Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

Hivi awamu ya kwanza ilipopambana na rushwa na kufanikiwa kwa kiwango cha juu wafadhili walishirikishwa?
 
Jamani hii sasa ni kashfa...yaani huyu mdudu rushwa mpaka tusaidiwe kutoa na hawa wazungu????this is a joke!Mie naanza kuhisi na hawa wahisani nao wana mkono huko..Makashfa yako wazi lakini wanakula ndumu.. TAKUKURU yenyewe yategemea fadhila la Rais kusurvive unategemea nini...ndio maana wanaishia kukamata vidagaa na kuwaclear akina Richmond! Stupid!
 
Sijui kama kuna mtu aliyeitupa hii habari humu ndani, lakini si vibaya kuileta. Wenye pesa wanasema, rushwa na zawadi au kwa jina la kitaalamu Takrima inaongezeka, jee Membe atakasirika na kukaripia?

Mheshimiwa Raisi anafanya nini kusahihisha hili? Angalieni kumi bora zilizowekwa hapo chini kuwa ni vizingiti vinavyozuia maendeleo!

Latest World Bank report says:Corruption still on the rise in Tanzania‏

’’The cost in unofficial’ payments made by a typical firm to get things done in the country during 2006 was equivalent to 2.70 per cent of sales, compared to 2003 when it was just 0.23 per cent of sales?’’

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam


FINDINGS of a new World Bank survey say that Tanzanian society is more corrupt today in some areas than it was four years ago, with many investors asserting that they have to pay substantial amounts in bribes to win lucrative government contracts.

According to the report compiled by the World Bank-commissioned Enterprise Surveys, businessmen in Tanzania said they had to pay more bribes to get things done and win contracts last year than they did in 2003.

The report says that doing business in Tanzania may require making ’unofficial’ payments to clear red tape, and offering gifts to tax inspectors or officials involved in issuing government contracts.

To measure the perception of corruption, some 419 firms were surveyed in the country with business leaders asked how much they spend to get things done.

The findings, according to the report, show that the cost in ’unofficial’ payments made by a typical firm to get things done in the country during 2006 was equivalent to 2.70 per cent of sales, compared to 2003 when it was just 0.23 per cent of sales.

Figures for Tanzania in this aspect are a fraction higher than the sub-Saharan Africa average of 2.14 per cent, the report further states.

It also notes that the ’’value of gift expected to secure a government contract’’ in Tanzania was last year found to be equivalent to 2.94 per cent of the contract, on average.

This is a slight increase from four years ago, when businessmen operating in the country reported that they had to give ’gifts’ to government authorities amounting to 2.90 per cent of the value of the contract.

However, the survey says there was a notable decrease in the number of businesses that had to give local tax officials ’gifts’ in 2006, compared to 2003.

It is reported that 14.70 per cent of companies polled in Tanzania last year said they were expected to offer some sort of ’gifts’ in meetings with visiting tax inspectors, compared to 2003 when 22.41 per cent of businesses polled said the same.

The survey, covering a total of 103 countries worldwide, showed that businessmen felt there were more instances of corruption in Tanzania than the sub-Saharan average.

Within the East African Community (EAC) bloc, Burundi businessmen paid most bribes as a percentage of sales at 4.4 per cent, while Rwandan businessmen paid the least at 2.13 per cent of sales.

The report said Ugandan businessmen paid the most to win contracts, while Rwandans paid the least at less than one per cent of the contract value. Uganda was perceived as overall more corrupt than Tanzania and Rwanda, but less corrupt than Burundi in the EAC.

There were no figures available for Kenya during 2006.

In other business-related areas, senior management time spent in dealing with requirements of government regulation was at 4.01 per cent last year, compared to four years ago when bureaucracy ate up 14.39 per cent of the time of senior management.

At the same time, it is reported that the confidence level in Tanzania’s judiciary system increased to 60.42 per cent last year, compared to just 44.91 per cent four years ago.

In 2006, security costs as a percentage of business company sales in the country were pegged at 2.71 per cent, a slight increase from 2.29 per cent recorded in 2003.

There was also a significant decrease in company losses caused by theft, robbery, vandalism, and arson, to just 0.47 per cent of sales compared to 1.94 per cent four years ago.

