Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

Kasheshe nakuunga mkono, nadhani ingefaa faini za makosa ya barabarani zikalipiwa TRA kwa kufuata TIN namba ya gari hii itasaidia uhakiki wa mapato ya serikari pamoja na ufatiliaji wa makosa barabarani, pia wasafirishaji wa abiria wanaweza kupata tax relief kwa the best safe operators, na makampuni yanayoongoza kwa ajali yaongezewe insurance charges na taxation yao iwe juu zaidi.
 
Kasheshe,

system yaweza kuwa nzuri sana........kama watendaji (Government officers)......na sisi wenyewe wananchi tukiwa wabovu wa rushwa....ndio basi tena!!!

hebu jaribu kuangalia wenzetu........ukikamatwa na kosa......tena utaitwa "Sir" kwa heshima zote........atakuelimisha kosa lako na kukupatia tiketi.........period.

Hivi Kasheshe ulishawahi kukamatwa na traffic police..........niambie ilikuwaje.....au hata wale wakaguzi wa TRA wameshawahi kukukagua........ukawasikia wanavyoongea!!!.........i reform ya hali juu inahitajika kuweka system zetu sawa sawa........

na sio kwamba hakuna solution.......zipo ila wakubwa eti hawazioni hata tukiwapeleka seminar Ulaya......bado hawaoni/hawakumbuki.........halafu the same people wanabaki kubeza technolojia
 
wana JF ninaomba kwa yeyote mwenye kuweza kunipatia nakala ya ripoti ya warioba,anifanyie msaada huo.kwani nina shauku kubwa sana ya kuisoma.
Natanguliza shukrani
 
Naamini ipo kwenye website mojawapo za serikali ila sikumbuki ni ipi ntakutafutia
 
Mapolisi barabarani siwaelewi,hasa MIKUMI wamezidi! Magari makubwa wakisimamisha huenda moja kwa moja kwa mlango wa dereva nakuufungua! Basi utaona dereva kanyosha mkono na askari anapokea KITU na hupeleka mfukoni. There after gari linaruhusiwa bila checking yoyote. I've a certain duty ambayo hunifanya kusimama pale na kujionea,kama unabisha go and observe. Sasa hii ni halali? Na kama si halali tuiteje basi? If is corruption,do PCCB aware with it?...yeah! let you jot anything you grasp.
 
MAKALA
Nakala chapishi
Mtumie mwenzio
Jiandikishe utaarifiwe

Tunajenga jamii ya kiharamia

Paul Mabuga Machi 19, 2008

WIKI iliyopita nilikuwa katika mji mdogo wa Maganzo ambao ni maarufu Tanzania na nje, hususani katika soko la vito la Ubelgiji, kutokana na biashara ya almasi. Niliona kipande cha chuma chenye maandishi ya kuwekwa kwa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami, kimeng’olewa.

Barabara hii ni ile ya kutoka Mpakani mwa Mkoa wa Mwanza na Shinyanga eneo la Nyasamba hadi Tinde na nyingine ya kutoka Nzega kupitia Tinde hadi Isaka. Zote hizi zilijengwa kwa msaada wa jumuia ya Ulaya na jiwe lake la msingi liliwekwa na rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Niliozungumza nao juu ya kitendo hicho wanaona ni jambo la kawaida, na kufikia hatua ya kusema, “kuna jamaa alihamisha kuganga njaa.” Lakini kingine cha ajabu, wanasema, “Maganzo ni mji wa matanuzi na kila siku ni Jumapili, ukikosa ng’ana (almasi), tafuta cha kuuza uishi.”

Pengine huu nao ni ufisadi katika ngazi fulani, hata hivyo, kuwalaumu wananchi hawa kwa hujuma hii bila kwenda mbali zaidi inaweza kuwa ni haraka mno maana hii ni dalili ya mambo mengi yaliyofichika, juu ya suala na dhana ya uzalendo inayosistiza, pamoja na mambo mengine, kujali zaidi maslahi ya umma kabla ya ya binafsi. Nani katufikisha hapa ndiyo mjadala wa haki.

