Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

i195_rushwa.jpg

Mgambo wa jiji aliyevalia kiraia, (katikati) akikokota mkokoteni ulio na mananasi baada ya kumkamata kijana aliyekuwa akifanya biashara kwenye eneo lisiloruhusiwa Kariakoo Dar es Salaam jana. Kulia ni kijana mwenye biashara hiyo akionekana kumbembeleza huku akimpatia pesa ili aweze kumwachia biashara yake, mgambo hao wamekuwa wakiwakamata wafanyabiashara za mkononi na kuwanyang'anya bidhaa zao na kuwaomba rushwa ili kuwaacha waendelee na biashara zao.
 
asante kwa mada kama hii. Rushwa kumalizika Tanzania ni kama kuzuia binadamu wasivute pumzi. Rushwa ndio maisha ya kwetu. Tangu juu mpaka chini ngoma inayochezwa ni hii hii tafauti ni mlio tu. Mabadiliko yaweko ya hali ya juu sana kuweza kuwadhibiti na kuweza kuweka mambo sawa. Maadamu bado tupo chini ya CCM tusitarajie mabadiliko.
 
Ndiyo, rushwa itasiah tu. Ila kwanza tunahitaji kutunga katiba mpya na kubadilisha mfumo wa uongozi ili kuimarisha mfumo wa utawala unaofuata sheria kamaq zilivyoandikwa vitabuni.
 
Ndiyo, rushwa itasiah tu. Ila kwanza tunahitaji kutunga katiba mpya na kubadilisha mfumo wa uongozi ili kuimarisha mfumo wa utawala unaofuata sheria kamaq zilivyoandikwa vitabuni.

sasa wa kutunga sheria hiyo ni nani?
kama hata wanaoshiriki kutunga sheria hizo wanakamatwa hivi sasa kwa makosa hayo hayo wanayotakiwa kuyatungia sheria?
 
sasa wa kutunga sheria hiyo ni nani?
kama hata wanaoshiriki kutunga sheria hizo wanakamatwa hivi sasa kwa makosa hayo hayo wanayotakiwa kuyatungia sheria?

hilo ni swali zuri sana, tukishalijibu hilo tutakuwa tumetatua asilimia hamsini ya tatizo la rushwa.

hata hivyo, one day yes.
 
Ndiyo, rushwa itasiah tu. Ila kwanza tunahitaji kutunga katiba mpya na kubadilisha mfumo wa uongozi ili kuimarisha mfumo wa utawala unaofuata sheria kamaq zilivyoandikwa vitabuni.

Kwa mwendo huu rushwa haiwezi kuisha. Kumbuka kuwa rushwa imeshakuwa ni tabia na hasa hasa imegeuka kama mila na desturi ya Mtanzania. Ipo kwenye akili zetu, damu zetu na hata imekwisha halalishwa "kiFikra" kama imani zetu za dini; na taboos! Then how to uproot corruption? What we miss? We have laws and a constitutions which must be ammended to some extent. Kuondoa rushwa kwa generation moja kwa Tanzania ni impossible; will need three or four generations to go! This mean, we need a new order now; this order have to addup in our school teachings; enforced by laws, for new generation to takeup the leardership. Only serious people can see this; but for the current generation; i don't see any hope!
 
Interested Observer,
Maneno yako msumari mkuu wangu..Kusema kweli mimi nimeanza kukata tamaa kwa sababu nimeshaona wapi tunakwenda na viongozi wetu wote toka chama tawala hadi vyama vya Upinzani wote wanakwepa jukumu kubwa la kufuta Ufisadi. wanalalamika tu kwa kutafuta baadhi majina ya watu na sio swala zima la Ufisadi na rushwa.
Kwanza wabunge wote na viongozi wetu wameshindwa kukubaliana kwamba viongozi wopte waliohujumu uchumi wetu wnaatakiwa kufikishwa mahakamni kihsheria..Sintajali matokeo ya hukumu zao isipokuwa maadam hatua ya kwanza imefanyika kurudisha rule of law itachukuliwa. Na kufikishwa kwao mahakamani kutarudisha imani kwa wananchi kwamba rushwa ni adui wa haki, ndio kazi ya mahakama,
Pili viongozi wote na wabunge wetu wameshindwa kukubali kwamba Azimio la Zanzibar ndilo sugu la Ufisadi nchini, lazima lifutwe..Hivyo hadi siku nitakapo msikia kiongozi yeyote akisimama nyuma ya mambo haya mawili ndio naweza kuweka tumaini jipya..Na ndio siku kiongozi huyo atachukua kura yangu, nje ya hapo nimechoka na siasa za Kibongo..