Delays for companies obtaining electrical connection in Tanzania was down to an average of 44.28 days last year, compared to 54.59 days in 2003.

On the other hand, delays in obtaining landline telephone connection remained almost unchanged, from 23.07 days in 2003 to 23.25 days last year.

The Enterprise Surveys focus on the many factors that shape the decisions of firms to invest, are conducted by the World Bank and its partners across all geographic regions, and cover small, medium, and large companies.

In the Tanzanian case, the survey this year lists the top 10 constraints for investment as being electricity, access to and cost of financing, tax rates, transport, access to land, crime, theft and disorder, skills & education of workers, informality, tax administration and business licensing & permits.
 
Waandishi waikosoa sheria ya rushwa

na Tamali Vullu na Joseph Malembeka, Morogoro
Tanzania Daima

WAANDISHI wa habari kanda ya mashariki, wamesema kifungu namba 37 cha sheria mpya ya kuzia na kupambana na rushwa nchini, kitadhoofisha mapambano dhidi ya rushwa na kusababisha madhara yanayoweza kuchochea ongezeko la rushwa kwenye taasisi za serikali na sekta binafsi.
Walibainisha wasiwasi huo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa kuhitimisha mafunzo elekezi juu ya sheria hiyo kwa waandishi zaidi ya 40 toka mkoani Dar es Salaam, Pwani na Morogoro mjini hapa.

Walisema kuwa kifungu hicho kinahitaji marekebisho ili kuondoa ukiritimba wa kuzuia kwa muda usiojulikana kuandikwa kwa habari kuhusu matukio yanayochunguzwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU).

Kifungu hicho kinawataka waandishi kuwasiliana na ofisa wa TAKUKURU pindi wanapopata taarifa za mtu, taasisi au kampuni kujihusisha na rushwa na kuwa ni kosa kutoa siri zilizo kwenye uchunguzi katika taasisi hiyo.

“Kutokana na uzoefu uliopo, kwa wenzetu TAKUKURU kuna urasimu wa kukaa na taarifa za rushwa bila majibu hata mwaka. Hiyo pekee inaonyesha wasiwasi wa kutofanyiwa kazi na taarifa hiyo kuharibiwa makusudi kutokana na kukaa muda mrefu,” alisema Bonventure Mtalimbo.

Katika mafunzo hayo yaliyoshirikisha pia maofisa wa TAKUKURU, waandishi hao walitoa mfano wa tatizo la kifungu hicho katika uchaguzi uliopita wa CCM, kuwa katika uchaguzi huo baadhi ya wajumbe walikamatwa na maofisa hao wa TAKUKURU, lakini waandishi walipotaka ufafanuzi walielezwa kuwa bado wako kwenye uchunguzi hadi sasa.

Akifafanua uwepo wa sheria hiyo, Mkurugenzi wa Miradi wa shirika lisilo la kiserikali la msaada wa sheria (nola), Kaleb Gamaya, alisema kuwa sheria hiyo tayari ipo, na inatakiwa kufuatwa ingawa pia inahitaji kufanyiwa marekebisho ili ikidhi haja ya mapambano ya rushwa.

“Kwa sasa hatuna budi kuitekeleza pamoja na mapungufu yake na hizo changamoto zichukuliwe ili sheria hiyo ikatazamwe upya isiathiri mapambano yaliyokusudiwa kufanywa,” alisema Gamaya.

Sheria hiyo mpya ilianza kutumika nchini Julai 2007 na imeainisha makosa 24 kutoka kosa moja, lililokuwa ndani ya makosa ya jinai sheria ya mwaka 1974.

Baadhi ya makosa yaliyoainishwa ni kutoa na kupokea rushwa, rushwa ya mikataba, rushwa ya ngono, matumizi mabaya ya mamlaka, minada, ajira na hongo kwa maofisa wa umma.

Aidha, waandishi waliainisha mambo mengine yanayoweza kukwamisha mapambano dhidi ya rushwa kuwa ni pamoja na ushirikiano mdogo kwa waandishi wa habari kutoka kwa maofisa wa TAKUKURU, kuogopana kati ya taasisi hizo na TAKUKURU kutotoa taarifa zake kwa umma kupitia waandishi kama ilivyo kwa Jeshi la Polisi.
 
