Jana usiku ITV ilirusa kipindi maalumu cha Mheshimiwa Lembeni Mbunge wa Kahama akikabidhi hundi ya sh. 100,000,000.00 ambayo ilitolewa na Mwenkikiti wa Makampuni ya IPP Bwana Reginald Mengi kwa VIKOBA Kahama. Sina shida na uchangiaji wa Bwana Mengi, bali ni staili iliyotumika katika kuikabidhi hundi hiyo kwa walengwa. Kipindi hicho kilionyeshwa Mh. Lembeni akianza kwa maelezo sifa, vijembe, sifa na shukrani kwa makundi na watu tofauti ambao aliwahusisha na VIKOBA. Moja wapo ya maneno aliyoyasema ni kwamba hataacha kusaidia VIKOBA hata kama atakuwa siyo Mbunge wa Kahama.
Baada ya Mh. Lembeni kumaliza ya kwake, alifuatiwa na Nape Mnauye ambaye ni Mjumbe wa NEC na kwenye tukio hilo alikuwa mgeni rasmi. Na hapa ndipo mimi nilipoanza kukwazika. Miongozi mwa maneno ya Bwana Nape ambayo aliyasema na mimi kunikwaza hi haya; Katika NEC moja wapo ya mambo ambayo tumekubaliana ni kwamba Mbunge anayetekeleza ilani ya CCM kwa vitendo, anatufaa kwa uchaguzi wa mwaka 2010, na Mh. Lembeli kwa tukio hili anatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, hivyo anatufaa kwa uchaguzi wa 2010. Sawa wadau haya mazingira siyo ya kutoa rushwa? Mh. Lembeli amekabidhi hundi ya sh 100,000,000.00 kwa VIKOBA, halafu inafuatiwa na yeye kufagiliwa kuwa anafaa kuwa Mbunge tena wa Kahama, mnaonaje hapo?
Lakini jingine ninalojiuliza Bwana Mengi atatoa sh. 100,000,000.00 kwa wabunge wangapi katika kutekeleza ilani ya uchaguzi wa CCM?
Naliweka jamvi wazi kwa mjadala