Chukulia huyu muuza mananasi hapo sokoni Kariakoo, kaweza vipi kufika pale na kuanza kuuza mananasi!.. ina maana kuna mchezo huchezwa yaani wahusika huwaacha hawa jamaa wafike kwanza kisha ndio waje kuwakamata na kuchukua kitu. Kifupi management ya soko lenyewe ndio mbaya.. haiwezekani mtu kuja na mananasi akaweka meza mlangoni kwako kila siku ya Mungu hata baada ya kuitiwa mgambo kesho yake anaamkia hapo hapo.
 
Mimi naamini rushwa itaisha Tanzania kama Watanzania tukiamua kupambana nayo bila woga au kificho katika kila kona ya nchi yetu.

Angalia hili swala la mafisadi, tuliwahi kuambiwa hadharani na Waziri Mkuu Pinda, Mwanasheria Mkuu Mwanyika na Mkuu wa polisi nchi kwamba mafisadi ni watu ambao wana utajiri mkubwa hivyo haiwezekani kuwafikisha mahakamani maana kufanya hivyo nchi itawaka moto na kushindwa kuiongoza. Lakini hadi hii leo tumeshaona vigogo mbali mbali waliowahi kuwa na nyadhifa za juu ndani ya serikali wamefikishwa mahakamani na nchi bado haijawaka moto na kuna habari wengine zaidi watafikishwa mahakamani.

Angalia swala la Mkapa, ambapo JK aliwahi kutwambia kwamba, "Mwacheni Mzee wetu apumzike kwa amani." lakini juzi tumesikia kauli ya Waziri Mkuu Pinda akisema kwamba Serikali haimugopi Mkapa na hakuna aliye juu ya sheria Tanzania kama kuna dalili za kujitajirisha kwa njia za haramu.

Pale mambo ya nje kulikuwa na rushwa ya hali ya juu katika utoajia wa Passport. Membe alipowekwa pale kama Waziri wa mambo ya nje akapambana nayo na kwa muda mfupi sana passport zikawa zinatoka haraka mno tena bila kutoa hongo. Na wakati huo huo nchi ilikuwa imegubikwa na giza nene kutokana na kukosekana umeme. Aliamrisha inunuliwe jenereta ili kuwawezesha wafanyakazi wachape kazi, aliamrisha zipangwe shift 3 za wafanyakazi wote wanaohusika na utoaji wa passport kutokana na maombi mengi ya passport za Watanzania ndani na nje ya nchi. Na alihakikisha anapambana na wote wale ambao walitumia nyadhifa zao pale katika ofisi ya utoaji wa passport kujitajirisha.

Kama Watanzania tutaendelea kutoa rushwa ili tupate huduma haraka na yale tunayotaka ndani ya serikali au taasisi mbali mbali za umma halafu kulalamika pembeni kwamba, "Nchi hii rushwa imezidi" basi kamwe rushwa haitaisha lakini tukiamua kupambana nao wanaodai rushwa ili watuhudumie pamoja na kuwa ni haki yetu kupata huduma hizo basi hakuna kitakachoshindikana.

Kama serikali ikiamua kutoa somo kali kupitia TV, Redio na magazeti kuhusu haki za Watanzania kupata huduma bila kutoa rushwa na kuweka sheria kali dhidi ya watoaji na wapokeaji rushwa ikiwamo kifungo cha miaka 10 au zaidi, kazi ngumu na kufukuzwa kazi basi ushindi dhidi ya rushwa unaweza kabisa kupatikana.

RUSHWA NI ADUI WA HAKI, SITAPOKEA WALA KUTOA RUSHWA.
 
........
Pale mambo ya nje kulikuwa na rushwa ya hali ya juu katika utoajia wa Passport. Membe alipowekwa pale kama Waziri wa mambo ya nje akapambana nayo na kwa muda mfupi sana passport zikawa zinatoka haraka mno tena bila kutoa hongo.

Hivi zimewahi kutolewa na wizara ya mambo ya nje hizi passport?
 
Heheheheheee....dude got caught with his hand in a cookie jar! Rushwa itachukua muda mrefu sana kuisha. Ngoja kwanza, kuisha kabisa sidhani kama itawezekana. Kinachowezekana ni kuipunguza ingawa hilo nalo litakuwa jambo gumu sana maana sasa [rushwa] imekuwa norm (kitu cha kawaida). Sasa kubadilisha kitu cha kawaida kwenda katika kitu kisicho cha kawaida hususan tabia, mienendo na utamaduni wa jamii fulani ni kazi ngumu kweli kweli.