Ndugu zangu kwa bahati mbaya tuliibahatika kuwa na kaka mhalifu,, yeye alikuwa anaitwa EDGAR, natumaini bwana CHICO anawatambua walikuwa wazee wa kazi,,,

Huyu kaka yetu ametusumbua sana sana na wengine walibaki maskini. Katika kesi hii huyu mama yetu Lyamuya aliisimamia. Jamani mimi nilisema tunajitahdi kumtoa lakini ikishindikana tumwache aishie huko. Hakuna ambae hakula hela ya familia kuanzia mfagizi wale wa mafaili (jamani jamani huko ndio hakufai); faili halionekani kesi imesomwa wiki 2 zilizopita! Pesa anapelekewa watu wa usafi au police wa kawaida. Tulihangaishwa faili halionekani huku mheshimiwa na ma PP wake kila hela unayopeleka anchukua kesho yake waambiwa wenzake hawakuridhika. Hili naongelea labda sababu tulipata kiuwezo cha kutoa hela! Je huyu mlalahoi wa kawaida anapata wapi hela ya kumpa PP + Hakim + Mtunza mafaili?

Nilikuwa mmoja wa watu wenye fuuraha sana kusikia hii habari! Nasikitika kuona kwenye gazeti leo mkuu wa mahakimu anadai hakuna rushwa kabisa. Ndugu Hosea huko unapoenda kukagua rushwa unatafuta dhambi za millele! Nenda au tuma watu wako waende pale Kisutu, natumaini utaahamishia ofisi yako pale kwa idadi ya watu utakaopata.

Naomba waziri husika wa sheria afatile hili swala ndugu zangu huu ni mwaka wa haki zetu, tutafute hata kwa kukesha
 
Ndugu zangu kwa bahati mbaya tuliibahatika kuwa na kaka mhalifu,,yeye alikuwa anaitwa EDGAR,natumainibwana CHICO
anawatambua walikuwa wazee wa kazi,,,huyu kaka yetu ametusumbua sana sana ,,na wengine,,walinaki maskini,,katika kesi hii huyu mama yetu lyamuya aliisimamia,,jamani mimi nilisema tunajitahdi kumtoa lakini ikishindikana tumwache aishie uko,,,hakuna ambae hakula hela ya famili kuanzia mfagizi,wale wa mafaili jamanijamani huko ndio akufai,,faili alionekane kesi imesomwa wiki 2 zilizopita,,pesa anpelekewa watu wa usafi,,au police wa kawaida,,tuliangaishwa faili alionekani huku mheshimiwa,na ma pp wake kila hela unayopeleka anchukua kesho yake waambiwa wenzake hawaridhika,,,,hili naongelea labda sababu tulipata kiuwezo cha kutoa hela,,je huyu mlalahoi wa kawaida anapata wapi hela ya kumpa pp+hakim+mtunza mafaili,,,,
Nilikuwa mmoja wa watu wenye fuuraha sana kusikia hii habari,nasikitika kuona kwenye gazeti leo mkuu wa mahakimu anadai hakuna rushwa kabisa,,ndugu hosea uko unapoenda kukagua rushwa unatafuta dhambi za millele,,nenda au tuma watu wako waende pale kisutu,natumaini uutaahamisha ofisi yako pale kwa idadi ya watu utakaopata,,,,naomba waziri husika wa sheria afwatile hili swala ndugu zangu huu ni mwaka wa haki zetu,tutafute hata kwa kukesha


pdidy nadhani ni bora uanzishe link pekee kuhusu rushwa mahakamani la sivyo hayo unayoongea yanaweza mezwa yakapotea humu. ni ushauri tu
 
kaka yetu huyu kama mnavyojua pesa sabuni ya roho akabahatika kutoka kwa kupewa mdhamana,,nasikitika ndugu yetu mmoja alimtolea mdhamana ,,alikaribia kuwa maskini wa kutupa,,
akakimbilia arush,,hivi niwwaambiavyo ndie aliekuwa front na majiran zetu wakenya kwenye swala la NBC kule machame,,,,na ametangaziwa akionekana basi aje kama maiti,,amefanya sana uhalifu moshi arusha akishirikiana na wakina selemani,,frank(marehemu),nk ana uwezo wa kuingia ndani na kutoka,na kila ukimwambia acha anakwambia watu watakula wapi??haya ndio mambo ya mahakama kaka,,mwacheni B fatma apige kelele
 
Askofu aanika wala rushwa wakuu

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Dkt. Odernberg Mdegella, ametaja idara na taasisi zinazotakiwa kujisafisha kwa rushwa.