Jambo muhimu zaidi katika barabara hii, ni kwamba imejengwa kama hatua muhimu ya kuunganisha ukanda wa kati, kwa maana ya njia ya kutoka Bandari ya Dar es Salaam, kupitia Dodoma hadi mpakani na nchi ya Burundi. Balozi wa Rwanda nchini Zeno Mutimura aliwahi kusema ukanda huu ni muhimu sana kwao kutokana na unafuu wake ikilinganishwa na ukanda wa kaskazini.

Wakati barabara ya ukanda wa kati zimeharibiwa na mvua mwaka jana, wafanyabishara wa Rwanda walilazimika kusafirisha bidhaa zao kupitia ukanda wa kaskazini, kutoka bandari ya Mombasa, Kenya kupitia Uganda hadi Kigali umbali wa kilometa 1792. Njia ambayo ni aghali ikilinganishwa na ukanda wa kati, bandari ya Dar es Salaam, kupitia Isaka hadi Kigali ambao una mrefu wa kilometa 1620.

SIETCO wakitengeneza barabara Manyoni

Watanzania kwa wakati huo walipiga kelele baada ya maelezo ya Serikali kuwa, mkandarasi aliyepewa zabuni ya kujengwa barabara ya ukanda huo kipande cha kati ya Manyoni na Singida, Sietco, ana uwezo mdogo na ndiyo maana alikuwa nyuma ya ratiba ya utekelezaji kwa miezi mingi.

Hapa swali la kujiuliza ni kwamba kwa nini unampa kazi mkandarasi ambaye uwezo wake ni mdogo na kwa nini usifanye tathmini ya kina ya uwezo wake kabla ya kutoa zabuni? Ama kuna kishawishi? Ni kitu gani hasa kinaonekana kama kishawishi na kuna tofauti gani katika vigezo vya uzalendo kati ya hali hii na wale jamaa wa Maganzo?

Ukweli ni kwamba Sietco, wana rekodi mbaya linapokuja suala la ujenzi wa barabara katika eneo la Afrika ya Mashariki, hasa baada ya kuwa wametimuliwa katika kazi ya upanuzi wa mradi wa Umeme wa Owen nchini Uganda mwaka 1996.

Katika kumbukumbu za Bunge la Uganda, kikao cha Aprili 12, 2000, inaelezwa kuwa kampuni hiyo ilishindwa kufanya kandarasi hiyo nchini Uganda kutokana na mpango duni wa kazi, udhibiti na mawasiliano duni na kukosekana mamlaka na uwajibikaji miongoni mwa watendaji wake na uwezo mdogo .

Sietco walishinda kazi hiyo nchini baada ya kuonekana kuwa gharama zao zipo chini ikilinganishwa na wakandarasi wengine 43 waliokuwa wamejitokeza kufanya kazi hiyo, mnamo mwaka 1993. Hata juhudi za kumaliza suala hili halikufanikiwa hadi pale serikali ya Uganda ilipovunja mkataba na kampuni hiyo Septemba, 2006. Hapa tuwasifu Waganda.

Kingine cha kushtua kidogo, ni kwamba taarifa ya mapendekezo ya mpango wa kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa nchini Uganda ya Mwaka 1998, ulinukuu vyombo vya habari juu ya madai ya watendaji wa Sietco kwamba walitumia asilimia 30 ya gharama ya mradi kuwahonga maafisa wa Bodi ya Umeme nchini humo.

Kauli iliwahi kutolewa na serikali kuwa mkandarasi huyu alipewa kazi hii, eti kwa sababu gharama zake zilikuwa chini ikilinganishwa na wengine.Pia iliwahi kukiri kuwa kushindwa kukamilika kwa zabuni ya kampuni hiyo ndani ya muda ni ushahidi kuwa uwezo wa mkandarasi huyu mdogo na serikali imejifunza.

Katika mazingira kama haya, kwa nini kusiwe na hofu kuwa katika kutoa kazi kwa mkandarasi ambaye hana uwezo kuna mazingira yanayotia shaka, uzalendo ulikuwa wapi ama uliharibiwa na nini hadi tathmini ya kina isiwepo. Ni kwa nini kazi itolewe kwa kampuni ambayo inadaiwa kulalamika kuwa iliwahi kutoa rushwa watoa zabuni serikalini na tena si mbali, ni hapo nchi jirani ya Uganda.

