliyotuletea na City Water! Kisa wao ndiyo wametoa pesa za kukarabati mfumo na mtandao wa maji wa jiji! Hata ActionAid UK waliwapinga kwa hilo.
Angalia walivyoshinikiza Muhimbili iwe na Mkurugenzi waliyemtaka kutoka kwao Dr David Trevigong. Mshahara wake 10m. Kachemsha kaondolewa "unceremoniously". Kisa wao wametoa pesa kusaidia ukarabati wa Muhimbili.

Wamarekani: angalia ubeberu wao duniani kwa kiinimacho cha demokrasia. Angalia nchi walikojiingiza wakidai wanapigania demokrasia. Mfano wa karibu Iraki. Angalia wanapata pesa kiasi gani katika kupeleka domo-krasia huko Iraki. Biashara kwa makampuni yao ya silaha na vyakula kutoka kwa wakulima wao. Kupitia World Food Programme, ambayo wao wanaichangia kwa karibu 90%, wanahakikisha chakula kinachopelekwa kwa wakimbizi hata walioko Kigoma au Ngara kinatoka kwa wakulima wa Marekani. Maharage yenu (Bukoba na Kibondo) mnaambiwa "hayana ubora wa kiwango kinachotakiwa". EL mwenyewe kashangaa hilo huko Kigoma.

Wafaransa:angalia jinsi walivyotaka kumuua Mme Eva Jolly yule mama, mwendesha mashtaka Mfaransa mwenye asili ya Norwei, aliyekuwa anafuatilia tuhuma za rushwa za makampuni ya mafuta ya Ufaransa, ikiwemo Elf, huko Angola na Gine ya Ikweta (Equatorial Guinea). Kisa hao viongozi wenyewe wanahusika kwenye hizo rushwa. (Juma lililopita huyo mama alikuwa anaongea kwenye BBC Hard Talk). Kwa kiasi kikubwa Wafaransa wanahusika na suala la mauaji ya kibari huko Rwanda na ndiyo maana sasa wanataka kumgeuzia kibao Kagame ili wajioshe.

Wakanada: waliamua kumnyima Mzee Mwinyi misaada wakati ule wa mwisho mwisho wa utawala wake, kisa alisita kuruhusu makampuni ya Kanada kuja "kuiba" madini yetu. BM alivyoingia (inasemekana alikuwa rafiki yao tangu alipokua balozi Kanada) akawaruhusu basi wakajifanya "wanamwaga misaada" na kuanza "kumsifia kwa utawala bora na kukuza uchumi". Ndiyo maana Mwalimu Nyerere alisema "...ukiona Wazungu wanamsifia sana kiongozi wa Afrika basi ujue kuna tatizo, huyo kiongozi ana matatizo". Kwa maana nyingine wanakutia upumbavu, kichwa kivimbe, wao wale kiulaini.
Leo hii makampuni ya Kanada ambayo baadhi yao yanatuhumiwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na rushwa na hata mauaji Bulyanhulu etc ndiyo wamiliki wakubwa wa migodi Tanzania. Mliwasikia hao Denmark na wenzao wanasema lolote kuhusu hilo? Au kuitaka serikali yetu ichunguze tuhuma hizo za mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu? Kimyaaaa!

Skandinavia: hao kina Finland ndio wenye Wartsilla wenye hizo jenereta za IPTL etc. Mbona wasikemee mkataba wa IPTL? Hao Finland walitaka kununua maelfu ya ekari za misitu huko Morogoro kwa bei ya kutupa katika mazingira ya utatanishi. Kisa, wao ndiyo wamekuwa wafadhili wetu wa sekta ya misitu kwa miaka! Waliopinga na kuhoji walitishiwa kuuawa. Wao kimyaa! Sana sana wakadai kulikuwa na "open tender". Aliyefanya uthamini wa thamani ya huo msitu (valuation) kampuni ya kwao na iliyolipiwa na serikali yao!
Uswidi (Sweden) wao et al (WB etc) walishinikiza TANESCO ipewe menejimenti ya kigeni. Serikali ikasema haina pesa za kuwalipa, wao wakasema watatoa mkopo. Niliambiwa Netgroup wamekuwa wakilipwa kwa pesa ya mkopo kutoka Sweden kulingana na makusanyo yao ya mwezi. Kwa nini hiyo pesa isingepelekwa kwenye usambazaji umeme vijijini, au miradi ya nishati mbadala (solar energy, windmills etc)?

Hao kina Norwei na Denmark ndiyo wafadhili wakubwa wa sekta ya barabara. Walishinikiza mtu wao ndiye awe bosi TANROADS. Mshahara 10m. Walimuongezea mkataba wee! Mpaka leo yupo Mghana pale. Kisa Mswahili hawezi hiyo kazi! (Twaambiwa hatujasoma, hatuna uzoefu wala viwango). Magufuli alivyoibana TANROADS kuacha ubadhirifu watoa pesa (wafadhili) hawakufurahishwa. Alivyoyabana (yeye na naibu wake Mwenegoha) makampuni yao yafuate mikataba bila kubadili vipimo na kuiba kiujanjaujanja wakanuna! Hizo tuhuma za Magufuli zilianza kupikwa siku nyingi; bahati yake BM alimsimamia kwani walishinikiza (ikiwemo World Bank) BM amtose. Magufuli alivyobuni sera ya serikali kujenga barabara kwa fedha zake na kuwapa tenda Wachina etc hawakufurahia. Walitaka wao "watoe pesa" kisha makampuni yao ndiyo yajenge hizo barabara. Magufuli alivyobana magari ya miradi ya wahisani yasajiliwe na namba za "DFP" na kusimamia matumizi yake kwani hizo pesa ni mkopo kwa serikali walikuja juu!

Mifano ni mingi...Leo hao hao ndiyo wanajidai wanatujali sana sisi! Kichekesho.

Pamoja na yote, sitetei uoza na ufisadi. Ila nakerwa na unafiki na undumilakuwili wa hao wanaojiita wafadhili wetu! Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania!
 
Back
Top Bottom