Askofu huyo hata hivyo ametaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa ya kwanza kufanya hivyo, na kuwataka viongozi wa dini kutokuwa waoga katika kukemea rushwa.

Aliyasema hayo wakati akichangia mada juu mbinu inayotakiwa kutumika ili kupunguza rushwa au kuepusha rushwa katika taasisi za Serikali, dini, vyama vya siasa, mashirika na watu binafsi.

Mada hiyo ilijadiliwa katika kipindi cha Jukwaa la Siasa kinachoendeshwa na kituo cha Televisheni ya Manispaa ya Iringa (IMVT) kwa kushirikisha viongozi wa vyama vya siasa, dini, waandishi wa habari na wananchi wa kawaida.

Alisema rushwa ilianza tangu mwaka 1995 wakati Serikali ya Rais Benjamin Mkapa ilipoingia madarakani na kuwa Rais Jakaya Kikwete aliikuta na amekuwa akifanya jitihada kubwa kuikomesha ila baadhi ya watu wamekuwa wakikwamisha jitihada hizo, kwa kubuni mbinu mpya kila kukicha.

Hata hivyo alisema anaposema TAKUKURU hana maana ya Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt. Hosea, ila anaitaka TAKUKURU kama taasisi kwa ujumla wake kuwa ya kwanza kujiosha.

Hivyo alisema vita dhidi ya rushwa ni ngumu iwapo viongozi wataendelea kuisema bila kutekeleza kwa vitendo mapambano yake.

Alisema baadhi ya wagombea wamekuwa wakilazimika kutoa rushwa baada ya kuona uwezo wa kushindana kwa hoja na wapinzani wao unakuwa mdogo na baadhi yao wakiomba mikopo kutoka vyama vya ushirika au benki huku mdhamini kwenye kampeni za uchaguzi.

“Hivyo Serikali pia imekuwa ikishiriki kutoa rushwa kutokana na kudhamini baadhi ya wanasiasa kuchukua fedha za kampeni kwa madai ya kuanzisha miradi…mimi nafikiri nitaje orodha kama waandishi wa magazeti mkiandika nitashukuru tu.”

Dkt. Mdegella alisema rushwa haitamalizika au kupungua kama wanasiasa wataendelea kutumia fedha kuomba nafasi mbali mbali za uongozi, hivyo alisema kwa upande wake ameona ni vyema kuwataja hadharani wale wote wanaopaswa kuanza kujisafisha.

“Kweli nasema kuwa wa kwanza kujisafisha awe TAKUKURU kwani wao ndio wapokeaji wa rushwa wakubwa. TAKUKURU wakisema nithibitishe nitawaonesha vitu tena watatia aibu, heri wasiniulize,” alionya.

Hata hivyo katika orodha hiyo, alisema nafasi ya pili ya watu wanaotakiwa kujisafisha ni viongozi wa vyama vyote za siasa, wakati kundi la tatu alilitaja kuwa ni Ikulu na kusisitiza kuwa hana maana ya Rais.

Dkt. Mdegella alitaja kundi la nne kuwa ni mawaziri ambao aliwataka wakutane na kuweka mkakati wa kutotoa rushwa katika uchaguzi wowote ujao.

“Mawaziri wetu waanze kumsaidia Rais Kikwete katika mapambano dhidi ya rushwa, kwa kuweka kikao cha pamoja na kusema kuwa uchaguzi ujao uendeshwe bila rushwa.

"Kweli wakae na kujisafisha, kwani rushwa inayotolewa kwa wapiga kura ni ya aibu; yaani unapikiwa wali halafu nawe unasema ni rushwa hiyo...mwenzako anakwenda kukaa miaka mitano wewe unakula wali siku moja au kitenge na mpira,” alisema.