Linapokuja suala la kutoa zabuni, na katika mazingira kama haya, kuna dalili kuwa wasomi wetu wanawachuuza wananchi. Wanasahau yale maneno tuliyokuwa tukikakarishwa shuleni, kwamba, aliyepata bahati ya kupata elimu ni sawa na aliyetumwa mbali kwenda kutafuta chakula na jamii yake yenye njaa na kinachotarajiwa ni yeye kurudi na nafaka na kuwakomboa ndugu zake.

Wao badala yake wanashiba na kuvimbiwa huko ugenini na wanatangaza kimya kimya kutorudi kwa waliowatuma. Tunaona kwa dalili nyingi, hawa jamaa waliotumwa na jamii yenye njaa, wana mali zisizo na maelezo, na bahati yao hakuna mwenye ubavu wa kuwauliza kwa dhati kuwa wamezipata wapi. Inanikumbusha habari moja ya skari polisi wa cheo cha chini mwenye kitambi na hoja kuwa atamkimbizaje mwizi.

Tanzania imefikia pahala, wasomi na hususani viongozi wamewasaliti wananchi, hawatendi tena yale ambayo wanyonge wanayatarajia, haya yote yanatokana na kukosekana kwa maadili ya kitaifa. Mhadhiri mmoja wa chuo kikuu aliwahi kuonya kuwa ni hatari sana kuwa na msomi asiyekuwa na maadili. Lakini wananchi nao wanaona, kusoma ma kusikia juu ya jinsi wanavyosalitiwa na wasomi na viongozi wa nchi yao.

Wasiwasi wangu ni kwamba kuna siku ambayo wananchi watachoka, baada ya kutotimia kwa matarajio yao. Watageuka na kuwa kama Watanzania wa Maganzo, na nchi haitakalika.

Source Raia Mwema
 
Wewe huwatakia lakini wala rushwa wenzao ambao ni CCM wanawataka sana.Hawa si rushwa pekee bali hata ukatili na kuua bila ya kujali .Asili yao na asili ya serikali yao .
 
Yo i love ur avatar...im jacking it and adding to one my favourite quotes!! 🙂
 
Ukitaka kujua CCM wao huwafuata wala rushwa na wakandamizaji waone viongozi waendako kutafuta maendeleo, Thailand mara nvua kumbe rushwa imelala kule , Malyasia na Nchi yeyote ambayo ina ukaidi na uvunjaji wa haki za watu ndio CCM wanaweka Mizizi.Zimbabwe , Iran nk
 
Leo wachina, kesho wajapane na keshokutwa je? Hii ndiyo Tanzania waliyoko madarakani wanapata mpunga kitesi tonge limao. nimesema siku zote tupige kelele kwa sasa lakini siku moja wakati utawahukumu hawa wasaliti wa taifa letu, tumewapa madaraka lakini wametusaliti , Mungu tupiganie . Wamesahau kama si watanzania.
 
Wana Jf Tuna Shughuli Nyingi Sana Za Kufanya Ambazo Kwa Namna Moja Au Nyingine Huchangia Kusambaratisha Na Hatmaye Kutokomea Kwa Mitandao Ya Ufisadi Ambayo Imekuwa Ikichangia Kuludisha Nyuma Shughuli Za Maendeleo.kuna Habari Nyepesi Nyepesi Kuwa Ndani Ya Idara Ya Takwimu Kumekithiri Rushwa Na Ukabila,kama Wana Jf Mnazo Full Data,please Ziwekeni Hapa Ili Tuangushe Mizizi Ya Ufisadi.
 
Ni Kweli Kuna Rushwa Haswa Katika Kutoa Baadhi Ya Takwimu Kuna Baadhi Ambazo Ni Lazima Kwa Mwanafunzi Kuzijua Ukifika Pale Utoe Kidogo

Kuna Mmoja Ya Wafanyakazi Mule Ndani Degree Yake Ni Ya Kuforge Tena Ya Chuo Cha Mzumbe , Siku Za Karibuni Sijamwona Sijui Yuko Wapi Lakini Ukweli Ndio Huo

Hapo Idarani Yuko Na Ndugu Yake Ambaye Pia Alisoma Hapo Hapo Mzumbe
 
Rafiki yangu alipata kazi kwa kutoa laki 3 kuitwa kwenye interview, na 200000 kuwa shorlisted ndio ndugu yake akafanya mpango achukuliwe statistcis wizara ya viwanda.
Ana vyeti vyote kabisa na ni intelligent wa kutosha tu. ila basi ndio hivyo, kwa hiyo sishangai sana unalosema.
 