Hmmm! Mimi sikubaliani na rushwa kama ni kitu cha kawaida. Unapofungua mashtaka mahakamani dhidi ya mtuhumiwa ambaye amekutapeli kiwanja chako au pesa zako chungu nzima unategemea haki itendeke ili huyo jamaa aonekane ana hatia na ikiwezekana akulipe pasa zako au akurudishie kiwanja chako. Mwambie mfanyakazi ambaye alistahili kupata promotion lakini hakupata na promotuon hiyo kupewa mfanyakazi mwingine asiyestahili kama rushwa ni kitu cha kawaida kama atakuelewa. Mwambie Mtanzania ambaye alistahili kupata nafasi kwenda nje kwa masomo ya juu lakini nafasi hiyo kupewa mtu mwingine asiyestahili kwamba rushwa ni kitu cha haki kama atakuelewa. Waambie wazazi wa mtoto aliyestahili kupata nafasi ya kuingia UDSM/IDM n.k. lakini kutokana na rushwa nafasi hiyo kupewa mtoto mwingine kwamba rushwa ni kitu cha kawaida kama atakuelewa.

Inapotokea huyo mtuhumiwa akatoa hongo kwa hakimu na sheria kupindishwa na hatimaye kuonekana hana hatia yoyote tayari dhuluma imeshafanywa dhidi yako kama mfungua mashataka. Hapa rushwa si kitu cha kawaida hata kidogo inapotokea chombo cha dola kinapindisha sheria na kukufanya wewe ukose haki yako.

Ndipo nasema kwa Watanzania ambao wanaoona 'rushwa ni kitu cha kawaida' hivyo kuwa tayari kutoa au kupokea rushwa bila woga wowote rushwa itadumu milele, lakini kama Watanzania wote tutakuwa na msimamo mmoja na kusema RUSHWA NI ADUI WA HAKI NA KAMWE HAKIWEZI KUWA KITU CHA KAWAIDA KATIKA JAMII YETU na hivyo kuamua kupambana na watoaji na wapokeaji rushwa basi ipo siku TANZANIA ITAKUWA HAINA RUSHWA NA HILI LINAWEZEKANA KABISA ni uamuzi tu wa Watanzania kusema sasa basi na serikali kulivalia njuga hili swala kwa mapana na marefu bila woga au kificho. Rushwa ni sawa na uokma au ukimwi tunabidi kupambana nayo kila kukicha na kamwe tusikubali kwamba rushwa ndani ya jamii yetu ni kitu cha kawaida. Dhuluma ndani ya jamii yoyote ile hata siku moja haiwezi kuwa kitu cha kawaida.
 
i195_rushwa.jpg

Mgambo wa jiji aliyevalia kiraia, (katikati) akikokota mkokoteni ulio na mananasi baada ya kumkamata kijana aliyekuwa akifanya biashara kwenye eneo lisiloruhusiwa Kariakoo Dar es Salaam jana. Kulia ni kijana mwenye biashara hiyo akionekana kumbembeleza huku akimpatia pesa ili aweze kumwachia biashara yake, mgambo hao wamekuwa wakiwakamata wafanyabiashara za mkononi na kuwanyang'anya bidhaa zao na kuwaomba rushwa ili kuwaacha waendelee na biashara zao.

Mbona hatujaona mgambo wakiwakamata wauza ice cream wanaotumia tri-cycles nyeupe au machinga nao wanunue tri-cycles ili wasikamatwekamatwe na kupigwa marungu kama tunavyoshuhudia mara nyingi? Nijuavyo mimi, rushwa haiwezi kuisha kamwe: ila inaweza tu kuongezeka au kupungua kadiri watu wanavyozidi kuya'control' maisha yao.

Na kwa hapa Tz inaongezeka hasa kutokana na kuvunjika kwa maadili na kuwapo kwa sheria zinazowalinda wakubwa na kuwakandamiza wadogo. Hata sijui kama huko wanakopelekwa hao machinga, je, huwa wanarudishiwa mali zao au zinachukuliwa? Na pia sijui kama kweli mara zote huwa ni wao tu wanaokosea na siyo mgambo!

Ninachoona kuna 'abuse of administrative law' na kunahitajika hao wanaonyanyaswa waombe msaada wa kisheria ili haki itendeke na inapowezekana hata waweze kudai fidia ya mali zao. Mgambo siku hizi wanaogopwa sana! Maana wakiamua tu kukupiga utaonekana umevunja sheria na sijui wao wanatumia sheria zipi hapa Tanzania kwa vile wana haki ya kumpa mhalifu adhabu wanayofikiria inafaa kwao.
 