Alisema kundi la tano ni Polisi, la sita Mahakama na kundi la saba ni watoa vibali mbali mbali katika halmashauri na kundi lingine ni sifa za wagombea wa nafasi mbali mbali.

Katika hilo alisema kwa upande wake hawezi kukubali mtu ambaye hajafika kidato cha sita, kwenda kugombea ubunge na kuwa iwapo inatokea hivyo katika mkoa wa Iringa, yeye akiwa Askofu atasimama kupiga kampeni ili mtu huyo asishinde.

Hata hivyo, alisema rushwa haina dini wala chama, hivyo ili kuisaidia Serikali katika mapambano ya rushwa, ni vyema kujitokeza kuikemea.

Alisifu ujasiri wa Mchungaji Christopher Mtikila katika kupambana na masuala mbali mbali na kumtaja kuwa mmoja wa viongozi wa dini, ambaye amekuwa akikubali kufungwa jela na anapotoka anaendeleza mapambano zaidi.

Source: Majira
 
Katika hilo alisema kwa upande wake hawezi kukubali mtu ambaye hajafika kidato cha sita, kwenda kugombea ubunge na kuwa iwapo inatokea hivyo katika mkoa wa Iringa, yeye akiwa Askofu atasimama kupiga kampeni ili mtu huyo asishinde.

Mheshimiwa Bishop sasa nakubaliana na walutheri kwa kukunyima ukuu wa kanisa lao ambao ulikuwa unaulilia kila kukicha" Inakuwaje kiongozi wa imani,mtumishi wa mungu tena mzoefu ambaye nikikukumbuka miaka ya mwisho ya 80 na mwanzoni mwa 90 pale ulipokuwa ukiuimba ule wimbo Shosholoza wa Kishona ktk tamasha moja Ukwata mjini Ifunda Tech ,umenikatisha tamaa sana kwani sasa kweli umeanza kuwa mbaguzi usiye na haya.

Bunge letu linawakilisha jamii zote za wa TZ wazamivu,wazamili wenye shahada,stashada,astashahada wachundo na Memkwa na wale ambao wanasaini kwa dole gumba ni hao ndio wenye haki ya kuchagua lakini pia kuchaguliwa sasa mzee wewe unataka kidato ndio kiwe kigezo ?? !! CCM walimbana Mrema kwa hilo ila wanafahamu kuwa walitenda dhambi,iweje wewe ushindwe kuiona dhambi hiyo ilihali i uchi?!!!!!!!!!! Huna haya Mdegela ni vema ukacha madhabahu ili uende ktk siasa kama swahiba wako Mtikila; Rushwa ni tatizo kubwa kwa TZ tangu enzi za Kambarage mpaka sasa,kumponda Mkapa kuwa ndio muasisi wa rushwa nchi hii inanifanya nianze kupunguza mwendo kanisani lakini tunashukuru The Comedy jana wametupatia fasiri halisi ya wimbo "UTANITAMBUAJE KUWA NIMEOKOKA WA BON MWAITEGE"

Iringa kuna nini ? Mbona kila kukicha 2007 ni vituko?

Tunashukuru kwa maoni yako maana umetusaidia kuujua upande wa pili wa sura yako Mzee Mdegera
 
Vigogo wagombea mgawo wa rushwa

Frank Leonard, Iringa
HabariLeo; Tuesday,December 18, 2007 @00:02

WAKURUGENZI wa Halmashauri tatu za Mkoa wa Iringa, wahandisi na wenyeviti wa halmashauri hizo, wanadaiwa kugombea mgawo wa rushwa unaotokana na miradi ya barabara, hivyo kusababisha kazi nyingi za miradi hiyo kukwama. Inadaiwa ugomvi huo unatokana na wakati mwingine rushwa inayotolewa kuonekana haitoshi kwa kuzidiana ujanja; ameibainisha Mkuu wa Mkoa huo, Amina Mrisho.