Mmh!

Hii hoja ingeweza kuwa HOT ila aliyeileta anategea! Kaboka, naamini una kitu unachokijua au ulichoambiwa ila umeamua kuiacha hoja hii kiwa bila mama wala baba!

Leta maneno tunakusubiri!
Wenye data pia leteni kwa fujo!
 
Inawezekana kabisa kuna ukabila pale maana Mkuu wa kile kitengo ana mwelekeo huo. Siwezi kubisha kabisa. Nikipata YATOKANAYO toka kwa Kaboka nitazidi kuchangia. Hii ni JF Bwana hukosi mambo!!!!
 
WanaJambo wenzangu naomba niwasalimu... Hii nimekutana nayo kwenye Tanzania Daima website na kwa kweli inasikitisha mpaka naona kama weekend yangu ndio ishakuwa soo tena.... Rushwa ya 3,000?? Tena kibaya zaidi ni kwa Trafiki Polisi kwenda mahakamani kwa hili?? Pamoja na kwamba sipendi rushwa kama nisivyopenda ukoma, sidhani kama TZS 3000 inapelekea mahakama nzima kukaa kusikiliza kesi hii..... Ina maana Jeshi la Polisi hawana kamati za maadili kwa ajili ya kuwaadhibu jamaa wanaochukua vijirushwa vya njaaa..... Looking at it huyu jamaa sio kwamba amefanya hili kwa sababu nyingine zaidi ya NJAAAAAAAAAAAAA!!!!!

Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.......

Trafiki kizimbani kwa rushwa

na Asha Bani

ASKARI wa Kikosi cha Usalama Barabarani, X WP 2846 CPL Sauda Habibu Kaijage, jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, akituhumiwa kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya sh 3,000 kutoka kwa dereva wa daladala.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Bernadeta Beda, Mwendesha Mashitaka, Inspekta wa Polisi Francis Mboya, alidai kuwa Machi 31 majira ya saa 3:00 asubuhi, mtuhumiwa akiwa katika Barabara ya Nyerere maeneo ya Kamata, aliomba fedha hizo kutoka kwa Somadu Mzallah, aliyekuwa anaendesha gari lenye namba T 781 ALS, kama kishawishi ili asimshitaki kwa kosa alilofanya.

Mwendesha Mashitaka alidai kuwa mnamo Machi 31 majira ya saa 4:30 asubuhi katika eneo la Gerezani huko Kariakoo, mtuhumiwa alimtumia askari polisi mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Asteria kama ajenti wa kumchukulia fedha hizo kutoka kwa dereva huyo wa daladala.

Mtuhumiwa alikana shitaka hilo na mwendesha mashitaka alidai kuwa upelelezi umekamilika na kumuomba hakimu kupanga tarehe ya mtuhumiwa kusomewa maelezo ya awali. Hakimu alipanga Mei 22 mwaka huu.

Mshitakiwa huyo yuko nje kwa dhamana yenye masharti ya wadhamini wawili na ambao watasaini kila mmoja bondi ya sh 3,000.

Courtesy:
http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/5/9/habari21.php
 
Hizi ndo kesi ambazo mahakama inapenda kusikiliza kwani ushahidi wake hupatikana mapema sana na watuhumiwa ni wadogo tu, na hapa kazi ya Hosea inaonekana kufanikiwa katika upande wa kuzuia rushwa. Kwangu mimi hata kama amekula hii suala hili linahitaji kuangaliwa kwa kina na kwa hakimu asiyetafasiri sheria hukumu hapa inaweza kuwa ya ajabu. Mahakimu wengi hawatafasiri sheria bali wanatekeleza sheria (enforcement) na dhana dhma ya mahakama inaonekana kama ni kwa ajili ya baadhi ya watu.

Siungi mkono rushwa ya aina yoyote lakini kwa hapa nadhani juhudi kubwa zingefanywa kuwakamata kina Balali na wenzake na wale wote wanaopita na kuwahonga wannchi kwa janja ya kujisafisha, waende mahakamani

Kazi ya mahakama si kutekeleza sheria, ni kutafasiri na kuona kila upande ulio mbele unapata haki yake stahili
 
Back
Top Bottom