Last edited:
- Huwezi kuondoa rushwa bila ku-offer an alternative ndio maana Warioba hupiga makelele sana kuhusu rushwa lakini akiulizwa alternative huwa ananyamaza kimyaaa, what is an alternative ukiondoa rushwa Tanzania?
 
Mkuu FMES,
Dunia nzima hupiga vita Unga, wizi na Ujambazi hivi kuna alternative gani! Hivi kweli crime zina alternative maanake mimi naona rushwa ni sawa na magonjwa pamoja na kwamba hayawezi kwisha lakini hatuwezi kuyaacha yakasambaa!.. tutakufa wote. Rushwa ikisambaa tutakufa kiuchumi..
 
- Crime au Rushwa yes zina alternative, nayo ni kuwalipa wananchi mishahara mizuri inayokidhi maisha yao, mfano mzuri ni Hospitali mbili Aghakan na Muhimbili, ukienda Ahgakan hakuna mfanyakazi atakayekudai rushwa kwa sababu wanakula mishahara safi pale, lakini ukija Muhimbili si unajua mkuu bila ngawila hupewi kitanda.

Yes rushwa in alternative, kama ilivyo crime ingawa matatizo ya unga ni more than what is being said, leo ukisimamisha uuzaji wa unga ina maana unafunga sekta nyingi sana za kazi US na the West, sasa utawapa kazi gani hao watakaotoka huko kwenye sekta za unga, ndio maana the West hawana mpango wa kusimamisha hiyo biashara hata siku moja ni wazugaji tu!
 
Mkuu Sauti ya Umeme, kama mishahara minono ingekwua ndio alternative ya rushwa, basi mawaziri wasingeongoza kwa rushwa kubwakubwa wka sababu wao ni miongoni mwa wanaolipwa mahela mengi hapa nchini
 
Mkuu Sauti ya Umeme, kama mishahara minono ingekwua ndio alternative ya rushwa, basi mawaziri wasingeongoza kwa rushwa kubwakubwa wka sababu wao ni miongoni mwa wanaolipwa mahela mengi hapa nchini

Pia maofisa wa TRA wasingekuwa wala rushwa.
 
Rushwa haiwezi kwisha kabisa.Tunachoweza kufanya ni kuipunguza ifikie kiwango cha kutoweza kuathiri uchumi wa nchi.Kiwango kilichoko sasa ni kikubwa mno,kwa vile kimefika mahali kimeathiri kila secta.Mikataba fake ya madini,umeme,barabara,afya,manunuzi nk.nk.List ni ndefu sana.Tunahitaji kugeuka na seriously kusema hatuwezi kuendelea hivi tena.

i195_rushwa.jpg

Mgambo wa jiji aliyevalia kiraia, (katikati) akikokota mkokoteni ulio na mananasi baada ya kumkamata kijana aliyekuwa akifanya biashara kwenye eneo lisiloruhusiwa Kariakoo Dar es Salaam jana. Kulia ni kijana mwenye biashara hiyo akionekana kumbembeleza huku akimpatia pesa ili aweze kumwachia biashara yake, mgambo hao wamekuwa wakiwakamata wafanyabiashara za mkononi na kuwanyang'anya bidhaa zao na kuwaomba rushwa ili kuwaacha waendelee na biashara zao.
 
Mkuu Sauti ya Umeme, kama mishahara minono ingekwua ndio alternative ya rushwa, basi mawaziri wasingeongoza kwa rushwa kubwakubwa wka sababu wao ni miongoni mwa wanaolipwa mahela mengi hapa nchini

- Hela ya mishahara wanayolipwa ni ndogo sana, infact hawako mbali sana na wabunge kwa mishahara, wao hutegemea safari hasa za nje, ndio maana wanakuwa mstari wa mbele kupora haraka haraka wakipewa tu!

- Wananchi wasiolipwa vizuri na pension za kuchekesha kama zetu bongo huishia kuwa wapenda rushwa, mkuu angalia NMB huko watu wanalipwa inavyotakiwa, juhudi zote za Mkapa, Sumaye, na Idd Simba kuibinafsisha zilikwama sababu, watu wanalipwa vizuri huko wabunge wakasimaia kidete mpaka hawa mafisadi wakakimbia wenyewe, hebu nenda hizi benki za kigeni bongo uone kama kuna mwananchi anayeweza kukubali rushwa akupindishie ishu, never watu wanalipwa safi wataishia kukuripoti polisi tu.

Wananchi wanaolipwa vizuri kulingana na hali ya maisha, hawawezi kutaka wala kushirki kwenye rushwa.
 
Back
Top Bottom