Pamoja na kuzionya halmashauri hizo, Mkuu huyo wa mkoa ameionya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) mkoani hapa kwa kudaiwa kuchelewesha utoaji wa zabuni kwa misingi hiyo hiyo ya mpaka wapewe rushwa.

Mrisho alitoa onyo hilo wakati akifunga kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Iringa kilichofanyika jana katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa. Bila kuzitaja halmashauri hizo, alisema viongozi hao wala rushwa wanajivunjia heshima pamoja na kupunguza ufanisi wa miradi ya barabara.

“Kazi nyingi katika halmashauri hizo zinakwama kwa sababu ya rushwa. Viongozi hao wa halmashauri hizo wanagombana kwa sababu rushwa wanayopewa wakati mwingine inaonekana haitoshi kwa kuzidiana ujanja,” alisema Mkuu wa mkoa. “Nawataka mjirekebishe mara moja vinginevyo nitawaumbua na kuwachukulia hatua kali za kisheria,” aliongeza.

Wakati huo huo, Meneja wa Tanroads Mkoa wa Iringa, Paulo Lyakurwa amewataka wananchi wasaidie kutoa taarifa ya makandarasi wanaokiuka taratibu za ujenzi ili kuongeza ufanisi katika kazi. Pamoja na ombi hilo, amesema wilaya ya Makete na Ludewa zinakabiliwa na tatizo la makandarasi. “Wilaya ya Ludewa ina mkandarasi mmoja tu huku ya Makete ikiwa haina mkandarasi hata mmoja,” alisema.

Alisema kujitokeza kwa makandarasi hao kutarahisisha utekelezaji wa miradi ya ujenzi hususani katika ngazi ya wilaya ambayo imekuwa ikijengwa na makandarasi kutoka nje ya wilaya hizo. (mwisho) Maalbino kumuona JK kupinga mauaji Na Theopista Nsanzugwanko CHAMA cha Maalbino Tanzania (TAS) kinatarajia kufanya maandamano ya amani kumuona Rais Jakaya Kikwete, kwa ajili kuitaka serikali kuunda tume maalumu ya kushughulikia mauaji ya maalbino nchini.

Maandamano hayo yatakayokwenda sambamba na kongamano kubwa la kujadili suala hilo, yatafanyika Januari mwakani na yatamalizikia Ikulu, Dar es Salaam na kupokelewa na Rais. Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara Habari (MAELEZO), Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Ernest Kimaya, alisema wamechukua hatua hiyo baada ya kuona hakuna jitihada zozote zinazofanywa na serikali za kukabiliana na vitendo vinavyoendelea vya kuwaua maalbino na kufukua makaburi yao, ambavyo vinatokea katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Arusha.

Alisema pia wako katika maandalizi ya kukutana na mamlaka zinazohusika zinazoshughulikia masuala ya haki za binadamu kama Wizara ya Usalama wa Raia, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ili kuona namna bora ya haraka ya kukomesha mauaji ya dhuluma yanayofanywa dhidi ya watu hao.

Alisema suala la mauaji hayo ni kipaumbele kama yalivyo matukio mengine, kwani muda si mrefu lilikuwapo tukio la utata wa upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambalo serikali ililazimika kuunda tume ya kuchunguza suala hilo na tukio lililotokea Hospitali ya Maswa ya kufariki mtoto wa miaka saba kwa kukosa Sh 12,000, imeundwa Tume.

Alisema licha ya watu wanne ambao ni albino kutoka mikoa ya Arusha, Mara na Mwanza, kuripotiwa kuuawa kinyama na wazazi wao au majangili wa binadamu na baadhi ya makaburi kufukuliwa, hakuna hatua yo yote iliyochukuliwa zaidi ya kuliwazwa kwa kisingizio wameuawa kwa imani za kishirikina.

“Kwetu sisi tunaamini kwamba huu ni uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu huku dola ikionyesha udhaifu mkubwa kulinda raia zake na kutufanya tuishi kwenye mazingira ya mashaka huku tukiamini kama si leo, basi kesho arobaini zangu zitafika; hivyo kuamini kwamba dola linatutoa kafara,” alidai.

Alisema maamuzi hayo yamekuja baada ya chama hicho kwa kushirikiana na wadau wengine kufanya warsha ya siku mbili Desemba 10 na 11, kwa madhumuni ya kujadili hali ya kuzorota kwa usalama wa maisha ya jamii ya maalbino nchini kutokana na mauaji ya mfululizo yanayofanywa dhidi yao.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Esaka Mugasa, akizungumzia suala hilo, alisema Polisi haiwezi kupuuzia suala lolote linalohusu mauaji, hivyo mauaji ya maalbino yanafahamika katika jeshi hilo na yanaendelea na upelelezi ili kupata ushahidi utakazowawezesha kuwafikisha mahakamani wahusika wa matukio hayo.
Source link: HabariLeo.

SteveD.
 
Mimi naomba niulize maswali matatu

1. Taja mapendekezo matano kumshauri raisi kokomesha rushwa.
2. Je ndugu yako au rafiki anayefanya kazi serikalini kama benki kuu au TRA akikupigia simu na kukuambia amepata pesa nyingi za rushwa na kajenga nyumba ya pesa nyingi kwa pesa hiyo Je utamsifia au utamkana?
3. Je unaamini rushwa imekua utamaduni (culture) au ni kwa sababu ya umasikini?

Naomba majibu mafupi
 
Naona majibu hayaji!!. Watanzania ili tuweza kufanikiwa inatubidi tuwe na nia, moyo na uhakiki wa mawazo yetu. Hatuwezi kwa upande mmoja tunalalamika raisi hafanyi kazi ya kutosha kukomesha rushwa na upande mwingine tunawasifia marafiki wala rushwa kwamba wamepiga deal!, na walarushwa wengi tunawaita wafanya biashara wakati biashara yao kubwa ni rushwa.Rais hawazi kuwa police wa culture bali anaweza kujaribu kuweka sheria za kukomesha rushwa. Ili lengo letu la kukomesha rushwa lifanikiwe inabidi Watanzania tubadilishe culture ya kusifia walarushwa na tabia ya kufikiri raisi amechaguliwa kubadili culture yetu ya rushwa. Unafiki wa kufikiria upande mmoja utaleta vigoigoi na vicheko vingi kwenye mtandao lakini kama kweli tunataka mabadiliko ni lazima tukubaliane kuwa tatizo kubwa la Watanzania ni Watanzania na sub-culture mbaya zinazoingia kwenye nchi yetu na rasi pekee sisolution.Tusipokuwa makini tutakuwa kama Nigeria wana wasomi wengi kuliko nchi za kiarabu, wanamawazo mengi ya kisomi, na vilevile wana mafuta lakini ni masiki wakubwa kwa sababu ya culture ya rushwa. Matatizo mengi ya nchi yetu ni culture mfano ukimwi, rushwa na elimu.Watanzania tunatakiwa tupunguze ushabiki wa kitoto na tuangalie kwa kina je tufanyeje kuiokoa nchi yetu. Tunatakiwa kuwa na mwamko wa pamoja wa kukomesha rushwa na mambo mengine yanayo zuia maendeleo.
 
I wish we had more people in our beloved country with the same attitude like yours. Thank you so much for your contribution. Mla rushwa ni mla rushwa tu hata akiwa ni ndugu yako wa tumbo moja. Siku zote inabidi aogopwe kama ukoma. Rushwa ni dhuluma na binadamu mpenda haki siku zote hawezi kumkumbatia anayedhulumu watu wengine ili yeye ajitajirishe.
 
Hakuna thread ya rushwa? ni mara ya kwanza ruswa kujadiliwa hapa?

Tulishachanganua sana aina za rushwa na kutoa mapendekezo- angalia kule kapuni!
 
Mzalendo, nashukuru sana lakini sisi ni watu tunaojifunza kila siku hivyo topics zinaweza kuja hata mara mia kwasababu mawazo ya watu yanabadilika, kila siku tuna jua vitu vipwa hivyo mawazo si msimamo bali ni elimu hivyo tuache watu wamwage mawazo yao ya rushwa hapa. Nashukuru
 
Kamundu heshima yako Mkuu,

haya maswali yako sikuyaona hapo awali....ngoja nijaribu

Mapendekezo matano
1. iweke PCCB independent
2. Pandisha mishahara ya wafanyakazi serikalini ili wafnayakazi waweze kujikimu
3. Top figures wawe wanachaguliwa na kupitishwa na kamati maalum ya Bunge na wawajibike huko huko bungeni
4. Mtu akithibitika na rushwa................mali zake zote na zinazohusishwa nazo ( kama katumia majina ya ndugu zake nk) zifilisiwe na afungwe si chini ya miaka mitano jela
5. Cut and paste zoezi la Sokoine (RIP) la wahujumu uchumi...halafu waadhibu kutumia No 4.

Swali lako la pili umeuliza kwamba je ndg yangu mla rushwa nitamsifia au nitamkana??.............naona umenichagulia majibu...............anyway SITAMSIFIA, kumkana ndg yangu siwezi..........kwani siwezi kuuondoa undugu.....ila nitamuogopa na kukaa naye mbali

Swali lako la tatu
Ninaamini umaskini uliokithiri umechochea rushwa kwa miaka mingi na hatimaye inaonekana kama culture fulani miongoni mwetu
 
Naomba kuuliza na Kueleweshwa!

Kwa kuwa kila kila gari lina unique registered number Txxxxxx!
na kwa kuwa kila gari ni lazima liwe na road license na insurance ili litembee barabarani!
na kwa kuwa kila gari lazima li-renew license na insurance kila mwaka.

Swali kwa Wabunge, Serikali, Wananchi haswa hawa wa JF.
1. Ni kwanini gari likiwa na makosa barabrani, faini isipelekwe kwenye account ya hiyo gari TRA, ili mmliki anavyokuja ku-renew road license akute faini yake iko kwenye account tayari, kwa maana hata-renew mpaka alipe faini na road license fee? (kwa maana nyingine they are should be only document exchange in the road and nothing else)

2. Kuna sababu gani za msingi za kutowaamuru wenye makampuni ya bima kwamba kabla ya ku-insure gari lolote, lazima mmliki akabidhi renewed road license.
(a) faida yake ni kwamba system mbili (insurance + road license) zinasaidiana hivyo kuongeza mapato kwa serikali na kwa wakati!
(b) Mwenye faini za usalama barabarani hawezi kukukwepa malipo kwa kuwa anabanwa kwa road license, na insurance.


Au ndio tumeweka corrupt system ili tule rushwa kwa mtindo mmoja?
 
Kasheshe,

Utaratibu uliokuwepo sijui kwa sasa, ukipatikana na kosa (driving Offfence) unapewa kitukinaitwa notification (yellow paper) ambayo ilikuwa inakuhitaji within certain period of time uwe umeshalipia hiyo fine kwenye kituo cha polisi/mahakamani n.k na kuwakilisha nakala ya malipo for reference short of that walikuwa unawekwa kwenye wanted list.

Suala kuweka fine kwenye account ya TRA il wakati wa renewal wamcharge mhusika. Tembea Bongo ndugu yangu kuna watu wanatembea na gari bila kurenew hiyo licence, kuna magari hayana valid insurance.Na ieleweke sio gari linalofanya kosa ni driver/mmiliki na pili mmiliki anaweza kubadilika hapo kati kati so who will bear the cost?

Kinachoweza kufanyika ni mpaka tuwe na satelite system ya kumonitor magari kama Ulaya na kwingineko kiasi kwamba kama hujarenew license na gari inatembea wanajua, na wanaweza kukufuatilia. Insuarer muda wake ukiisha haihitaji kukufuatilia maana ukipata ajali huimhusu hadi pale utakaporenew.

Kinachouzi bongo gari ndio inatozwa fine na sio mtu. Mfano dereva akifanya kosa akakimbia mwenye gari anadhibiwa na gari lake kukamatwa badala ya Dereva.

Tunapaswa kuwa na Utaratibu kwamba ukifanya kosa unaadhibiwa na driver anapewa onyo ndani ya miezi 6 asikutwe na kosa lingine la namna hiyo vinginevyo license yake iwe revorked, insurance nao wanahitaji kuwacharge gharama wenye magari kutokana na historia yao ya uendeshaji wa magari ama ajali alizowahi kufanya.
 
Back
Top Bottom